Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 yatangazwa

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 yatangazwa

uran

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
18,488
Reaction score
30,806
Ufaulu Umepanda.

Futatilia hapa.



Kupata Matokeo fungua link hii: https://matokeo.necta.go.tz/results/2025/csee/index.htm

---
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika kuanzia Novemba 17, 2025.

Matokeo hayo yametangazwa leo Jumamosi Januari 31, 2026 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Profesa Said Mohammed.

Jumla ya wanafunzi 569,883 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari waliosajiliwa katika shule 5,864 na watahiniwa na kujitegemea wakiwa 25,927 waliosajiliwa katika vituo 813.

Taarifa ya Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohammed ya Novemba 16, 2025, ilieleza idadi ya watahiniwa wa mwaka 2025 ni ongezeko la asilimia 7.67 ikilinganishwa na wa mwaka 2024.

Kati ya watahiniwa wa shule 569,914 waliosajiliwa mwaka 2025, wavulana ni 266,024 sawa na asilimia 47 na wasichana ni 303,859 sawa na asilimia 53.

Mahudhurio katika mtihani huo yalikuwa asilimia 97.5 sawa na wanafunzi 555,606.

Takwimu zinaonesha kuwa ufaulu umepanda kwa asilimia 2.61 na kufikia asilimia 94.98 ambapo watahiniwa 526, 620 wamefaulu kwa kupata daraja I,II, III na IV.

Ufaulu kwa waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu wameongezeka wakiwa wanafunzi 255,404 sawa na asilimia 46.1.

Mwananchi
 
Vijana 1.7 wamepiga za kutosha kabisa!!
ishu ni kwamba hiyo one ya saba haina msisimko kama zamani. Zamani mwanafunzi akipata hiyo nchi nzima mtamjua anatoka shule gani. Sasa hivi hata hao wahitimu hawana habari kujua hao waliopata hiyo one wanatoka shule gani na wakoje. Hizo one za siku hizi ni ceremonial tu
 
Hizo one nyingi si za kujivunia, still wahitimu hawana uwezo wa ku sustain na kufanya analysis kwa maarifa yote waliyofundishwa. Kwanza peper lenyewe wanalofanya ni rahisi mno, wanatungiwa mtihani huo ili wafaulu. Paper la zamani ukiwapa hawa wototo wanafeli wote. Zamani mtihani ulitungwa kwa lengo la kufeli na kufaulu. Ukifaulu we ni kichwa kweli kweli! Paper lilikuwa lina mitego mingi mwanzo hadi mwisho, ukiliparamia tu kwa kuwa unajiona unamudu masomo utajikuta umefeli na wengi watashangaa umefeli vipi wakati darasani ulikuwa kinara! Paper la siku hizi ni maji sana ili watoto wafaulu
 
Back
Top Bottom