Maskini RFA, ndiyo kwaheri hivyo

Maskini RFA, ndiyo kwaheri hivyo

Kuna kipindi Vodacom nao waliyumba asa kipindi Rostam alipouza Isa zake za VODA
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Enzi za R.F.A

Mtangazaji: unaitwa nani
Mwili obare:naitwa Mwili obare kutoka musoma Mara
Mtangazaji: mwili obare

Naaaaaàaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaàaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaammm

Yani jamaa alitika mpaka radio Betri zikaisha.
Mwili Obare kutoka kwa watu wazito Igoma Mwanza. Alikuwa hakosi line pale RFA wakati wengine wakihangaika kupiga simu yeye utafikiri alikuwa na line yake peke yake. Naaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam
 
Kweli na mm nimewacheki ni mlio wa DW tu nahisi dialo na bwana Mkubwa kuna sehem hawakwenda sawa, tusubir 2020 itafufuliwa kwenye kampeni
Mbona wagumu kuelewa? Tatizo lililoikumba sekta binafsi,/wafanyabiashara na pesa ni pana Sana, si wao tu Kama media pia wamo hata ipp Hali tulisikia hali ni tete mishahara kulipana, , New habari wao tayari gazeti limesimama, wale channel ten na magic FM wameokolewa na chama kuamua kuinunua kampuni
Kwa hiyo ndio hali halisi ni sawa tu kama mlivyosikia mkutano wa wafanyabiashara kua kampuni za mabasi zaidi ya 50 zimeshasimamisha Huduma
 
Inasikitisha sana... nakumbuka enzi nikiwa kachalii nilivipenda vipindi vya RFA kama vile Sindano 5 za moto by Fred Waa, Show time, Weekend Fever, Search Line, Je wajua? na Michezo.
Ukisikia Neeeeews ..sauti za watangaza news zilikuwa nzuri na makini sana...
God!
Ilikuwa noma sana jingle linapiga neeews kisha anasikika kusoma habari Lazaro Matalange jamaa alikuwa na vocal ya zege...kweli RFA inamuhitaji mwokozi
 
mm nilikiwa nakipenda sana kipind cha magazet sa 12 na nusu asbh na dw na bbc jion na sa saba mchana
Yes nakumbuka 1999 hicho kipindi cha udondozi wa magazeti walikuwa wanakiwasilisha Hamisi Dambaya na Egbert Mkoko redio mkoa tulikuwa utaipata kwa AM(Amplitude Modulation)...wakati huo nawasilikiliza kwenye karedio kangu ka Rising kwenye geto lililobandikwa magazeti ukutani yenye picha za Notorious B.I.G , Lil Bow Wow,JLo nk...
 
Kuendesha kituo cha redio au television ni gharama sana.
Kwa muda mrefu tu Sahara Media wamekuwa wakiendesha kwa hasara, ndio maana madeni yamekuwa mengi, including ya serikali (TRA). Hakuna waangaliaji, hivyo wamekuwa wakipoteza wadhamini/matangazo.

Mikopo ingesaidia mno kama wangejaribu kuji-reinvent kabisa. Lakini walibaki vile vile.
Tunasikia nowdays kwenye media za dini kila siku zikitangazia A/c No. za benki na namba za simu ili waumini/washiriki wao na watu wengine wazichangie.

Na wanapata shekeli za kutosha, kuna media nyingine za dini makanisa yao wamewekewa kiasi cha kutoa (asilimia)
 
Tunasikia nowdays kwenye media za dini kila siku zikitangazia A/c No. za benki na namba za simu ili waumini/washiriki wao na watu wengine wazichangie.

Na wanapata shekeli za kutosha, kuna media nyingine za dini makanisa yao wamewekewa kiasi cha kutoa (asilimia)
Inabidi tu.
Mfano mzuri ni Radio Maria. Kwa kuwa ni ya dini na haina matangazo kabisa, ukienda taasisi karibu zote Catholic Tanzania utakuta kibubu cha kuchangia. Na hapo kumbuka hiyo redio ni non profit, kwa hiyo ina punguzo za tozo serikalini kama TCRA.

Sasa imagine watu kama sahara halafu hawana mapato makubwa na hawachangiwi. Hii biashara ni changamoto sana sasa hivi. Redio na TV zina mbadala online.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom