Matokeo ya form 4 yanaonesha wazi mikoa ya kaskazini iko juu sana kielimu, tofauti yao hawapendi kujisifu na kujigamba kama mikoa mingine inayofuata

Matokeo ya form 4 yanaonesha wazi mikoa ya kaskazini iko juu sana kielimu, tofauti yao hawapendi kujisifu na kujigamba kama mikoa mingine inayofuata

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,450
Nimekutana na matokeo haya ya mikoa, ya kwanza ni kwa ufaulu wa division 1 hadi 3, ya pili ni division 1 hadi 4, Matokeo nayoamini yanaonyesha ufaulu wa uhakika ni division 1 hadi 3.

1. Division 1 hadi 3

Top 3 zote zinaenda mikoa ya kaskazini na wala hakuna kelele.

1770023737554.png

2. Division 1 hadi 4

matokeo ya ufaulu yanapendeza sana, Nchi nzima 94% ya wanafunzi (wanafunzi 94 katika kila wanafunzi 100) wamefaulu.

1770114687772.png

Ni kweli huwa kuna wanafunzi wa nje ya mkoa husika lakini hili ni jambo la kawaida kwa mikoa yote, idadi ya wanafunzi wageni haizidi 10% ya wanafunzi wote katika shule zote, wageni hupatikana zaidi katika shule chache za vipaji maalum na shule binafsi zinazofanya vizuri kitaifa.
 
Elimu ya Tanzania ni magumashi tu.kama unapesa somesha nje ya nchi.Hapa nyumbani tutajifariji na vimatokeo uchwara kama hivi.
Kama hutaki mwanao asome elimu kwa mitaala ya Tz, Huna haja ya kusomesha nje, kuna international schools zimejaa mikoa ya kaskazini ada si chini ya milioni 20, wanatumia cambridge curriculum
 
Kama hutaki mwanao asome elimu kwa mitaala ya Tz, Huna haja ya kusomesha nje, kuna international schools zimejaa mikoa ya kaskazini ada si chini ya milioni 20, wanatumia cambridge curriculum
Dar pia zipo nyingi na wanasoma watoot wa wakubwa wengi tu zipo za mil30 pia nzuri tu ila malezi ndo utajuta kama hupendi mtoto mwenye tabia za ovyo
 
Dar Mkoa wa wakata mauno unapepelea mkia 😂😂
  • Kila siku matukio - shows za wasanii, mpira, beach, n.k.
  • Kuamka saa 10 kujiandaa kwenda shuleni
  • Jiji lenye vishawishi na utandawazi zaidi nchini
  • makundi mengi sana
  • vibanda vya games kila mtaa
  • vijimambo vya mitaani kama vigodoro.

Kufaulu Dar ni kazi sana
 
Dar pia zipo nyingi na wanasoma watoot wa wakubwa wengi tu zipo za mil30 pia nzuri tu ila malezi ndo utajuta kama hupendi mtoto mwenye tabia za ovyo
Dar ndio jiji kuu la nchi lakini nje ya hapo international schools zimejaa mikoa ya kaskazini Arusha, Kilimanjaro na Manyara, huwezi kukuta international school Kagera, Shinyanga, Mbeya, Lindi, Rukwa, n.k.
 
  • Kila siku matukio - shows za wasanii, mpira, beach, n.k.
  • Kuamka saa 10 kujiandaa kwenda shuleni
  • Jiji lenye vishawishi na utandawazi zaidi nchini
  • makundi mengi sana
  • vibanda vya games kila mtaa
  • vijimambo vya mitaani kama vigodoro.

Kufaulu Dar ni kazi sana
Sasa wanafunzi tu wanaitana familia kuna shughuli hapo? 😁
 
Back
Top Bottom