Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 yatangazwa

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 yatangazwa

ishu ni kwamba hiyo one ya saba haina msisimko kama zamani. Zamani mwanafunzi akipata hiyo nchi nzima mtamjua anatoka shule gani. Sasa hivi hata hao wahitimu hawana habari kujua hao waliopata hiyo one wanatoka shule gani na wakoje. Hizo one za siku hizi ni ceremonial tu
Sahihi...
 
Ufaulu Umepanda.

Futatilia hapa.


View: https://www.youtube.com/live/uwbLeIIRXOc?si=m-Iyj06qeAYHlPCl

Kupata Matokeo fungua link hii: https://matokeo.necta.go.tz/results/2025/csee/index.htm

---
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika kuanzia Novemba 17, 2025.

Matokeo hayo yametangazwa leo Jumamosi Januari 31, 2026 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Profesa Said Mohammed.

Jumla ya wanafunzi 569,883 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari waliosajiliwa katika shule 5,864 na watahiniwa na kujitegemea wakiwa 25,927 waliosajiliwa katika vituo 813.

Taarifa ya Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohammed ya Novemba 16, 2025, ilieleza idadi ya watahiniwa wa mwaka 2025 ni ongezeko la asilimia 7.67 ikilinganishwa na wa mwaka 2024.

Kati ya watahiniwa wa shule 569,914 waliosajiliwa mwaka 2025, wavulana ni 266,024 sawa na asilimia 47 na wasichana ni 303,859 sawa na asilimia 53.

Mahudhurio katika mtihani huo yalikuwa asilimia 97.5 sawa na wanafunzi 555,606.

Takwimu zinaonesha kuwa ufaulu umepanda kwa asilimia 2.61 na kufikia asilimia 94.98 ambapo watahiniwa 526, 620 wamefaulu kwa kupata daraja I,II, III na IV.

Ufaulu kwa waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu wameongezeka wakiwa wanafunzi 255,404 sawa na asilimia 46.1.

Mwananchi

Huo ufaulu wa divisheni 4 nina mashaka nao. Hizi takwimu zimepikwa kisiasa kwa manufaa ya maCCM.
 
Zamani div 1 F4 zolikua kwa st tu.
Utakuta st wanafunzi 90 wote Div 1.
Lkn hivi hata Zanzibar zinapatikana.
NECTA ya ndalichako ni tofauti na hii ktk swala la ufaulu. Sijaangalia islamic school, lkn inaonekana nako mambo yamebadilika
 
Zamani div 1 F4 zolikua kwa st tu.
Utakuta st wanafunzi 90 wote Div 1.
Lkn hivi hata Zanzibar zinapatikana.
NECTA ya ndalichako ni tofauti na hii ktk swala la ufaulu. Sijaangalia islamic school, lkn inaonekana nako mambo yamebadilika
Kwani elimu ya sekondari ni muungano?
 
Screenshot_20260131-121451.jpg

WATOE WAPI MATOKEO MAZURI? VILAZA TU
 
Nikaona "breaking news" nikaja nakimbia nikidhani tayari mambo yashaiva huko Magogoni/Tunguu nusu mlingoti kumbe matokeo tu wanatangaza!, ok kila la kheri kwa wahitimu wote!.
Ishu kama matokeo haitakiwi kuwa breaking nuzi.

Inakuaje breaking wakati yametangazwa na nekta na yamewekwa kwenye website??? How come ni breaking?

Breaking huwa ni habari ambayo haijakamilika hivyo watu hupewa taarifa vipande vipande tu kisha baadae ndio habari huja ki undani zaidi.

Je haya matokeo yamekuja nusu mpaka mseme ni breaking news?

Matumizi ya ule wino mwekundu yameshimiwe, mwenyewe nilivyoona breaking news nimestuka, kuja kucheki matokeo ya fm4
 
ndiyo sababu ya kuweka mtoto wake huko necta? lkn si haba angalau na muslims wa tanzagiza nao wameanza kwenda shuleni badala ya kushinda madrasa siku nzima kukariri Kurani …
Mtateseka sana,nowdays kwenye ajira na watahiniwa ni mwendo wa namba tu,hamna majina ndipo mtakapojua pumba ni zipi na mchele ni upi
 
Back
Top Bottom