Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Halafu watanzania tuache ukabila
Mie na wazee wangu si wachaga,maisha tu yalimfikisha mzee huko akajenga na tukazaliwa,moshi town kuna makabila mengi sana
Labda huko migomban,ila kwa pale mjini asilimia kubwa ni wakuja
So sio kila anayeiongelea moshi ni mchagga
Sote ni watanzania na tuna haki ya kuishi popote Tanzania, madhali huvunji sheria za nchi
Hii thread ni maalumu kwa wana moshi ,whether mchagga ama chasaka .Wengine tumezaliwa pale town ,tukakua tukasoma and our childhood memories ziko pale,so tujiue ili tusiikumbuke moshi?It's Gods plan.Naomba mjadala na uendelee.ukabila pembeni.we both Tabzanians apart from our tribal differences.
Mi mwenyewe sio mchaga ila nimekulia moshi
 
Hahahaha dah,Moshi ya kipindi kile ni nyoko. Kama wewe ni mgeni ukiwa na gari watu wanakufahamu kuwa huyu si mwenyeji na ukijifanya mjuaji gari inaibwa mchana kweupe kabisa. Nakumbuka kuna Mzee mmoja jina sitamtaja alikuwa mfanyakazi pale town tatizo lake alikuwa anatumia Cheo na hela zake kukamua mademu wa Watu. Sasa kuna siku akaenda zake club pale Alberto alipotoka nje hakukuta gari wacha aitafute mpaka kwenye koti. Kumbe wazee walishaichukua na kupelekwa kufichwa kule Kifumbu. Mzee akaambiwa atoe mpunga mrefu apate gari lake la sivyo hataipata kamwe. Akaambiwa ikifika kesho saa sita mchana afike pale Pub Alberto aweke mzigo kaunta then aondoke zake atapewa maelekezo mengine na ole wake aende na Polisi. Kweli Mzee akafanya aliyoambiwa akapigiwa simu aende Kifumbu ataikuta gari yake,kweli aliikuta.
Kuna mzungu fulani anamiliki hotel kule ziwa Tanganyika visiwani kipili,naye alilizwa vx mpyaa yaani ametoka njee anakuta hakuna kitu,
 
Moshi mji flan wa ajabu sana

Kama Chigaco hivi ama New Orleas ina watu wake kitambo na kitambo wanachoka lakini majina yao yanabaki palepale

Sijui miaka ya karibuni ila zamani watu maarufu kutoka Dar ilikua wakija Moshi hakuna mtu ana story nao hakuna kabisa

Ila Marehemu Mzee Ndesamburo akipita pale town na ile land rover nyeupe ya Keys kelele mji unalipuka kupita maelezo

Moshi ya leo story zimebaki kwenye Pombe Jumatatu mpaka Ijumaa watu wapo Mekus, Hugos, Qwine na Hapa Red Stone

Vijiwe vya kitambo Pub Albero na Malindi wanaenda watoto wa Njoro na Pasua...Aventure ndio bure kabisa siku hizi panafanyika vikao vya harusi tu....Ila Moshi itadumu milee na story zake za Kale
Acha ndesa apumzike bna,sidhani hata hizi purukushani za CCM kama zingeweza kumnyima jimbo ndesa pesa
 
Panaitwa Milans kwasasa. Hao waliotoka mji mpya primary ni miaka gani hiyo? However palikuwa popular, nadhani hata kama hukusoma pale mjini, lazima utakuwa umeshafika hapo kwani palikuwa soo popular kwa watoto especially wanafunzi kwasababu ya koni. Ndo alikuwa kama Bhakhresa wa Moshi.
Tisini tisini mkuu ,sikukuu hujaenda kwa jani hujatembea,au kwenda makutano na paradise kuangalia komando kipensi.
 
Tehe tehe.
Hata eneo la keep left cha shule ya majengo kipindi hiyo kulikuwa na hizo tetesi.
Kukatiza usiku ilikuwa ni balaa
Matukio ya pale yalihusiana pia na vyoo vya shule ya majengo visivyotumika nyuma ya hall LA majengo secondary.
 
I do that and am proud
Tatizo naona kuna watu wakisikia story za moshi wanageuza kuwa za wachagga.really?
Naamin ulikuwa mpango wa Mungu nizaliwe na nikulie pale moshi mjini
Sion kama kuna ubaya
And it's true moshi ulikuwa mji mtamu sana
Nimeinjoi maisha yangu ya utoto moshi
That's y daily nakumbuka
Ilikuwa nikiamka asuhuh nijiandae kwenda shule nauona mlima Kilimanjaro ulee,theluji iking'aa
Those are wonderful memories I will never forget
Tatizo ni ccm mkuu na chuki za kipuuzi.siasa chafu
 
Habari za mida wana jf

Kipindi nakuwa moshi town pale wenyewe wanapaita mji wa wagumu, kulikuwa na matajiri wanajulikana na kusifika sana.
Walikuwa maarufu sana hadi makanisani.Ukienda kanisani ukimwona hata mke wake unabaki waooo
Walikuwa hadi na siti zao kristu mfalme pale.waliishi uzungun,wengine njia ya old moshi.

Kuna siku tumeenda nyumbani kwa rafiki yetu mmoja tulikuwa tunasomanaye mafundisho kanisan maeneo ya uzunguni kule,huo mjumba looh tulibak mdomo wazi.Na ilikuwa first time naona swimming pool nyumban.

Anyway zama zimepita, wengi wameaga dunia,wengine wapo ila umaarufu sio kama zamani.Nilikuwa natoka familia ya kikapuku kabisa so nilitaman siku moja at least na sisi family yetu iweze kuwa na jina kama family zile ama hata visenti tu.

Kuna mzee mmoja alikuwa maarufu sana hapo moshi town,alikuwa na maduka,garages,mabar,mabasi na biashara kibao.Alikuwa anaheshimika kama mfanyabiashara mkubwa moshi.Na wengi tuliamini hivyo.Bwana weeh siku moja katika harakati zake,akapatwa na majanga kwenye mbuga za Kenya, akapigwa risasi akafa,wenzie walifanikiwa kukimbia.Ikaja fahamika mzee alikuwa mwindaji haramu kwenye mbuga ya tsavo,alikuwa anawinda tembo na kuuza pembe na ndio ulikuwa siri ya utajiri wake.

Alirudishwa moshi akaenda zikwa kwao migombani ,after wards Mali zile zikayeyuka kama barafu. Since then nikajifunza kutokutamani cha mtu kwani hujui kakipataje. Utajiri una siri kubwa so vijana wenzangu tufanye kazi.Usiamini story za nilianza na kushona viatu stend,huwa hawasemi ukweli.
Nomependa mistari yako ya mwisho, tena anakazia usikate tamaa, Fanya kazi kwa bidii sasa unawaza mbona naona wengi wakijituma na hawana? Utajiri ni siri kubwa.
 
Kawaida mbona because am smart
Mie naandika na kupresent maripot daily huku serikalin
So huwez kuta naandika kama kina nanihii
Nimepikwa nikapikika
Halafu mmezoea watu smart ni me tu
So pathetic
Nimeandika vitabu 5 hadi nagraduate
So it's normal
I know kujipresent
Siandikagi sentensi zenye xoxo kama kina f f f f
Vitabu 5 ? Well wewe ni Associate Professor au ?
 
Write your reply...makampuni ya mabasi tz karibu 40% ni ya wachaga,karibia mikoa yote tz basi la mchaga lipo
kidia one
Machame safari exp
ngorika exp
dar exp
meridian exp
lim Safari
ibra line
Osaka
princes muro
lucky star
happy nation
hai exp
ester exp
mtei exp
kimambo exp
MarAngu exp
arusha exp
tilisho exp
pia mmiliki wa precision air n mchaga,Michael ngaleku shirima
Umesahau BM coach za Morogoro
 
Kuna msela wa kiborloni tulikula nae bata
Sana siku moja na wachumba madai yake kaleta jiwe dar kuuza.
Kumbe anavizia Nissan patrol moja kipisi ya Abbas Mwinyi enzi hizo.
Timming ikakataa jamaa akaona asiondoke bure akaenda kuiba land cruiser ya elimu mshike mshike na polisi akikimbia wakamwangusha bagamoyo huko akitoroka.
Nakuja ona taarifa ya habari, jamaa ni yule yule tulikesha nae jana kumbe mtu wa issue.
Na alikua mstaarabu tu huwezi dhania
 
Sasa wewe ulozaliwa na kukulia sehemu ambayo mwanamke anachukuliwa kama chombo cha starehe nakujibu nini?
Tuma matokeo yako ya kidato cha nne kama wewe mwanamke kweli nami ntatuma yangu
Usishindane nami
Pambana na hali yako
Wakati wanakufukua wacheza ngoma and all that nilikuwa darasani
Nimeshika namba moja toka primary hadi chuo kikuu,gpa yangu huna na kamwe hata urudi darasani Huwezi ipata
Remember mimi si mwalimu
Unayoyawaza nishayafanya sana
I repeat stay on your lane
Ni vyema tukapunguza maneno unapoongea na mtu kama Mzigua90 ambaye humjui! Kidogo nikupe was igu wake! Ana damu ya kichagga kama wewe, alisoma PCM na ana digrii. Niishie hapo naogopa kuingilia huu ugomvi wenu maana nyie wote watoto wa wachagga
 
Write your reply...makampuni ya mabasi tz karibu 40% ni ya wachaga,karibia mikoa yote tz basi la mchaga lipo
kidia one
Machame safari exp
ngorika exp
dar exp
meridian exp
lim Safari
ibra line
Osaka
princes muro
lucky star
happy nation
hai exp
ester exp
mtei exp
kimambo exp
MarAngu exp
arusha exp
tilisho exp
pia mmiliki wa precision air n mchaga,Michael ngaleku shirima
Bm coach
Lakrome
 
Back
Top Bottom