Simulizi - change (badiliko)

Elton Tonny

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
262
1,877
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+


DISCLAIMER: Hadithi hii ni utunzi wa kubuni tu. Haina uhusiano na jambo lolote halisi lililowahi kutokea, na kila mhusika atajwaye aidha wa kubuni au mrejewa halisi ni kwa kusudi la kuburudisha tu msomaji. Hii siyo hadithi itakayomvutia kila mtu, hivyo endapo haitafikia matarajio ya watu fulani, wanaombwa kuachana nayo tu na kuwapisha wale watakaopenda kuifatilia zaidi. Misemo, matukio, mandhari, maeneo, na marejeo yote yaliyomo ni vitu vya muhimu kuifanya kazi hii ya utunzi ipendeze, na hayajakusudiwa kutoa ujumbe wowote kwa madhumuni mabaya. Busara kwa msomaji inahitajika.


★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KWANZA

★★★★★★★★★★★★★★


Ni usiku usiojulikana saa, giza ni zito haswa, ndani ya eneo lililo na uoto mwingi wa asili. Kuna mtu anakimbia ndani ya eneo hili, kukimbia kwake ni kwa njia ya woga mwingi alionao kwa sababu anakimbia ili kuokoa uhai wake. Lakini hawezi kuona vizuri mbele kwa sababu ya giza, naye anaanguka mara kwa mara kwa sababu ya kuhisi uchovu mwingi, maumivu mengi, na kizunguzungu kizito kichwani kwake. Anajaribu hata kupiga kelele, lakini anashindwa kwa kuwa mdomo wake unadondosha damu nyingi sana. Hana ulimi.

Mtu huyu ni binti mdogo mwenye miaka kumi na kitu tu, naye amejikuta ndani ya janga ambalo akili yake inatamani lingekuwa ni ndoto mbaya tu, lakini anaelewa wazi kwamba siyo ndoto, na kifo kiko nyuma yake. Anajaribu kuokoa uhai wake ingawa anaelewa wazi kwamba anachokikimbia, yaani kinachomfata, kiko karibu naye sana, lakini ni kama kinafanya mchezo pamoja naye kwa kuwa kinajua hawezi kufika mbali.

Hatimaye nguvu zinamtoka kabisa binti huyu, naye anaanguka chini na kubaki amelala tu huku akihisi ni kama kuna vitu vizito vimemlemea kwenye mwili wake, na hawezi tena kujongea. Anafumbua macho na kuyafumba kwa uzito sana, na kwa sekunde hizo chache, anahisi mwili wake ukishikwa sehemu ya kiunoni na kugeuzwa taratibu, ili awe kama amelala chali. Amelegea mno, akiona vitu mara mbili-mbili kama vile macho yenye makengeza yanavyoona. Kilichokuwa kimesimama katikati ya mwili wake uliolala chini hakikuwa kitu cha kibinadamu kabisa, na ingawa msichana huyu aliogopa sana, alikuwa amechoka mno kuonyesha hilo.

Kiumbe hiki kilisimama tu na kumwangalia kwa njia ya kikatili sana. Msichana huyo alipopata nafasi moja tu ya kukiona usoni ingawa ilikuwa gizani, aliona namna ambavyo macho ya huyo kiumbe yalivyokuwa mekundu na yenye lenzi zilizofanana na zile za macho ya nyoka mwenye sumu, na mdomo wake ulikuwa umechanika pande za pembeni kuruhusu meno makali na mengi sana yatokeze nje huku yakidondosha udende mzito wa damu nyeusi. Kisha likaanza kuupanua mdomo wake huku linatoa sauti ya kukwaruza kwa chini, halafu ghafla likaishika miguu yake na kuanza kumburuza kurudi upande aliokuwa ametoka, na kisha kutokomea naye gizani.....


★★★★


Moja kwa moja mpaka ndani ya jiji kuu; jiji kubwa sana kimaendeleo nchi nzima. Kama kawaida ya majiji makubwa, sikuzote huwa hakukosekani jambo fulani muhimu vya kutosha kutumiwa kama ubuyu kwenye taarifa za habari, iwe kubwa au dogo, ni lazima tu liwepo. Wakati huu, kulikuwa kumetokea ajali mbaya sana siku ya Jumamosi, iliyohusisha gari kubwa la kubeba mizigo na basi dogo la abiria (Costa), iliyosababisha vifo vya watu 17 na kuwajeruhi wengine 36; hiyo Costa ilikuwa imejaa, siyo mchezo. Taarifa za maafa hayo zilisambaa upesi, na hata baadhi ya watu walikuwa wamechukua video eneo la tukio kwa simu zao na kuanza kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii, na ndipo zikawafikia watu wawili muhimu sana ndani ya kisa hiki.

Blandina Sospeter. Mwanamke mrembo mwenye umri wa miaka 30. Sura na umbo zuri ni kati ya vitu vinavyomfanya mwanamke atamanike, lakini Blandina hakuwa tu na sura na umbo zuri, bali akili nyingi pia. Alikuwa na urefu wa wastani tu kawaida ya mwanamke, yaani si mfupi si mrefu sana, mwenye ngozi laini ya rangi ya maji ya kunde. Mwili wake ulikuwa umenawiri vya kutosha lakini hakuwa mnene sana, bali alibeba mapaja manono na hips zilizochoreka vyema kila mara alipovaa nguo zilizoubana mwili wake. Alikuwa na kalio kubwa vya kutosha hata kutikisika sana kwa nyuma endapo angevaa dera kubwa (pigia picha nguo za kubana sasa), na alikuwa na sura nzuri, fupi yenye midomo mizuri, macho madogo kiasi kama ya mchina wa Tanzania ya mbali, na alipendelea kusuka nywele za rasta ndefu au zenye muundo kama nywele laini za wazungu. Alijua sana kupendeza.

Kisha tunakuja kwa Namouih Donald Masoud. Ukisikia wale wanawake wanaoukaribia uzungu wa kiarabu au kihindi kwa mionekano yao, ndiyo alikuwa huyu sasa. Namouih alikuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 32. Alikuwa mrembo ajabu. Alikuwa mrefu, yaani urefu unaopita urefu wa kawaida kwa mwanamke, na alikuwa na ngozi nyeupe sana. Siyo kwamba labda alizaliwa kama chotala, hapana, ni kwamba tu ngozi yake ilikaribia weupe wa uzungu, na hata jinsi alivyoonekana usoni ilikuwa kwa njia hiyo pia ingawa wazazi wake wote walikuwa ni wazawa. Umbo lake lilikuwa zuri, akiwa siyo mnene wala siyo mwembamba sana, na hips zake zilikuwa zimenawiri na kutokeza mlima mnene kiasi huko nyuma uliofanya mwonekano wake wa kike uvutie zaidi. Usoni alikuwa mrembo mno; macho yenye mchanganyiko wa uarabu na uchina fulani hivi (wanaume wanayajua na kuyapenda macho ya hivi, huwa ni mazuri sana), na alikuwa na nywele ndefu na laini, ambazo mara nyingi alizibana au kuzisukia mitindo tofauti, na angeziachia kama angekuwa nyumbani.

Kwa ufupi ni kwamba hawa wanawake walibarikiwa kwa uzuri.

Namouih na Blandina walikuwa kama mapacha waliozaliwa na mama tofauti. Walikuwa marafiki wa karibu, wa karibu sana, tena kwa muda mrefu mno. Walikutana chuoni, na hasa kwa sababu wote walifuatilia aina moja ya kozi, kifungo chao cha urafiki kiliendelea kuimarika mpaka walipokuja kumaliza chuo na kuanza kazi. Wote walikuwa wanasheria. Lakini kulikuwa na utofauti baina yao katika ngazi zao kikazi, yaani, Namouih alimzidi Blandina cheo katika nyanja za utumishi ndani ya uanasheria. Namouih alikuwa mwanasheria mkuu (attorney), ilhali Blandina alikuwa mwanasheria wa kadiri/msaidizi wake (paralegal). Hii inamaanisha kwamba kuna mambo ambayo Namouih angeweza kufanya lakini kwa Blandina yalikuwa na mipaka, ingawa bado naye angeweza kutimiza majukumu mbalimbali ya kisheria kwa kusaidizana na rafiki yake.

Kwa mfano, kama kungekuwa na kesi, cheo cha Blandina kilimruhusu yeye kufanya kazi kama vile kuwasiliana na watu wao wa kesi ili kuwapa taarifa mbalimbali na kupitia taarifa zao, kuzipangilia, kutayarisha mambo yanayohitajika katika kesi, kuwahoji watu wao wa kesi na mashahidi, na kumuunga mkono mwanasheria wake mkuu katika kazi anazochukua na kuendesha mahakamani. Namouih akiwa kama mwanasheria mkuu, yeye alikuwa na uwezo wa kufanya mambo yote hayo kama Blandina, lakini vitu kama kuwapa ushauri wa moja kwa moja wa kisheria watu wao wa kwenye kesi, kukubali au kukataa kupokea kesi, kuwasimamia watu kwenye kesi mahakamani, na kusema kiwango cha malipo wanayotaka ili kusimamia kesi ya mtu, ni mambo ambayo yeye peke yake ndiye angeweza kushughulikia, na si Blandina.

Kwa muktadha huo inaweza kueleweka kwamba Namouih alikuwa kama "boss" kwa Blandina, ingawa Namouih hakumwona kama mfanyakazi wake bali kama msaidizi wake wa karibu sana. Na alipenda sana kufanya kazi pamoja naye kwa sababu walitoka mbali na bado hawakuwa wameachana mpaka kuanza kufanya kazi kwenye kampuni kubwa ya kibinafsi; Namouih akiwa ndiyo mwanasheria mkuu hapo. Kipato walichokipata kilikuwa kizuri, na wao ndiyo waliozitegemeza familia zao zilizoishi mikoa tofauti-tofauti.

Blandina alikuwa mwanamke mchapakazi, mbunifu, na mchangamfu sana. Alipenda kujiachia na kula bata kila mara aliyopata nafasi, kwa kuwa alikuwa na sera ya kibinafsi ya kwamba maisha ni mafupi hivyo ni bora kuyaishi kwa kujifurahisha. Siyo kwamba hakuishi kwa akili, ila angalau alijua kuponda raha. Alitoka na wanaume kadhaa kipindi cha nyuma na alipenda sana watu wenye tabia na mionekano mizuri, siyo kumaanisha alikuwa mbaguzi lakini, hivyo alikuwa mwenye kupendeka sana.

Tofauti naye kiasi, Namouih alikuwa mkali. Yaani hakupenda michezo ya kijinga kijinga kabisa, na sikuzote alitaka kuhakikisha mambo yanafanywa kwa mpangilio na ukamili. Hiyo haikumaanisha kwamba hakupenda kujifurahisha, ni kwamba tu akili yake sikuzote ilikazia fikira mambo muhimu kwanza kabla yake yeye mwenyewe, hivyo alikuwa na utu wa kivyake mno kama vile haijali dunia inayomzunguka. Ni akili yake nyingi na umakini wa hali ya juu ndiyo vitu vilivyomsaidia asiwahi kupoteza kesi hata moja tokea alipoanza mlolongo wake wa uanasheria (career). Alipenda hasa kushughulika na kesi zilizohusisha mambo kuelekea haki za wanawake na watoto, ingawa mara nyingine alichukua kesi za mambo mengine, na zote alishinda. Na ni Namouih pekee ndiye aliyekuwa ameolewa, tena na mwanaume mwenye pesa sana, na aliyempenda mno.

Sasa, siku hii ya Jumamosi baada ya taarifa za tukio lile la ajali kusambaa, ikawa imefika kwa utambuzi wa wanawake hawa kwamba mmoja wa rafiki zao alikuwa ameathiriwa na hiyo ajali. Yaani, rafiki yao mwingine mwanamke aliyeishi maeneo ambayo ajali hiyo ilitokea, alikuwa ameathiriwa nayo kwa sababu mume wake na mtoto wake walikuwa miongoni mwa abiria ndani ya Costa iliyogongwa, nao walijeruhiwa vibaya sana na kuwahishwa hospitalini. Rafiki yao huyo aliitwa Mwantum Ramadhan, ambaye naye walisoma pamoja naye chuo kipindi cha nyuma ingawa ilikuwa kozi tofauti. Hivyo wakawa wamewasiliana naye na kumpa pole kwa yaliyotokea, nao wakamwambia wangekwenda huko siku ya kesho ili kuwa pamoja naye na kumpa faraja.

Blandina, akiongea na Namouih baada ya kumaliza mawasiliano na Mwantum, alimsifu sana Mungu kwa kuwaepusha watu wa familia ya rafiki yao na kifo katika ajali hiyo. Namouih aliona ingekuwa jambo lisilo la busara kusema wamshukuru Mungu kwa sababu mume wake Mwantum na mwanaye waliokoka kifo, kwa kuwa bado kuna watu waliokuwa wakiomboleza vifo vya wengine kwenye ajali hiyo hiyo, kwa hiyo Namouih akamwambia Blandina tu hayo yalikuwa ni mambo yasiyotazamiwa na wala si mipango ya Mungu, nao wangehitaji tu kutoa mchango wao katika kuipatia faraja familia ya Mwantum kwa ujumla.

Wakakubaliana kukutana kesho asubuhi ili kuondoka kwa pamoja kuelekea kule kwa rafiki yao.


★★★


Ni Blandina ndiye aliyempitia Namouih asubuhi ya saa 2 hivi ili hatimaye waianze safari. Mwanamke huyu alikuwa na gari nzuri nyeupe aina ya Crown, na kwa sababu wangeondoka wakiwa pamoja, Namouih hakuona haja ya kuendesha gari lake mwenyewe, hivyo akaingia kwenye hilo la Blandina na wote kuondoka. Nyumba yake Namouih ilikuwa kubwa na ya kifahari sana, naye Blandina akawa anamwambia namna ambavyo siku moja atakuja kununua kubwa zaidi ya hiyo; huku na story zingine zikiendelea.

Wawili hawa walikuwa wamepanga kupita kwenye duka kubwa jijini ili kununua vitu kadhaa kwa ajili ya kumpelekea Mwantum na wagonjwa, hivyo wakafika kwenye sehemu iliyokuwa na jengo kubwa la soko la kisasa (mall), nao wakaenda ndani huko kuanza kutafuta bidhaa walizohitaji. Blandina alivaa suruali ya kubana ya rangi ya kaki, blauzi nyepesi yenye rangi nyeusi na viatu vya kike vya masai, huku akizibana nywele zake za rasta juu ya kichwa na usoni akivalia miwani ya urembo. Namouih yeye alibana nywele zake kwa mtindo wa kuacha njia kadhaa kichwani ili ziunde kama matuta-matuta mazuri sana, na alivaa nguo fulani ya blue, ikiwa kama gauni fupi lenye kubana lililooshia magotini kwake. Ilikuwa yenye mikono mifupi, iliyoufunika mwili wake wa juu mpaka shingoni, na sehemu za ngozi yake nyeupe zilizoonekana zilivuta macho ya wengi waliojali urembo aliobarikiwa kuwa nao. Blandina alipenda sana kujua kwamba waliua macho ya wengi, ingawa Namouih hakukazia fikira mambo hayo.

Wakiwa wanatoka ndani huko sasa kuelekea nje kwenye gari baada ya kununua vitu walivyohitaji, Blandina akawa anaongea na Namouih kwa utani kuhusu namna ambavyo mhudumu mmoja wa huko alivyokuwa anakosea kulisema jina la rafiki yake baada ya kulisoma. Namouih alikuwa ameandika jina lake kwenye karatasi ya cheki aliyompatia mhudumu huyo kwa ajili ya malipo, naye akawa analitamka kwa kumwita "Namoi" badala ya kulitamka "Namuuy" kama ilivyotakiwa, hivyo Blandina akawa anamwita rafiki yake "Namoi" ili kumuudhi. Namouih yeye alikuwa ameshamzoea rafiki yake kupenda kumchokonoa sana, hivyo akawa anamwacha tu aendelee na masihara yake.

Walipofika eneo la nje ya hilo soko kubwa, Blandina akapamiana ghafla na mtu mwingine ambaye hakuwa amemwona akija upande wake. Walipamiana kwa nguvu sana kiasi kwamba Blandina akaweweseka na kudondosha mifuko ya vitu alivyonunua, lakini hakuanguka kutokana na mwili wa Namouih kumkinga. Sauti za nguvu za vifaa vilivyokuwa ndani ya mifuko zikasikika, na ikawa wazi kwa haraka sana kwamba kuna kitu kilipasuka.

"Oh... sor... samahani... samahani sana dada..."

Blandina akamtazama mtu huyo aliyepamiana naye na kubaki amemwangalia tu kama anamshangaa. Namouih naye akamtazama kwa kuudhika sana. Alikuwa mwanaume kijana, mrefu kumpita Namouih kiasi, na mwenye mwili mpana uliojengeka kiume. Alivalia T-shirt ya rangi ya blue-nyeusi, kaptura fupi kufikia magotini, na viatu vyeupe kama raba. Shingo yake ilizungushiwa "headphones" nyeupe, na alionekana kuwa mtu wa mazoezi kwa sababu kifua chake kilikuwa kimetuna na hata T-shirt yake kumbana hasa kuzunguka mikono yake imara.

Lakini Blandina alikuwa akimwangalia zaidi usoni. Ingekuwa kwamba ni mwanamke, basi angemwita "mrembo sana." Alikuwa na sura nzuri huyo kaka; ndevu kutokea kwenye timba zilizochongwa vizuri lakini zikionekana kwa mbali sana, na macho yake hasa ndiyo yaliyomvutia haraka mwanamke huyu, yaani Blandina. Nywele za kichwa cha mwanaume huyu zilikuwa fupi kwa kukatwa namna hiyo hiyo kichwa kizima, yaani laini za kubrashi. Alikuwa na ngozi isiyo nyeupe sana, iliyoonekana kama weupe ulioukimbia weusi. Na kama ni kitu kingine ambacho kiliinyakua haraka akili ya Blandina kumwelekea jamaa, basi ilikuwa ni harufu yake. Alinukia vizuri sana.

Mwanaume huyo akachuchumaa na kuanza kujaribu kukusanya vitu vilivyokuwa vimeanguka. "Pole sana dada..." akawa akisema.

"Hivi kweli jamani watu mnashindwa kuangalia mnakoenda!" Namouih akaongea kwa ukali.

"Samahani yaani...."

Mwanaume huyo akasema hivyo, na ni hapo ndiyo akawa ameishika chupa ya chai ikiwa imepasuka mtungi wake wa ndani.

"Umeona sasa! Tayari umemtia hasara mtu kwa sababu tu ya kuwa careless," Namouih akasema.

Mwanaume huyo akamtazama Namouih kutokea chini hapo kwa umakini.

"Basi Nam, inatosha, haina shida," Blandina akasema.

"Haina shida?" Namouih akamuuliza.

Mwanaume huyo akasimama na kusema, "Nimemwomba samahani, siyo kwamba nimefanya makusudi. Ilikuwa tukio baya."

"Tukio baya wapi, kwani kuna giza sasa hivi? Na samahani inasaidia nini wakati umemvunjia vitu vyake vipya kabisa?" Namouih akamuuliza.

"Nam!" Blandina akamwita kumzuia.

"Kwa hiyo ukinilalamikia hivi vitu ndiyo vitarudi kuwa vipya?" mwanaume huyo akamuuliza kwa uthabiti pia.

Kuna watu kadhaa walikuwa wameanza kusimama na kuangalia kisa hiki kilichoongezeka utata.

"Mtu umemtia mtu hasara halafu bado unajifanya mkali," Namouih akamwambia.

Blandina alikuwa ameshindwa hata kusema lolote na kubaki kumtazama tu kaka huyo.

"Dada, naomba samahani tena. Hii chupa si umeinunulia huku?" akamuuliza Blandina.

"Ndiyo, lakini usi..."

"Hapana, tafadhali nisubiri nikakuchukulie mpya. Nakuja sasa hivi," mwanaume huyo akasema kwa ustaarabu.

Kisha akaelekea ndani kule kwenye maduka, akionekana kuharakisha.

Blandina akamwangalia Namouih na kumuuliza, "Hivi mbona nawe unakuwa hivyo?"

"Nakuwaje? Mtu kakutia hasara halafu unaendekeza unyonge?" Namouih akamjibu.

"Hata kama, usiwe mkali kihivyo bwana. Kaka mwenyewe anaonekana mstaarabu tu..."

"Mh... Yaani wewe nimeshakusoma, hauna lolote. Ustaarabu, ustaarabu gani ananifokea wakati yeye ndiyo mwenye dhambi? Ah-ah..." Namouih akaongea kwa kuudhika.

Blandina akaangalia upande ule alikoelekea jamaa, lakini hakumwona.

"Huyo kashakimbia dada, umeliwa. Hapa kilichopo turudi huko ndani tununue nyingine, maana hatuwezi..."

"Huyo hapo anakuja," Blandina akamkatisha.

Namouih akatazama huko na kumwona jamaa akija huku ameshikilia mfuko mdogo uliobeba kitu, bila shaka chupa.

"Siyo kila mtu yuko kama unavyofikiria dada yangu," Blandina akamwambia Namouih.

Namouih akamnyakua Blandina funguo za gari na kuondoka tu hapo akionekana kuudhika, naye akatangulia kwenye gari akimwacha Blandina anamsubiri "kaka mzuri." Jamaa alipomfikia Blandina, mrembo wetu akaachia tabasamu dogo, naye akapewa mfuko huo uliokuwa na chupa aina kama ile ile iliyopasuka.

"Samahani tena, eti?" mwanaume huyo akamwambia kiupole.

"Usijali, ondoa shaka kabisa kaka'angu," Blandina akamwambia.

"Hiyo utahitaji kuitupa, siyo? Leta nitakusaidia kuiwe..."

"Hapana usijali. Nitaitunza tu kama kumbukumbu," Blandina akamkatisha.

Mwanaume huyo akatabasamu huku akimwangalia kwa njia iliyoonyesha kwamba hakuwa amemwelewa vizuri.

"Naitwa Blandina," akajitambulisha huku akitabasamu.

Kijana huyu akatulia kidogo, kisha akasema, "Naitwa Draxton."

"Draxton. Jina zuri sana, kama wewe," Blandina akaanzisha uchokozi.

"Ahah... okay. Aa... nisikucheleweshe, tafadhali unaweza tu ku..."

"No, hapana, haunicheleweshi. Kiukweli, ningependa kama hii haingekuwa mara ya mwisho tunaonana... kama ikikupendeza," Blandina akamwambia, huku akimtazama kwa macho fulani hivi ya uvutio (seduction).

Mwanaume huyu akamwangalia kwa ufupi, kama vile anatathmini maneno ya mwanadada huyo, kisha akatazama upande mwingine na kumwangalia tena.

"Okay. Ungependa kuniona lini tena?" Draxton akamuuliza.

Blandina akacheka kwa haya kiasi, kisha akasema, "Unaonaje nikikupa namba?"

Bila hata kutoa jibu, jamaa akachukua simu yake kutoka mfukoni mwa kaptura na kumpatia Blandina ili aiandike namba yake mwenyewe. Blandina alikuwa akifurahi sana, lakini hakutaka ionekane kupita kiasi. Akamaliza kuandika na kumrudishia jamaa simu.

"Utanitext?" Blandina akauliza.

"Sure," Draxton akajibu kwa njia ya kawaida tu.

Alionekana kuwa aina ya mwanaume makini sana, na ni moja kati ya mambo mengi yaliyomvutia Blandina haraka. Mwanaume huyo akaanza kurudi nyuma taratibu huku akimwangalia Blandina kwa umakini, naye Blandina akawa ameibana midomo yake huku akimtazama pia. Jamaa akageuka na kuanza kuelekea upande mwingine akimwacha Blandina anamsindikiza kwa macho, kisha naye akaelekea mpaka ndani ya gari lake na kumkuta Namouih akiwa amekaa kwa kumsubiri.

Blandina alipomwangalia tu, Namouih akasema, "Tafadhali, please, na tafadhali sana, naomba usiniambie lolote kuhusu...."

"He's so hooot!" Blandina akamkatisha kwa kusema hivyo.

"Naomba uwashe gari twende," Namouih akaongea kwa kuudhika.

"Hahahahah... honey! Hilo HB limetokea wapi?" Blandina akauliza.

Namouih akabaki kimya tu.

"Ahahahah... Namoi bhana, unayumba sana. Mwenzio nimeombwa na namba on the first go, chezea msupu huu wewe!" Blandina akajisifia.

"Nimekwambia usiniambie, mtajuana wenyewe. Mtu mwenyewe hayuko care utakuja kumwingiza kwako ndani ya sekunde mbili nyumba imeungua," Namouih akasema.

"Anaitwa Draxton. Yaani unalitamka kizungu 'baby Drax-ten.' Aaah... walahi hapo najua sijakosea," Blandina akaendelea kuongea huku akiwasha gari.

Namouih akabaki tu kimya kwa kuwa alijua ikifika kwenye suala la wanaume Blandina alikuwa haambiliki.

"Halafu amesema nikwambie una bichwa kubwa," Blandina akamwambia kiuchokozi.

Namouih akamkata jicho kali sana, kisha akasonya na kuangalia pembeni huku akiwasha simu yake, kitu kilichofanya Blandina acheke sana. Akaligeuza gari kutoka hapo na kuwaondoa eneo hilo huku akiendelea kumchokonoa Namouih kama kawaida yake.

★★

Baada ya mwendo wa zaidi ya dakika 40, marafiki hawa wawili wakawa wamefika kwenye hospitali ambayo mume na mtoto wa rafiki yao wa karibu walikuwa wamelazwa. Walitakiwa kuivalisha miili yao khanga kwa chini ili kuwa na mwonekano wenye kusitirika kwa taratibu za hospitali, nao wakavaa na kuelekea kule ndani. Mume wake Mwantum aliitwa Selemani, na mwanaye aliitwa Islam. Blandina na Namouih walikuwa wamejitahidi kufika huko muda ambao hospitali ingeanza kuruhusu watu kuingia ili kuwaona wagonjwa, nao wakamtafuta Mwantum na kufanikiwa kumpata.

Mwanamke huyo alikuwa pamoja na watu wachache wa familia yake hapo na marafiki waliofika kuwatembelea wapendwa wake, naye akaingiwa na simanzi baada ya kuwaona Namouih na Blandina hapo mpaka akaanza kulia. Namouih na Blandina wakampa pole kwa kumkumbatia kwa pamoja, kisha wakaketi naye na kuanza kumtia moyo. Kwa sababu ya tukio lile la ajali kuwa kubwa, sehemu hiyo ilikuwa na watu wengi, na hata baadhi ya watu kutoka kwenye vyombo vya habari walikuwa hapo pia, na ilisemwa kwamba Waziri Mkuu wa Serikali alikuwa njiani kuja huku kufanya uzuru na kutoa pole zake pia.

Hazikupita dakika nyingi sana na mtu mwingine ambaye alikuwa ni rafiki ya wanawake hawa watatu akawa amefika pia. Huyu alikuwa ni mwanaume hodari, aliyefanya kazi ya upelelezi wa masuala ya kiaskari, naye aliitwa Felix Haule. Alikuwa mrefu kuufikia urefu wa Namouih, mweusi, mwenye mwili imara na mpana, naye kwa wakati huu alivalia kwa unadhifu kama mtu wa ofisini kwa shati jeupe lenye mikono mirefu, alilochomekea ndani ya suruali nyeusi ya kardet, na viatu vyeusi chini. Alikuwa na nywele fupi tu alizonyoa kwa mtindo wa "punk," naye alifika hapo pamoja na chakula kidogo na vifaa kadhaa alivyonunua kwa ajili ya kumletea Mwantum na wagonjwa.

Namouih na Blandina walijua kwamba Felix angekuja, nao wakaridhika na kufurahi baada ya kumwona. Wanne hawa kwa pamoja walisoma chuoni, na kabla ya kuachana miaka mingi baadaye walikuwa wamejenga urafiki wa karibu sana, kwa hiyo walipendana mno. Mwantum ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunga ndoa kati yao wote, kisha Felix, halafu Namouih, na sasa alikuwa amebaki Blandina tu. Felix alikuwa na watoto watatu, na alikuwa na umri wa miaka 37.

Wakaingia ndani ya chumba alicholazwa Selemani, ambaye alikuwa amevunjika mguu na kuwekewa muhogo, na bendeji nene kuzungukia kichwa chake, huku usoni akivimba sana kwa kujeruhiwa vibaya, nao wakampa pole ingawa hakuweza kurudisha shukrani kwa mdomo. Wakaonyeshwa na Islam pia. Mtoto huyo mwenye miaka 13 alikuwa ameumia ubavuni na kuwekewa muhogo mkononi pia, huku shingoni akizungushiwa bendeji nene kuzuia maumivu pindi ambapo angeigeuza, kwa kuwa aliumia hapo pia, nao wakampa pole na kumwachia zawadi nyingi.

Baada ya saa za kuwaona wagonjwa kuisha, Namouih, Blandina, Felix na Mwantum wakatoka pamoja kwenda nje kupata chakula kidogo kwenye mgahawa mmoja. Mwantum alikuwa na miaka 34, mwanamke mwenye mwili mnono kiasi uliokaribiana na wa Blandina, mweusi wa maji ya kunde, na alivalia nguo zenye ushungi wa kuzungushia kichwani kama hijab kwa ukawaida. Alikuwa mstaarabu tu lakini mwenye maneno mengi sana, na alifanya kazi mbalimbali zilizohusiana na masuala ya urembo na uanamitindo, yaani kila nyanja ya mitindo kuanzia ushonaji wa nguo mpaka upambaji wa shughuli kubwa kubwa. Yeye hakusomea mambo magumu magumu kama wenzake, lakini alikuwa na kichwa chepesi na mchapakazi.

Alifurahi sana kuwa pamoja na hawa rafiki zake ijapokuwa ulikuwa wakati mgumu sana kwake, naye akawashukuru na kuwaambia kwamba anathamini msaada wao wote waliompatia. Walikuwa wamempa kiasi kingi sana cha pesa kwa ajili ya kumtegemeza angalau, nao wakasema wangeendelea kuwa pamoja naye bega kwa bega. Yeye Mwantum akawa ameshiba sasa na kusema angerudi kule ndani, na marafiki zake wakamwambia wangeendelea kuwa hapo mpaka muda wa kuruhusiwa kuwaona wagonjwa tena ili waweze kwenda ndani ya hospitali pia.

Mwantum akanyanyuka na kuanza kuelekea hospitalini tena, na sasa Felix, Namouih na Blandina wakaendelea kula taratibu na kushushia juice huku wanaongelea masuala ya kikazi.

"Nyie wapelelezi mna jipya gani?" Blandina akawa anamuuliza.

"Hakuna jipya wala. Kila kitu doro tu," Felix akasema.

"Vipi ile ishu uliyosema mmeifatilia kwa muda mrefu? Mlifanikiwaga?" Namouih akauliza huku akinywa juice.

"Hamna bado Namouih. Huwezi kuamini yaani mpaka leo bado tunachunguza tu, halafu inazidi kuwa...." Felix akaishia tu hapo na kuendelea kula.

"Inazidi kuwa nini? Mbaya?" Namouih akauliza.

Felix akatikisa kichwa kukanusha huku akitafuna tonge kubwa.

"Ni ishu gani?" Blandina akauliza.

"Hakuwahi hata kuniambia ni nini, alisema tu ni ngumu saaana..." Namouih akasema.

"Si useme na we' naye," Blandina akamwambia Felix.

"Ah, potezea hiyo bwana. Nyie niambieni. Duo ya wanasheria mahiri mkoa mzima. Mnapiga kesi gani sa'hivi?" Felix akawauliza.

"Ya ubakaji," Namouih akasema.

"Kwa hiyo mnashughulika nayo kwa pamoja wakati huu?" Felix akauliza.

"Yeah, yaani mizungusho mingi kweli lakini ingetakiwa kuwa imeisha siku ya kwanza tu... Namouih yeye anataka iendelee, si unajua anavyopenda anasa za kesi," akasema Blandina.

"Siyo hivyo bwana, ila nataka tu challenge maana mpaka leo hakuna aliyeni-beat, na hii tutashinda tu so... kidogo inaboa ingawa ni nzuri," Namouih akasema.

"Aahahah... ni ya nani?" Felix akauliza.

"Kuna msichana amebakwa... tena na mtu aliyekuwa boyfriend wake," Blandina akasema.

"Mh? Kivipi?" Felix akauliza.

"Yaani... waliachana, kwa njia ya kuzinguana, ndiyo jamaa akamlala kinguvu. Afu' ukimwona ni mdogo tu anaonekana mstaarabu huwezi dhani anaweza kufanya kitu kibaya namna hiyo kabisa. Ila sura hazitudanganyi sisi... anakula miaka 30 jela," Namouih akamwambia.

"Halafu unajua haya mambo yenu huwa nayapenda sana lakini yananichanganya... em' nielezeeni hizo process zinaendagaje," Felix akawaambia.

"Zinaendagaje... hahahahah kwa kisukuma zaidi..." akasema Blandina.

"Wewe hautaki kutuambia mambo yenu halafu unataka maelezo ya mambo yetu?" Namouih akamuuliza Felix.

"Ni kaujuzi tu kidogo bwana acha kubania, ya kwetu mazito mno... na top secret," akasema Felix.

"Ahah... haya bwana. Mwambie paralegal wangu akuelezee," Namouih akasema huku akiendelea kula.

Felix akamtazama Blandina.

"Sawa nitakuelezea. Kwa shi'ngapi lakini?" Blandina akamuuliza Felix.

"Elezea kwanza, hela ipo tu," Felix akasema.

"Okay. Yaani, mtu akishakamatwa kama hivyo anapelekwa kwa jaji. Jaji anamwelezea mashtaka yake na kwamba kama hawezi kugharamia mwanasheria, basi atapewa mmoja ili amsaidie. Baada ya hapo ndiyo tunaingia kwenye hiki kitu kinaitwa preliminary hearing, yaani mahojiano ya awali, au niseme usikilizwaji kesi wa mwanzo kabisa. Hapo jaji anasikiliza ushuhuda kwa mashaidi na ushaihidi uliopo kutoka pande zote za wanasheria. Jaji akiona kwamba kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha mtuhumiwa amefanya maovu, ndiyo tunaingia kwenye kitu kinaitwa trial sasa..." Blandina akaeleza.

"Eeeh kwenye kurushiana maneno haswa..." Felix akasema.

"Ahahah... kama mahakama ndogo hakijaeleweka inapelekwa mahakama kuu. Lakini kabla ya siku ya trial, jaji anasema tarehe ambayo mtuhumiwa atasomewa mashtaka tena, ili achague kujitetea ikiwa anaona hana hatia, au kama atakubali ana hatia. Hiyo tunaiita arraignment..." Blandina akaendelea kueleza.

"Eh, hapo umeniacha... areement..." Felix akasema.

"Ahahaah... ni arraignment..." Namouih akamwambia.

"Okay... ntaicheki kamusini. Kwa hiyo... kama tuseme mtuhumiwa akikubali ana hatia kwenye hiyo arraignment... nini kinafanyika?"

"Trial inaahirishwa. Jaji atasema tarehe ambayo mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kusomewa hukumu kutokana na kile kilichopatikana kufikia hapo..." Blandina akasema.

"Hiyo ndiyo mnaita sentence..." Felix akaongea.

"Pigia mstari..." Namouih akasema.

"Na mnapoingia trial ndiyo kwenye majibizano sasa... napendaga sana hiyo, full drama," akasema Felix.

"Yeah, sasa... huyu kijana aliyebaka, anaitwa Japheth, alikuwa amepewa mwanasheria kutoka serikalini amsaidie. Ushahidi tuliokuwa nao sisi una nguvu, lakini kwenye tarehe ya arraignment akatoa plea ya kwamba hana hatia, kwa hiyo tunaenda trial... kwenye majibizano huko. Sasa mwanasheria wake ghafla tu sijui amefanyaje eti sijui kameza kijiko... hataweza kumsimamia, mambo ya dharura, kwa hiyo anapaswa kuchukua mwanasheria mwingine. Anataka mwanasheria ambaye atamtetea ili ashinde maana amekazania kusema hana hatia, lakini kila mtu anajua hiyo haiwezi tokea... kwa hiyo mpaka sasa hivi tunasubiri trial hajampata mwanasheria mwingine," Blandina akaeleza.

"Si ulisema jaji anaweza kumpa wa serikalini?" Felix akauliza.

"Ndiyo hataki sasa huyo kijana. Anafikiri akipewa yeyote tu atashindwa, so anataka atakayemsaidia kushinda," Namouih akasema.

"Heh... kwa Namouih ni kugonga mwamba tu hata akimtoa mwanasheria Marekani," Blandina akaongea.

"Na ndiyo challenge nayotaka, sema haiji," Namouih akasema na kuwafanya wote wacheke kidogo.

"Haya hela yangu..." Blandina akamwambia Felix.

Felix akatoa elfu kumi na kumpatia Blandina, naye Blandina akaanza kufanya kama anajipepea nayo.

"Kinapenda hela hiki," Felix akasema huku akila.

"Ndiyo sehemu ya kazi, hatuangalii urafiki wala undugu," Blandina akamwambia.

Namouih akacheka kidogo.

"Ila Felix nawe acha uzongaji bwana, si useme tu nini kinaendelea kwenu? Au unafikiri sisi ni Radio Free Africa?" Blandina akasema.

"Siyo hivyo. Ila... niseme tu ni mambo ambayo..."

"Felix we' tuambie. Usiwaze kabisa kuhusu taarifa mbaya kusambaa unajua sisi hatunaga porojo," Namouih akasema.

"Mmm?" Felix akafanya mguno huo kwa njia ya kejeli.

Blandina akacheka kidogo.

"Okay. Hayo mambo tuliyokuwa tunafatilia hayajaleta matokeo mazuri... tena ni mabaya sana. Kwa muda mrefu wasichana wadogo kwenye miaka ya kumi na, kumi na, wamekuwa wanapotea na bila kupatikana... na kutokea mwaka jana idadi ilipungua, tofauti na miaka miwili nyuma. Tumefukua na kufukua sana mpaka tukaanza kuwapata baadhi yao... lakini wengi walikuwa wameshaoza..." Felix akaanza kuwaambia.

Jambo hilo likawafanya wanawake hawa wawe makini sana.

"Unamaanisha walikuwa wameshakufa?" Blandina akauliza.

"Ndiyo. Tena kwa muda mrefu. Kila mara tulipowapata kwa kweli tulihuzunika sana, ilikuwa ngumu hata kuziambia familia zao lakini haikuwa na jinsi. Kila mara tulipompata msichana angekuwa ameshakufa. Lakini vifo vyao vimekuwa vikisababishwa na mtu au watu fulani. Kila msichana tunayempata... tunakuta alama ya kukatwa na kisu tumboni..."

"Kukatwa?" Namouih akauliza.

"Kuchanwa yaani... sehemu ya chini ya kitovu kidogo. Kila mmoja wao," Felix akasema.

Namouih na Blandina wakatazamana kimaswali.

"Wengi mliwapatia wapi?" akauliza Blandina.

"Wengi tumewapata wakiwa wamefukiwa sehemu tofauti-tofauti... na haikuwa rahisi kuwatambua mpaka miili yao ilipofanyiwa vipimo vya DNA. Lakini kwa hii miezi michache ya nyuma idadi yao ilipungua, ila tukaanza kuwapata wengine tena. Zamu hii imekuwa ni mmoja mmoja, na hawakuwa wakifukiwa kama kipindi cha nyuma lakini bado waliuawa kwa njia zile zile za kukatwa tumboni kwa kisu huku wakiwa na majeraha mengine mwilini. Njia moja tu. Ni mambo yanayosikitisha sana yaani... na mbaya zaidi ni kwamba...." Felix akaishia hapo na kuangalia chini.

"Watu wenu wanaficha hayo mambo, si ndiyo?" Namouih akauliza.

"Hawataki watu wa-panick kabla ya kujua tatizo ni nini. Aaah... yaani ni kero sana, nimeingia kwenye huu upelelezi tangu mwaka jana na bado hatujajua shida iko wapi. Hakuna viashirio vyovyote vinavyopatikana kwenye miili ya hao wasichana kwa hiyo hatuna lead yoyote ile," akasema Felix.

"Mh, jamani! Naonaga kwenye vipindi tu wanamsema fulani kapotea na nini... kumbe kati yao kuna hao wanaofanyiwa hayo?" Blandina akasema kwa sauti yenye huzuni kiasi.

"Yeah, ndiyo kama hivyo," Felix akajibu.

"Sasa kuficha jambo kama hilo si inamaanisha litaendelea kimya kimya tu bila watu kuwa na tahadhari? Inakuwa ni kama mnamlea muuaji," Namouih akasema.

"Waambie hivyo mabosi sasa," Felix akasema.

"Au ni wenyewe ndiyo wanafanya hayo?" Blandina akauliza.

"Ahahah... ningehakikisha wanaiona kuzimu kabisa. Ila msichana wa mwisho tuliyempata ilikuwa mwezi uliopita. Tulikuta yaani hana ulimi... ah alikuwa mdogo jamani! Yaani wakati mwingine nashindwa kuelewa watu wanaweza vipi kuchukua hatua za namna hiyo, ni unyama mkubwa sana! Lakini hapana. Nitafanya yote niwezayo kuhakikisha huyu mtu anakamatwa. Naombeni msimwambie yeyote kuhusu haya," Felix akasema.

"Usijali Felix, tunaelewa. Lakini unajua ni jambo la kuwaza... mimi nina mdogo wangu wa kike yuko huku anasoma... ni muhimu nimpe tahadhari lakini sitamwambia hayo yote. Eh, yaani umenifanya nimeanza kuwaza sana," Namouih akasema.

"Ndiyo maana sikutaka kusema. Siyo kitu kizuri... basi tu," Felix akaongea kwa hisia.

Marafiki hawa wakaendelea na maongezi yao mengine huku wakimalizia vyakula na vinywaji, kisha baada ya hapo wakaenda kutembea-tembea maeneo ya karibu na hapo, halafu wakarejea tena kule hospitalini ili kuwa pamoja na rafiki yao kwenye muda wa kutembelea wagonjwa ilipofika saa 11. Bado Mwantum na baadhi ya watu wa familia yake walikuwepo huko, na marafiki hao wakakaa kwa muda wote wa matembezi kwa wagonjwa mpaka walipokuja kuachana hatimaye na kutawanyika ili kurudi nyumbani. Felix aliondoka kwa gari lake kwanza, kisha Namouih na Blandina wakaondoka pia baada ya kumtia moyo Mwantum.


★★


Namouih na Blandina wakawa njiani sasa kurejea mjini kwao baada ya kutoka kuwatembelea wagonjwa na rafiki yao. Blandina mpaka sasa alikuwa akijihisi vibaya kwa sababu tofauti na matarajio yake kutokea asubuhi, kijana yule kwa jina la Draxton hakuwa amemtumia ujumbe wowote kwa simu kama alivyoahidi. Kama kawaida ya Namouih alikuwa akimshurutisha rafiki yake aachane na habari za kijana huyo na waangalie mambo mengine muhimu zaidi, kama vile shughuli zinazohusika katika kumaliza kesi ile ya ubakaji kwa ushindi. Blandina hakuwa akiwaza kuhusu hayo kabisa na kuendelea tu kulalamika kwa nini hajatafutwa, hivyo Namouih akaona ampuuzie.

Ikiwa imekwishaingia saa mbili sasa, walikuwa maeneo ambayo barabara ilikuwa katikati ya mapori mapori mengi pembezoni, wakiwa ndiyo wanaelekea kuingia sehemu za mjini kwenye majengo zaidi. Blandina ndiye aliyekuwa akiendesha, kwa kuwa ilikuwa ni gari lake, na kwa sehemu hizo hakukuwa na magari mengi waliyopishana nayo.

"Ikiwa huyu Japheth hatakuwa amepata mtu wa kumtetea naona ni kama wamenipotezea tu muda wangu," Namouih akawa anaongea.

"Kwa nini?" Blandina akauliza.

"Sasa faida gani kupatiwa kesi niishughulikie halafu mpinzani hana mwanasheria wa kumtetea?"

"Ih! Badala ufurahi tu kwamba huyo jamaa atapelekwa jela kwa alichokifanya bila usumbufu we' tena unalalamika... na hela si umeshalipwa?"

"Siyo hivyo, ni kwamba tu haeleweki. Jumanne kesho kutwa tu, siku ya trial. Bado sijataarifiwa kama ameshapata mwanasheria au vipi. Niko najiandaa vizuri kuishinda hii kesi halafu itokee akakosa mtu wa kumtetea, si nitakuwa nimejisumbua kujitayarisha? Kazi bure yaani..."

"Haina shida. Paycheck nene si unaipata?"

"Hata kama, me ningependa sana kupeleka hii kitu trial. Nimemiss," akasema Namouih.

"Ahahahah... unapenda mno kujibizana na watu mahakamani. Ila unajua nafikiri wanasheria wengine wanaogopa," Blandina akasema.

"Waogope nini?"

"Mtu tu akisikia hii ni kesi ya kubaka, halafu wewe ndiyo unamsimamia mtoa mashtaka aaaa... wanageukia mbali... maana unajulikana sana kwa kutowahi kupoteza kesi hata moja," Blandina akamwambia.

Namouih akacheka kidogo. "Well, akiachwa bila wa kumtetea basi atatakiwa kulipa maana ametoa ahadi fake... na bado miaka 30 jela ataila," akasema.

"Nina hamu sana ya kumuonja huyu jamaa, hajui tu," Blandina akasema.

"Aliyebaka?"

"What, no, namaanisha Draxton..."

"Hivi bado unaendelea tu na huo upuuzi? Wote ambao umeshawahi kuwaonja wana ladha gani tofauti na ya huyo mvunja chupa ambaye hata haumjui vizuri?" Namouih akasema.

"We' utajuaje Namouih, maana una kama muongo mzima hujatekenywa," Blandina akamwambia kiutani.

"Unataka nikutukane eti?" Namouih akasema.

Blandina akamwangalia huku akicheka.

Namouih alikuwa anamtazama kwa ukali wa kimasihara pia, pale kona ya jicho lake ilipoona jambo fulani kwa mbele na kumfanya atazame huko upesi. Ilikuwa ni kama mtu au kitu fulani kinapita haraka sana barabarani, kikiwa kinavuka kutoka upande wa kushoto wa barabara kwenda wa kulia, naye Namouih akashtuka sana.

"Blandina!"

Namouih akaita kwa sauti ya juu na kumfanya Blandina ashtuke na kutazama mbele, ambaye kwa sekunde hizo chache alikuwa bado amemwangalia rafiki yake. Akakanyaga breki kwa nguvu sana, na wakati huo taa za gari lake zilikuwa zimemulika vizuri zaidi umbo la kitu hicho kuwafanya wanadada hawa watambue kwamba ilikuwa ni mtu. Lakini tayari gari lilikuwa limemfikia na kumgonga kwa nguvu sana wakati ambao matairi ndiyo yalikuwa yamefika ukomo wa kusimama kwa ghafla.

Gari likasimama kwa upande kiasi katikati ya barabara baada ya Blandina kuwa amezungusha usukani kidogo kutokana na mwili kutenda kwa mshtuko, na marafiki hawa wakaona vizuri jinsi mtu huyo alivyorushwa hewani na kudondokea chini kwa nguvu, na mwili wake ukaviringika mara chache, na kisha kutulia tuli. Namouih akaweka kiganja chake mdomoni huku akiwa ametoa macho kwa mshangao sana, huku Blandina naye akishangaa na pumzi zake kuongezeka kasi.

"Mungu wangu! Nam... Nam... Nam nime...."

Blandina akashindwa hata kuendelea kuongea na kubaki amemwangalia rafiki yake.

"Okay, okay, tulia. Tunaenda kumsaidia haraka, hatuko mbali sana na hospitali, okay? Kila kitu kitakuwa sawa," Namouih akamwambia kumtuliza.

Blandina akawa anatikisa kichwa kujipa matumaini kwamba kweli kila kitu kingekuwa sawa, naye Namouih akamwambia aligeuze gari vizuri kutoka barabarani hapo ili kulisogeza karibu na upande ambao mtu yule aliangukia, kisha washuke kwenda kumtoa mtu huyo hapo chini kumwahisha hospitali. Wazo la kwamba huenda ajali hii ndogo ilisababisha kifo halikuwa mbali na akili za wanawake hawa, lakini ilikuwa rahisi zaidi kujipa moyo kwamba mtu aliyegongwa alikuwa mzima ili kuweza kuiondolea mbali hatia ya kuua; hata kama hawakukusudia.

Wakiwa wameshuka sasa na kuanza kumwelekea mtu yule, ni Namouih ndiye aliyekuwa kwa mbele kidogo kumtangulia mwenzake, kwa kuwa kwa kiasi kikubwa Blandina aliogopa. Mtu huyo alikuwa ameangukia pembezoni zaidi kutokea barabarani, hivyo kwa upande huo mwanga wa taa za gari haukumulika vyema kutokana na Blandina kulisimamisha kwa upande wa milango. Namouih akawasha tochi ya simu yake, akimmulika mtu yule pale chini, na wote wakabaki kushangaa kwa kile walichoona.

Mtu huyo waliyemgonga hakuwa na nguo hata moja mwilini mwake. Ulikuwa tupu kabisa! Ngozi yake ilikuwa nyeupe, weupe kama wa mzungu. Kwa haraka waliweza kutambua kwamba ilikuwa ni mwanaume, ingawa alilalia tumbo lake, huku mkono wake wa kulia ukionekana kuvunjika kutokea kwenye kiwiko na kuzungukia kwa nyuma, yaani ulikuwa umepindia mgongoni. Kichwa chake kilikuwa kimelala kwa uso kugusa ardhi, hivyo hawangeweza kuuona. Ingawa hivyo, nywele za kichwa chake zilionekana vyema, nazo zilikuwa ndefu kiasi na laini, zenye rangi nyeupe; rangi nyeupe pe.

Marafiki hawa ni kama walitulia kidogo wakitathmini mwili wa mtu huyo, na sauti za magari kama mawili matatu yakipita pale barabarani zikasikika, lakini umakini wao wote ulikuwa hapo chini. Mwili wa waliyemgonga ulionekana kuwa imara sana, na kwa sekunde chache Namouih akawa ametambua kwamba sehemu ya juu kwenye mgongo wa mtu huyo kulikuwa na tattoo ya maneno fulani ambayo yalisomeka, "LIVING IN MY HEART YOU ARE, SO YOU AREN'T DEAD."

Blandina akamshika mkono mwenzake na kuuliza wafanye nini, maana hali aliyokuwa nayo mtu huyo hapo chini ilitatiza kiasi. Akasema ikiwa wangeita msaada, basi hata kama jamaa bado alikuwa hai angekufa kwa sababu ya muda mrefu kupita, na yeye alikuwa anahisi asingeweza kuwa na ujasiri hata wa kumshika tu. Namouih akaendelea kummulika akijishauri cha kufanya, lakini ghafla mkono ule uliokuwa umekunjikia kwa nyuma wa mtu huyo ukajinyoosha kwa kasi na kushika chini!

Blandina akashtuka sana na hata kupiga kelele kidogo, naye Namouih akaingiwa na hofu pia, kisha wote wakalifata gari lao, Blandina akiwa wa kwanza kuingia ndani. Kabla Namouih hajaingia pia, akaangalia sehemu ile, naye akashangaa kumwona mtu huyo akinyanyuka mwenyewe na kusimama, akiwa amempa mgongo. Uajabu wa hali hii ulifanya asahau hata kufungua mlango wa gari na kubaki amepigwa na butwaa, huku Blandina akiwa anamwangalia jamaa huyo kwa hofu kutokea ndani ya gari lake pia.

Huyo alikuwa ni mtu, au kiumbe wa aina gani? Alisimama hivyo kwa sekunde chache, kisha akaonekana akianza kugeuka nyuma.

"Nam, Nam, Nam, Nam, Nam, ingia, harakisha!"

Blandina akaongea hivyo kwa hofu huku akiliwasha gari lake, na hakukumbuka hata ikiwa alilizima kabisa. Namouih akaingia upesi pia kwenye gari, huku akitazama upande ambao mtu yule alikuwepo. Lakini akashangaa kutomwona sehemu ile tena, ikiwa ni kama alitoweka ghafla kabisa, na ni wakati huu ndipo Blandina akawa amekanyaga mafuta na kuliondoa gari lake hapo upesi sana.


★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 787 604 893

email: eltontonny72@gmail.com
IMG_20230108_235349_632.JPG
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA PILI

★★★★★★★★★★★★★★


Blandina aliingia barabarani na kukanyaga mafuta zaidi, akiwa kama yuko kwenye mashindano vile. Namouih alikuwa ameweka kiganja chake kifuani huku akitazama mbele kama vile amezubaa. Blandina alikuwa akitazama kioo cha juu ndani ya gari na cha pembeni nje ya mlango mara kwa mara, ili tu kuhakikisha kwamba walikuwa mbali na kitu walichotoka kuona muda mfupi nyuma.

Waliangaliana mara chache kwa nyuso zilizoonyesha utata sana, lakini hawakusemeshana chochote mpaka wanafika sehemu za mjini zenye shughuli nyingi zaidi. Blandina akapeleka gari sehemu ya kujaza mafuta, kisha mhudumu akafika karibu na mlango na yeye Blandina kumpatia elfu hamsini ili amwekee lita za mafuta ya bei hiyo. Namouih alikuwa ameegamiza kichwa chake kwenye mkono usawa wa kioo cha gari, naye Blandina akamwangalia usoni.

"Nani atatuamini tukimwambia?" Blandina akauliza kwa sauti ya chini.

Namouih akatikisa tu kichwa kwa njia ya kufadhaika.

"Unajua till a few moments ago nilidhani nimeua mtu, lakini... nilichoona leo... haki ya Mungu!" Blandina akaongea na kuinamisha kichwa chake kwenye usukani.

Namouih alikuwa akiyatafakari maneno yale kwenye tattoo aliyoiona mwilini mwa mtu yule asiyeeleweka kabisa. "LIVING IN MY HEART YOU ARE, SO YOU AREN'T DEAD," ilimaanisha "NDANI YA MOYO WANGU UNAISHI, KWA HIYO HAUJAFA." Akili yake yenye udadisi ilikuwa ikimwambia hicho alichokisoma kilikuwa na maana fulani kubwa, na jinsi mtu huyo alivyokuwa wa ajabu kukamfanya atamani kama ingewezekana, apate kujua kumhusu. Lakini hicho kilikuwa ni kitu hatari sana, na alilitambua hilo.

Mhudumu wa kituo hicho cha mafuta akasogea sehemu ya mlango na kumwambia Blandina kwamba angeweza kuondoka sasa, lakini pia akamwambia kuhusu jinsi sehemu ya mbele ya gari lake ilivyokuwa imekunjika kiasi, akionelea kwamba alikuwa amegonga kitu fulani. Blandina na Namouih wakatazamana kiufupi kama kujikumbusha sababu ya jambo hilo, kisha Blandina akamshukuru tu mhudumu na kuliondoa gari hapo.

★★

Hatimaye Blandina akawa amewafikisha nyumbani kwa Namouih. Walipokelewa vyema na msaidizi wake wa kazi aliyeitwa Esma, ambaye aliichukua mizigo waliyoileta na kuipeleka ndani mpaka jikoni. Nyumba ya Namouih ilikuwa kubwa na pana, yenye ghorofa lenye vyumba kadhaa, na ilipangiliwa vizuri sana kwa kuwa na vitu vingi vya gharama na samani zenye thamani. Alikuwa akifuga paka pia, mwenye manyoya meupe, na aliyemwita kwa jina Angelo. Angelo alifurahia sana kumwona mfugaji wake baada ya kuwa wamefika ndani, na kwa muda fulani Blandina akawa anacheza naye kwa kuwa yeye pia alimzoea.

Wakati Esma alipokuwa akiandaa mambo ya msosi kwa ajili yao, marafiki hawa walitumia muda mfupi kuzungumzia tukio lile ambalo ingekuwa ngumu sana kulisahau kwa siku hii. Kutokana na wao kuwa wanasheria, walikuwa wakiangalia jinsi hali zile zilivyojitengeneza mpaka ikawa bonge moja la onyesho. Blandina alikuwa akisema yaani ikiwa waandishi wa habari wangepata kuchukua tukio lile, basi ingekuwa taarifa moja kubwa sana ambayo ingezagaa nchi nzima kama ugonjwa wa malaria au popo bawa.

Angalau waliingiza na utani kiasi kwenye mazungumzo yao katika suala hilo, lakini pointi muhimu ilikuwa ni usalama wa watu wengine maeneo ambayo kiumbe yule angekuwa. Ikiwa mtu kama huyo angeendelea kuwa hadharani, na kama hakuwa mtu mzuri, basi ingekuwa hatari kwa wengi. Ila ni nani angewaamini hata kama wangejaribu kusema walichokiona bila kuwa na uthibitisho? Kwa hakika wangeweza kumwonyesha yeyote mkunjo mbele ya gari la Blandina, lakini hata hiyo haingethibitisha kwamba aligonga "mtu," halafu "mtu" huyo akanyanyuka tu kama kujipangusa vumbi na kuondoka. Kwa hiyo ikaonekana kuwa mwisho wa siku wangetakiwa tu kuigiza kana kwamba jambo lile halikuwahi kamwe kutokea, naye Blandina akajiahidi kuwa mwangalifu zaidi katika uendeshaji wa gari.

Esma alimaliza maandalizi ya msosi, kisha wote wakapata chakula kwa pamoja. Walifurahia kweli mlo huu, na baada ya kumaliza, marafiki hawa wakaingia kwenye ofisi ya Namouih ya hapo nyumbani kwake kupitia mambo machache pamoja huku wakifanya maongezi, kisha ukafika muda ambao Blandina alihitaji kuelekea kwake hatimaye. Bado alikuwa amekwazika kwa sababu kijana yule aliyemwahidi kumtafuta asubuhi ya leo hakufanya hivyo, naye Namouih akaona amtie moyo kwa kusema angepata tu mkali mwingine wa kutuliza mahitaji yake. Akamsindikiza mpaka kwenye gari lake na kumsihi awe makini sana barabarani, kisha wakakumbatiana kwa upendo na Blandina kuondoka.

Hii ikiwa ni mida ya saa tano ya saa sita usiku sasa, Namouih akaamua kwenda tu chumbani kwake ili hatimaye ajipumzishe. Alipanda kitandani, akimwacha Angelo amepanda kwenye kagodoro kake pia hapo kwa chini. Akajilaza huku akiperuzi mitandao ya kijamii kuangalia mambo ya hapa na pale, na ndipo wazo lile likamwingia. Ile tattoo. Mgongoni kwa jamaa. Waliyemgonga kwa gari. Alikuwa anawaza kwamba maneno yale yalikuwa na maana fulani, kama fumbo, naye akajaribu kutafuta maana zozote zile kwenye Google zinazohusiana na maneno hayo.

Alipata misemo na maana tofauti-tofauti, lakini hakukuwa na chochote chenye kuendana na hali aliyojionea leo kilichomridhisha. Msemo wa karibu zaidi ulioendana na maneno yale ni kutoka kwa Thomas Campbell, lakini hata na hapo hakuona kama kuna ulingano wa kutosha kuleta maana fulani iliyofichika. Alikuwa karibu kuiweka simu yake pembeni baada ya kumaliza hayo ili aanze kuutafuta usingizi, pale ilipoanza kuita. Akaangalia jina la mpigaji kwa ufupi, kisha akapokea hatimaye.

"Hallo..." akasema Namouih.

"Hey sweety... how are you?" ikasikika sauti upande wa pili.

Alikuwa ni mume wake, aliyekwenda kwa jina la Efraim Donald.

"Am good. Za huko?" akajibu Namouih.

"Serene. Lakini nakukosa sana mpenzi..."

"Mimi pia..."

"Usijali my dear, tutakuwa wote soon..."

"Mikutano haijaisha bado?"

"Ndiyo tumemaliza, nilikuwa nimeboeka sana. Niliposema soon nilimaanisha tomorrow soon," Efraim akamwambia.

"Oh! Unamaanisha kesho ndiyo unakuja?"

"Yep!"

"Ahah... okay. Nafurahi sana. Natamani kesho ifike ndani ya dakika mbili yaani, uwepo wako huku pamoja nami ni wa muhimu mno Efraim..."

"Wewe pia. Yaani vitanda vyote navyolalia vina baridi tupu kwa sababu joto lako ndiyo linakosekana..."

"Mhmhm... bado hujaachana na mashairi eeh?"

"Kwako hayazimi... nakupenda mke wangu..."

"Nakupenda pia husband... niko nakusubiri..."

"Asante sana. Uwe na usiku mwema eeh?"

"Kwako pia..."

Namouih akamalizia maongezi hayo mafupi, na kisha simu ikakatwa. Akaiweka simu yake kifuani na kutulia kidogo, akitafakari mambo kadhaa kuhusu ndoa yake hii iliyokuwa imemaliza mwaka mmoja tu sasa. Kuna vitu vingi vilivyokuwa vikiendelea tokea alipoolewa na Efraim Donald, na hakuhisi kama alitakiwa kuwa na sababu yoyote ya kutoridhika na maisha aliyokuwa amefanikiwa kuyapata akiwa naye, lakini bado kuna jambo fulani lililomfanya ahisi kuvunjika moyo kila alipomfikiria mume wake.

Akaona isiwe kitu cha kumpa msongo mwingine wa mawazo kwa wakati huu, hivyo akaiweka simu yake pembeni, kisha akaufunika mwili wake kwa shuka na kuanza kuutafuta usingizi.


★★★


Alikuja kuamka na kukuta kuna giza, ikionekana bado ni katikati ya usiku, naye akaamua kuchukua simu yake ili kutazama saa na kukuta ni saa kumi usiku. Alihisi kiu kiasi cha kumtaka atoke na kwenda kule chini ili kupata kikombe kimoja cha maji, pale alipoanza kusikia sauti za vishindo, bila kutambua vilitokea wapi. Zilisikika kama hatua za mtu anayetembea. Akajaribu kuiwasha taa ndogo iliyokuwa pembeni na kitanda, lakini ikawa haiwaki. Ajabu.

Akawasha tochi ya simu yake na kuanza kuielekeza huku na huku, akifikiria kunyanyuka kwenda kuwasha taa ukutani, na mwanga wa tochi hiyo ukatulia kwenye muundo fulani kama mtu aliyeinama kwenye kona ya chumba hicho. Akapiga kelele kidogo kwa hofu na kuidondosha simu yake chini, na hiyo ikasababisha izimike baada ya kudondoka vibaya. Akaanza kujitahidi kuiokota ili kuiwasha upya, lakini ni hapa ndiyo akakumbuka kwamba kwenye kona ile kulikuwa na stendi ya kutundikia makoti, na bila shaka alichokiona hapo ilikuwa ni koti refu jeusi lililotundikwa.

Akashusha pumzi kwa kupata utulivu kiasi. Tochi ya simu yake ilikuwa imezimika ndiyo, lakini akatambua kuwa chumba hiki kilikuwa na mwangaza fulani hafifu kutokea nje. Haukuwa ule mwanga wa taa za nje, ilikuwa ni kama mwanga wa mapambazuko. Akajiuliza ikiwa tayari asubuhi ilikuwa imefika, lakini akakumbuka aliangalia simu yake na kuona kweli ni saa kumi usiku. Sasa ni nini kilichokuwa kikifanya chumba kiangazwe?

Akatoka kitandani vizuri zaidi na kujaribu kupapasa chini ili aichukue simu yake, lakini hangeweza kuiona, na akashindwa kuipata. Akatoka alipokuwa na kuanza kutembea kuelekea sehemu ya ukuta yenye soketi za kuwashia taa, lakini alipowasha, hazikuwaka. Akafikiri kuwa huenda umeme ulikata, ingawa bado wazo la taa za nje kuwaka lilikuwa akilini lakini ikawa kama vile halijalishi sana, hivyo akaamua kuelekea nje ya chumba kwa uzoefu tu wa kuijua nyumba yake mpaka alipofika kwenye korido lililoelekea kwenye ngazi ili ashuke kule chini.

Mwangaza ule ni kama ulizidi kuijaza sehemu hiyo, na ni hapa ndipo akajiuliza swali hili: ikiwa alichoona kwenye kona muda ule kilikuwa koti, basi ni nini kilichokuwa kinatoa sauti zile za vishindo baada ya yeye kuamka? Akaendelea kupiga hatua chache mbele, lakini akahisi kitu fulani. Akasimama. Akageuka taratibu na kutazama nyuma yake. Aliweza kuona kitu chanye muundo wa mtu fulani, kama kivuli, lakini kikiwa kimesimama, na kilikuwa kimevaa moja ya makoti ya mume wake aliyotumia kwa ajili ya kuvaa kazini. Hakuweza kuuona vizuri uso wa kitu hicho kilichoonekana kama kivuli kilichosimama, lakini alitambua kwamba kilikuwa kinatoa tabasamu.

Mapigo ya moyo wake yalidunda kwa nguvu sana kwa hofu kubwa iliyomwingia, kana kwamba moyo wake ulitaka kuruka kutoka kifuani kwake. Akaanza kukimbia kama kichaa, akigeuka nyuma ovyo ovyo mpaka alipofikia sehemu ya mwanzo ya kushuka kwa ngazi, naye akaanza kuzishuka upesi sana. Ilikuwa kwa tukio zuri kwamba hakuanguka kwa kushuka haraka-haraka, kwa sababu ingawa mwangaza ule ulimwonyesha baadhi ya vitu, bado ilikuwa hatari kushuka ngazi jinsi alivyozishuka.

Akafika chini na kuanza kuelekea upande wenye mlango wa kutokea, lakini hakuelewa kwa nini alikoelekea palibadilika na kumfanya aufikie ukuta wa eneo hilo la chini. Akajigonga hapo kidogo na kugeuka nyuma. Ilikuwa ni kama vitu vyote viliondolewa sehemu hiyo, lakini tena kama vile bado vilikuwepo. Mwangaza uliomzunguka ukaanza kuwa kama moshi mzito, naye akafikiria kukimbia tena, lakini hofu yake ikafanya miguu iwe kama imenasa hapo hapo alipokuwa, kwa hiyo akashindwa kutoka.

Akatazama huku na huku asijue la kufanya, na ni hapa ndiyo akahisi akishikwa kwa mikono miwili mabegani kutokea nyuma. Hakugeuka haraka, kwa sababu mtetemo uliopita mwilini mwake ulimfanya ahisi ni kama amepigwa shoti kali mwili mzima. Alipokuwa amesimama, nyuma yake kulikuwa na ukuta. Mikono iliyomshika ilitoka wapi? Akajitahidi kujitoa hapo na hatimaye kugeuza mwili wake, na ndipo akaona kinywa chenye meno mengi makali na marefu kikifunguka na....

"Aaaaaaaah!"

Alipiga kelele kwa sauti ya juu sana na kujinyanyua kuketi. Alikuwa anapumua kwa presha sana, huku mwili wake ukitoa jasho. Alipojitazama, akatambua kwamba alikuwa kitandani, upande ule ule aliokuwa amelala na kuamka usiku mpaka kisa hicho kilichoonekana kuwa ndoto kumpata. Hapo hapo msaidizi wake wa kazi akaingia bila hodi, akiwa anaharakisha sana na kumfikia karibu.

"Dada... vipi? Kuna shida gani?" Esma akamuuliza.

Namouih akamwangalia usoni kwa umakini, asijue la kumwambia hata kidogo.

"Ulikuwa unaota ndoto mbaya?" Esma akamuuliza kwa kujali.

Namouih alipoangalia kwenye kona ile yenye stendi ya kutundikia nguo, akaona kwamba koti la mume wake lilikuwa hapo bado. Akatazama huku na huko kwenye chumba chake, na kila kitu kilikuwa kwenye mpangilio wake mzuri.

"Dada?" Esma akamwita tena.

Namouih akamwangalia na kusema, "Aam... ndiyo... ilikuwa ndoto mbaya."

"Oh pole. Pole sana. Nimeshtuka yaani umesikika hadi chini..."

"Nimepiga kelele kwa nguvu sana?"

"Sana, yaani mpaka nikaogopa..."

"Okay, usijali niko sawa. Ni saa ngapi?"

"Nafikiri saa mbili."

"Okay. Angelo ume..."

"Eh ndiyo nimeshampa maziwa. Chai tayari... nimekuwekea mezani."

"Asante..."

Msaidizi wake akatoka na kumwacha akiwa ameketi tu bado kitandani. Kitu kilichokuwa kimetokea muda mfupi nyuma hakikuonekana kama ndoto, kilikuwa halisi kabisa kwake. Akajiuliza mambo mengi sana kuhusu "ndoto" hiyo, lakini hakupata majibu. Akaamua tu kuacha kuitafakari na kujiondoa kitandani ili kwenda kuusafisha mwili wake. Hakukuwa na shida tena baada ya yeye kumaliza kuoga na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kazi, na hata kuifikiria ndoto hiyo hakukumsumbua kama jinsi ilivyomsumbua wakati alipoamka.

Akatia mwili wake vazi refu lenye kubana, kama gauni, lililokuwa na rangi nyeusi na nyeupe kulizunguka, likiwa la mikono mirefu mpaka kwenye viganja na kuacha uwazi katikati ya kifua chake ulioonyesha mstari wa kati wa matiti yake kwa mbali. Nywele zake alizibana vizuri nyuma ya kichwa, na usoni alipendeza sana kwa kupaka lipstick yenye rangi ya maroon-nyeusi mdomoni. Viatu vyeupe vya kuchuchumia alivyovaa viliongezea zaidi urefu wake, na baada ya kumaliza kupata kiamsha kinywa akamwachia Esma maagizo machache, kisha akaondoka hatimaye.

★★

Baada ya kufika ofisini, Namouih alianza kushughulika na mambo kadha wa kadha ya kikazi, na ndipo Blandina akaingia hapo na kuanza kumsemesha kuhusiana na ile kesi ambayo wangeishughulikia kesho, akimwambia pia kwamba alilipeleka gari lake kufanyiwa matengenezo asubuhi hiyo. Ofisi ya Namouih ilikuwa pana na yenye mwonekano wa gharama sana, ikizungukwa na vitu vingi na samani za vioo; yaani meza yake pana, viti vya humo na madirisha mapana yalikuwa ya vioo vizito. Pembeni ilikuwepo sehemu yenye masofa mawili na meza ndogo ya kioo pia.

Lakini kwa muda wote ambao Blandina aliongea toka ameingia ndani hapo, Namouih hakusema mambo mengi, na alionekana kuwa makini kupita kawaida, kitu kilichofanya Blandina ahisi rafiki yake alikuwa na tatizo.

"Vipi wewe?" Blandina akauliza.

"Bee... vipi nini?" Namouih akauliza pia.

"Nilikuwa nakwambia kuhusu Mwantum. Biashara yake haimlipi sana tokea mwezi juzi mpaka leo, na nahofia anaweza akakosa njia za kujikwamua zaidi maana sa'hivi mambo mengi yatamwangalia. Tunamsaidiaje?" Blandina akamwambia.

"Jamani Mwantum si alisema jana kila kitu kiko sawa? Hayo ya kumsaidia yanatoka wapi?"

"Siyo lazima mpaka aseme nawe, yule anaweza kufa na tai shingoni kabisa na hajaomba msaada. Ila nimefatilia nikagundua vitu vingi vinampiga vibaya dear, hasemi tu. Namwonea sana huruma," Blandina akasema kwa hisia.

"Haina shida. Kitakachohitajika we' tu unaniambia, sawa?" Namouih akaongea kibaridi sana, bila hata kumtazama rafiki yake.

Blandina akamtathmini kwa sekunde chache, kisha akauliza, "Una tatizo gani Nam?"

Namouih akaacha kubofya keyboard na kumwangalia. "Unamaanisha nini?" akauliza.

"Nimekwambia kitu cha muhimu sana lakini unaonyesha ni kama haujali vile. Umekuwaje?"

Namouih akabaki kumtazama tu.

"Bado ajali ya jana inakusumbua akili?" Blandina akauliza.

"Hapana."

"Sasa shida ni nini?"

Namouih akaitazama tena kompyuta yake, kisha akasema, "Efraim anakuja leo."

Blandina akatabasamu huku akitikisa kichwa chake na kumtazama rafiki yake kiutundu. "Oooh... kumbe kitunguu maji anarudi leo?" akauliza kiutani.

Namouih akatikisa kichwa kimasikitiko kiasi.

"Ahahahah... kwa hiyo, ndiyo uko tense kihivyo kwa sababu mumeo anarudi?" Blandina akauliza.

"Nimefurahi. Nimefurahi kwamba anarudi... hii ni kawaida every time, atarudi, mambo yatakuwa safi..."

"Kweli? Sasa mbona uko hivyo?"

Namouih akakaa kimya tu.

"Najua ni maisha yako binafsi lakini lazima niwe advocate wako kwa hili. Nam, itabidi uongee naye. A woman has needs. Hai-make sense hata kidogo, yaani, mwaka mzima amekuoa halafu...."

"Basi Blandina, tuachane na hayo. Nitakuwa sawa. Nitakuwa sawa," Namouih akamkatisha.

"Utakuwa sawa ya kwamba utatafuta suluhisho, au ndiyo utabaki kimya tu?" Blandina akamuuliza.

Namouih akachukua makablasha fulani na kumpatia, akisema, "Mpelekee Edward ayatie saini."

"Unakwepa swali langu, si ndiyo?" Blandina akamuuliza.

Namouih akamkazia macho kama kumwambia afanye alichomwambia.

"Yes ma'am..." Blandina akasema na kuyachukua, kisha akatoka ofisini hapo.

Baada ya Blandina kuondoka, Namouih akampigia simu yule msichana ambaye ndiyo alikuwa anamtetea kwenye kesi hii ya ubakaji, aliyeitwa Agnes, akimuuliza ikiwa alikuwa tayari kwa kesho, na kwa jinsi mambo yalivyokuwa, ilionekana kwamba kusingekuwa na mengi mno ya kufanya kwa sababu wangekuja tu kusikiliza hukumu ya yule jamaa endapo kama kufikia kesho angekuwa bado hajapata mwanasheria wa kujaribu kutetea upande wake. Agnes akamwambia kwamba hakusahau hilo, na kesho angefika mahakamani kwa muda uliopangwa. Akamuuliza Namouih ikiwa huyo Japheth angefungwa na kulipa faini kesho, naye Namouih akamwambia hayo yalikuwa mambo ya uhakika, kilichokuwepo ni kusubiri kesho ifike.

Alipomaliza hilo, akakaa kwa utulivu kwanza akifikiria yale ambayo Blandina alikuwa ametoka kusema muda mfupi nyuma. Maneno yake yalikuwa ya ukweli, na kuna sababu iliyofanya yawe kweli. Kuna kitu fulani ambacho kilikuwa kikisumbua akili ya Namouih toka Efraim Donald alipomuoa, na kwa kipindi kirefu alikuwa amejaribu kujifanya kwamba angeweza kupuuzia na kuendelea na mambo mengine tu, ila kwa wakati huu alihisi kuchoka. Sasa leo kwa kuwa Efraim angerudi, Namouih akawa amekusudia "kutafuta suluhisho," kama vile Blandina alivyopendekeza.

★★

Baada ya muda fulani, Namouih akajiunga na mkuu wa kampuni hiyo, yaani Mr. Edward Thomas, kwenye mlo wa mchana, wakiwa pamoja na watu wengine maalumu kutoka kampuni za mikoa tofauti kuzungumzia masuala ya kikazi yaliyohusisha mambo mengi. Namouih alikuwa hapo kama kichwa kikuu cha masuala ya sheria kutokea upande wao, nao wakafanikiwa kufikia makubaliano mazuri katika kuendeleza misingi imara ya kimaendeleo na kisheria kwenye kampuni zao na watu waliotaka kuwasaidia. Blandina yeye alikuwa amepewa mgawo wa kusaidizana na mwanasheria mwingine wa kampuni yao kusuluhisha tatizo ambalo lilikuwa mzozo mkubwa baina ya pande mbili zilizodai kupewa haki ya umiliki wa mali; pande moja ikidai kupewa mali zote, na nyingine ikipinga hilo kwa kutaka igawanyishwe kwa usawa. Walikuwa ni wanandoa waliotalikiana kipindi hiki hiki, hivyo kulikuwa na mzozo mkali baina yao.

Kwa hiyo marafiki hawa wakawa bize kwa mambo mengi muhimu ya hapa na pale mpaka walipokuja kukutana mida ya jioni, nao wakaamua kwenda sehemu fulani kama hoteli na bar waliyopendelea kwenda mara nyingi kupata kinywaji kimoja au viwili ili kujiliwaza kidogo. Kama kawaida ya Blandina, alikuwa akitazama sehemu hiyo kuona ikiwa angepata mwanaume ambaye angefaa kutoka naye, lakini hakuna hata mmoja aliyeona anafaa.

"Ridiculous... lame... too short... too sweaty..." Blandina akawa anawabagua wanaume hao kwa kuwahukumu namna hiyo.

"Ahahahah... unaiga maneno ya kwenye George of the jungle eeh?" Namouih akasema.

"Aaih... Draxton wangu amekwenda wapi jamani? Nimejaribu hata kuwatafuta ma-Draxton wote FB lakini sura yake sijaipata. Bora tu kama mimi ndiyo ningechukua namba yake jana, ona anavyonitesa..."

"Usihofu sana Blandina. Atakuja tu. Nina uhakika atatokea maana Mungu aliwakutanisha, kwa hiyo usipoteze matumaini. Amini tu mtaonana tena," Namouih akamwambia.

"Kweli eti?" Blandina akauliza.

"Hapana," Namouih akasema.

Blandina akasonya na kunywa kileo chake.

Namouih akatabasamu na kuuliza, "Vipi kesi yenu?"

"Aaagh, yaani kuna watu wanachosha! Mgogoro wenyewe wa mali utafikiri ni Bangalore kumbe nyumba ya mabati sita tu!"

"Hebu acha masihara bwana. Niambie umefanya nini kusuluhisha..."

"Hakukuwa na tabu. Tumewafanya wakakubaliana kugawana pasu maana huyu wa kwetu alitaka share yake aitumie kujiendeleza na masomo..."

"Na huyu mwingine si ni mume wake?"

"Alikuwa. Alikuwa mume wake. Talaka ndiyo inamwasha huko chini, alikuwa mgumu vibaya mno. But you know me, hakuna chai ngumu mbele ya mkate wangu," Blandina akajisifia.

Simu ya Namouih ikaanza kuita alipokuwa akitabasamu kidogo kutokana na maneno ya rafiki yake, naye akapokea na kuiweka sikioni. Blandina akamuuliza kwa ishara ya mdomo "ni Donald?" naye Namouih akatikisa kichwa kukanusha. Akaongea na mtu huyu wa upande wa pili, akionyesha umakini kiasi, kisha baada ya hapo akaishusha simu kutoka sikioni.

"Well, angalau kesho haitaboa sana," Namouih akasema.

"Kwa nini? Kuzurura na Edward leo kumekuboa sana?" Blandina akauliza.

"We' acha tu, alikuwa amening'ang'ania kweli..."

"Ahahahah... nani huyo?" Blandina akauliza na kunywa kinywaji chake.

"Mtu fulani sijui nani, alikuwa ananifahamisha kwamba huyo Japheth amepata mwanasheria atakayemsimamia kesho... so tunaingia trial," Namouih akajibu.

"Wacha! Kwa hiyo unapiga prosecution ya nguvu kesho eeh?"

"Ndiyo maana yake. Uzuri ni kwamba ushahidi tunao, mashahidi watakuwepo, kwa hiyo..."

"Ulichokuwa unalilia umekipata..."

"Yeah. Haijalishi sana, maana huyo Japheth ni lazima nihakikishe anafundishwa somo kwa alichomfanyia Agnes. Kwa hiyo nafurahi kwamba amepata mtu wa kujaribu kuutetea upuuzi wake ili niwakomeshe wote," Namouih akasema.

"Ahahahah... atakuwa anafanya kazi yake tu bwana, lakini inaonekana jamaa hajasoma kujua anapingana na wewe..."

"Hamna kikubwa hapo. Ni kesho kuingia mahakamani, mimi kushinda, Agnes apate haki anayostahili, na mbakaji wake afungwe hata milele. Mwanasheria anayemtetea mpumbavu ili tu kupata pesa sikuzote namwona kama mpumbavu, ingawa hatutakiwi kujaji hivyo," Namouih akaongea.

"Hakukuwa na namna maana unajua majaji wasingekubali Japheth achukuliwe hatua bila kupata mwanasheria. Ilikuwa kama wote wamemkimbia," akasema Blandina.

"Yaani!" Namouih akasema hivyo na wote kucheka.

"Donald anaingia home saa ngapi?" Blandina akauliza.

"Amesema atakuwa ameshafika kwenye saa mbili. Tena nataka niwahi kurudi nyumbani ili anikute kabisa," Namouih akasema.

"Eeeh... akukute kabisa! Utakuwa umekaa style gani kwenye sofa?" Blandina akauliza kiutani.

Namouih akacheka kidogo.

"Ile ya spoon? Au ile ya lamba ubweche? Ama panua memory card 4GB?"

"Ahahahah... hebu acha mambo yako bwana. Nataka tu kumwandalia bonge la msosi. Nime-miss kula pamoja naye," Namouih akasema, huku sura yake ikionyesha hisia sana.

"Leo hakikisha kinaeleweka. Akikataa niite kukusaidia tumuue pamoja, umenielewa?" Blandina akamwambia.

Namouih akatabasamu tu, naye Blandina akanyanyua chupa yake kumwelekea, kisha Namouih akachukua yake pia na kuigongesha hapo, nao wakaendelea kushusha vinywaji vyao taratibu.

★★

Wawili hawa walikuja kuachana kwenye mida ya saa kumi na mbili jioni, Blandina akielekea kule ambako alipeleka gari lake lirekebishwe, na Namouih akielekea nyumbani. Alikuwa amempigia yule Agnes kwa mara nyingine tena kumjulisha kwamba kesi ya kesho ingekuwa na upinzani, na ingawa aliona hilo halingekuwa na shida, akamtaka awe tayari kujibu maswali kwa uhakika endapo angeulizwa vitu vingi vilivyompata kwenye mkasa wake wenye kusikitisha.

Alifika nyumbani na kuvalia kwa njia ya kawaida, kisha akaanza kusaidizana mapishi na Esma, wakitengeneza vyakula vizuri sana kwa ajili ya ujio wa mume wake. Walipomaliza, wakaandaa meza ya chakula vyema, kisha Namouih akaelekea chumbani tena ili kujiweka sawa hata zaidi. Ilikuwa ni kama vile hawajaonana kwa miezi mingi ingawa zilikuwa ni wiki tatu tu ndiyo hawakuonana. Hakuhitaji kujiremba sana, alijiweka sawa katika maana ya kwamba mume wake angefurahia zaidi kumwona akiwa "fresh," na yeye alipenda sana mara zote ambazo Efraim alimsifia kuwa mzuri sana.

Ilifika saa mbili na dakika kadhaa hatimaye, na nje ya geti ikasikika horn ya gari. Mlinzi wa getini, aliyeitwa Alfani, alikwenda kufungua geti hilo na gari aina ya Range Rover Vogue nyeusi kuingia na kuelekea mpaka sehemu ya maegesho. Kwenye sehemu ya mwingilio wa nyumba yao alisimama Namouih, akiwa anaangalia upande huo wa gari hilo kwa subira, na mlango wa mbele wa dereva ukafunguka, akishuka mwanaume aliyekuwa dereva-baunsa wa mume wake, aliyeitwa Suleiman. Akafungua mlango wa nyuma wa gari hilo, na hapo akatoka Efraim Donald mwenyewe. Alikuwa amevalia shati lenye mtindo fulani kama batiki yenye rangi ya samawati, suruali nyeusi, na viatu vyeusi pia. Machoni alikuwa amevaa miwani nyeusi ya mitindo, na kichwani kofia iliyozungukia pande za kichwa chake (aina ya fedora).

Namouih akatabasamu kwa furaha, naye Efraim Donald akaanza kuelekea pale mke wake aliposimama huku akifuatwa na Suleiman kwa nyuma. Akamfikia karibu na kuitoa miwani yake machoni, naye akamkumbatia mke wake kwa upendo. Walipoachiana, miili yao bado ilikuwa imegandana pamoja, Namouih akimwangalia kwa njia fulani ya kudeka, naye Efraim Donald akambusu kwenye paji la uso. Kisha wakaanza kuongozana kuelekea ndani huku wakishikana viunoni, na wakiongea kwa furaha sana kuhusu mambo mengi ambayo yalitokea kwao ndani ya hizi wiki tatu ambazo hawakuwa pamoja.

Efraim Donald alikuwa mwanaume mwenye miaka 40, mweusi, mrefu kuendana na urefu wa Namouih Ingawa nywele au viatu virefu vingefanya Namouih aonekane mrefu kidogo kumzidi. Alikuwa mtu mstaarabu na mkarimu sana, aliyefanya mambo mengi yaliyompa mafanikio na hivyo kusaidia watu wengine wengi waliomzunguka. Alijulikana zaidi kwa kumiliki kampuni kubwa sana iliyohusiana na biashara za magari; usafirishaji au uingizaji wa magari ndani na nje ya nchi, akishirikiana kwa ukaribu sana na kampuni za nchini Dubai. Alikuwa mtu wa safari mara kwa mara, yaani kila mwezi angetoka na kwenda sehemu au mkoa mwingine kushughulika na mambo ya kikazi, na ndiyo kurudi kwake kungekuwa namna hii baada ya siku au wiki chache. Alipenda kumtendea mke wake kwa njia nzuri sana hasa mara zote ambazo angekuwa naye, na Namouih alikuwa anamwamini sana na kujitahidi kumwonyesha upendo katika njia nyingi.

Baada ya Efraim Donald kuwa amefika sasa kutoka kwenye mikutano yake, Namouih akampakulia chakula, nao wakala pamoja na Suleiman na Esma. Mlinzi alikuwa na kawaida ya kula chakula chake ndani ya nyumba ndogo ya nje ambako ndiyo alitunza vitu vyake na kupumzikia huko. Walifurahia maongezi mpaka muda ambao walimaliza kula na kwenda tena kukaa kwenye masofa ili wapatane zaidi, kisha ukafika muda ambao Efraim Donald alihitaji kwenda juu chumbani kujimwagia maji ili kuutoa uchovu. Kulikuwa na vyumba kadhaa vya wageni, naye Suleiman akaenda zake kujipumzisha pia. Mwanaume huyu alikuwa kama mlinzi wa Efraim Donald, na alimfanyia kazi kwa kipindi kirefu, hivyo alionwa kuwa kama sehemu ya familia hii ndogo.

Efraim Donald alikwenda kujimwagia maji na kuutoa uchovu wa mwili kweli, kisha akarudi sehemu ya chumba na kuishia kusimama sehemu ya mlango wa kuingilia ndani ya bafu lao pana. Alikuwa amevalia taulo kiunoni, na macho yake yalielekea upande ambao kulikuwa na kitanda cha ndoa; kikubwa sana. Hapo alikuwepo Namouih. Jinsi alivyokaa ndiyo jambo ambalo lilimfanya Efraim Donald awe kama amezubaa.

Mwanamke alikuwa amekaa kwa kuegamia mwanzoni mwa kitanda hicho kulipoundwa kuta fulani ya sofa laini (ya kitanda) iliyopendeza sana, akiwa amenyoosha mguu wake mmoja na mwingine kuukanyagisha kitandani karibu na huo aliounyoosha. Mwili wake mweupe sana haukuwa na nguo zozote isipokuwa sidiria nyekundu iliyoficha matiti yake yaliyotuna kuelekea mbele, na chupi ya mikanda laini na nyekundu pia iliyoonekana kubanwa kiasi na sehemu ya kati ya mapaja yake manono. Sura yake nzuri, laini, na nyeupe sana ingefanya hata mapigo ya moyo ya mwanaume yeyote gaidi yasimame kwa jinsi ilivyotamanisha. Alikuwa anamtazama Efraim kwa njia iliyoonyesha wazi kwamba alitaka afatwe hapo kitandani ili ashughulikiwe haswa, naye Efraim Donald akaachia tabasamu dogo na kuanza kukielekea kitanda.

Mwanaume akamfikia karibu na kuketi usawa wa ubavu wake, huku akimtazama kwa njia iliyoonyesha wazi kwamba alimtamani sana. Namouih akapeleka kiganja chake kifuani kwa mume wake, akimwangalia kwa upendo mwingi sana, kisha akaifata midomo yake na kuanza kumbusu kimahaba. Efraim Donald aliipokea busu ya mke wake vizuri, lakini baada ya sekunde chache, akajitoa mdomoni mwake na kumshika pande za mikono yake.

"Tulale mpenzi... sijihisi vizuri sana."

Namouih akamtazama usoni kwa njia fulani ya kawaida tu, lakini Efraim alijua wazi kabisa kwamba jambo alilosema lilimkwaza mke wake. Mwanamke alikuwa amejiandaa vizuri kabisa kumpatia kitu kitamu kuliko hata chakula, lakini yeye akaona kulala ndiyo jambo bora zaidi. Efraim Donald akanyanyuka kutoka hapo na kuifuata kabati kubwa yenye nguo zao nyingi, huku Namouih akimwangalia tu, naye akavaa kaushi na bukta nyepesi, kisha akatoa nguo ya kike ya kulalia (night dress) na kumsogelea tena Namouih, aliyekuwa amekaa vile vile.

"Chukua... vaa. Usingizi ni mzito sana honey... tutatafuta muda mwingine ku...." Efraim akaishia tu hapo.

"Lini?" Namouih akauliza.

Efraim Donald akamwekea tu nguo hiyo mapajani na kugeuka nyuma ili azungukie upande mwingine wa kitanda.

"One year!"

Maneno hayo ya Namouih yakamfanya Efraim asimame tuli huku akiwa amempa mgongo, kwa kuwa yalisemwa kwa njia iliyomwambia kwamba mke wake alitaka kusema mambo mazito.

"Mwaka mmoja Efraim! Mwaka mzima umepita... every time... unakuwa umechoka?" Namouih akauliza.

Efraim Donald akaanza kupiga hatua kuzungukia kitanda mpaka alipofikia upande wake wa kulala, naye Namouih akaikunja miguu yake na kuketi huku anamtazama kwa hisia kali.

"Si naongea na wewe?" Namouih akasema.

Efraim Donald akamtazama kwa ufupi, akiwa amesimama sasa, kisha akasema, "Unajua mambo ni mengi... nikikwambia nachoka ujue nachoka kweli."

"Kuchoka kivipi Efraim? Kunichoka mimi au?"

"Siyo hivyo, usiongee namna hiyo bwana..."

"Unataka niwaze vipi? Efraim umenioa kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini haujawahi kushiriki nami haki yetu ya ndoa! Una shida gani?!" Namouih akauliza kwa hisia.

"Sina shida yoyote Namouih, nimekwambia nimechoka tu..."

"Efraim naomba usicheze na akili yangu. Tafadhali. Kama kuna kitu fulani juu yangu kinachofanya usitake kunigusa ni kheri kuniambia ili nijue... nirekebishe... siyo kunifanyia hivi. Ndoa yetu ina maana gani kama hatutimiziani mahitaji yetu muhimu?"

Efraim Donald akapanda kitandani na kuanza kulifungua shuka ili aufunike mwili wake, lakini Namouih akalichukua kwa nguvu na kulitupa chini!

"Namouih ni nini laki...." Efraim Donald akaishia hapo baada ya kumwangalia Namouih usoni na kukuta anakaribia kuanza kulia. "Namouih..." akamwita kwa upole.

"Niambie Efraim... nataka uniambie kwa nini unanitendea hivi. Sina chochote cha kulalamikia kwa sababu umekuwa mume mzuri kwangu, na kwa kipindi kirefu niliona nikuache tu kwa kudhani labda ulihitaji muda... lakini kwa ajili gani? Kuna kasoro fulani unayoiona kwangu au?"

"Namouih tafadhali... nina uchovu wa...."

"Kesho utanipa kisingizio gani? Kichwa kinauma? Unafata utaratibu wa mazoezi? Sukari imepanda? Au kuna sehemu unawahi, na ukirudi tena umechoka?"

Efraim Donald akaangalia pembeni.

"Hhh... mara ya kwanza tumekutana uliniambiaje? 'Namouih... sitaki na sitaki kukuona unaumia.' Kwa nini sasa unaniumiza wakati huu Efraim? Ikiwa hii ni adhabu yangu kwa sababu mwanzoni sikukukubalia...."

"Hapana, siyo hivyo Namouih..."

"....basi nimekuelewa, na ninafikiri muda umepita vya kutosha kulisamehe hilo. Kwa nini basi unifanyie hivi? Mimi ninakuhitaji Efraim... ninahitaji kujua kwamba unanihitaji pia," Namouih akaongea kwa hisia sana.

Efraim Donald akajaribu kumvuta ili akilaze kichwa cha mke wake kwenye kifua chake kumpa bembelezo, lakini Namouih akaweka mgomo kabisa na kunyanyuka kutoka hapo, kisha akaenda bafuni na kujifungia.

Hii ndiyo iliyokuwa hali halisi ya ndoa yake. Efraim Donald alikuwa mume mzuri kwa Namouih; alimpenda, alimpa mahitaji yoyote ya kifedha na kihisia na hata vitu ambavyo Namouih hakutaka kupewa, na mambo mengi na makubwa sana kipindi cha nyuma alikuwa amemtimizia, lakini tangu alipomuoa, kulikuwa na jambo moja ambalo hakuwahi kumpa, yaani, haki yake ya ndoa. Mwanamke kama Namouih, hakuwa na papara, na sikuzote aliacha tu mambo yawe namna yalivyo kama hangeelewa vizuri kwa nini yako hivyo.

Lakini huyu alikuwa ni mume wake. Kilikuwa kitu ambacho hakingefikirika kwa yeyote kwamba Efraim hakuwahi kabisa kufanya mapenzi na Namouih, na mwanamke huyu alijitahidi kuacha tu hali hiyo ipite kwa muda fulani lakini sasa na yeye alikuwa anamhitaji sana mume wake. Efraim Donald hakuwahi kumpa mke wake sababu yoyote kwa nini hakushiriki naye mapenzi, na ni kitu kilichomuumiza sana Namouih kwa kumfanya ahisi labda haonwi kama mwanamke anayeweza kumtosheleza mwanaume. Namouih alikuwa amepitia kwenye hali ngumu kabla ya kukutana na Efraim Donald, na ni mwanaume huyu ndiye aliyemsaidia sana, kwa hiyo alitaka amwonyeshe jinsi alivyomthamini sana lakini yeye akawa anakataa kupokea moja kati ya mambo ambayo Namouih alitamani sana kumfanyia.

Akiwa bafuni baada ya jaribio lake muda mfupi nyuma kushindwa kuzaa matunda, Namouih akawa amesimama tu sehemu yenye kioo kipana sana, akijitazama hapo kwa huzuni. Sura nzuri alikuwa nayo. Mwili wenye mvuto alikuwa nao. Akili alikuwa nazo. Na uaminifu kwa mume wake licha ya yeye kutompa haki yake alikuwa nao. Shida ilikuwa wapi?"



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Itakuwa ikiruka hapa siku za Jumamosi na Jumapili. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 787 604 893

e-mail: eltontonny72@gmail.com
IMG_20230108_235349_632.JPG
f
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA TATU

★★★★★★★★★★★★★★


MWAKA MMOJA NA NUSU ULIOPITA


Tunarudi miezi mingi nyuma kupata kujua mambo kadhaa kuhusu maisha ya mwanamke mrembo sana, Namouih. Jina lake halisi ni Namouih Alhaji Masoud, na yeye ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza katika familia iliyobarikiwa kuwa na watoto wanne.

Baba yake aliitwa Masoud Alhaji, mwanaume mwenye ngozi nyeupe na mwenye nguvu aliyefanya kazi migodini kwa muda mrefu. Alikuwa ni mtu wa Pemba, naye alikuwa mstaarabu na mchapakazi sana, aliyejitahidi kuiandalia familia yake mahitaji yao mengi licha ya kufanya kazi ngumu mno zilizomwathiri kwa njia mbaya ndani ya miaka aliyozifanya. Hakuwa mtu mwenye makuu, na sikuzote alimwongoza vizuri Namouih kwa kumwambia asome kwa bidii kwa sababu elimu ingemsaidia aweze kuboresha maisha yake baadaye. Aliipambania sana familia yao, naye alikuwa na umri wa miaka 54.

Mama yake Namouih aliitwa Zakia Masoud, aliyekuwa na miaka 48 wakati huu, naye alikuwa mweupe pia, mwenye sura nzuri na umbo namba nane kama wengi waliitavyo japo kwa njia yenye unene kiasi. Alikuwa ni mtu wa Arusha, naye alipenda sana mambo ya urembo na kujishughulisha na ususi kwenye saluni za wanawake na urembaji wa maharusi. Alikuwa mwongeaji sana, mkali, na ambaye sikuzote alipenda kujitanguliza kwanza kwa mambo mengi ingawa aliipenda familia yake kwa ujumla.

Wadogo zake Namouih walikuwa ni Sasha, Nasri na Nasma. Sasha alikuwa binti mwenye miaka 18, mweupe na mrembo, mrefu kumkaribia Namouih, na mwenye umbo zuri sana la kike. Wakati huu alikuwa anaelekea kumaliza kidato cha nne, naye alikuwa mpole sana na mwenye akili kama tu dada yake kwa kuwa alifanya vizuri sana kwenye masomo. Aliyefuata alikuwa ni Nasri, lakini mvulana huyu alipoteza uhai wake alipokuwa na miaka 6 kwa kuliwa na mnyama hatari wa porini, ingawa mpaka kufikia wakati huu haikueleweka alikuwa mnyama gani. Alikuwa mvulana mjanja sana aliyependa michezo, na kama angekuwa hai bado basi wakati huu angekuwa na miaka 13. Nasma ndiyo alikuwa wa mwisho, binti mdogo mwenye miaka 10, naye alikuwa anaendelea na elimu ya msingi wakati huu. Wote walibarikiwa kwa sura nzuri na weupe, ingawa Sasha hakuwa mweupe sana kama watoto wengine wa familia hii.

Familia yao ilikuwa na mgawanyiko mdogo wa kidini, kwa sababu Masoud alikuwa mwislamu na alipokutana na Zakia kabla ya kuitengeneza familia, mwanamke huyo alikuwa mkristo, na alikwenda kwa jina la Christina. Walipendana, na wakiwa bado vijana wadogo wakaonyeshana upendo wao na kusababisha Christina apate ujauzito wa Namouih wakati akiwa anasoma sekondari bado. Watu wa kiukoo wa Christina walikasirishwa sana na jambo hilo, nao wakamfukuza kutoka nyumbani kwa sababu ya jambo hilo. Wakati huo Masoud alikuwa amepanga chumba kimoja tu, akifanya biashara za hapa na pale, hivyo akampokea Christina na kumwahidi kwamba wangemtunza mtoto wao pamoja.

Kulikuwa na upinzani mkubwa kutoka pande zote za familia zao kwa sababu ya jambo hilo, lakini Masoud alikuwa na msimamo imara, naye akaendelea kupambana haswa ili amtunze mpenzi wake na mwanaye mtarajiwa. Ndiyo baada ya muda fulani kupita, Christina akawa amebadili jina lake na kujiita Zakia, ili kuendana na hali ya uislamu ya Masoud ingawa hakubadili dini kabisa, ndiyo wakafunga ndoa kwa misingi hiyo baada ya Namouih kuwa amezaliwa. Walitengwa na ndugu zao wengi, na hata mara ambazo walipitia magumu kiasi cha kujaribu kuomba msaada kwa ndugu, hawakupata chochote zaidi ya masimango tu, hivyo ilikuwa ni kupambana wao kama wao. Wawili hawa kwa pamoja hawakuwa na baba wala mama, mayatima, kwa hiyo hawangeipata huruma kutoka kwa wanaukoo walioendekeza chuki dhidi yao.

Misukosuko mingi waliipitia pamoja, na kwa miaka yote bado waliendelea kuwa pamoja mpaka kufikia wakati huu, ila sasa kukawa kumezuka tatizo kubwa. Namouih ndiyo alikuwa amemaliza masomo ya chuo kikuu na kupata digrii ya sheria, na ndiyo alikuwa mwanzoni tu kwenye masuala ya kazi akijijengea maisha yake na ili aendelee kuisaidia familia yake pia, pale alipopata taarifa kwamba baba yake ana ugonjwa mbaya sana, na alikuwa amepelekwa hospitali kupatiwa matibabu lakini hakuwa na muda mrefu sana wa kuendelea kuishi endapo kama hangefanyiwa upasuaji maalumu uliokuwa ghali mno.

Ugonjwa wake ulikuwa ni saratani ya mapafu. Ulisababishwa na vumbi kali lenye madini fulani ambayo yalimwathiri kwa kipindi kirefu sana alichokuwa akifanya kazi, na saratani hiyo ilikuwa ndani yake kwa kipindi kirefu bila yeye kujua, na hivyo sasa ilikuwa imefikia hatua mbaya na ndiyo maana ikamzidia ghafla na kudhoofisha mwili wake. Zilikuwa ni habari zenye kushangaza kwa sababu bwana Masoud alionekana sikuzote kuwa na afya nzuri, na ikawa wazi kwa wengine kuwa huenda alijua kabisa kwamba anaumwa lakini akakaa kimya tu na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili aikimu familia yake. Na alikuwa amewafanyia mambo mengi sana.

Namouih alihuzunika mno. Yaani aliacha mambo mengi na kwenda hospitalini ili kuweza kufanya lolote kuokoa uhai wa baba yake. Alitumia pesa zozote alizokuwa nazo, na rafiki yake, Blandina, alikuwa pamoja naye katika hilo pia. Lakini kila jambo alilofanya lilikuwa njia tu ya kusaidia kumwongezea bwana Masoud siku za kuishi, siyo kuliondoa tatizo lake kabisa. Kama angepata pesa ya kutosha, basi mzee wake angefanyiwa upasuaji huo, lakini jinsi siku zilivyozidi kwenda ndiyo ambavyo Masoud angeendelea kudhoofika, ingawa dawa alizopewa zilisaidia kumsukuma kimaisha, na zilikuwa za gharama SANA. Mwanamke alikuwa ametumia njia zote kuhakikisha anakusanya pesa hizo, lakini zilizohitajika zilikuwa nyingi mno, na hasa kwa sababu angehitaji kuendelea kumsaidia baba yake apate dawa, ilimhitaji atoe pesa ambazo alitunza.

Familia yake ilimfahamu Blandina kuwa rafiki wa karibu sana wa Namouih kwa kipindi kirefu, hivyo naye alikuwa huku hospitalini mkoani kwao kuwapa mchango (support) wake wote alioweza. Yeye Blandina alikuwa na ndugu yake mwingine huku hivyo alikaa kwake kwa muda wakati akiendelea kuwa karibu na Namouih. Bwana Masoud angeongea mara kwa mara na binti yake kumwambia kwamba asisumbuke sana kutafuta njia za kuokoa uhai wake kwa sababu angepoteza hela nyingi na mwishowe mzee angekufa tu, lakini hilo ni jambo ambalo Namouih hangesikiliza kamwe. Alimpenda sana baba yake, naye alikuwa amejiahidi kufanya kila kitu alichoweza ili kumwokoa.

Kufikia kipindi hiki, Masoud na Zakia walikuwa na nyumba yao kabisa. Ilikuwa ya kawaida tu yenye vyumba kadhaa, ikipakana na zingine za majirani, na Namouih pia alikuwa anasaidia sana kuwawekea mambo mengi mazuri na ya kisasa ili ipendeze zaidi. Ni kwa jitihada zao na kutokata tamaa ndiyo vitu vilivyowafikisha huku ingawa ndugu zao wengi waliwatupa, na hata kuna baadhi yao walianza kujipendekeza kwa familia hii baada ya kuona vitu fulani vinanyooka kwao lakini Zakia hakutaka kabisa familia yake ijihusishe nao kwa lolote.

Basi, siku fulani ndani ya kipindi hiki ambacho bwana Masoud alikuwa amelazwa, Namouih akawa nyumbani pamoja na mama yake, wakifanya mambo ya hapa na pale kabla ya kujiandaa kwenda hospitalini kumwona mzee, kisha wakaketi kwenye masofa ili kula na kupumzika kidogo. Kule hospitalini alikuwepo Sasha kwa wakati huu. Zakia alikuwa anamwangalia sana Namouih wakati mwanamke huyu alipokuwa anafanya miamala fulani kwa simu yake, na kwa kutambua kwamba mama yake alikuwa anamtazama mno, Namouih akamuuliza shida ni nini, naye Zakia akaangalia tu pembeni kwa njia ya kukwazika.

Namouih akaweka simu chini na kumwangalia vizuri, kisha akasema, "Litakuwa jambo zuri ukiniambia shida ni nini maana unaniamgalia kwa njia inayoonyesha kuna tatizo."

"We' unaonaje? Hakuna matatizo?" Zakia akamuuliza.

"Kwa upande wako sijajua," Namouih akasema.

Zakia akamwangalia kwa ufupi, kisha akauliza, "Hii hali ya baba yako itakuwa na suluhisho, au ndiyo tunasubiri msiba tu?"

"Mama!" Namouih akasema hivyo kwa ukali kiasi.

Zakia akaangalia pembeni.

"Maneno gani hayo?" Namouih akauliza.

"Naongelea hali halisi. Masoud yuko vibaya, gharama ni kubwa, inahitajika jambo la haraka la sivyo...."

"Unapendekeza tufanye nini?" Namouih akamkatisha.

"Nimekutafutia mchumba mwanangu," Zakia akasema.

"Nini?" Namouih akauliza kama vile hajasikia vizuri.

"Ndiyo. Kuna... mwanaume fulani... rafiki yangu, aliniambia kwamba huyo mwanaume kijana anakupenda sana na anataka kukuoa pia," Zakia akamwambia.

"Ahah.... acha masihara basi!" Namouih akashangaa.

"Sikutanii."

"Unataka kuniozesha kwa mtu ambaye simjui?"

"Utakuwa na muda wa kukutana naye, kujuana naye vizuri,..."

"Mama, sina muda wa kuolewa kwa sasa. Mambo ni mengi, vitu vingi vinaniangalia mimi na wewe, unawezaje tu hata kunipangia jambo kama hilo bila me kujua? Tuko India hapa?"

"Hapana nisikilize. Ni kijana mzuri, ni mtaratibu..."

"Naona bado hujanielewa. Hilo suala sitaki kulisikia tena. Mama... napigana kwa ajili ya baba na wadogo zangu halafu unaniambia masuala ya kuolewa? Ndiyo yatasaidia kuleta hilo suluhisho unalotaka?" Namouih akauliza kwa uthabiti.

Mama yake akabaki kumtazama tu. Namouih akatikisa kichwa kwa njia ya kukerwa, kisha akanyanyuka na kuanza kuondoka kutoka hapo.

Zakia akasimama pia na kusema, "Namouih... Namouih nisikilize kwanza... ana pesa..."

Namouih akasimama, kisha akamgeukia mama yake. "Nini?" akamuuliza.

"Ana hela. Ukiolewa naye, kila kitu kitakuwa safi," mama yake akamwambia.

"Unamaanisha nini?"

"Ikiwa utaolewa naye, hautapaswa kuwaza kuhusu wadogo zako, sijui tiba ya baba yako... atakusaidia kwa hayo yote."

Namouih, akiwa ameweka uso ulioonyesha maswali mengi, akamsogelea mama yake karibu zaidi.

"Mama... unataka kuniuza?" akamuuliza kwa hisia.

"Hapana siyo kihivyo... namaanisha... baba yako anahitaji sana msaada, hali yake ni mbaya, na mimi nimefungwa mikono. Mkopo wako wa chuo bado unalipia, Nasma bado yuko shule unamlipia, na kuna huyo mdogo wako mwingine tunayemlipia..."

"Unashindwa nini kumwita kwa jina mama...."

"Nisikilize!" Zakia akamkatisha kwa ukali.

Namouih akaangalia pembeni.

"Hapa ni moja tu, hakuna mbili. Kwa muda mrefu tumemtegemea zaidi baba yako, na mimi biashara zangu haziendi, mambo ni magumu. Ingekubidi ukatishe mwaka wako wa mwisho... yaani... Namouih... wewe ndiyo uliyebaki kuwa tegemeo kuu hapa...."

"Mama... lakini..."

"Hata kama akikuoa, haimaanishi utaacha kufanya mambo unayotaka. Niamini, huyu mwanaume anakupenda, na siyo kwamba nataka tu akuoe kwa ajili ya faida, hapana. Ila kwa sasa ndiyo njia ya haraka itakayo...."

Namouih akawa anatikisa kichwa kukataa na kusema, "Mama... hapana. Naweza kuongea naye ukitaka, ni... nimweleze hali... labda hata anaweza kutusaidia, lakini siyo...."

"Tumia akili wewe binti! Nani sasa hivi atakupa vya bure?!" Zakia akamkatisha kwa ukali.

"Mama!" Namouih akashangaa.

"Kaa ukitambua hili. Ikiwa baba yako atakufa... akifa, Namouih... basi itakuwa ni makosa yako," Zakia akamwambia.

Namouih akabaki kutikisa kichwa kwa njia iliyoonyesha alifadhsishwa sana na njia ya mama yake ya kufikiri. Zakia akaondoka sehemu hiyo akimwacha binti yake anatafakari vitu vingi. Hiki ni kitu ambacho moyo wake ulipinga kabisa kuwa suluhisho la tatizo walilokuwa nalo. Akiwa anahitaji kutuliza akili yake kidogo, akaamua kumpigia rafiki yake kipenzi ili amsaidie kutoa misongo kwa kadiri ambayo ingetosha.

★★

Muda mfupi baadae, mwanadada Namouih akawa ameondoka nyumbani na kwenda upande wa mji huo uliokuwa na harakati nyingi zaidi za hapa na pale. Blandina alikuwa ameshafika sehemu fulani waliyoahidiana kukutana mjini huko, ikiwa ni ya starehe kiasi kwa wengi, ili kupata kinywaji na maongezi pia. Baada ya Namouih kufika, kama kawaida macho ya wengi yalikuwa kwake, lakini yeye alipuuzia watu na kwenda kuketi kwenye meza alipokaa rafiki yake. Alikuwa amevalia baibui lenye rangi nyeusi na hijab iliyoacha sehemu ya uso wake wazi, na Blandina alikuwa amevaa gauni jeupe lenye maua-maua lililoubana mwili wake vyema.

Rafiki yake aliona wazi kwamba Namouih alikuwa na mkazo sana. Akamwitia mhudumu na kumwambia amletee kinywaji fulani kimoja mwanamke huyu alichopendelea, na mhudumu huyo akakileta na kwenda zake. Namouih akaanza kumwelezea Blandina namna mama yake alivyoongea muda fulani siku hiyo, akiona kwamba alikuwa amevuka mipaka yake kama mzazi na kumtaka afanye jambo hilo kwa kumbebesha yeye Namouih hatia kwa hali iliyokuwa imempata baba yake. Ilimtia huzuni sana, kwa sababu alihisi sasa kwamba alikuwa ameshindwa kumsaidia kabisa baba yake.

Blandina akawa anamtia moyo kwa kusema mambo yangekuwa sawa tu, na ndiyo akauliza kuhusu huyo mwanaume ambaye Namouih alitafutiwa na mama yake ili aolewe naye. Namouih akamwambia hata hakujua jambo hilo lilitokea wapi, yaani lilikuja ghafla sana, na ilimkera sana kujua mzazi wake angefikia hatua ya kumshauri afanye kitu kama hicho ambacho hakingekuwa na utofauti na kujiuza ili kupata pesa.

"Kwani me wanaume siwaoni? Ni wangapi wenye pesa waliotaka kuwa nami lakini nikawakataa? Sitaki mwanaume mimi kwenye maisha yangu, niliyopitia yanatosha. Sasa sa'hivi natakiwa tu kuwa na mtu kwa kuwa eti ana pesa, ili amsaidie baba yangu... nisipompenda? Mimi sijabumbwa kwa njia hiyo kabisa aah," Namouih akawa anaongea kwa hisia.

Blandina akatulia kwa ufupi, kisha akauliza, "Kwa hiyo... unamaanisha kwamba ingekuwa bora baba yako akifa kuliko wewe kuolewa ili kumsaidia?"

Namouih akamwangalia kwa macho makali.

"Samahani, namaanisha kwamba... najua yule mzee amewapigania sana kipindi cha nyuma. Kama kuna chance ya kuweza kumtoa kwenye teseko lake Nam... ni bora kuichukua nafasi hiyo haraka..."

"Teseko ndiyo nini? Sijawahi kusikia hilo neno..."

"Namouih..."

"Hivi kweli Blandina, na wewe unakubaliana na wazo la mama? Niende tu, nikutanishwe na mtu, anioe, halafu nimwombe sasa hela, 'baba yangu anaumwa, mlipie matibabu kwa sababu umenioa,' does that make sense?" Namouih akauliza kwa hisia sana, mpaka machozi yakawa yanakaribia kumtoka machoni.

"Ninajua hali mliyo nayo ni ngumu, na sikushauri ufanye kile ambacho moyo wako unakataa. Lakini umeshajaribu mambo mangapi rafiki yangu? Na muda unazidi kwenda. Sitaki kusema vibaya, lakini, mama yako...."

"Ninajua anataka tu niolewe na huyo mwanaume kwa sababu ya pesa, wala siyo kwamba baba ndiyo sababu kuu. Anautumia ugonjwa wake kama kigezo tu..."

"Usimhukumu vibaya namna hiyo, ingawa sipingi hilo. Lakini jaribu tu kuangalia uwezekano wa kupata suluhisho haraka kwa njia hiyo hiyo..."

"Unamaanisha nini?"

"Siyo lazima mpaka akuoe. Unaweza kumkubalia mama yako, akakuunganisha naye, halafu mkishajuana, wewe utampanga huyo mwanaume... yaani... Nam mpaka nashindwa nifanye nini kukusaidia rafiki yangu," akasema Blandina kwa hisia.

"Nimpange? Kwamba nimpe kitu fulani ili nipate pesa, kama hivyo si ndiyo?" Namouih akauliza kiupole.

Blandina akabaki kimya tu na kutazama chini.

Namouih akafumba macho yake kidogo, kisha akaangalia pembeni, akionekana kutafakari.

"Nikuagizie kinywaji kingine?" Blandina akauliza.

Namouih akatikisa kichwa kukanusha, kisha akatoa simu yake na kumpigia mdogo wake, yaani Sasha. Akamwambia kwamba angeelekea huko huko hospitalini muda si mrefu, hivyo ajiandae tu kuondoka na yeye ndiye angefika kukaa na baba yao. Baada ya kumaliza kuongea na Sasha, akamwambia tu Blandina anataka kuondoka, hivyo kama yeye bado alitaka kuendelea kubaki hapo basi ingekuwa sawa. Lakini Blandina akamwambia angeenda pamoja naye huko huko hospitalini, ili aweze kumsalimu baba yake Namouih pia.

Wawili hawa wakaanza kuondoka hapo baada ya kulipia, na giza lilikuwa limekwishaingia. Wakiwa wanaelekea upande ambao wangechukua usafiri, mvua ikaanza kunyesha. Ilianza taratibu tu, na walikuwa wanajitahidi kuharakisha ili kuwahi usafiri kabla haijawa kubwa, lakini ikaongezeka sana na kuwafanya waamue kujikinga usawa wa maduka lli kuepuka kulowana. Watu kadhaa walionekana kujikinga pia hapa na pale, huku wengine wakikimbizana na mvua hiyo, nayo ikazidi kuongezeka na kuwa kubwa zaidi.

"Jamani, mambo gani tena haya!"

Blandina akamsemesha Namouih kwa sauti kubwa ili asikie, naye Namouih akatikisa kichwa huku akijishika pande za mikono yake ili kusitiri baridi ndogo iliyomwingia. Alipotazama upande mwingine wa eneo hilo, aliweza kuona sehemu ya mbali kiasi iliyokuwa na jengo dogo, na hapo kulikuwa na mtu amesimama. Mwonekano wake kwa umbali huo ungemfanya yeyote adhani kwamba alikuwa amejikinga tu kutokana na mvua hiyo, lakini baada ya mwanga wa radi kumulika vyema kufikia upande huo, Namouih akatambua kwamba uangalifu wa mtu huyo ulielekezwa sehemu aliyokuwa amesimama yeye na Blandina. Hakuweza kumwona vizuri kutokana na giza ingawa mianga ya taa za nje ilimulika vyema, lakini Ilikuwa ni kama anawaangalia.

Namouih akampuuzia mtu huyo na kuangalia tu chini, na ni hapa ndiyo Blandina akamwambia ingekuwa bora zaidi wakizima simu zao kwa kuwa alihofia radi zingeweza kusababisha tatizo. Akaitoa yake na kuizima, na ile alipopeleka macho yake upande ule, akakuta mtu yule bado amesimama tu kwa njia ile ile. Yaani, kwa wakati huu, Namouih aliamua kutokwepesha macho yake na kumtazama moja kwa moja, na ilikuwa ni kama anaangalia sanamu kwa sababu mtu huyo hakutikisika hata kidogo. Ni hapa ndipo aliweza kutambua kwamba mwilini mwa mtu huyo kulikuwa na jaketi kubwa lililofunika mpaka kichwa chake, uso wake ukifichwa kama vile wote umeingia ndani ya kifuniko cha kichwani cha jaketi hilo.

Jambo hili likamfanya akerwe kiasi na kutazama pembeni tu, lakini hangejizuia kupeleka macho yake upande huo mara kwa mara, na alichokiona mwanzo kilibaki kuwa namna hiyo hiyo tu. Ilianza kumfanya ajiulize ni mtu wa aina gani angesimama namna hiyo, bila hata kujigeuza kidogo huku na huko. Mvua iliendelea kunyesha kwa nguvu, zikiwa zimepita kama dakika kumi, naye Blandina akasema ingekuwa bora kama wangekuja na miamvuli kwa kuwa hakupenda kusubirishwa namna hiyo.

Namouih akamshika mkono rafiki yake kwa chini na kumsogelea mpaka karibu na sikio, naye akamwambia kuhusu jambo hilo aliloona upande ule mwingine. Akamwambia amtazame mtu yule, kwamba alikuwa anawaangalia sana na hakutikisika hata kidogo.

"Wapi?" Blandina akauliza.

"Kule hivi ambako kuna gari dogo limepaki mbele ya duka, amesimama hapo," Namouih akasema bila kuangalia huko.

"Hakuna mtu hapo mbona?" Blandina akamwambia.

"Ah... we naye, unataka mpaka nimnyooshee kidole. Basi sa..."

Namouih alikuwa akisema hivyo huku akigeukia tena upande ule, lakini maneno yake yakakata baada ya kukuta kweli sehemu ile haikuwa na mtu kabisa.

"Wapi kuna nyani amesimama?" Blandina akamuuliza kiutani.

Namouih akawa amebaki kuangalia huko kwa umakini.

"Au ni kwingine?" Blandina akauliza.

"Hamna. We hukuona labda mtu anatoka hiyo sehemu?" Namouih akauliza.

"Hamna sijaona. Macho yako tu," akasema Blandina na kuangalia kwingine.

Kwa dakika chache, jambo hilo likawa limeichanganya kiasi akili ya Namouih, lakini mwishowe akapotezea na kuendelea kusubiri mvua ikate.

★★

Mvua ilipungua taratibu mpaka kufikia hatua ya kudondosha matone madogo madogo, na sasa zilikuwa zimekwishapita dakika zaidi ya ishirini wanadada hao wakiwa wamejikinga hapo. Wakaanza mchakato wa kuondoka eneo hilo, wakiwa waangalifu kwenye mwendo wao kwa kuwa barabara ilikuwa na utelezi kwa chini kutokana na ardhi kuwa tope pia. Wakafanikiwa kuifikia barabara ya lami, na kwa pande zenye mitaro barabarani hapo yalionekana maji mengi yakiwa yamejaa na kusonga kuelekea upande mmoja. Wakapata taxi na kuingia pamoja, kisha wakaanza sasa kuelekea kule hospitalini.

Walipofika, wakaelekea mpaka kule alikolazwa bwana Masoud, na hapo wakamkuta Sasha pamoja na Zakia. Namouih alikuwa ametarajia kumkuta mama yake huku, na baada ya Sasha kuwaona wawili hawa akawafata na kuwasalimu, kisha akamwambia dada yake kwamba mama yake pia ndiyo alikuwa amefika tu muda siyo mrefu. Blandina akaenda kumsalimia Zakia na kuuliza hali ya mgonjwa, na mama huyu akamwambia kwamba bado hali yake haikuwa nzuri na madaktari walisema watarajie lolote lile kwa muda wowote. Namouih alijua vizuri sana kuwa mama yake alisema hivyo ili kumuumiza, naye Blandina akampa tu mama huyu pole na kusema yuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu. Namouih akampatia pesa Sasha na kumwambia atangulie nyumbani ili kuwa pamoja na Nasma, naye Sasha akatii kisha kukusanya vitu vichache vya kwenda navyo huko.

Baada ya Sasha kuondoka, Namouih akamsogelea baba yake na kumwangalia kwa hisia sana, kisha akakishika kiganja cha mama yake. Zakia akamwangalia binti yake kwa njia fulani iliyoonyesha ni kama amemkasirikia, lakini Namouih akamwambia alihitaji kuzungumza naye, hivyo watoke nje mara moja. Blandina akasema angebaki hapo pamoja na mgonjwa wakati huo, hivyo Namouih akatangulia nje, akifuatwa na mama yake nyuma. Wakaelekea mpaka sehemu iliyokuwa njia ndefu ya hospitali iliyoelekea pande mbalimbali, nao wakasimama kwenye kingo ya chuma; Namouih akimwangalia mama yake, lakini Zakia akitazama chini.

"Umekuja mvua imeshaanza kunyesha?" Namouih akaanzisha maongezi.

"Imenikuta njiani," Zakia akajibu.

"Baba alikuwa ameshalala ulipofika huku?" Namouih akauliza.

"Alikuwa macho," Zakia akajibu bila kumwangalia.

"Amekula angalau?"

"Mdogo wako anasema hakula chochote, alikuwa anasumbua. Nimefika nikampa juice. Amekunywa, ndiyo akalala..."

"Bado dawa za maji zinahitajika, si ndiyo?"

"Kila siku. Leo tu imekatika laki mbili, na mifuko inaisha, hela inakata. Ikifikia hatua pesa ikakosekana ndiyo basi tena."

"Usijali, nitapata tu ya kusukuma kwa wiki za mbeleni..."

"Utapata wapi?" Zakia akasema huku sasa akimwangalia.

"Kuna ishu ninafuatilia. Kilichopo tu ni kusubiri haitachukua muda mrefu na...."

"Ingekuwa afadhali kama ungechagua kazi inayolipa kwa uhakika na siyo kwa kubahatisha, maana kukaa kusubiri kitu ambacho hauna uhakika nacho inamaanisha Soud atakuwa ameshakufa kufikia muda huo..."

"Mama usiongee hivyo tafadhali..."

"Ni ukweli. Namouih nisikilize. Baba yako huyu amefanya kazi ngumu sana kukujengea maisha mazuri, na najua hakuwa na... matarajio labda tuseme... uje ulipie. Najua umefuata ndoto zako, lakini zinachukua muda sana kutimia ili wewe angalau uwe msaada kwetu. Ndugu zetu wametutenga tokea zamani, siwezi hata kufikiria kuwaomba msaada maana wanajua kabisa hali aliyonayo Masaoud lakini wametuacha... yaani tukome..."

Namouih akatazama tu chini.

"Baba yako ni mtu mzuri sana Namouih, anastahili kuishi maisha marefu, na kama kuna nafasi ya kumwokoa tunapaswa kuichangamkia. Kwa huu muda wote ambao tumejitahidi kupigana, ni kama jitihada zetu zinaelekea mwisho sasa... tunahitaji suluhisho la kudumu. Namouih me sitaki baba yako afe. Au wewe unataka afe?"

"Mama..."

"Najua unampenda pia. Lakini utapaswa kuonyesha hilo kwa kuzuia hatma hii. Mimi naipinga kabisa. Amebakiza wiki chache sasa, na angekuwa ameshaenda mapema tu. Unajua ni kwa nini bado yupo? Bado anataka kuishi Namouih. Anataka kuishi, kuziona sura zetu, kufurahia siku za mbeleni akiwa pamoja nasi. Kwa nini tumnyime hilo?"

Maneno ya Zakia yalimchoma sana binti yake, kwa kuwa alikuwa akimfanya ahisi hatia moyoni kwa kufikiria kwamba alishindwa kufanya jambo fulani kumsaidia baba yake. Ilikuwa wazi mama yake alitaka afanye nini, na kwa sekunde chache akabaki kimya tu akitafakari vitu vingi.

"Hapa hakuna msaada zaidi kwa baba yako, ni ubabaishaji tu yaani wanakula hela zetu kwa ajili ya dawa lakini hata wewe unajua hizo hazitasaidia lolote, anahitaji tiba nzuri.... ni kama wanamsogeza zaidi kwenye...."

"Okay, mama inatosha. Tafadhali," Namouih akamkatisha kwa ustaarabu.

Zakia akatazama tu pembeni.

Namouih akashusha pumzi, kisha akauliza, "Anaitwa nani?"

Zakia akamwangalia.

"Huyo mwanaume... anaitwaje?" Namouih akauliza tena bila kumwangalia.

Zakia akatabasamu kwa mbali, kisha akavishika viganja vya Namouih akionekana kufurahi. "Anaitwa Donald. Ni kijana mzuri sana Namouih, anakupenda sana," akamwambia.

"Una uhakika gani? Mtu anawezaje kunipenda halafu asijaribu hata kunitafuta?"

"Hapana, siyo hivyo. Huyu rafiki yangu aliyeniambia kumhusu ni Mage, unamkumbuka aunty Mage?"

Namouih akatikisa kichwa kukubali.

"Eee... yeye ndiye aliniambia. Huyo kaka inaonekana ameanza kukufatilia kwa muda mrefu. Mage yeye anafanya kazi kwenye moja ya maduka ya huyo kaka yaani anamiliki kampuni na maduka mengi... ndiyo alikuja kumsikia siku moja anakuongelea kwa rafiki yake, alikuwa anamwonyesha picha yako. Alikuwa anasema yaani kama ni kuoa anakuoa wewe tu... ndo' Mage akaja kuniambia sasa," Zakia akaelezea.

"Kwa hiyo inamaanisha kumbe hujawahi hata kukutana naye? Mbona ulisema umenitafutia mchumba kana kwamba mnajuana, wakati bado hata hujaongea naye?"

"Mage ndiyo ilibidi amwambie kwamba anakujua, na amesema kwa sababu kuna mambo mengi ya kikazi hapo nyuma Donald alikuwa bize, ila akaniambia kwamba amepanga kukutafuta. Mage alikuwa anataka kukuunganisha naye haraka lakini hakuwa na namba yako, na mimi sikuona inafaa kumpatia kabla hatujaongea. Namouih, ukiolewa na huyu kaka itakuwa jambo zuri sana kwa familia yet- kwa baba yako... na wadogo zako pia," Zakia akasisitiza.

"Nahisi ni kama nitajiweka kwenye hali mbaya nikijaribu kuchukua hayo maamuzi," Namouih akaongea kwa hisia.

"Hapana mwanangu, usifikirie hivyo. Huyo kaka atakufaa. Mage ameniambia ni mtu mmoja mstaarabu sana, hata aliponi-boost kidogo hela kwa ajili ya baba yako ni kwa sababu analipwa vizuri sana na Donald..."

"Ungekuwa ndiyo mimi ungeolewa naye hata sasa hivi kabisa eeh..."

"Ahah... Namouih acha mambo yako. Bahati imekuangukia wewe. Nataka tu uitumie vizuri ili kumwondolea baba yako mateso. Mambo mengine yatajipa tu, amini hilo," Zakia akaongea kwa ushawishi huku akikishika kichwa cha binti yake.

Namouih akatulia kidogo, kisha akasema, "Sawa. Fanya umpe rafiki yako namba yangu, ampe huyo Donald, anitafute. Tutaangalia na jinsi mambo yatakavyokuwa."

Wakati alipokuwa akisema hayo, Zakia alikuwa ameachia tabasamu lililoonyesha dhahiri kabisa kwamba alifurahi kupita maelezo. Uso wa Namouih ulionyesha hali ya hisia za kawaida tu, kwa kuwa alisema hayo kwa kinywa lakini hayakutoka moyoni. Ni kwamba tu katika pambano hili la kutaka kumwokoa mzee wake, ilionekana suluhisho lililokuwa limebaki ni yeye kutumiwa ili achune pochi ya mwanaume mwenye pesa ili kupata njia nzuri ya kumtibu baba yake. Ni jambo ambalo lilipingana kabisa na aina ya mambo aliyotaka kwenye maisha yake, lakini badiliko hili la hali lilifanya iwe lazima kwake kuchukua uamuzi huo; akiona jukumu la kuokoa maisha ya bwana Masoud lilikuwa lake.

Mama yake akamkumbatia kwa furaha, na kwa utani akamwambia kwamba anajua asingemwangusha maana alikuwa amezaa "pisi kali." Namouih hata hakutoa itikio la furaha ya kujilazimisha, naye akasema tu warudi kule ndani kuwa pamoja na baba yake. Walimkuta Blandina akiwa ameketi pembeni ya kitanda alicholazwa bwana Masoud, akiwa anapitia mambo fulani kwenye simu yake. Wakaendelea kukaa hapo kwa dakika kadhaa huku wakiangalia mahitaji ya mgonjwa, kisha Zakia akaaga kwenda nyumbani, kwa kuwa Namouih ndiyo angebaki hospitali kwa usiku huo.

Baada ya mama mtu kuondoka, Blandina aliuliza ikiwa kila kitu kilikuwa sawa, naye Namouih akamwambia sasa kwamba aliamua kumtafuta huyo Donald ili wayajenge, na kama ikiwezekana aweze kumwomba amsaidie baba yake. Bado huyu dada aliliona jambo hilo kuwa lenye kutatiza sana; hakutaka kabisa kufanya hivyo. Lakini alikuwa amekwishaishiwa mawazo mazuri na ya haraka ya kusuluhisha tatizo la mzee wake, kwa hiyo ingekuwa lazima kuvaa moyo wa chuma ili jambo ambalo mama yake alitaka afanye litimie. Blandina akamtia moyo tu kwa kusema asiwaze sana, na kusema kwa utani kwamba angetakiwa kuonyesha mautundu yake mengi kwa huyo jamaa ili apagawe na kumwaga mamilioni. Angalau ni Blandina ndiye aliyeweza kulifanya tabasamu la Namouih lionekane kidogo kwa maneno yake yenye utani.

Muda uliposonga zaidi, Blandina alirudi kule alikokaa kwa wakati huu pia akimwacha Namouih hapo. Kama kawaida, mwanadada huyu akaendelea kukaa pembeni ya mzee wake mpaka usingizi ulipomchukua na kumpeleka kwenye ulimwengu wa ndoto.



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


WhatsApp no: +255 787 604 893

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA NNE

★★★★★★★★★★★★★★


Asubuhi ilipofika, tayari Namouih alikuwa macho akishugulika na mambo kadhaa yaliyohitajika kwa ajili ya kumweka baba yake katika hali nzuri. Bwana Masoud alipoamka, Namouih akamsaidia kupata chakula chepesi, naye akatulia kidogo mpaka daktari alipofika na kuanza kuangalia hali yake. Akamsogeza Namouih pembeni na kumwambia jinsi alivyoyaona mambo, kwamba ingawa mzee wake alijitahidi sana kuonyesha yuko imara, alikuwa na maumivu makali sana. Muda si muda yangekuja kwa kasi zaidi na kusababisha mfumo wake wa upumuaji ukate, na habari hii ikamwongezea simanzi mwanadada huyu.

Daktari akamtia moyo pia kwa kumwambia Mungu ni mkubwa, hivyo ingetakiwa tu kusubiri mikono wake wa neema utue kwao, labda ingekuja njia ya kumwokoa. Kila kitu kilihitaji pesa, na kumsukuma mzee huyu aendelee kuishi kwa hizi wiki chache zilizopita ilitokana na dawa alizokuwa akipata, lakini bado ugonjwa wake uliendelea kumtafuna. Upasuaji wa gharama kubwa ndiyo uliokuwa suluhisho kwake. Akamwacha Namouih baada ya maongezi yao, na mwanamke huyu akarudi kwa mzee wake; akiketi pembeni yake.

Bwana Masoud alikuwa akimtazama Namouih kilegevu, macho yake yakionyesha kuchoka sana, lakini akaweza kuachia tabasamu dogo kumwelekea binti yake. Namouih akatabasamu pia, naye akakishika kiganja chake.

"Daktari alikuwa anakupiga swagger gani?" Masoud akauliza.

"Alikuwa ananiambia kuhusu hali yako. Anasema uko imara sana," Namouih akamwambia.

"Imara... imara kwamba ninajua ninakufa na nimelikubali hilo?"

"Baba usiseme hivyo. Bado una maisha marefu, na utayaishi..."

"Ahah... Namouih... kila mtu ana wakati wake...."

"Baba nimekwambia usiongee hivyo...."

"...ni lazima kuufikia tu. Roho inaniuma kujua kwamba umeacha baadhi ya mambo muhimu kwenye maisha yako ili kuwa hapa... Namouih... unapaswa tu kukubali hili pia, kwamba hautakuwa na mimi sikuzote. Wewe endelea na mambo mengine, jitahidi kuboresha maisha yako, yangu yanaelekea tamati yake...."

"Kwa sababu yangu. Ni kwa sababu yangu maisha yako yanaelekea tamati, na mimi siwezi kukaa kukuangalia tu...."

"Unamaanisha nini Namouih? Hujanisababishia lolote. Wewe ndiyo umenipa hii kansa?"

"Umekuwa ukifanya kazi hiyo kwa ajili yangu, ili nisome, nije kufanikiwa. Siwezi kuelewa ni nini umepitia huko migodini baba lakini naelewa kwamba ulikuwa unapigana kwa ajili yangu... kwa ajili yetu sisi sote. Sitaacha kupigana kwa ajili yako baba. Hili suala litakwisha. Nakuahidi," Namouih akasema kwa hisia.

"Mhm... una kichwa kigumu sana wewe. Utapoteza muda, pesa, na mambo mengine halafu bado mwisho wa siku nitaenda tu. Mimi sitajali hata nikifa Namouih. Nachojali tu kwa sasa... ni kuwa nawaona nyie wote kwa hizi siku chache nilizo...."

"Baba please..."

"...bakiza... usijali Namouih, usijali. Kila kitu kitakuwa sawa, na sitaki ulazimishe mambo yasiyokuwa na ulazima. Ninakujua vizuri sana. Niahidi hautafanya jambo lolote la kipuuzi. Niahidi hautaharibu maisha yako kwa sababu yangu... tafadhali..." Masoud akamwomba binti yake.

Machozi yalikuwa yameanza kumjaa machoni mwanamke huyu, naye akajikaza kutoyaruhusu yamwagike, kisha akaketi kwenye kitanda alicholala baba yake usawa wa kichwa chake, akikinyanyua kidogo na kukiweka kwenye paja lake.

"Niimbie basi," Masoud akamwambia akiwa amefumba macho.

"Ahah... nikuimbie hapa?"

"Ndiyo. Niimbie kale kawimbo kazuri ulikokuwaga unamwimbia Nasri..."

"Mhmhm... bado unaukumbuka mpaka leo?"

"Siwezi kusahau sauti yako ilivyo nzuri..."

Namouih akavuta pumzi kiasi, kisha akaanza kumwimbia mzee wake kwa sauti ya chini lakini iliyosikika vyema kwa Masoud. Baba yake akatabasamu tu kwa furaha aliyohisi kuona jinsi binti yake alivyompenda sana, naye akafumba macho akisikilizia jinsi sauti tamu ya Namouih ilivyoikonga nyoyo yake, na hii ikamfanya ahisi amani sana.

Muda mfupi baadae, Zakia akawa amefika hapo pia na vifaa kadhaa, na moja kwa moja akaanza kumweleza Namouih kuhusiana na suala la Donald. Akamwambia kwamba tayari alikuwa amempatia Mage namba yake, na Mage pia alikuwa ameshaanza mipango ya kumuunganishia kwa boss wake huyo ili mambo yatie tiki. Kwa hiyo Zakia akawa anamshawishi sana bintiye kwamba pindi ambapo mwanaume huyo angemtafuta, afanye juu chini ili amzuzue zaidi na hatimaye aweze kupata faida ambayo itasaidia kuokoa uhai wa baba yake haraka.

Namouih hakuonyesha hisia yoyote ile kuelekea shauku kubwa ya mama yake, naye akasema tu angeondoka kwenda kununua dawa zaidi za maji ili kuja kumwekea mzee kwa ajili ya siku hii. Hata Zakia alijua wazi kwamba binti yake alikubaliana na jambo hilo kwa shingo upande, lakini aliona ilikuwa bora kuliko kama angekataa kabisa. Akawa tu anaombea kwamba asije kuvuruga mambo wakati alikuwa amemtengenezea vizuri sana mitambo hiyo.

★★

Ilipofika mida ya saa 7 mchana, tayari Namouih alikuwa ameshaondoka hospitalini kule kwenda kufanya mizunguko ya hapa na pale mjini. Kwa muda huu baba yake alikuwa chini ya uangalizi wa wauguzi hospitalini huko, na mama yake kama kawaida alikuwa kwenye shughuli zake pia, wadogo zake wakiwa shuleni. Ni wakati alipokuwa ndani ya taxi kuelekea nyumbani pale alipopata ujumbe kutoka kwenye namba ngeni.

'Habari yako.'

Ulisomeka hivyo. Namouih akawa amekisia kwamba huyu bila shaka ndiyo angekuwa mwanaume tajiri aliyemtaka, hivyo akajibu ujumbe huo kwa salamu pia. Mwenye namba ngeni akajitambulisha kwa jina la Efraim Donald, akisema ameipata namba ya Namouih kupitia kwa "shangazi yake," yaani yule Mage, rafiki yake Zakia. Namouih akamkaribisha vizuri, na hapo ndiyo mwanaume huyo akasema alihitaji sana kupata nafasi nzuri ya kuja kuonana naye kwa sababu kuna mambo mengi alitaka waongee.

Akaomba samahani kwa kwenda moja kwa moja kwenye hilo kwa kuwa Namouih hata hakumfahamu, naye akamwambia angependa waendelee kufanya mawasiliano ili wajuane vizuri zaidi, na hata akitaka basi angemrushia picha zake ili amwone. Mwanzo ingekuwa kwamba wanatakiwa tu kufahamiana na kujenga urafiki, ili mwishowe wakija kukutana basi aweze kumwelezea hayo "mambo mengi," kwa sababu alikuwa na hamu kubwa sana ya kuzungumza naye.

Namouih kama Namouih hakuwa na kipingamizi, kwa kuwa tayari hili ni jambo lililokuwa limepangwa. Ingekuwa kwamba limekuja kwa kushtukiza angempiga "block" ya nguvu mwanaume huyo. Kwa hiyo Namouih akamwambia tu kwamba yeye yuko huru muda wote, hivyo atakapotaka kumtafuta afanye hivyo, na ili kuweka hali fulani ya mazoea kiasi, akasema ana hamu ya kukutana naye pia. Mwanaume huyo akasema angemtafuta baadaye kutokana na kuhitaji kumalizia kazi fulani, hivyo angeshukuru kama Namouih angeitunza namba yake. Mwanamke akamwambia mwanaume asiwaze, na baada ya hapo wakaagana.

Ingekuwa rahisi kwa mwanamke mwingine kupata hata hisia za msisimko kwa kujua ndiyo alikuwa ametoka kuongea na mchumba mtarajiwa, lakini kwa Namouih haikuwa hivyo. Yaani hisia zake za moyoni zilikuwa zimefukiwa ndani sana, kwa kuwa kilichotawala mawazo yake ilikuwa ni baba yake tu. Akafika nyumbani na kushughulikia mambo kadhaa mpaka Nasma na Sasha waliporejea kutoka shuleni, naye akapumzika kidogo huku akisoma-soma mambo yake ya kisheria.

Ilipofika saa kumi jioni, akaelekea tena hospitalini kumwona mzee wake mpaka ilipofika usiku wa saa mbili ndiyo akarudi nyumbani tena. Blandina akawasiliana naye kuuliza mambo yalikwendaje, kwa kuwa yeye alikuwa bize kufuatilia mambo mengine kwa leo, naye Namouih akamwambia mambo yalikwenda kama kawaida, bila kugusia kuhusu Efraim Donald. Ni Zakia ndiye aliyekwenda kukaa na mume wake hospitalini baada ya kumaliza kuzurura, hivyo Namouih akawa ametulia ndani na wadogo zake.

Mida ya saa nne hivi usiku, Efraim Donald akamtumia ujumbe Namouih, akimsalimu na kutaka "wachati." Siyo kwamba Namouih alikuwa akisubiri ujumbe kutoka kwa mwanaume huyo, lakini akili yake ilimwambia kwamba hizo ndiyo njia za mwanzo ambazo zilikusudiwa kumwaminisha kwamba kweli ana nia naye. Hata ingawa alikuwa anapangwa akubali tu ikiwa mwanaume huyo ataomba wawe na mahusiano, hiyo haikumaanisha angekubaliana tu na kila jambo bila kudadisi vitu fulani. Hata akawa anawaza ikiwezekana amchune tu halafu amwache kwenye mataa, lakini hakuwa aina ya mtu mwenye viwango vya namna hiyo.

Walihamishia maongezi yao kutoka kwenye jumbe za kawaida kwenda WhatsApp, na hapo sasa ndiyo Namouih akaweza kumwona mwanaume huyo kwa sura baada ya ya kurushiwa picha yake. Picha ambayo Efraim Donald aliituma ilimwonyesha akiwa ameegamia gari jeupe aina ya Range Rover, akiwa ameshikilia simu huku akitazama camera ya mpigaji. Mwili wake ulikuwa mkubwa kiasi, yaani mpana, hata T-shirt aliyovalia kwenye picha ilimbana vyema, lakini haukuwa ule uliojikata sana kimazoezi ingawa alijaa kwa kadiri fulani. Alikuwa mweusi, mrefu, mwenye nywele fupi na ndevu zilizochongwa vizuri kutokea kwenye timba mpaka kidevuni, na alikuwa na macho makubwa kiasi.

Kumwangalia kwenye picha hiyo kulimfanya Namouih afikirie labda huyu jamaa alikuwa tapeli, naye akatabasamu tu na kutikisa kichwa chake kwa kujihisi kama mpuuzi kuendelea kufanya huu mchezo.

'Ndo wewe huyo,' Namouih akaandika baada ya kuiona picha sasa.

'Ndiyo mie,' Efraim Donald akamwandikia pia.

'Naona umenirushia picha uliyokaa karibu na gari kabisa. Impression ni kwamba?'

'Hahah we unadhan nataka kutoa impression gani?'

'Ndiyo uniambie'

'Napenda tu hiyo picha. Ninazo zingine kama utataka nikurushie'

'Sawa'

'Sijairusha hiyo kwa sababu ya gari, na hilo siyo gari langu'

'Kumbe'

'Ni la mteja ambaye ni rafiki yangu pia, hapo nilikuwa namuuzia ndiyo akawa anatwanga foto'

'Haya sawa. Kwa hiyo ulinijuaje mimi'

'Nilikuona ndotoni'

'Wapi?'

'Hahahah natania. Wewe siyo mpenzi wa utani eti?'

'Siyo sana'

'Ooh sawa, nanote hilo. Nilikuona mara ya kwanza kwenye conference fulani. Nafikiri ulikuwa kama intern wa mtu sijui maana ulivalia nadhifu sana na ulionyesha uko professional mno'

'Wewe ulikuwa unafanya nini hapo?'

'Nilikuwa kama mfadhili mdogo wa biashara zilizoendeshwa'

'Mdogo?'

'hahahaha napenda jinsi unavyoniuliza maswali, ikimaanisha unataka sana kuniingia'

'Hahaha.. siyo kihivyo. Ni kwamba me ni mwanasheria kwa hiyo maswali ni kitu yangu sana, samahani lakin'

'Oh no, nimekwambia napenda. Hiyo inamaanisha tutakuwa na mambo mengi sana ya kuongelea tukikutana. Ntakufanya uwe prosecutor wangu'

Namouih hakuweza kujizuia kutabasamu kwa kauli hiyo. 'Kwa hiyo kuanzia hapo ndo ukaanza kunifuatilia eeh?'

'Siyo kama stalker lakini ndiyo, nilijaribu kukutafuta ila nikakukosa. Baadae nikaja kupata picha yako. Nilikuwa naitazama kila siku yaani'

'Kwa nini?'

'Ulinivutia sana'

'Kwa nini?'

'Unaonaje tukija kukutana ili nikujibu vizuri zaidi'

'Lini?'

'Wakati wowote utakao'

'Wakati wowote nitakao? Nikikwambia uje sasa hivi?'

'Nimeshafika'

Namouih akazungusha macho kikejeli.

'Hizo swaga tu kaka'

'Ndiyo najua unajua hilo. Nataka tu uhisi kile ambacho nitasema kuwa kweli Namouih, na kwenye simu haitatosha. Najua unaelewa nitakakoelekea, lakini sitaki iwe kwa POV yako tu, bali yetu sote. Niambie kama unataka nitakuja hata kesho'

'Kweli?'

'Kabisa'

Namouih akatulia kidogo, kisha akamwandikia, 'Sawa, njoo kesho basi'

'Ondoa shaka, nitafika'

'Unajua pa kunipata?'

'Nimeshakupata tayari, so just relax, mimi ndiyo nitakuja kwako'

Namouih akacheka kidogo kwa kuguna, akiona mambo haya yote kuwa maigizo ya hali ya juu sana. Ni kwamba kuna ile hali tayari aliijua kuhusu jinsi wanaume wanavyokuwa wanapoanza kumshawishi mwanamke ili kupata watakacho, kwa hiyo kwake maneno hayo mazuri hayakulegeza ugumu wa moyo wake kuelekea jinsi alivyochukulia jambo hilo. Baada ya story fupi za hapa na pale, Efraim Donald akamtakia usiku mwema, akimwambia kwamba kesho angefika mjini kwao upesi ili wakutane na kuweza kuzungumza ana kwa ana. Akasema angepangilia kila kitu, hivyo kile ambacho Namouih angetakiwa kufanya ilikuwa ni kutulia tu. Wakaagana. Namouih akaingia kulala. Usiku ukapita.


★★★


Asubuhi na mapema, Namouih alikuwa ameamkia kufanya usafi nyumbani, akisaidizana na Sasha. Hii ilikuwa ni siku ya Jumamosi, hivyo Nasma alikuwa ameupiga usingizi tu kufidishia siku zote tano alizokuwa akiamka mapema sana kwenda shule, kama kawaida ya watoto wanaopenda usingizi. Sasha binti mrembo kama dada yake alikuwa na mpango wa kuandaa chakula kizuri sana kwa ajili ya baba yake siku hii, naye Namouih akampongeza na kumwambia yeye pia ana hamu ya kuja kukionja, kwa kuwa alijua angepika vizuri sana na baba yake angekifurahia. Kwa hiyo baada ya Namouih kumaliza mambo kadhaa hapo, akabeba chakula kidogo kwa ajili ya asubuhi ili yeye atangulie hospitalini, akimwacha Sasha anashughulika na vitu vingine baada ya Nasma kuamka.

Zakia bado alikuwepo hospitali Namouih alipofika, na mwanamke huyu akamkuta baba yake akiwa macho tayari na kuanza kumnywesha uji taratibu. Bwana Masoud alipenda sana Namouih alipomlisha, zaidi hata ya Zakia, kwa hiyo alijitahidi kumaliza wote na chakula chepesi cha asubuhi Namouih alichomsisitizia ale. Mama mtu alitaka kujua ikiwa Namouih alikuwa ameshaanza kuongea na Donald, akimuuliza bila Masoud kusikia, lakini Namouih akamwambia mambo hayo wangeyazungumzia baadaye. Akamwambia mama yake aende nyumbani kujiweka sawa kimwili ili baadaye aje tena pamoja na Sasha.

Zakia alikerwa sana na jinsi ambavyo binti yake hakutaka kufunguka haraka, kwa hiyo akaondoka hapo akiwa ameudhika, na Namouih alilielewa hilo vizuri. Akaendelea tu kukaa na mzee wake hapo, akipiga naye story moja mbili tatu zenye kufurahisha. Dawa alizokuwa akiendelea kupewa hapo zilimfanya Masoud asiihisi sana saratani yake ilivyomtafuna, lakini Namouih alijua kweli muda si mrefu mwili wa baba yake ungeshindwa kustahimili maumivu yaliyokuwa njiani kumpata.

Ilipofika mida ya saa nne asubuhi, Namouih akapigiwa simu na Efraim Donald. Ilimbidi atoke nje ya chumba cha wodi ya baba yake ili aweze kuzungumza kwa faragha. Baada ya kupokea, Efraim Donald akamwambia kwamba alikuwa ameanza kuja kutokea kwenye jiji alipokuwa, na ingawa Namouih alishangaa kiasi kuona jinsi jamaa alivyoonyesha hatanii, hasa kwa sababu ya jiji hilo kuwa mbali, hakuuliza. Efraim Donald akasema alikuwa tu anamtaarifu mapema ili akifika na kumfata asishtuke sana, naye Namouih akasema haikuwa na shida; angemkuta tu. Basi wakaagana, naye Namouih akarudi kwa baba yake. Alikuta usingizi ukiwa umempitia mzee wake, naye akabaki tu kumtazama akiwa anawaza jinsi ambavyo maisha yake yangebadilika kwa sababu ya uamuzi aliokuwa karibu kuuchukua.

★★

Muda ulisonga mpaka inafika saa saba mchana. Upande wa nyumbani kwake Masoud, Sasha alikuwa amemaliza kumpikia chakula kizuri sana baba yake, na ndiyo alikuwa tu akipangilia mambo yaliyobaki ili aambatane na mama yake kuelekea hospitalini. Nasma angekwenda pamoja nao pia ili kumsalimu baba yake, hivyo naye alikuwa amemaliza kujiandaa. Zakia akiwa anamsubiria Sasha, akafika mgeni hapo ambaye hakutarajiwa. Ilikuwa ni Blandina, naye Zakia baada ya kumwona akamkaribisha ndani.

"Za hapa mama?" Blandina akasalimu.

"Salama tu," Zakia akajibu.

"Shikamoo," Nasma akamwamkia Blandina.

"Marahaba baby. Umependeza kweli, unaenda wapi?" Blandina akamsemesha.

"Naenda kwa baba," kakajibu.

"Oooh mnaenda hospitali eeh? Ni vizuri maana na mimi nataka kwenda pia," akasema Blandina.

"Una mgonjwa kwani?" Zakia akauliza.

"A... ahah... hapana, namaanisha naenda pia kumsalimu ba Nam," Blandina akasema.

"Aaaa... sawa basi twende wote. We' Sasha... em' harakisha bana!" Zakia akaongea na kusema hivyo kwa sauti kubwa.

Blandina akatabasamu, na alipokuwa anataka kusema jambo fulani, Sasha akawa amefika hapo walipokuwa wamesimama.

"Ulikuwa unafanya nini nawe?" Zakia akaongea kabla ya Sasha kumsalimia Blandina.

"Nilikuwa na... nilikuwa..."

"Unajivuta mno wakati usafiri wenyewe unajua mgumu mwishowe usababishe mtu mwingine afe..." Zakia akasema hivyo na kusonya.

Kauli hii ilivuta umakini wa Blandina, na kwa sekunde akawa amemwangalia Sasha na kuona jinsi alivyoinamisha kichwa chake kwa njia iliyoonyesha huzuni. Blandina alielewa kwamba maneno hayo yenye chumvi yalimaanisha kuwa kwa kuchelewa, Sasha angesababisha Masoud afe, lakini Zakia kusema "mwingine" kulifanya Blandina ahisi mwanamama huyo alikuwa na maana nyingine.

"Twendeni tukachukue daladala sasa," Zakia akasema huku akianza kutoka.

"Oh, nimekuja na gari, haina haja ya kuchukua usafiri wa kulipa. Twendeni kwenye gari," Blandina akasema alichokuwa anataka kusema mwanzoni.

"Heh! Umenunua gari?" Zakia akamuuliza.

"Ahahah... hapana, ni la rafiki," Blandina akajibu.

"Mmmm la rafiki wapi?"

Zakia akamuuliza hivyo kichokozi huku akimbonyeza begani, na wote wakacheka isipokuwa Sasha. Wakatoka na kuelekea kwenye gari alilokuja nalo Blandina na kuanza safari kuelekea hospitalini. Njia nzima wanawake hawa waliongelea mambo kadha wa kadha, lakini Sasha hakujihusisha na maongezi. Haikumchukua muda mrefu Blandina kuelewa kwamba maneno ya mama yake yalikuwa yamemchoma sana binti huyo, lakini akawa anataka kujua kiundani zaidi sababu zilizofanya Zakia aseme maneno yale bila kujali hisia za mwanaye.

Walifika hospitalini na kumkuta Namouih akiwa hapo bado. Hii ikiwa ni saa ya kutembelea wagonjwa, sehemu nyingi zilikuwa na watu wengi waliokuja kuwatembelea wapendwa wao walioumwa, na hakuna kitu kilichompa furaha bwana Masoud zaidi ya kuiona familia yake yote ikiwa hapo. Nasma alipomlalia kifuani kwa njia ya kumkumbatia, Masoud alidondosha machozi utadhani ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kumwona baada ya kipindi kirefu. Kakaanza kumfuta machozi kwa upendo, naye Sasha akamkaribia zaidi na kuanza kumsemesha pia.

Baada ya wote kutulia, Sasha na Nasma ndiyo wakawa wanamlisha baba yao kwa zamu, huku na wenyewe wakila kidogo pia na maongezi ya mambo ambayo Nasma amekuwa akifanya yakiendelea. Zakia alikuwa pembeni na simu yake akionekana ku-chat na rafiki, naye Namouih alikuwa akiwaangalia wadogo zake na baba yao kwa upendo sana. Blandina, akiwa bado anafikiria kuhusu maneno ya Zakia kumwelekea Sasha, akamuuliza Namouih ikiwa alikuwa ameshakula, naye akakanusha na kusema angekula baadaye. Blandina akamwambia anataka waongee kidogo hivyo watoke nje mara moja, na mwanadada huyu akakubali. Wakawaacha wengine hapo na kwenda nje ya chumba hicho.

"Vipi mommy, unaendeleaje?" Blandina akamuuliza.

"Unamaanisha nini?" Namouih akauliza pia.

"Well, tulipoachana ile juzi ulisema ungemtafuta yule jamaa, lakini bado hujanipa ubuyu," Blandina akasema.

Namouih akatabasamu kwa mbali, kisha akasema, "Nilimtafuta."

Hii haikuwa kweli moja kwa moja kwa kuwa ni Efraim Donald ndiye aliyemtafuta yeye, lakini Namouih aliona yote kuwa yaleyale.

"Enhe, imekuwaje?" Blandina akauliza.

"Anakuja leo kuonana nami," Namouih akasema.

"Wewe... acha basi!"

"Sure kabisa..."

"Wow! Siku moja tu tayari amelewa mziki' wako eeh?"

"Hapana bwana... ahah... anakuja tu ili ndiyo uwe mwanzo wa kufahamiana vizuri. Ngoja nione itakavyokuwa..."

"Hii ikimaanisha haujapanga kumwambia kuhusu baba yako leo-leo, siyo?"

"Yaani hata sitaki kufanya hivyo kabisa."

"Lakini hamna namna, ikiwa kweli ana pesa huenda akakusaidia. Me naona ni bora umwambie kuhusu hii changamoto ili kama ni kukusaidia akusaidie mapema. Sidhani kama itakuwa busara kusubiri mpaka muoane huko, maana haitakuwa nzuri kwa mzee Masoud..."

"Ndiyo, najua. Ni kwamba tu... nahisi ni kama ni.. a.. yaani... hhhh... Blandina maisha yangu yatageuka kuwa maigizo makubwa sana. Natamani sana kama ingekuwa rahisi kwangu kufanya hivi, sijui tu hata nitaigizaje kwa huyu mtu kwamba...."

"Namouih, usi-stress hivyo. Nakujua jinsi ulivyo shupavu, we' ni jasiri utaweza tu, hii ishu mbona ni Tuesday? Just relax, kila kitu kitakuwa sawa darling," Blandina akamtia moyo.

Namouih akashusha pumzi na kuangalia chini tu.

"Bila shaka mama yako amefurahi sana," Blandina akasema.

"Usiniambie," Namouih akaongea huku ameendelea kutazama chini.

"Baba yako je? Utamwambia kwamba...."

"No. Hapana. Hatakiwi kujua kuhusu hilo kwa sasa. Nitapaswa tu nifekishe mambo mengi vizuri. Sipaswi kumshtukiza sana, na sitakiwi kumwacha kwenye mataa. Nataka tu kuhakikisha kwamba anabaki sehemu nzuri kimtazamo baada ya haya yote... Nasma na Sasha pia," Namouih akamwambia.

"Okay. Halafu... kuna kitu nataka kuuliza Nam," Blandina akasema.

"Ndiyo..."

"Hivi... mama yako huwa ana tatizo gani na Sasha?"

Namouih akamtazama na kumgeukia vizuri zaidi. "Kwa nini unauliza hivyo?"

"Yaani kuna nyakati ambazo nimeshawahi kuona anamfokea, ah... ile tu unachukulia kawaida kwamba ni mama na mtoto, huwa ipo. Ila Nam kuna maneno ambayo Zakia anaweza kumsemesha Sasha ni mazito sana mpaka huwa nashangaa..."

"Maneno kama yapi?" Namouih akauliza kwa umakini.

"Kipindi kile kwenye birthday ya Nasma, alitaka kwenda naye wapi sijui nje ya nyumba mida kama ya saa mbili, nilimsikia mama'ako akisema, 'unaenda naye wapi? em' mwache usije ukaniulia mtoto mimi.' Hiyo niliona ni kama alikuwa amemkasirikia labda, lakini na leo tena alikuwa anamwambia aharakishe kabla hajasababisha mtu mwingine kufa..."

Namouih akafumba macho na kuinamisha kichwa.

"Nam, Sasha mara nyingi namwonaga huwa ni kama anakosa amani hasa mama yako akiwepo, na huwa anaonekana mstaarabu tu lakini nimekuja kugundua kuwa hiyo ni huzuni. Kuna kitu chochote ambacho kimewahi kumpata huyu mtoto?" Blandina akauliza kwa kujali.

Namouih akamtazama rafiki yake kwa sekunde chache, kisha akasema, "Ni story ndefu Blandina. Ila nitahitaji kuongea kwanza na mama, nawe nitakuja kukusimulia. Shukran kwa kuniambia."

"Huwezi hata kuniambia kwa kifupi?"

"Mambo ni mengi. Ngoja tu kwanza nishughulike na haya yaliyopo sasa, nitakuja kukuelezea," Namouih akamwambia.

Blandina akaridhia kwa hilo na kumpa pole kwa sababu ya changamoto hizi za kihisia, naye akamwambia labda akikutana na huyo Donald huenda angemsaidia kuziondoa kweli. Wakarejea ndani tena baada ya hapo kujiunga na wengine.

★★

Muda mfupi baadaye, Namouih akapigiwa simu na Efraim Donald, akimwambia kwamba tayari alikuwa amefika mjini kwao, na yeye Namouih aende sehemu fulani kukutana naye hatimaye. Kwa kutaka kuwa mwangalifu, Namouih akamwambia kwamba angekwenda na dada yake, akimaanisha Blandina, naye Efraim Donald hakuwa na kipingamizi. Mwanaume huyo akamwambia Namouih ikiwa angependa basi eti atume gari mpaka alipo ili limchukue na kumpeleka, lakini mwanadada wetu akakataa na kusema angekwenda kwa usafiri yeye mwenyewe. Alikuwa mgumu balaa! Mwanaume huyo akasema tu kwamba sehemu ambayo angekutana naye ilikuwa ya hadharani, kwenye mgahawa wa kisasa nje ya hoteli kubwa, hivyo angemsubiri tu hapo yeye na dada yake.

Baada ya kumaliza maongezi hayo, Namouih akamjulisha Blandina kuhusu kila kitu, na rafiki yake huyo akafurahi sana kujua aliunganishwa kwenye "collabo" hii. Akamwambia ni vizuri kwamba alikuja na gari, hivyo angempeleka Namouih nyumbani kujiandaa kisha ndiyo waende. Lakini Namouih akapinga hilo, akisema hakukuwa na haja ya kuoga wala kujiandaa; angeenda kuonana naye hivyo hivyo. Blandina alimshangaa sana kwa sababu alielewa kwamba alikuwa akifanya hayo kwa makusudi tu, na hakuwa na jinsi ila kumwacha afanye atakavyo. Akamwambia mwanaume akimkimbia kwa sababu ya kuogopa harufu ya jasho basi ndiyo atajua alikuwa amebugi sana.

Wawili hawa wakawaaga wengine kwa kusema wanatoka kidogo, naye Namouih akamwahidi baba yake kurudi baadaye tena kukaa pamoja naye, kisha wakaondoka hospitalini hapo.

★★

Ndani ya dakika ishirini tayari Blandina akawa amemfikisha Namouih alipotakiwa kwenda. Hawakushuka kwanza, bali Namouih akampigia jamaa simu na kumwambia wameshafika eneo hilo, naye akasema angekuja kumpokea. Alikuwa ameweka loud speaker ili na Blandina asikie, na rafiki yake huyu akamwambia Namouih kweli jamaa anaonekana yuko "sharp." Namouih alikuwa amekwishamwonyesha Blandina picha ya Efraim Donald, na shosti yake alimsifia kweli jamaa akisema yaani ingekuwa ni yeye ndiyo amepata hiyo bahati asingekuwa anadengua kama Namouih alivyokuwa akifanya.

Sekunde chache zikapita, na Namouih akamwona Efraim Donald kwa mbele, akiwa amesimama pembezoni mwa barabara ya lami nje ya eneo lililoizunguka hoteli ile ya kifahari kiasi. Alikuwa amevalia T-shirt yenye mtindo wa pundamilia lakini rangi zikiwa nyeupe na blue-bahari, suruali nyeusi ya jeans na viatu vyeusi vilivyong'aa sana. Blandina akamwona pia, naye akatabasamu na kuanza kumbonyeza-bonyeza Namouih mkononi kwa shauku, lakini Namouih akawa anamwangalia tu mwanaume huyo kwa umakini.

Efraim Donald alionekana kuangaza huku na kule, kisha akanyanyua simu yake na kuiweka sikioni, na ndani ya gari walipokuwa wanadada hawa simu ya Namouih ikaanza kuita. Akapokea, na jamaa akauliza mrembo alikuwa upande gani. Namouih yeye akasema ameshamwona, hivyo asimame hapo hapo alipo na yeye angemfata. Simu zikakatwa. Blandina akamwambia wawahi kwenda sasa maana alikuwa na hamu sana ya kuisikia tu hata sauti ya pedeshee huyo mubashara, naye Namouih akatikisa kichwa na kutoka ndani ya gari pamoja naye. Wakaanza kuelekea mpaka sehemu ile aliyosimama pedeshee sasa, na baada ya Efraim Donald kuwaona, akaachia tabasamu la mbali na kubaki amemwangalia tu Namouih.

Blandina akamsukuma Namouih kidogo kichokozi walipokuwa wamemkaribia jamaa na kumfanya mwanadada huyo ajikaze kucheka, na sasa wakawa wamemfikia kamanda.

"Mambo," Efraim Donald akawasalimu.

"Saaafii," Blandina akajibu huku akitabasamu.

"Naitwa Efraim, ukipenda niite Donald," akajitambulisha kwa Blandina.

"Sawa, Donald, mimi ni Blandina. Pacha mweusi wa Nam-Nam," Blandina akajitambulisha pia.

"Ahahah... sawa. Mmependeza sana warembo..."

"Asante," Blandina akasema.

Efraim Donald akamwangalia Namouih. Mwanamke huyu alikuwa anamtazama kwa njia ya kawaida tu.

"Uko poa?" Efraim Donald akamuuliza.

Namouih akatikisa kichwa kukubali bila hata kutabasamu. Blandina akaikaza midomo yake kucheka na kuangalia pembeni.

Efraim Donald akachekea kwa chini na kisha akauliza, "Mbona umenuna?"

Blandina akashindwa kujizuia kucheka kidogo sasa, lakini akajikaza zaidi.

"Sijanuna," Namouih akamwambia.

"Tabasamu sasa kidogo nione ma-dimple hayo," Efraim Donald akasema.

Namouih akatabasamu kidogo na kumwangalia Blandina, ambaye alikuwa ameibana midomo yake kuficha kicheko.

"Vipi sasa, unanionaje? Bado sionekani kama Prince Charming?" Efraim Donald akauliza.

"Ahah... unakaribia lakini siyo sana," Namouih akamwambia.

"Ahahahah... halafu alisema eti hawezi utani," Efraim Donald akamwambia Blandina.

"We,' anaongea huyu! Hujamkuta akiwa kwenye mahakama yaani hakuna anayemshinda maneno," Blandina akasema.

Namouih akatabasamu zaidi sasa, na ni kweli tabasamu lake lilifanya ma-dimple yake yakaonekana zaidi. Efraim Donald akafurahia sana urembo wa mwanamke huyo, nao wakatazamana machoni kwa sekunde chache. Kisha...

"Karibuni bwana. Nimefurahi sana kukutana nanyi. Tunaweza kuelekea pale kukaa kama itawafaa..." Efraim Donald akasema.

"Ndiyo, bila shaka," akajibu Namouih.

Pedeshee akaanza kuwaongoza kuielekea hoteli ile. Ilikuwa na ghorofa 6, na kwa nje kulikuwa na sehemu pana kiasi ya maegesho ya magari na upande mwingine kama mgahawa mpana kwa ajili ya vyakula na vinywaji. Namouih na Blandina walikuwa wakitembea huku wameshikana viganja vyao, Efraim Donald akiwa pembeni yao, naye akawa anawaambia kuhusu safari yake kutokea mkoani alikokuwa mpaka kufika huku mjini kwao Namouih, akisema haikuwa mara ya kwanza kuja huku, isipokuwa tu kufika kabisa maeneo ya huku walikokuwa hawa warembo.

Wakaifikia meza moja na kuketi kwenye viti vilivyoizunguka. Zilikuwa meza za duara, zilizotengenezwa kwa vitu vyenye ufanani wa mkeka lakini mzito na mgumu sana, na hata viti vilikuwa vya namna hiyo hiyo. Namouih akawa amekaa pembeni yake Blandina, huku Efraim Donald akikaa upande ambao aliwatazama wanawake hawa kwa pamoja.

"Vinywaji?" Efraim Donald akasema.

"Napendelea Serengeti Li...."

Namouih akamkanyaga Blandina alipokuwa akisema hivyo, naye akamwangalia usoni kimaswali.

"Okay, Serengeti Lite. And you?" Efraim akageuza swali kwa Namouih.

"Mimi niko sawa," Namouih akajibu.

"Eti ni kweli yuko sawa?" Efraim Donald akamuuliza Blandina.

"Hapana, yaani hajala kutokea asubuhi, sijui yukoje!" Blandina akasema.

"Lakini Bla...." Namouih akaishia tu hapo na kuweka kiganja karibu na mdomo wake.

Efraim Donald akatabasamu, kisha akasema angekwenda kumwagizia Blandina kinywaji na kumfatia Namouih chakula. Kabla hata Namouih hajapinga, tayari jamaa akawa amenyanyuka na kuondoka hapo.

"Eh-eh! Bibi tunafatiwa vyakula, oh nimekosea, unafatiwa chakula. Haki ya Mungu kupendwa ndiyo huku," Blandina akasema na kuanza kucheka.

"Halafu una kisebengo wewe, yaani bora tu hata ningekuacha!" Namouih akamwambia.

"Ahahahah... halafu nipitwe na hizi raha? Sahau! Kwa mashemeji ndiyo sehemu ya kuwa bibi we," Blandina akamwambia.

"Siyo kirahisi dear. Mtu hata sijui katokea wapi, anataka nini kwenye maisha yake, halafu niwaze ndoa naye haraka hivyo?"

"Umeanza tena!"

"Siendi kichwa kichwa. Je kama ameenda kuweka madawa kwenye hicho chakula anachokileta?"

"Basi ujue utakufa huku unatabasamu!"

Namouih akampiga kofi laini begani, naye Blandina akawa anacheka. Baada ya dakika chache, Efraim Donald akarejea na kuketi hapo pamoja nao, naye akawaambia kwamba msosi ulikuwa njiani kufika. Mhudumu mmoja akaleta chupa tatu za Serengeti na glasi na kuziweka mbele ya Blandina, naye akafurahi sana. Efraim Donald akamwambia Namouih amwambie mhudumu kinywaji cha kumletea pia, naye akasema aletewe maji tu. Mhudumu akaondoka, naye Efraim Donald akawa anamtazama tu Namouih usoni.

"Namouih ni jina zuri sana," Efraim Donald akavunja ukimya.

"Asante," Namouih akamwambia.

"Kwa hiyo kwa pamoja nyie ni wanasheria... mnaosaidizana?" Efraim Donald akauliza.

"Yeye ndiye attorney, me ni paralegal wake. Ni kama boss na assistant, ila kwa ukaribu sana," Blandina akamwambia.

"Aaa... okay. Nadhani itakuwa jambo zuri nikija kukuona unavyoshughulika na kesi..."

"Kwa nini?" Namouih akauliza.

"Ili nione ulivyo na maneno mengi," Efraim akamwambia, naye Namouih akatabasamu.

Chakula kikaletwa hapo. Ilikuwa ni nyama choma ya mbuzi iliyowekewa na roast, soseji chache na chips kavu nyingi na vionjo muhimu kama pilipili na tomato; zote zikiwekwa mbele ya wanawake hawa, bila kusahau maji ya Namouih. Blandina akamtazama mwenziye huku akitabasamu, na Namouih akamwangalia pia.

"Mnajua yaani na me sijagusa chakula safari yote kwa hiyo, karibuni tupate hii kitu pamoja," Efraim Donald akasema.

"Umekuja kwa usafiri gani kutoka huko?" Namouih akauliza.

"Nimepaa kwa ndege ndogo," Efraim Donald akajibu.

"Wow, kweli?" Blandina akauliza.

"Ndiyo. Kwa kawaida huwa zinawahi, ila niliyochukua leo sijui kwa nini ilinichelewesha kufika kwako," Efraim akamwambia Namouih.

Blandina akachekea kwa chini, naye Namouih akaendelea kumwangalia tu jamaa.

Efraim Donald akawakaribisha kwa mara nyingine tena, nao kwa pamoja wakaanza kupata chakula. Yalifata maongezi kuhusu sehemu ambayo Efraim Donald aliishi zamani mpaka anakua mkubwa, akisema familia yake iliishi maisha ya hali ya chini sana. Akawasimulia jinsi ambavyo alifanya kazi nyingi kwa bidii kwa muda mrefu sana bila kupata mafanikio, lakini mwisho wa siku Mungu akamwonyesha rehema na mambo yakamwendea vyema. Biashara alizokuwa ameanzisha ziliendelea kukua, naye akazidi kufanisika kadiri miaka ilivyosonga, hivyo kwa wakati huu alihitaji kuwa na mtu wa kufurahia naye maisha, ampe kila kitu atakacho, yaani amtendee kama malkia wake.

Blandina alipendezwa haraka sana na Efraim Donald, na hata Namouih alipendezwa na ufasaha katika njia ya kuzungumza ya mwanaume huyu. Efraim Donald akaanza pia kuwauliza kuhusu maisha yao wakiwa kama marafiki; jinsi walivyokutana na mambo waliyojionea. Blandina hasa ndiye aliyezungumza kwa niaba yake na Namouih, na mara kwa mara Efraim alishindwa kujizuia kumtazama sana Namouih, akionyesha wazi kwamba umakini wake ulikuwa kwa mwanamke huyu zaidi.

Wakiwa katikati ya mlo wao, Blandina akapigiwa simu, na baada ya kuongea na aliyempigia, akamwambia Namouih kwamba aliyempatia gari alihitaji alirudishe kwa kuwa alitaka kwenda sehemu, hivyo hii ingemaanisha angepaswa kuwaacha tu wawili hawa peke yao. Efraim Donald akamuuliza ikiwa huko alikohitaji kulirudisha gari ilikuwa mbali, naye Blandina akakubali. Akamwambia asubiri kwanza. Akatoa simu yake na kupiga namba fulani, kisha akasema tu "njoo" na kukata. Namouih na Blandina hawakuelewa alichokusudia kufanya mpaka mwanaume fulani mwenye mwili mkubwa alipofika hapo na kuwasalimu wanawake hawa, kisha akamkazia uangalifu Efraim.

Efraim Donald akawaeleza kwamba huyo alikuwa ni dereva wake, na bodyguard pia, aliyeitwa Suleiman, kisha akamwambia jamaa achukue gari, aende kule Blandina atakapokwenda, halafu atarudi naye. Yaani, atalifuata gari la Blandina mpaka kule atakapoliacha, halafu Blandina ataingia kwenye hili la Suleiman ili amrudishe huku na hivyo waendelee kuwa pamoja. Blandina akasema haikuwa na haja hasa kwa kuwa alihisi ingekuwa vyema kuwaacha wawili hawa peke yao, lakini Efraim Donald akasisitiza kwamba arudishwe tu, kwa sababu alifurahia uwepo wake pia. Jambo hili lilimfurahisha sana Namouih, ila hakuna aliyejua hilo.

Basi Blandina akaondoka na Suleiman baada ya hayo, akiwa ameichukua chupa moja ya Serengeti Lite kwa kuwa nyingine mbili alikuwa amezimaliza, akisema angepita nyumbani kuiweka huko kabisa ili baadaye aweze kuitumia. Efraim Donald alikuwa amemtania kwamba akirudi angekuta kreti linamsubiri, na kwa haraka ikawa wazi kwamba walizoeana upesi. Wakawa wamebaki wapendanao hapo, isipoeleweka vizuri ikiwa ni wapendanao tayari kwa sababu hata urafiki haukuwa umekita mizizi.

"Naona Blandina anakupenda sana," Efraim Donald akamsemesha.

"Ndiyo, ni mbali tulikotoka," Namouih akamwambia.

"Hakukuwahi kutokea zile za 'umenichukulia bwana wangu'?"

"Ahahahah... hapana. Mimi kwenye ku-date sikuwa active sana."

"Ila yeye?"

"Ni kipaumbele."

"Ahahahah... anaonekana anajua kujiachia. Inanifanya nikisie kwamba na wewe una hiyo side, na ninataka sana kuiona..."

"Ahah... hapana. Mimi sina fujo sana kaka'angu..."

"Niite Efraim..."

Namouih akatabasamu na kuangalia chini.

"Yaani unajua kiukweli bado ni ngumu kuamini kwamba uko nami now... niliisubiri siku hii kwa muda mrefu sana," Efraim akasema.

"Why?"

"Kwa sababu hakuna mtu mwingine aliyeiteka akili yangu namna ambavyo wewe ulifanikiwa kufanya..."

"Hiyo yote kwa sababu tu uliniona kwa conference... na penyewe hata sikumbuki ni conference gani hiyo..."

"No, siyo kwa sababu tu nilikuona. Ni kwa sababu moyo wangu ulikupenda sekunde hiyo hiyo niliyokuona. Yaani sikuacha kukutazama. Ilikuwa ni kama nimeona kitu fulani kigeni kabisa machoni pangu. Nilitaka kukujua. Nilitaka kukufata hata tu kukuuliza 'hey, hivi mbona kama nakufahamu? Tulishawahi kucheza makopo pamoja?'"

Namouih akatabasamu kidogo.

"Yeah... yaani nilitamani nikufate niseme chochote tu mradi niongee nawe, lakini nikakukosa kwa sababu ya kushughulika na mambo mengi. Sasa hivi ni kama siku hiyo imejirudia tena. Nahisi kupaa yaani," akasema Efraim Donald.

"Ahah... ni vizuri kujua wewe ni mwanaume unayeweza kuji-express. Nimependa hilo kuhusu wewe," Namouih akamwambia, lakini maneno hayo yalikuwa ya kumfurahisha tu jamaa siyo kwamba yeye alifurahia kuyasema.

"Najua bila shaka hivi siyo jinsi ulivyotazamia kuanzisha urafiki wa kimapenzi na mtu fulani, siyo?" Efraim akauliza.

"Kwa nini unauliza hivyo?" Namouih akauliza pia.

"Ni kwa sababu ya hali unazopitia..."

Namouih akabaki kumtazama tu.

"Baba anaendeleaje?" Efraim akauliza kwa kujali.

Namouih hakuwa ametegemea swali hilo, hivyo kwa sekunde chache akabaki kimya, kisha akauliza, "Umejuaje kuhusu..."

"Usijali my dear, usijali. Ninakuelewa vizuri sana. Magreth aliponipa namba yako aliniambia kwamba baba yako anaumwa sana, na ndiyo maana ulikuwa huku kwa kipindi hiki. Nilianza kujiuliza ikiwa ingekuwa busara kukufata kwa wakati huu, lakini nilishindwa kujizuia. Nataka tu kuwa karibu nawe angalau... kama kukupa faraja, na kwa jambo lolote litakalohitaji msaada, basi nipo hapa kwa ajili yako. Okay?" Efraim akaongea kwa kujali sana.

Namouih akabaki tu kumwangalia usoni, na mwanaume huyu akakishika kiganja chake kilichokuwa mezani kama kumpa faraja, kisha akasema ikiwa angependa kuzungumzia hali ya baba yake, basi yuko tayari kumsikiliza. Namouih akaanza kumwelezea tu kwa kifupi kuhusu tatizo la baba yake, akisema kwamba mwanzoni walifikiri alikuwa na ugonjwa wa kawaida tu ambao wangeweza kuupatia suluhisho la kawaida, lakini sasa walitambua kwamba alihitaji upasuaji wenye utaalamu na gharama ya juu kwa kuwa mzee wake alikuwa na saratani kwenye pafu lake. Akasema kwa hizi wiki kadhaa za nyuma yeye na familia yake wamekuwa wakijitahidi kumpatia msaada wa kitiba, lakini alikuwa akiendelea kudhoofika taratibu hasa kwa kuwa alikaa nayo kwa muda mrefu sana bila kujua.

"Kwa hiyo madaktari wakasema uwezekano wa yeye kupona upo kabisa?" Efraim Donald akamuuliza.

"Ndiyo, lakini ndiyo itahitaji mambo mengi ambayo kiukweli sijui ikiwa yatamsaidia au kumwongezea maumivu tu. Yaani mpaka naogopa," Namouih akaeleza kwa huzuni.

"Usiogope. Sikia. Ninataka sana kukusaidia Namouih... ninaomba tu uniruhusu nifanye hivyo..."

"Sitaki matatizo yangu kuwa mzigo kwako Efraim..."

"No, usiseme hivyo. Ninatamani, ninatamani sana kukuondolea jambo lolote lile linalokutatiza. Yaani Namouih sitaki na sitaki kukuona unaumia. Nitafanya kila kitu kwa ajili yako kukuonyesha jinsi gani ninavyokupenda Namouih..."

"Ahah... yaani... ki... kihivyo tu? Hata kama tuseme nyumba yetu ingeungua kwa...."

"Ningekununulia mbili zaidi," Efraim akamkatisha na kusema hivyo.

"Kwa nini? Kwa nini umenipenda mimi?" Namouih akamuuliza.

"Naweza kusema ni moyo tu. Moyo hauna hiyana," Efraim Donald akamwambia.

Namouih akatabasamu kidogo na kuangalia chini. "Sijui nisemeje... yaani... sikutegemea..."

"Njoo," Efraim akasema huku akisimama.

Namouih akamwangalia tu bila kuelewa alichomaanisha.

"Njoo nami, twende," Efraim Donald akamwambia.

Namouih akasimama na kuanza kumfata.

Walielekea mpaka ndani ya hoteli ile, nao wakafika mpaka kwenye chumba kimoja ghorofa ya tatu, naye Efraim Donald akaufungua mlango wake. Akamwambia aingie na asiwe na wasiwasi, naye Namouih akapita na kuingia ndani. Efraim Donald akaelekea mpaka kitanda kilipokuwa, na tayari Namouih alikuwa ameona kisanduku kidogo sana cha rangj ya samawati hapo. Efraim Donald akakichukua, kisha akamsogelea Namouih na kukifungua mbele yake. Namouih akabaki kuutazama tu mkufu mzuri sana aliouona hapo, kwa haraka akitambua ulikuwa wa gharama kubwa mno. Akamtazama tu Efraim usoni, kwa njia ya kawaida na si shauku.

"Ninataka ukiwa nami, kila kitu utakachotaka, na hata kama hujakiomba, ukipate kutoka kwangu. Nitaka kugeuza huzuni zako kuwa furaha Namouih, na lolote litakalokupa furaha niliongeze maradufu zaidi. Ninaomba tu uniruhusu niwe sehemu ya maisha yako," Efraim Donald akasema kwa hisia.

Namouih akatulia kidogo, kisha akauangalia mkufu huo tena. Efraim Donald akautoa kwenye kisanduku chake na kisha kuzungukia nyuma ya mwanamke huyu, naye akaupitisha shingoni mwake na kumvalisha akiwa kwa nyuma. Kulikuwa na kioo sehemu ya mwanzo ya kuta za chumba hiki, hivyo Efraim akamsogeza vizuri hapo na kumtazamisha jinsi alivyopendeza shingoni kwake. Kupitia kioo hicho, Namouih angeweza kumwona Efraim, jinsi alivyotabasamu kwa matarajio mengi, naye Namouih akatikisa tu kichwa chake, kuonyesha kwamba alikuwa amekubali kile Efraim Donald alichomwomba.

Mwanaume huyu alifurahi sana, naye akaugeuza mwili wa Namouih taratibu ili watazamane. Sura ya Namouih kiukweli bado ilionyesha kutokuwa na uhakika, lakini kuona jinsi ambavyo Efraim alifurahia sana kukamfanya tu atabasamu pia. Efraim Donald akaanza kuusogelea uso wake Namouih zaidi, akionyesha ni kama anataka kumbusu, naye Namouih akatulia tu bila kuonyesha itikio lolote lile. Efraim alipoukaribia mdomo wa Namouih, akatulia kidogo, kisha akaahirisha kumbusu na kuamua kumkumbatia tu. Hili wala halikumshangaza Namouih, bali kwa utulivu wake akaendelea kubaki ndani ya kumbatio la jamaa.

"Mimi na wewe, bado tuna safari ndefu. Sitachoka kusubiri mpaka moyo wako unikubali kwa asilimia zote. Always remember that. Nakupenda."

Maneno hayo yaliyosemwa kwa njia nzuri sana na Efraim Donald yalimtuliza sana Namouih, kwa kuwa ni kama alikuwa akisema yuko tayari kusubiri mpaka hisia za Namouih kumwelekea zikite mizizi zaidi, yaani ampende kama vile yeye anavyompenda. Kuamini mwanaume tena lilikuwa jambo fulani gumu kwake hasa kwa sababu aliwahi kupitia usaliti uliomuumiza sana, lakini kwa wakati huu angetakiwa kujitahidi kuonyesha yuko tayari kupenda pia, hasa kwa kuwa mwanaume huyu alionekana kuwa mtu mzuri sana.

Taratibu nwanamke huyu akaipitisha mikono yake mgongoni kwa Efraim Donald, akirudisha kumbatio lake pia, naye akafumba macho yake kwa hisia akiwaza mambo ambayo yangefuata baada ya kukubali ombi la mwanaume huyo.



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE Jumamosi na Jumapili ijayo. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 787 604 893

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA TANO

★★★★★★★★★★★★★★


Baada ya Namouih kuwa amemkubalia Efraim Donald, wawili hawa wakatoka ndani ya chumba hicho baada ya dakika hizo chache, wakiwa na lengo la kwenda kule nje kwa sababu Blandina alikuwa amekaribia kufika huku tena; akirejeshwa na Suleiman. Wakiwa ni wapenzi rasmi siku hiyo hiyo tu waliyokutana, Efraim Donald alimwambia Namouih kwamba alikuwa na mengi sana ya kumwonyesha kuhusu maisha yake yeye, na alitaka kujifunza mengi pia kuelekea maisha ya mwanamke huyu mrembo. Lakini kwanza, akamwambia jambo muhimu zaidi kwa wakati huu lingekuwa kumsaidia mzee Masoud, hivyo angekuwa naye bega kwa bega kwa kila jambo ambalo lingehitajika.

Walikuwa wameenda kuketi tena pale pale walipokuwa mwanzoni, Efraim Donald akiwa anamsemesha Namouih kuhusiana na mambo yaliyomfanya aweze angalau kutabasamu mpaka Blandina aliporejea hapo. Rafiki huyu akamshukuru Efraim Donald kwa ukarimu wake, akiuliza pia ikiwa gari ambalo Suleiman alitumia kumwendesha lilikuwa lake kabisa, lakini Efraim akasema alikodisha baada ya kufika huku kwa kuwa alikuja na ndege. Ilimpendeza sana Blandina kujua Efraim alikodisha gari aina ya V8, tena kutoka kwa wauzaji na siyo kwa mtu, ikionyesha pochi aliyokuwa nayo ilikuwa nzito hatari.

Baada ya sekunde kadhaa, Blandina akawa ameuona mkufu wa dhahabu aliokuwa amevaa rafiki yake shingoni, naye akaanza kumsifia sana akisema amependeza mno. Lakini akauliza alikuwa ameutoa wapi ndani ya muda huo mfupi, na ndiyo Efraim Donald akaingiza vidole vyake ndani ya kiganja cha Namouih na kusema kwamba walikuwa wapenzi sasa. Blandina akashangaa kiasi na kuuliza kiutani nini ambacho Namouih alikuwa amefanya ndani ya muda huo mfupi alioondoka kilichopeleka mambo baina ya wawili hao hatua nyingine, naye Namouih akacheka kidogo huku akimwangalia mpenzi wake mpya kwa hisia.

Efraim Donald akamwahidi Blandina zawadi nzuri sana kwa kuwa rafiki bora kwa Namouih, naye akachukua namba zake pia. Baada ya kuwa wazi kwa wote kwamba Efraim alijua kuhusu hali ya bwana Masoud, akawa amewaambia kwamba wangekwenda pamoja kesho hospitalini ili aweze kuongea na daktari kwa kina kuhusu mambo yaliyohitajika kwa ajili ya tiba yake, halafu pia kwamba angependa kujitambulisha kwa wazazi wa Namouih ikiwa ingemfaa. Ingawa Namouih bado alihitaji muda kumjua Efraim vizuri na kumzoea, alithamini utayari wake wa kutoa msaada mapema, na hivyo akakubaliana na hilo.

Kwa sababu alihitaji kurudi hospitalini, Namouih akasema yeye na Blandina wangeondoka sasa, hivyo angewasiliana na Efraim baadaye. Mwanaume huyo akamtia moyo mpenzi wake kwa mara nyingine tena, akisema yuko hapo kwa ajili yake kwa lolote lile atakalohitaji, na marafiki hao wa kike wakatazamana na kutabasamu. Efraim Donald akamwita Suleiman hapo na kumwambia awapeleke wanawake hawa walipotaka kwenda, na mwanaume huyo akatii na kutangulia kwenye gari huku Efraim, Namouih na Blandina wakifata nyuma yake taratibu. Efraim hata akatembea karibu na Namouih huku amekishika kiganja chake, akisema vitu vya utani vilivyofanya marafiki hao wawili wamfurahie sana.

Baada ya kuagana sasa na mchumba wake mtarajiwa, Namouih na Blandina wakapelekwa mpaka eneo lisilokuwa mbali sana na hospitali, kisha Suleiman akawaacha ili kurudi kule kwa Efraim Donald. Blandina alitaka kujua kila kitu kilichotokea alipoondoka muda ule mpaka kukuta tayari wawili hao wamekuwa wapenzi, naye Namouih akamwambia watafute sehemu ya kuketi ili wazungumze kwa ufupi. Wakaelekea kwenye eneo la wazi lenye mabenchi na uwanja wa kupumzikia kwa yeyote aliyetaka, kukiwa na watu kadhaa eneo hilo, nao wakaketi kwenye benchi moja lenye sehemu ya kuegamia na kuendeleza mazungumzo.

"Wacha! Akakuingiza na muchumba kukuvalisha necklace? Ikawaje?" Blandina akaendelea kuomba simulizi zaidi.

"Hakukuwa na mambo mengi... nikakubali tu ndiyo akanikumbatia," Namouih akasema.

"Hata kiss hamna?"

"Kiss ya nini?"

"Ish! Najua utakuwa ulikaza hilo lisura lako mpaka akaogopa kukupiga busu..."

"Na ndiyo lisura langu hili hili kalipenda sasa..."

"Ahahahah... dah, hii ni noma. Kiukweli Nam, ninajua kuna pressure kubwa sana kwako cause of this, lakini Donald anaonekana kuwa mtu mzuri sana. Jipe nafasi kwake... yaani, jiruhusu umpende pia. Eventually mambo yatakuwa mazuri especially kwa sababu ana pesa! Utakuwa na taabu gani mommy?"

"Ila wewe..."

"Ni kweli. Umeacha kuwaamini wanaume kwa kipindi kirefu sana, lakini siyo wote wako hivyo kama utakavyodhani. Usiishi kwa kuhofia tu kwamba vitu kama vya wakati uliopita vitakupata tena, sasa hivi ndiyo wakati wa kuijenga future yako kwenye upande wa mapenzi Namouih. Matatizo huwa yapo tu, lakini hata wewe unajua ajali huwa hazifanyi watu waache kuendesha magari. Kwa njia hiyo hiyo, usiogope kutengeneza kitu kizuri na Donald. Hebu jipe nafasi kwake honey," Blandina akaongea kwa kujali.

Namouih akainamisha uso wake huku akitabasamu kwa mbali na kusema, "Sijui ningefanya nini kama nisingekuwa na wewe kwenye maisha yangu Blandina."

"Ahah... always my friend. Wewe ndiyo dada yangu ambaye sikubarikiwa kumpata kwa tumbo moja," Blandina akasema.

Namouih akaangalia mbele na kusema, "Nitajitahidi. Efraim anaonekana kweli kuwa na moyo mzuri, lakini hakuna mwanaume mzuri kwa asilimia zote. Siyo kwamba nataka ukamilifu ila... bado tu sikuwa tayari. Nataka tu haya yote yaende vyema bila kuweka drama nyingi. Ni muda mrefu umepita sijawa kwenye mahusiano kwa hiyo... sijui kama nitamtendea haki..."

"Utaweza tu. Tena wewe hauhitaji hata kufanya lolote yaani, yule atakuwa anakupa kila kitu kabisa."

"Ni rahisi kuwaza hivyo kwa sasa ila inabidi kungoja tu kuona. Kilicho kwenye akili yangu zaidi kwa wakati huu ni baba... hata Sasha na Nasma pia," Namouih akasema.

"Halafu kweli... kuhusu Sasha. Hali ya yule binti imekaaje Namouih?" Blandina akauliza.

Namouih akashusha pumzi na kuanza kueleza. "Familia yetu kama unavyojua ina mgawanyiko kidini. Sisi tumefuata dini ya baba, na ijapokuwa mama alibadili jina lake kabisa lakini hajawa mwislamu kwa asilimia zote..."

"Ndiyo..."

"Yeah sasa, kuna kipindi fulani ilitokea kama... ugomvi kati ya baba na mama, na ingawa nilikuwa mdogo wakati huo niliweza kuelewa kwamba ilihusiana na tofauti zao ilipokuja kwenye suala la kidini, hasa kwa kuwa mimi nilifata upande wa baba badala ya upande wa mama kama alivyotaka. Kuna vitu alivyopenda mama ambavyo alitaka mimi pia nifurahie, lakini kwa misingi ya dini yetu havikuwa halali. Hiyo ilifanya wazinguane sana Blandina. Mambo mengine mengi yaliyoongezeka sijui sana lakini ilifikia kipindi mpaka wakatengana kwa muda mrefu..."

Blandina akaguna kwa kushangaa.

"Baba alienda kukaa mwenyewe sehemu nyingine, me nikabaki na mama. Mama... mama kama unavyojua siyo mtu wa kukaa sehemu moja... akawa anatoka na kijana mwingine, vile vile na baba pia... akaanza kutoka na mwanamke mwingine. Kwa mama ilikuwa kama fun tu, ila baba... inaonekana baba alimpenda huyo mwanamke aliyetoka naye kimapenzi. Huyo mwanamke aliitwa Sasha..."

Blandina akamwangalia kwa njia iliyoonyesha kwamba alielewa kule Namouih alikokuwa anaelekea.

"Yeah. Huyo mwanamke alipata ujauzito wa baba. Alipojifungua mtoto alipatwa na maumivu makali sana yaliyosababisha kifo chake siku 10 baada ya kujifungua, kwa sababu kuna sehemu nyingi ndani ya mfumo wake wa uzazi zilizoharibika vibaya. Huyo mtoto aliyezaliwa aliachwa na mama yake akiwa na siku 10 tu, ndiyo maana baba akamwita Sasha..."

"Masikini..." Blandina akasema kwa huzuni kiasi.

Namouih akaendelea kusema, "Ingekuwa ngumu kwa baba kumlea mtoto mdogo namna hiyo peke yake, kwa hiyo akamtafuta mama na kumwomba wasameheane kwa yaliyopita, ili amsaidie kumlea mtoto pamoja. Mama hakukataa. Alimlea Sasha kama binti yake wa kumzaa. Na anampenda. Ila sema tu... kuna mambo yalikuja kutokea baadaye yanayofanya anakuwa anamtendea jinsi ulivyoona anamtendea..."

"Ni nini kilitokea?"

"Nasri. Unafahamu kwamba mdogo wangu alikufa kwa kutafunwa na mnyama..."

"Ndiyo... uliniambia..."

"Well, wakati huo mimi nilikuwa chuo. Hiyo siku Baba na wengine wote walienda kutembelea wapi sijui... sehemu fulani ya kujivinjari, baba alikuwa ndiyo amerudi kutoka migodini huko kwa hiyo akawapa treat... hhh... Sasha alikuwa na miaka 10 wakati huo. Nasri 6. Si unajua michezo ya watoto wanaweza wakawa wanakmbia mara huku mara kule, kwa hiyo hata kama wangeenda mbali haikuonekana kuwa hatari kwa sababu mama alijua mtoto yuko na dada yake kwa hiyo...."

Namouih akaishia hapo tu na kubaki anatikisa kichwa kwa huzuni.

"Kwa hiyo... unataka kusema hilo janga lilipotokea, Sasha alikuwa pamoja na mdogo wako, lakini yeye akaokoka kifo. Kwa hiyo mama'ako anamlaumu Sasha kwa kilichompata Nasri, si ndiyo?" Blandina akasema kwa utambuzi.

"Alikuwa na miaka 10 tu Blandina. Na yeye alikuwa mtoto. Lile halikuwa jambo alilofikiria lingetokea yaani huwa sielewi ni kwa nini mama bado anamtendea vibaya kwa sababu hiyo... ni miaka mingi imepita... ah," Namouih akaongea kwa huzuni.

"Kama ujuavyo, uchungu wa mwana aujuaye...."

"Hata kama Blandina. Amemtendea vibaya sana tokea wakati huo, na mpaka kufikia kipindi hicho Sasha alikuwa hajui kama yeye siyo mtoto wake wa kumzaa lakini mama ndiyo akamwambia makusudi kabisa ili kumuumiza. Baba aliongea naye mara nyingi sana juu ya kumtendea Sasha bila heshima lakini hasikii. Sawa Nasri amekufa, kumtendea Sasha vibaya ndiyo kutamrudisha? Hizo kauli zake mbaya mbaya yaani Blandina nitahakikisha nazikomesha. Sikuwahi kuongea na mama juu ya hilo lakini niliona mengi, na yalinichukiza sana. Kwa hiyo ulivyoniambia amefanya vile leo nimeumia sana... yaani anamtendea mtoto bila ufikirio... eti anamwita muuaji...."

"Basi Namouih, basi..."

Blandina akaanza kumtuliza baada ya kuona kwamba Namouih alilemewa na hisia sana mpaka akawa karibu kulia tena.

"Inasikitisha sana. Lakini uko sahihi. Itakubidi uongee naye," Blandina akamwambia.

Namouih akajifuta machozi na kumwangalia.

"Hakuna mtu mwingine ambaye ataweza kuongea na mama yako vizuri kuhusu hili kama siyo wewe. Mwambie ajue anachokifanya siyo kizuri. Sasha anahitaji kuwa huru," Blandina akasema.

Namouih akatikisa kichwa kukubali ushauri huo, naye Blandina akavishika viganja vya rafiki yake na kuendelea kumtia moyo zaidi.

Dakika kadhaa kupita, wawili hao wakatoka sehemu hiyo na kurudi hospitalini hatimaye. Walikuta baadhi ya marafiki zake Masoud wakiwa wamefika kumpa pole, na wakati huu wadogo zake Namouih walikuwa wamesharudi nyumbani, akibaki Zakia pekee kumwangalia mumewe. Wakaendelea kukaa pamoja naye mpaka wakati ambao wengine waliondoka na kuwaacha Namouih, Blandina, pamoja na Zakia tu.

Namouih akaongea na baba yake. Akamwambia kwamba kesho alitaka kumtambulisha kwa mtu fulani muhimu sana, hivyo asishangae sana endapo angemleta mgeni huyo. Masoud alitaka kujua ni nani na kwa nini alikuwa dili kubwa sana, naye Namouih akasema angepaswa kutulia tu ili kesho ifike aweze kujionea. Zakia kama Zakia alikuwa ameshakisia kwamba inawezekana huyo mtu akawa ndiyo Donald, lakini alitaka kuhakikisha zaidi. Baada ya muda fulani mama huyo akawaambia wanadada kwamba yeye angebaki hapo usiku huo kuangalia mahitaji ya mume wake, hivyo wao wangeweza kwenda nyumbani tu.

Ilikuwa imeshafika usiku sasa, na ndiyo Namouih na Blandina wakamuaga mzee Masoud ili kwenda nyumbani. Wakati wakiwa wanaondoka, Zakia akawafuata na kuwasimamisha walipofika nje ya vyumba vya wodi, akisema anataka kuongea na binti yake mara moja. Blandina akamwambia Namouih anatangulia nje, hivyo akawaacha wawili hao sehemu hiyo. Namouih tayari alijua kile mama yake alichotaka kusema, kwa hiyo akatulia tu ili amsikilize.

"Huyo mgeni unayemleta kesho ni nani?" Zakia akauliza.

"Nimewaambia msubiri... mtamwona akija kesho," Namouih akasema.

"Si useme na we' naye... kwani ukiniambia atakufa?"

"Kwani nisipokwambia we' utakufa?"

"Namouih usiniletee nyodo. Haijalishi umekuwa mkubwa kiasi gani mimi bado ni mama yako, nikikuuliza swali nakuomba unipe jibu."

"Na wewe bado unaniona mimi kama mtoto wako? Basi naomba unipe jibu. Kwa nini bado unamtendea Sasha vibaya?"

"Nini?" Zakia akauliza kwa kutotambua swali hilo limetokea wapi ghafla.

"Bado hujaondoa kinyongo chako kisichokuwa na faida yoyote kwa huyo mtoto kwa nini?"

"Unaongelea nini... nani amekwambia... mbona me..."

"Mama nakujua vizuri. Na siyo kwamba nakuhukumu kwa sababu kila mtu ana mapungufu yake. Lakini unapoendelea kumtolea maneno makali Sasha, unamkandamiza sana. Mama huyu binti hastahili hayo, haikuwa makosa yake. Ninajua unaelewa nachomaanisha..." Namouih akasema kwa upole.

Zakia akabaki kumtazama tu kwa umakini.

Namouih akavishika viganja vyake Zakia na kusema, "Mama, wewe ni mtu mzuri, na unaweza kuwa mzazi bora zaidi kwetu. Ni suala la kukiondoa tu kinyongo chako kwa huyu mtoto, hakuna jambo lolote unalochukia juu yake ambalo ni makosa yake mama. Mliyopitia wewe na baba ni mengi, na wakati huu... sisi kama familia tunatakiwa kushikamana sana. Unaposema au kufanya vitu vinavyoumiza... unasababisha Sasha anaacha kukazia fikira mambo mazuri anayoweza kutimiza na badala yake anakuwa anajitenga... anajichukia. Mama tafadhali nakuomba. Usiwaze mengine. Sasha ni mtoto wako. Mtendee kama hivyo."

Zakia alikuwa ameachwa njia panda, akiwa hajategemea kabisa kwamba Namouih angeongelea jambo hilo muda huo, hivyo akabaki kimya tu kwa kutafakari maneno ya binti yake.

Namouih akaviachia viganja vya mama yake na kusema, "Ni huyo kaka uliyenitafutia ndiyo anakuja kesho. Usimwambie lolote baba mpaka mimi nimtambulishe kwake... sawa?"

Zakia alikuwa amekwishaishiwa pozi, lakini akafanikiwa kutikisa kichwa chake kwa njia ya kuonyesha ameelewa.

Namouih akageuka zake tu na kuanza kuelekea kule nje ambako alielewa Blandina alikuwa akimsubiri, huku akimwacha mama yake anafikiria vitu vingi sana. Hakuelewa ni kwa nini Namouih aliliongelea hilo wakati huu lakini alijua kile alichosema kilikuwa kweli kabisa, na ukweli huo ulimgusa sana moyoni. Akarudi tu kwa mume wake baada ya hapo.

★★

Namouih alikwenda nyumbani kwao pamoja na Blandina, nao wakapokelewa vyema na wadogo zake waliokuwa wametulia tu kutazama TV. Namouih akamsihi Blandina alale hapo kwa usiku huo, na rafiki yake huyo akakubali. Alikuwa anatania kuhusu namna ambavyo familia hii iliishi hapo kukiwa na wanawake tu kwa muda mrefu, yaani akionelea kwamba ni muhimu kuwepo mwanaume ili angalau kuwe na hali ya ulinzi, lakini Nasma akasema yeye ndiye aliyekuwa mlinzi wa wote hapo.

Baada ya kupata chakula pamoja na kuendelea kutulia ndani, Namouih akawa anaongea na Sasha kuhusu mambo yake binti, na kiukweli Sasha aliongea mambo mengi kwa uwazi mzuri sana kwa sababu alimzoea mno Namouih. Alizungumza kwa uchangamfu pia, na dada yake akamtia moyo aendelee kukomaa na masomo hasa kwa sababu mitihani ya kuhitimu kidato cha nne ilikuwa njiani. Vile vile na Nasma pia, ambaye alikuwa anakaribia kuanza mitihani ya darasa la tano, akatiwa moyo kusoma kwa bidii. Walikaa kupiga story na kuangalia vichekesho kwenye simu za Namouih na Blandina mpaka ulipofika wakati wa kwenda kujipumzisha, hasa baada ya Nasma kusinzia.

Mtoto wa kike akapelekwa chumbani kulala, akifuatwa na Sasha pia, kisha marafiki hawa wawili wakaendelea kukaa sebuleni kwa muda mrefu zaidi mpaka inafika saa saba usiku. Namouih akawa amemwambia Blandina kuhusu ile ishu ya mama yake, akisema alijitahidi kuongea kwa ufupi tu na kwa njia nzuri ili imguse moyoni, na kwa hilo Blandina akampongeza. Yalifuata maongezi kuhusu Efraim Donald, ambaye kwa muda wote ambao wawili hawa waliendelea kukaa sebuleni alikuwa anatumiana jumbe na Namouih zilizoonyesha upendo kwa mwanamke huyu. Alionekana kudata sana kwa Namouih mpaka Blandina akawa anasema kiutani kwamba wangemla hela mpaka zimwishie.

Basi, baada ya Namouih kutakiana usiku mwema na Efraim Donald kwenye simu, marafiki hao wakawa wameamua kwenda kulala, nao wakazima taa za sebuleni na kuingia chumbani. Wangelala kwenye chumba cha wazazi wa Namouih kilichokuwa na vitanda viwili, nao wakavua nguo walizokuwa nazo na kuvalia khanga kwa kuisitiri miili yao vizuri. Wakati Namouih alipokuwa amesogea dirishani ili kulifunika pazia vizuri, jambo fulani likavuta umakini wake kutokea nje ya dirisha hilo; kutokana na uwazi mdogo uliokuwa umeachwa na pazia. Akalisogeza pazia hilo kidogo sana na kuchungulia huko nje, na ndipo mapigo ya moyo wake yakaanza kukimbia kwa kasi kutokana na hofu fulani iliyomwingia.

Huko nje, kukiwa na sehemu zenye nyumba za hapa na pale za majirani na miti na vichaka kadhaa, aliweza kuona umbo la mtu aliyesimama gizani, tena kwa njia ile ile kabisa kama jinsi ambavyo alimwona mtu yule siku ya juzi wakati yuko mjini na Blandina mvua ilipoanza kunyesha. Lakini wakati huu mtu huyo aliweza kuonekana machoni, machoni tu, na ingawa ilikuwa kwa umbali fulani, Namouih angeweza kutambua kwamba macho yake yalikuwa yanamtazama yeye moja kwa moja, kana kwamba alikuwa ameona kwa uhakika kabisa sehemu hiyo ndogo sana ambayo Namouih alisogeza pazia.

Mwanamke huyu alishindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea, lakini jambo hilo lilianza kumwogopesha sana. Akiwa anataka kumhakikishia Blandina wakati huu kwamba alimwona mtu yule, akaamua kutoacha kumwangalia kabisa ili amwite rafiki yake hapo bila kumpoteza machoni mtu huyo kama ilivyokuwa juzi.

"Blandina... njoo... njoo haraka..."

Namouih akamwita kwa sauti ya chini sana, naye Blandina, aliyekuwa anajipaka mafuta ya kulainisha ngozi miguuni, akaona kwamba hapo kulikuwa na jambo fulani muhimu sana, hivyo akanyanyuka kutoka kitandani na kusogea alipokuwa mwenzake. Bado Namouih aliweza kumwona mtu yule asiyeeleweka alikuwa na shida gani, na baada ya Blandina kufika hapo akachungulia nje huko pia, wakati huu Namouih akipanua zaidi uwazi ule kwenye pazia ili kumruhusu mwenzake aone huko nje.

Blandina akamwangalia Namouih kiufupi, kisha akaangalia nje tena, halafu akamwangalia rafiki yake tena na kuuliza kwa sauti ya chini, "Nini?"

Namouih hakuwa ameacha kumtazama mtu huyo huko nje, naye akamwambia Blandina, "Angalia pale kwenye kona... ile nyumba ya ma' Gati."

Blandina akatazama huko tena kwa sekunde chache, kisha akasema, "Kwani kuna nini? Sioni chochote zaidi ya hiyo kona."

Namouih bado aliweza kumwona mtu yule pale, hivyo kauli ya Blandina ikamshangaza sana, na hofu yake ikazidi kupanda.

"Blandina acha masihara basi!" Namouih akasema hivyo huku akitazama macho ya mtu yule huko nje.

Blandina akamwangalia rafiki yake kwa kujali na kuuliza, "Tatizo nini Nam?"

Namouih akamwangalia rafiki yake kwa ufupi, na ile aliporudisha macho yake upande wa dirisha, mtu huyo aliyekuwa nje sasa akawa amesimama karibu kabisa na dirisha hilo, akimtazama Namouih kwa njia ya kikatili!

"Aaaah!"

Namouih akapiga kelele na kurudi nyuma kama vile amesukumwa mpaka akaanguka chini! Blandina alishtuka sana na kumfata hapo chini, akiuliza tatizo lilikuwa nini, lakini Namouih akaanza kurudi nyuma-nyuma mpaka alipoishia kwenye kabati la nguo za mama yake, huku akitazama dirishani kwa hofu. Blandina akamwacha chini hapo na kusogea dirishani tena, akaangalia nje kwa mara nyingine na kutoona jambo lolote lenye kutatiza, hivyo akalifunika pazia vizuri zaidi na kumfata rafiki yake hapo chini. Namouih alikuwa anapumua kwa presha, hivyo Blandina akakishika kichwa chake na kukikumbatia ili kumtuliza.

"Namouih... niambie umeona nini..."

Blandina akamwambia maneno hayo kwa sauti tulivu baada ya dakika chache kupita, na sasa Namouih alikuwa amefumba macho akijitahidi kurejesha utulivu.

"Nini kinaendelea Blandina?" Namouih akauliza baada ya sekunde chache.

Blandina akamwachia kichwani na kumwangalia usoni kwa ukaribu. "Nini? Niambie. Umeona nini?" akamuuliza.

"Yaani sielewi. Naota au? Hicho kilikuwa nini?" Namouih akaongea kwa kutatizika.

Blandina akaona ingekuwa vyema kumtoa hapo chini ili wakakae kitandani, naye akamsaidia Namouih kunyanyuka taratibu na kwenda kuketi hapo kitandani; Blandina akikaa karibu yake sana.

"Kulikuwa na kitu umeona hapo nje?" Blandina akauliza.

"Ndiyo. Nimeona... nimeona sijui ni mtu, sijui ni nini... oh Allah... this has to be a dream... nitaweza kulala kweli?" Namouih akasema kwa kughafilika.

"Nam niambie umeona nini... huyo mtu... wapi..."

"Unakumbuka juzi wakati... tuko nje mvua ikanyesha... nilikwambia utazame kule nilikoona mtu amesimama?"

"Ndiyo... nakumbuka. Ndiyo huyo uliyemwona sasa hivi tena?"

"Sijui kama ndiyo yeye au la, lakini alikuwa amesimama kwa njia ile ile kabisa. Nashangaa hujaweza kumwona. Nimekuangalia kidogo tu mara akawa ameshafika dirishani... eh Mungu wangu... nini hiki?" Namouih akazungumza kwa hisia.

"Mh... Namouih unaniogopesha..."

"Sikutanii Blandina..."

"Labda tusingechelewa kukaa mpaka sasa hivi... inawezekana wachawi wameanza yao..."

"Wananitaka nini mimi sasa? Niwaone mimi tu kwa nini? Utafikiri sina mambo ya kuwaza afu' hii mijitu inaanza kunisumbua akili... agh," Namouih akaongea kwa kuudhika na kusonya kwa hasira.

Blandina akawa anamtuliza kwa kuusugua mgongo wake taratibu, kisha akasema, "Vipi tukisali kwa pamoja?"

Namouih akatikisa kichwa kukubali, na marafiki hawa wakashikana viganja na kuanza kusali, lakini kila mmoja akisali kimoyomoyo kwa sababu ya dini kutofautiana. Baada ya hapo, Blandina akamwambia Namouih apande kitandani ili yeye aizime taa, kisha wangelala pamoja kitandani ili amsaidie rafiki yake kuituliza hofu yake. Akaenda na kuzima taa, kisha akapanda kitandani ambapo palikuwa pameshushiwa neti, halafu akaifunika miili yao kwa mashuka na kulala nyuma ya mwili wa Namouih akiwa kama amemkumbatia. Angalau jambo hili liliweza kumpa Namouih utulivu zaidi kutokana na hofu aliyoipata baada ya kuona jambo lile lisiloeleweka muda mfupi nyuma, na hatimaye usingizi ukawachukua warembo hawa kwa pamoja baada ya dakika chache.


★★★


Siku iliyofuata, ikiwa ni Jumapili ya mapumziko kwa wengi, Namouih na Blandina waliamka pamoja mida ya saa 2 na kuanza kujiandaa kwa kufanya mambo machache kwa ajili ya siku hii. Sasha alikuwa ameamka mapema sana na kufanya usafi wa nyumba pamoja na kuandaa chai, hivyo wakubwa wakafanya yao na kutulia kidogo kabla ya kuanza safari ya kuelekea hospitalini. Namouih alikuwa ameamka vizuri tu, na waliligusia suala lililotokea usiku wa kuamkia sasa kwa Sasha pia, aliyeshangaa na kusema pia kwamba lazima ilikuwa ni wachawi. Wakatania kuhusu jinsi ikiwa wangekuwa walokole namna ambavyo maombi yangepigwa mpaka asubuhi, wakiwaamsha majirani kwa sauti za juu kama namna ambavyo wanadini hao hufanya.

Basi, Blandina akiwa ndiyo msaidizi wa karibu wa Namouih, akawa amempa taarifa juu ya masuala fulani ya kikazi ambayo Namouih angehitaji kuyashughulikia upesi, kumaanisha kwamba hakuwa na muda mrefu wa kuendelea kukaa huku kwenye mkoa wao wa nyumbani; wangehitaji kurudi jijini kwao walikofanyia kazi ndani ya muda mfupi. Namouih akasema haikuwa na shida, na kwa sababu leo angetakiwa kushughulika na suala la Efraim Donald, akamwomba rafiki yake amsaidie kumpendezesha kiasi. Blandina alifurahi sana na kuanza kumpamba rafiki yake baada ya Namouih kumaliza kuoga.

Kuna kiwango fulani hivi cha msisimko uliomwingia Namouih kila mara ambapo Efraim Donald angemtumia ujumbe au Blandina kuanza kumwongelea vizuri, ikiwa wazi kwake sasa kwamba alikuwa ameanza kuufungua moyo wake kumwelekea pedeshee wake huyo, ingawa kwa asilimia ndogo sana. Akavaa gauni jeupe na refu lenye urembo wa maua, lililofunika sehemu kubwa ya mwili wake wote lakini kwa njia iliyoendana vizuri na umbo lake. Akaziachia nywele zake na Blandina kuzitengeneza kwa mtindo mzuri sana wa mikunjo-mikunjo (curls), huku akimwambia kwamba Zakia ndiye angeweza kumtengeneza vizuri hata zaidi kama angekuwa hapo. Namouih hakutaka kupendeza kupita kiasi, lakini hata kwa kiasi hicho kidogo ilionekana kama amepitiliza. Alikuwa mzuri mno.

Wote wakamaliza kujiandaa na kubeba yaliyohitajika kwa ajili ya kwenda nayo hospitalini, na ambaye angebaki hapo nyumbani ni Nasma kwa kuwa Sasha angeenda kubaki hospitalini na Zakia angerudi nyumbani kujiweka sawa kimwili. Walichukua usafiri kwa pamoja mpaka hospitalni, na Namouih akawa amewasiliana na Efraim Donald ambaye akasema hangekawia kufika huko, kwa hiyo Namouih awe tayari kwa ajili yake. Wanawake hao wakamkuta Zakia na mzee Masoud pamoja kwenye wodi, wakionekana kupata maongezi, naye Namouih akamuuliza mama yake kuhusu jambo lolote jipya lililosemwa na daktari. Hakukuwa na mengi yaliyohitajika kwa hapo zaidi ya uangalizi aliokuwa akipata mzee huyo, jambo la muhimu likiwa kumpa dawa na kutafuta njia ya kumfanyia upasuaji anaohitaji.

Haukupita muda mrefu sana Namouih akapigiwa simu na Efraim Donald, akimwambia kwamba tayari alikuwa hospitalini hapo, naye akaenda nje ili kumpokea. Alitoka nje ya jengo la hospitali lakini akiwa bado ndani ya uzio wa kulizunguka, naye akamwona Efraim akiwa amesimama usawa wa gari lake la V8 hapo. Alikuwa amevalia T-shirt nyeupe yenye mikono mirefu, suruali ya jeans na viatu vyeusi vilivyong'aa haswa. Mkononi alivaa saa yenye mwonekano wa dhahabu, naye alikuwa anamtazama Namouih baada ya kumwona mwanzoni mwa ngazi za kutokea kwenye jengo lile.

Namouih akataka kumfata hapo, lakini Efraim Donald akamwonyesha ishara kumwambia asimame tu; yeye ndiyo angemfata. Upepo ulipuliza nywele za Namouih na kufanya kiasi zimzibe usoni, naye akawa ametambua kwamba baadhi ya watu walimwangalia sana, lakini akawapuuzia na kuendelea kumsubiri mtu wake. Efraim Donald alipomfikia karibu, akamkumbatia moja kwa moja kabisa, naye Namouih akarudisha kumbatio lake na kuachia tabasamu la mbali, kisha wakaachiana na kuangaliana usoni.

"Najua siyo mahali pazuri sana kusema hivi but, you look stunning... umependeza sana," Efraim Donald akasema.

"Asante. Wewe pia," Namouih akamwambia.

"Mama na baba wote wako ndani eeh?" Efraim akauliza.

Namouih akatikisa kichwa kukubali.

"Okay, ni vizuri," Efraim akasema na kuangalia pembeni.

"Unaogopa?" Namouih akauliza kimasihara.

"What... ahah... hapana. Najiuliza tu kama wewe umeshakuwa na uhakika juu ya hili," Efraim akamwambia.

Namouih akabaki kumwangalia tu usoni.

Efraim Donald akamsogelea karibu zaidi na kusema, "Naomba ukumbuke jambo hili. Ninataka kufanya mambo yote kwa ajili yako kwa sababu nakupenda, na sitarajii uone labda muungano wetu kuwa kama malipo. Ninataka unipende pia. Kwa hiyo huu ni mwanzo tu, bado tuna mambo mengi ya kutimiza pamoja Nam-Nam."

Namouih akatabasamu kwa hisia sana na kutikisa kichwa chake kuonyesha amemwelewa.

"Okay. Twende," Namouih akasema.

Wawili hawa wakaongozana kuelekea ndani huku Efraim Donald akimwambia Namouih kuwa baada ya kumaliza kumtambulisha yeye kwa wazazi wake, angehitaji kuwa pamoja na Namouih wakati ambao angekwenda kuzungumza kwa undani na daktari aliyesimamia suala hilo la saratani ili apate mwanga zaidi wa mambo yaliyohitajika kufanywa. Namouih akakubali juu ya hilo, na wawili hawa wakawa wamefika sasa pale alipolazwa bwana Masoud. Zakia alimsalimu mwanaume huyu kwa shauku, akimkaribisha vizuri sana, naye Namouih akamtambulisha Sasha kwa Efraim pia. Kwa kuwa tayari jamaa alifahamiana na Blandina salamu yao ilijawa na tabasamu za furaha, na ndipo akasogea sasa kujitambulisha kwa mzee.

"Pole sana bwana Masoud kwa hali yako," Efraim Donald akamwambia.

"Asante," Masoud akaitikia.

"Mimi naitwa Efraim Donald..."

"Efraim... nafurahi kukujua. Ni wakati mbaya kukutana namna hii... ingekuwa vizuri hata kupeana mikono..." Masoud akaongea kivivu.

"Ahah... usijali mzee wangu. Utatoka hapa... na tutapeana mambo mengi zaidi ya mikono tu," Efraim akamwambia.

"Wewe ni mchungaji?" Masoud akauliza.

Wengine wakatabasamu kidogo, naye Efraim akamwangalia Namouih.

"Baba... Efraim ni... ni mchumba wangu," Namouih akasema.

"Mchumba?" Masoud akauliza.

"Ndiyo baba. Nimekuja kumtambulisha kwako...."

Masoud akaanza kukohoa kwa nguvu kiasi, na wanawake hapo wakajaribu kumtuliza.

"Pole... pole..." Sasha akawa anamwambia huku akiwa karibu yake.

"Samahani kijana wangu..." bwana Masoud akasema.

"Haina shida mzee wangu. Mchumba aliyeshuka tu ghafla na kufika hapa lazima ashangaze kidogo," Efraim akasema.

Masoud akacheka kidogo, na jambo hilo likafanya wengine watabasamu pia.

"Sawa Efraim. Namouih hajawahi kukuongelea kabisa maana ni... msiri mno... nafurahi kwamba amenitambulisha kwako," Masoud akasema.

"Mimi pia. Samahani sana kwa kuja ghafla... ila usijali, tutakuwa na mambo mengi sana ya kuzungumzia pamoja... wakati huo tukiwa tunaangalia na mechi za watani wa jadi," Efraim Donald akasema kiutani.

"Ahah... sawa. Una miaka mingapi kijana wangu?" Masoud akauliza.

"Thelathini na tisa," Efraim akajibu.

"Ahaa... sawa. Namouih..." mzee Masoud akaita.

"Bee... " Namouih akaitika.

"Umekua mama. Sasa hivi umeshapata na mchumba, utafunga ndoa, itakuwa jambo zuri sana. Natamani ningeishi muda mrefu vya kutosha kucheza na wajukuu wangu..."

"Masoud usiongee hivyo bwana... tena mbele ya mgeni siyo vizuri..." Zakia akamkatisha.

Namouih akawa ameingiwa na simanzi kiasi, hata Blandina alitambua hilo. Efraim Donald akasogea karibu yake na kuingiza kiganja chake kwenye kiganja cha Namouih, naye akampa ishara kwa kichwa iliyomwambia mwanamke huyu kwamba alimaanisha waondoke haraka kwenda kuongea na daktari. Akakubali, kisha akamwambia baba yake kwamba wanatoka mara moja kisha wangerudi muda si mrefu, naye bwana Masoud akakubali kwa njia iliyoonyesha uchovu wake mwingi.

Efraim Donald na Namouih wakaondoka hapo wakiwa pamoja na Zakia, na mwanaume huyu alikuwa akimtia moyo mama yake Namouih kwa kusema kwamba yeye na binti yake wangefanya kila kitu kusaidia hali ya mume wake, hivyo asiwe na msongo kabisa. Akamwambia kwamba wangehitaji kulishughulikia hili upesi sana ndiyo mambo mengine yafuate, hasa kwa kuwa hawakutumia muda mwingi kuweza kujuana vizuri, naye Zakia akamshukuru sana kwa hilo. Mama ya mrembo wetu akarudi kwa mumewe, akiwaacha wawili hao wanaelekea kumwona daktari. Walihitaji kusubiri kwa muda fulani kabla ya kuonana naye, ndipo wakaingia ofisini kwake ili kuweza kupata maelezo muhimu kuhusu mzee Masoud.

"Naitwa Efraim Donald," mwanaume akajitambulisha kwa daktari.

"Okay. Niite Doctor Sunil. Wewe ni mmoja wa familia hii?" daktari akauliza, akiwa ni mwanaume mtu mzima na mhindi pia.

"Ni mchumba wangu," Namouih akajibu.

Efraim Donald akakishika kiganja cha Namouih kwa kufurahi kusikia amesema hivyo ingawa hawakuwa wachumba rasmi.

"Ooh... okay sawa. Hali ya mgonjwa wenu bwana iko kama nilivyokwambia mwanzo... inaendelea, na itaendelea kuwa mbaya kwake kadiri siku zinavyosonga endapo kama hatapata matibabu sahihi..." daktari Sunil akasema.

"Doctor... nahitaji unielezee vizuri kila kitu kinachompata mzee wetu, na option zote best zilizopo ili kumpa msaada utakaofaa... specifics," Efraim Donald akamwambia daktari.

"Saratani aliyonayo imesababishwa na yeye kuvuta gesi ya radon. Hii hutoka kwenye chembe ndogo ndogo za kitu kinachoitwa uranium, ambacho huwa kipo ndani ya mawe-mawe yenye kutoa vumbi... na ikivutwa kwa muda mrefu ndiyo kama hivyo, huathiri au kuyaharibu kabisa mapafu. Tulipompiga X-ray na CT scan kweli tuliona ana cancer, na ili kujua aina ya matibabu yatakayomfaa tukafanya vipimo kwa njia ya PET-CT scan. Mzee Masoud ana saratani stage 3A ya mapafu, na imeathiri pafu lake lote la kulia. Najua kutokea mwanzo tumewaambia kwamba atahitaji upasuaji, lakini sasa hivi saratani yake imetanuka zaidi, na hiyo inamaanisha mtapaswa kufanya uchaguzi wa matibabu ambayo mtaona yanafaa kwa huyu mzee ili apatiwe..." daktari huyo akaeleza.

"Unamaanisha nini doctor?" Namouih akauliza.

"Matibabu ya kawaida huwa yanasaidia kuua seli za saratani kutokea pale zinapoanzia, yaani kwenye kiini chake. Upasuaji na huduma ya radiotherapy ndiyo matibabu ya kawaida. Lakini matibabu ya kutumia mifumo ya ndani zaidi huziua seli hizo popote zilipo ndani ya mapafu au hata zikiwa zimeshaanza kusambaa mwilini. Hizo ni kama chemotherapy, immunotherapy na zingine. Wakati mwingine radiotherapy na chemotherapy huunganishwa ili kuleta matokeo mazuri zaidi baada ya upasuaji kufanyika..."

"Mm-hmm..." Namouih akaguna kwa njia ya kumaanisha daktari aendelee.

"Stage ya kwanza mpaka 3A ya saratani ya mapafu zinaweza kutibiwa kwa upasuaji, lakini kuanzia stage 3b mpaka 4 huwa wanatumia muunganiko kwa radiotherapy na chemotherapy pia kwa sababu upasuaji pekee hauwezi kusaidia level hizo za saratani. Yeye ana 3A, lakini kutokana na muda ambao mzee huyu ameishi nayo, itabidi, kama akipata upasuaji, uunganishwe na huduma ya radiotherapy au chemotherapy..."

"Mwili wake una uimara wa kutosha ku-handle aina yoyote ya upasuaji... au hizo therapy?" akauliza Efraim Donald.

"Ndiyo, naweza kusema ana nguvu sana kwa sababu angetakiwa hata kuwa ameshafika stage 4 lakini mwili wake ulikuwa unapambana nayo sana... sema ni umri tu. Kwa hali yake, mkiamua kumpa upasuaji wa kawaida, basi inatakiwa kuwa moja kati ya njia hizi: lobectomy au pneumonectomy. Kwenye lobectomy, sehemu kubwa ndani ya pafu lake iliyoathiriwa na saratani itaondolewa, hasa kwa sababu ya kwake imo ndani ya pafu moja. Na kwenye pneumonectomy... pafu lote litaondolewa," daktari akasema.

"Pafu lote?!" Namouih akasema kwa mshangao.

"Ndiyo, naelewa unawaza ikiwa baba yako ataweza kuendelea kupumua akibaki na pafu moja lakini usijali... inawezekana kupumua vizuri hata ukiwa na pafu moja tu. Kwa hiyo... hivyo ndivyo hali ilivyo," daktari Sunil akawaambia.

"Asante doctor kwa kutuelezea hayo. Tunataka kutumia njia bora zaidi itakayomsaidia. Upasuaji kama ulivyosema... ninaona kutakuwa na risk. Sidhani kama kuna nyenzo nzuri sana kwenye hospitali hii au yoyote itakayohakikisha ushindi... kumradhi lakini," Efraim Donald akamwambia.

"Ndiyo uko sahihi. Kiukweli... itahitajika apelekwe kabisa nje ya nchi kwenye hospitali iliyo na wataalamu wengi zaidi... huku kuna limit," daktari akaongea.

"Ahh... doctor yaani ndiyo unatuambia hayo sasa hivi?" Namouih akashangaa.

"Haingefika huku ikiwa asingekaa kwa muda mrefu hospitalini. Ingawa dawa anazopata zinasaidia lakini siyo kwa kasi inayotakiwa kusaidia apate matokeo mazuri kama angefanyiwa upasuaji wa cancer yake huku huku. Samahani sana kwa hilo dada," daktari Sunil akamwambia.

Namouih akafumba macho na kutikisa kichwa kwa kusikitika.

"Doctor... ninaomba mfanye mipango yote itakayohitajika kumtoa hapa na kumpeleka kwenye hospitali ambayo atapata matibabu hayo haraka sana," Efraim Donald akasema.

Namouih akamtazama usoni.

"Unamaanisha... nje ya nchi?" daktari Sunil akauliza.

"Ndiyo. Wapi itakapokuwa sehemu nzuri zaidi kumpeleka?" Efraim akamuuliza.

"The best option naweza kusema London... Ulaya," daktari akajibu.

"Okay. Ninaomba taratibu zianze kufanywa haraka. Tutagharamia kila kitu huku, na kitakachohitajika huko," Efraim akasema.

Daktari akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa, kisha akaanza kumpanga Efraim Donald kuhusu mambo ambayo yangefanyika ili kukamilisha hilo suala.

Namouih bado alikuwa anamtazama sana Efraim, asiamini kama kweli mwanaume huyo angejitoa kugharamia kila kitu kilichohitajika kwa ajili ya matibabu ya baba yake mpaka nje ya nchi. Mwanzoni lilikuwa jambo la kawaida tu kwa sababu alidhani kwamba matibabu ya baba yake yangefanyikia hapa hapa nchini, lakini mpaka nje ya nchi ingekuwa jambo zito na la gharama sana. Alihisi furaha iliyoambatana na mshangao kwa kutotegemea kabisa kwamba mwanaume huyu aliyemjua kwa siku mbili tu alikuwa anafanya haya yote kumwonyesha anampenda kwa dhati, na kiukweli aliguswa sana moyoni na kitendo hiki cha Efraim.

Efraim Donald alipomwangalia Namouih usoni, akakuta anatazamwa kwa njia yenye kuonyesha hisia nyingi sana za shukrani karibu machozi yamtoke mwanamke huyo, na mwanaume huyu akatabasamu na kumwonyesha ishara kwa kufumba macho kwamba asijali, kila jambo lingekwenda vizuri kabisa. Namouih akatabasamu kwa hisia sana, akiviunganisha viganja vyake vyote kwenye viganja vya Efraim Donald, na baada ya hapo wakatoka kwa pamoja kwenda kushughulika na mambo mengi waliyoambiwa na daktari.



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 787 604 893

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+


Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA SITA

★★★★★★★★★★★★★★


Maandalizi ya kumwondoa bwana Masoud kutoka hospitalini yakaanza haraka sana kwa madaktari kuhakikisha anasafirishwa kutoka hospitalini kwa usalama. Efraim Donald akiwa sambamba na Namouih alishughulikia mambo yaliyohusiana na gharama za usafiri, vitambulisho vya kuhama nchi, gharama ya huduma ambazo mzee huyo angepokea kutoka huku mpaka kule London kwa muda WOTE ambao angepokea matibabu hayo mpaka wakati ambapo angetakiwa kurudi tena nyumbani. Huyu mtu alikuwa na hela sana, na njia aliyozitumia ilionyesha kweli alikuwa na pendo kuu kumwelekea Namouih.

Ilkuja kwa kumshangaza kiasi bwana Masoud baada ya kuambiwa kwamba angepelekwa nje ya nchi ili kupata matibabu, lakini alijitahidi kuwa mtulivu na kutouliza mengi sana. Alijulishwa kwamba angepelekwa London ndani ya siku tatu tu, hivyo kwa muda huo watu wake wa familia wangehitaji kuwa karibu naye zaidi kabla ya kumuaga. Zakia alikuwa na furaha sana, kwa sababu Efraim Donald ndiyo alikuwa kila kitu ambacho sikuzote alitazamia binti yake angechagua kuwa nacho maishani. Mwanaume huyo aliwatendea kwa fadhili na upendo sana mpaka ingekuwa rahisi kwa yeyote kufikiri kwamba alijuana na familia hii kwa muda mrefu.

Sasa ikiwa imebaki siku moja tu kabla ya bwana Masoud kupaishwa kwa ndege, Efraim Donald alikuwa ametoka pamoja na Blandina, Zakia, na Nasma kwenda sehemu fulani kupata kama mjumuiko wa pamoja kisha ndiyo waende tena hospitali, hiyo yote ikiwa mwanzo wa kufahamiana vizuri. Aliwapeleka sehemu nzuri sana na hata kumnunulia Nasma na Zakia vitu vizuri, nao wakazidi kumpenda. Ni Namouih na Sasha ndiyo waliokuwa hospitalini wakati huo pamoja na baba yao, na sasa mzee Masoud akawa amepata nafasi nzuri ya kuzungumza na binti yake mkubwa bila uwepo wa wengine hapo.

"Sasha..." Masoud akaita.

Sasha alikuwa ameketi pembeni yake, naye akaitika, "Bee..."

"Naomba kuongea na dada yako mara moja..." Masoud akasema.

"Sawa baba..." Sasha akajibu.

Binti akanyanyuka na kuondoka sehemu hiyo, naye Namouih, aliyekuwa pembeni pia, akawa anamwangalia baba yake kwa umakini.

"Vipi baba... unataka kuniambia nini?" Namouih akamuuliza.

"Namouih... unafanya nini?" Masoud akauliza.

Namouih akatulia kidogo, kisha akauliza, "Unamaanisha nini?"

"Huyu mwanaume uliyempata ghafla-ghafla tu... mara ni mchumba wako... mara kidogo sijui naenda Marekani, sijui wapi... Namouih..."

"Baba..."

"Nilikuwa sijasema chochote kabla lakini mimi siyo mjinga. Ninakujua vizuri wewe mtoto. Unajiharibia... maisha yako kutafuta suluhisho kwa jambo lisilokuwa na faida... kwa nini?"

"Baba usirudie tena kusema hivyo. Maisha yako yana faida mara mia zaidi kuliko yangu..."

"Kwa ajili gani? Namouih... umeamua kutafuta tu mwanaume mwenye pesa bila kumjua vizuri ili.... akikunyima furaha je? Akikugeuza kuwa mtumwa wake je? Si uliniahidi usingefanya jambo lolote la kipuuzi... hivi ni nini lakini...."

Namouih akakishika kiganja chake na kusema, "Baba... usijali. Efraim namjua. Ni mchumba wangu. Usiwaze hayo kabisa. Cha muhimu zaidi wakati huu ni wewe kwenda...."

Maneno ya Namouih yakakatishwa baada ya Masoud kukitoa kiganja chake kutoka mkononi kwa binti yake. Alionyesha kukwazika sana, na jambo hilo likamwacha Namouih bila amani moyoni. Alipomwambia Blandina kwamba alitaka mambo yaende vizuri bila kuwepo kwa drama nyingi alimaanisha kama hivi, isipokuwa tu haya hayakuwa maigizo kutoka kwa baba yake; alijua amemkwaza kiukweli. Lakini akijua kabisa kwamba alifanya haya yote ili kumwokoa, ikampa nguvu ya kujihakikishia kwamba alikuwa sahihi hata kama baba yake hakupenda.

"Maamuzi nayochukua siyo kwa sababu za kibinafsi baba. Ninakupenda, na ninahitaji uendelee kuishi kwa sababu bado sisi wote tunakuhitaji. Usiwaze kuhusu mimi... Efraim ni mwanaume mzuri sana... ananipenda," Namouih akasema.

"Efraim Donald. Inamaanisha yeye ni mkristo... umemzoa tu huko wapi sijui unamleta eti mchumba wako... Namouih, umeshafikiria kuhusu tofauti mtakazokuwa nazo kwa sababu hiyo? Unaelewa kwamba mama yako na mimi tulitibuana mpaka ikawa shida kubwa kwa saba...."

"Baba... tafadhali acha kufikiria hivyo. Siku hizi hakuna hayo mambo sana, haijalishi dini wala nini, kikubwa ni kwamba watu wamependana na wako tayari kuwa pamoja," Namouih akamwambia.

"Unampenda huyo mwanaume Namouih?" mzee Masoud akauliza.

Namouih akabaki kimya tu na kubaki kumwangalia baba yake.

"Najua siwezi kukuamulia namna ya kuendesha maisha yako. Lakini ikiwa utaingia kwenye mikazo kwa sababu hii itakuwa ni kama mimi ndiyo nimesababisha hilo. Sijui ni kwa nini una king'ang'anizi sana we' mtoto. Nakuombea tu mazuri binti yangu, na inanifariji kuona jinsi unavyopambana kunisaidia. Ninataka tu uwe na furaha," Masoud akasema.

Namouih akakishika kiganja chake tena na kusema, "Usijali baba. Niko mwangalifu. Na huyu mwanaume sijamzoa kokote tu, ametokea mbali pamoja nami. Nachohitaji tu kwa wakati huu ni wewe kuniahidi kwamba utapambana kwenye mambo yote watakayokufanyia huko ili afya yako irudi kuwa nzuri zaidi. Niahidi."

Mzee Masoud akatabasamu na kufumba macho kwa njia iliyoonyesha kwamba amekubali kutoa ahadi hiyo.

Namouih akalaza kichwa chake karibu na bega la baba yake huku akimwimbia wimbo kwa sauti ya chini na kwa upendo sana, kama tu baba yake alivyopenda. Baada ya muda mfupi, Efraim Donald na wengine wakawa wamefika hapo na kujiunga nao, wakipata mazungumzo mengi na kutumia muda mwingi pamoja na mzee wao mpaka muda ambao wangetakiwa kumwacha. Efraim Donald akamwahidi Namouih na wadogo zake kuwa baada ya kumsafirisha baba yao wangetumia muda mwingi kutembelea maeneo mengi ambayo wangefurahia sana, hasa ukifika wakati ambao watoto wangepumzika kimasomo.


★★★


Hatimaye ilifika siku ambayo bwana Masoud alipanda ndege na kupelekwa nchini London kwa ajili ya matibabu yake. Wanafamilia na marafiki zake wengi walimuaga, na Nasma alilia sana kwa kuwa alijua baba yake alikuwa anapelekwa mbali. Masoud angekuwa chini ya uangalizi maalumu wa timu ya madaktari na wauguzi kwa muda wote ambao angekaa London, hivyo hakukuwa na haja ya yeyote kati ya watu wake wa familia kwenda huko kwa kuwa Efraim alihakikiaha kila jambo limepangiliwa vyema.

Kutokea wakati huo, Namouih na Blandina walirudi jijini kwao walikofanyia kazi, na ni huko huko ndiko Efraim Donald alitokea. Kwa hiyo mwanaume huyu alianza kumfanyia vitu vizuri Namouih kama kumpeleka matembezi, kupata milo kwenye sehemu za kifahari na kumnunulia vitu vingi vya gharama. Ingawa Namouih hakuwa aina ya mwanamke aliyehitaji mwanaume tu ndiyo amfanyie kila kitu, alivutiwa na jinsi ambavyo Efraim alijitoa kwake, naye akaendelea kujitahidi kumwingiza zaidi moyoni taratibu. Efraim Donald hata aliiboresha zaidi nyumba ya Masoud na Zakia, na alishiriki mambo mengi na mama yake Namouih hasa baada ya kumzoea kutokana na mwanamke huyo kupenda vitu vizuri-vizuri, au kwa maneno mengine, pesa.

Ikafika wakati ambao Efraim Donald alimpeleka Namouih kumwona mama yake mzazi. Aliishi mkoa mwingine tofauti na jiji hilo, naye aliitwa Halima. Mara ya kwanza kumwona Namouih, Halima alimsifia sana na kumkaribisha kwa upendo, akikazia kwa mwanaye kwamba angepaswa kumuoa mwanamke huyu haraka sana. Ndugu zake Efraim Donald walimpokea vizuri pia, na hawakuwa wengi sana mara hiyo ya kwanza kumfikisha Namouih kwao. Akiwa huku, Namouih alipata kusikia mambo fulani kuhusu familia ya Efraim Donald ambayo yalichukiza sana. Kuna ile hali fulani mtaani unakuta kwamba mtu alikuwa na maisha ya chini halafu akaja kutajirika, hivyo maneno ya wivu au fitina huwa hayakosekani, na hata Namouih aliweza kuyasikia lakini akaona ayapuuzie kwa kutojali wafitini.

Mpaka kufikia wakati huu, Namouih hakuwa amewahi kushiriki mwili wake na mwanaume huyo, kwa sababu ilikuwa wazi kwamba Efraim Donald bado alikuwa anamsubiria azielekeze hisia zake kwake kwa asilimia zote kama alivyomwahidi. Hii ilionyesha mwanaume huyu alikuwa na subira, na ni kitu kilichompendeza Namouih. Baadaye mwanamke huyu akarejea tena kazini. Alikuwa akipata taarifa kwamba hali ya mzee Masoud huko London iko kawaida (stable) baada ya taratibu za upasuaji wa mwanzo kwenda vizuri, kwa hiyo lilikuwa ni suala la muda tu na mambo mengine yangejulikana baada ya upasuaji wote kukamilika.

Baada ya Sasha na Nasma kuwa wamefunga masomo yao, Efraim Donald aliwachukua wote pamoja na Zakia kwa ajili ya kwenda kutembelea jijini kwao kama alivyosema kipindi kile wako hospitalini. Na akawatembeza kweli kweli. Wakati huu Namouih alikuwa akiendelea kusifika kuwa mwanasheria mzuri sana sambamba na rafiki yake, Blandina, naye alijiunga nao katika matembezi kila wakati alipopata nafasi. Efraim aliwapeleka ufukweni, kwenye mahoteli, kwenye kampuni yake, na nyumbani kwake pia; ile ile nyumba kubwa. Wakiwa hapo kwake ndiyo mwanaume huyo akatoa tangazo dogo la kutotarajiwa la kumvisha Namouih pete ya uchumba, naye akaikubali, Walifurahia sana siku hiyo, na Efraim Donald akasema asingechelewa hata kidogo kumuoa mwanamke huyu mzuri.

Efraim Donald kama kawaida alikuwa mtu wa safari za hapa na pale, lakini kila nafasi aliyopata ya kuwa jijini alijitahidi kumwonyesha upendo malkia wake kwa kumtoa matembezi, kumtambulisha kwa rafiki zake wengi, au kumnunulia zawadi. Blandina angemtania mara nyingi Namouih kwamba alitakiwa kujiandaa kwa ajili ya siku ya kumpa mwanaume huyo zawadi yake tamu, na kweli Namouih alikuwa ameshafikiria kuhusu hilo hasa kwa kuwa alikuwa ameshamzoea Efraim Donald, siyo kama mchumba kwake tu, bali kama rafiki wa muhimu sana.


★★★


Siku moja, Efraim Donald alimpeleka Namouih kwake, pale kwenye nyumba yake. Walipata mlo na maongezi, na kilichozungumziwa hasa ilikuwa ni kuhusiana na mipango ya ndoa yao. Kwa sababu ya dini kutofautiana, wote walielewa kwamba wangetakiwa kufunga ndoa kwa njia ya maandishi, yaani ndoa ya kiserikali, lakini bado Efraim alitaka sherehe ya ndoa yao iwe kubwa kupita maelezo, kwa hiyo alikuwa anapanga vitu vingi sana vya kumfanyia mrembo wake kumwonyesha jinsi alivyo wa pekee. Wakahamishia makao yao kutoka chini sebuleni na kwenda mpaka chumbani kwake Efraim, wote wakiwa na hisia nzuri sana kuelekeana na wakielewa kule ambako jambo hilo lingewafikisha.

Ilikuwa ni usiku, na Namouih alikuwa amevalia gauni fulani refu la blue lenye kuvutika na mwonekano mzito kama limelowana kwa maji, hivyo lilimbana kwa njia fulani iliyoonyesha umbo lake vyema na hasa kumchoresha nyuma vizuri sana; yaani endapo angetembea palikuwa ni mtikisiko tu. Alikuwa amezibana nywele zake kwa nyuma, huku usoni mwake akiwa amejiremba kwa kadiri, naye akasimama usawa wa kitanda kikubwa cha humo ndani akikiangalia kama vile anakitathmini. Akahisi pale ambapo Efraim Donald alimgusa kutokea nyuma yake, halafu mwanaume huyo akaibusu shingo yake taratibu.

"Napendaga unavyonukia mpenzi wangu," Efraim Donald akamwambia.

Namouih alikuwa ameanza kupandwa na hisia nyingi sana za kimahaba, lakini kwa sababu fulani, akawa anajitahidi kuzizima ili zisipitilize. Akapiga hatua nyingine mbele na kukaa kitandani, ikiwa ni kama vile amemkwepa Efraim, lakini akamtazama machoni kwa hisia.

"Sikuwahi kukuuliza. Umeshaleta wanawake wangapi hapa?" Namouih akauliza.

Efraim Donald akatabasamu na kusema, "Umechagua wakati mzuri sana kuuliza hilo swali."

Namouih akatabasamu pia.

Efraim Donald akamsogelea na kukaa naye kitandani, kisha akasema, "Sijawa na wanawake wengi sana. Maisha niliyokuwa nayo mwanzoni yalinifanya nionekane kama siwezi kummudu mwanamke, na mimi kiukweli sikuwa mtu wa kuwaza sana wanawake. Hata Mungu alipokuja kunisaidia kupata hivi vyote... nilikuwa nimezama zaidi kwenye kuboresha maisha yangu na ya familia yangu kwanza... hasa mama. Alikuwa amepitia shida nyingi mno. Kwa hiyo nilipotulia kidogo ndiyo nikaona nikutafute wewe ili nitulie zaidi."

Efraim alikuwa anasema hayo huku anasugua kiuno cha Namouih taratibu kutokea kwa nyuma, naye Namouih akatabasamu.

"Kwa hiyo sijui kama utaniamini nikikwambia kwamba sijawahi kulala na mwanamke yeyote kwenye hiki kitanda?" Efraim Donald akasema.

"Mmm... kweli?" Namouih akauliza.

"Ahahah... nataka wewe ndiyo uwe wa kwanza, na wa mwisho," Efraim akasema.

Namouih akaangalia chini kwa hisia, kisha akamtazama tena machoni.

Efraim Donald akaupandisha mkono wake uliokuwa kiunoni kwa mwanamke huyo mpaka nyuma ya shingo yake, kisha akakivuta kibanio kidogo cha nywele kilichozishikilia nywele za mrembo, nazo zikamwagika. Akazilaza upande mmoja wa bega la Namouih, halafu akamfata mdomoni na kuanza kumpiga denda taratibu. Midomo ya Namouih ilikuwa laini sana, na ulimi wake ulikuwa na ladha tamu sana iliyofanya Efraim apandishe mzuka hata zaidi. Akaanza kumtomasa kidogo sehemu ya titi lake la kulia, huku bado akimnyonya mdomo, kisha akaanza kumsukumia kitandani taratibu ili alalie mgongo. Namouih alikuwa ameshaanza kuguna kwa sauti ya chini baada ya hamu yake kuongezeka sana, naye Efraim akaanza kuivuta sehemu ya begani ya nguo ya mwanamke huyo ili ayafichue matiti yake.

Sehemu ya gauni la Namouih iliyofunika bega lake ilipovutwa chini, ilifanya sidiria aliyovaa ionekane zaidi, naye Efraim akawa analisugua titi la Namouih likiwa bado ndani ya sidiria hiyo. Alipotaka tu kulitoa ndani ya sidiria, Namouih akamshika pande za mikono yake kwa njia ya kumzuia, naye Efraim akajitoa mdomoni mwake na kumtazama kwa ufupi. Namouih akawa anamwangalia kwa njia legevu, kisha akajinyanyua na kuketi kama awali. Efraim bado alikuwa amelalia ubavu wake huku akimwangalia kwa hisia, naye Namouih akaanza kupandisha gauni lake juu ya mkono wake tena.

"Vipi?" Efraim akauliza.

Namouih akabaki kimya tu, akiinamisha uso wake kama vile kuonyesha kuna kitu kinamsumbua.

Efraim akaona akae pia, lakini wakati huu akiwa karibu zaidi na uso wa mwanamke huyu, kisha akauliza, "Uko sawa?"

Namouih akatikisa kichwa kukanusha na kusema, "Am sorry."

"Niambie tatizo nini Namouih. Kuna sehemu yoyote hujapenda nilipo...."

"No, siyo hivyo. Yaani... hhh... nisamehe Efraim... nina... sijui hata nikuelezeeje..."

Efraim akaishika shingo ya Namouih kwa wororo na kuanza kuzilaza-laza nywele zake.

"Sijawa ndani ya mahusiano kwa muda mrefu mpaka nilipokuja kukutana nawe... na hiyo ni kwa sababu kuna jambo fulani lilinipata kipindi cha nyuma lililosababisha niache... au niseme... niwachukie wanaume. Kuna mwanaume nilimpenda sana wakati nasoma chuo. Nilimpa kila kitu Efraim. Baadaye nikagundua kwamba... kila mara tulipofanya mapenzi... alikuwa anachukua video zetu... anawaonyesha watu wengine kabisa. Unajua ingekuwa bora kama nisingejua, lakini kilichoniumiza ni kwamba baada ya kumweleza kuwa sikupenda jambo hilo... akanitolea maneno machafu... kashifa nyingi sana... yaani ilikuwa ni kama vile sikumjua au.... hakunijua kabisa. Kati ya wanaume wote ambao niliwahi kutoka nao, angalau yeye ndiyo alionekana kuwa mature zaidi kwa muda wote niliodumu naye... lakini baada ya kitendo hicho... nilishindwa, yaani nilishindwa kuwaamini wanaume tena," Namouih akaeleza.

Machozi yalikuwa yameanza kumtoka alipokuwa akisema hayo, naye Efraim akamfuta kwa upendo.

"Pole sana. Sikutanii nikisema kwamba kama ningemjua huyo mwanaume ningemuua saa hiyo hiyo kabisa," Efraim akasema.

"Ahh... iliniumiza sana yaani. Sasa kwa sababu iliniathiri vibaya ndiyo maana imekuwa kama...."

"Moyo wako ni mgumu," Efraim akamalizia maneno yake.

"Am sorry Efraim... kwa mambo yote uliyonifanyia najua haustahili kabisa malipo ya namna hii."

"Namouih aliyekwambia mimi nahitaji unilipe chochote ni nani? Huyo mwanaume alikuchezea tu. Wewe sasa unaenda kuwa mke wangu. Tuna muda mwingi vya kutosha kukuruhusu uwe tayari kunionyesha upendo wako pia. Haujawahi kuniambia, lakini ninajua unanipenda..."

Namouih akamwangalia na kutabasamu.

"Kwa hiyo usiwaze. Picha zozote mbaya za mambo yaliyopita nitajitahidi kukusaidia ili uzifute... am here for you," Efraim akasema.

Namouih akakilaza kichwa chake begani kwa Efraim, na mwanaume huyu akawa anasugua bega la mrembo taratibu ili kumpa kitulizo.

"Kwa hiyo kutokea wakati huo haujawa na mwanaume yeyote kabisa?" Efraim Donald akauliza.

Namouih akatikisa kichwa kukubali.

"Ni miaka mingi eeh?"

"Ulikuwa mwaka wa tatu toka nilipoanza chuo... kwa hiyo... kufikia sasa imepita kama... miaka minne-mitano kufikia sita..." Namouih akasema.

"Wow. Ninajua nitafaidi sana kwako yaani..."

"Mhm... kwa nini?"

"Wewe una hali fulani hivi inayonifanya nitambue unajua sana romance... so sitakuwa na papara. Hilo jambo limekuchanganya sana naelewa, kwa hiyo si lazima iwe leo, maana kuna kesho na kesho kutwa pia... na ninajua utanipa mambo mazuri na matamu mno," Efraim akaongea hivyo na kumtekenya mbavuni.

Namouih akafurahi sana na kupitisha mkono wake kiunoni kwa Efraim. "Asante kwa kuwa na subira Efraim. Asante kwa kila kitu yaani," akasema kwa sauti ya deko.

"Kama nilivyokwambia... am here for you. Halafu kuna jambo nilitaka kukwambia. Aam... kuna hii kanpuni kubwa ya kibinafsi... CEO wake ni Edward Thomas, unampata?"

Namouih akaketi vizuri na kumwangalia usoni, kisha akauliza, "Edward Thomas... kwenye kampuni ya..."

"Ngoja nikuonyeshe kwenye simu. Ni rafiki yangu. Alikuwa amenitafuta hiyo juzi aliposikia nimekuvisha pete... alikuwa anakulenga wewe yaani. Anataka kuweka mtu awe kichwa cha masuala ya sheria kwenye kampuni yake, na amekuchagua wewe," Efraim Donald akasema.

"Kweli?" Namouih akauliza huku akitabasamu.

"Ndiyo. Namouih, ninakusihi uchukue hii kazi, ni kampuni kubwa, wanalipa vizuri sana, na wewe ukiwa kichwa pale... aisee!" Efraim akaongea kwa shauku.

Namouih akacheka kidogo na kuendelea kumsikiliza alipomwelezea mambo yote kuhusu suala hilo. Hapo ndiyo ungekuwa mwanzo sasa wa Namouih kujiingiza ndani ya kampuni ile kubwa, na alipokubali kuja kwenda huko, alitaka Blandina aendelee kuwa mwanasheria wake msaidizi hivyo naye apewe nafasi pia. Wakamtafuta huyo Edward Thomas, naye Namouih akaongea naye vizuri mpaka mipango ya yeye kwenda kuanza kazi ndani ya kampuni hiyo kubwa ikaanza mwendo. Alimshukuru sana mume wake mtarajiwa kwa kila kitu ambacho alikuwa anamfanyia, na kadiri ambavyo siku zilikwenda akawa anajitahidi kuonyesha kweli kwamba alimpenda, ingawa bado hakushiriki naye tendo la mapenzi.

Mara kwa mara Efraim Donald alijaribu sana kufanya naye mapenzi, lakini Namouih alionekana bado kuhitaji utulivu zaidi ili akija kumpa mwanaume huyo tunda, picha zote za maumivu ya nyuma ziwe zimemwondoka na ampe kwa moyo wote. Ingekuwa rahisi kusema kwamba muda mrefu vya kutosha ulikuwa umepita hivyo hakukuwa na sababu yoyote kwa mwanamke huyu kuwa mgumu bado, lakini ni kwamba tu hakuwa na moyo mwepesi sana baada ya kufanyiwa vibaya na mwanaume yule aliyempenda kipindi cha nyuma, kwa hiyo subira ya Efraim Donald bado ingeendelea kuhitajika.


★★★


Ndani ya miezi miwili hivi baada ya Namouih kuvishwa pete, tayari maandalizi ya sherehe yao ya ndoa yalikuwa yamekamilika, nao walikuwa wamealika ndugu na marafiki zao wengi kwa ajili ya kuhudhuria. Ndoa ilihalalishwa kiserikali, kisha ndiyo wangefanya sherehe yao ndani ya moja kati ya kumbi kubwa sana jijini hapo. Watu walikuwa wengi, vyakula kwa wingi, vinywaji vingi, furaha nyingi, na wanandoa hawa walipendeza sana siku hiyo.

Namouih alikuwa anatamani mno kama baba yake angekuwepo wakati huu ili kushuhudia mambo haya mazuri sana. Mzee Masoud bado alikuwa London, na kipindi hiki alikuwa amekaa tu kule baada ya upasuaji wake kufanikiwa, lakini angetakiwa kutulia kwanza ili awe na uimara kwa kutosha kuweza kurudi nchini. Ingawa hivyo, familia yake ilikuwa imemuunganisha kupitia simu kwa video aweze kuyaona mambo hapo, na alitoa baraka zake nyingi kwa binti yake na mumewe.

Basi, usiku huo baada ya wanandoa hawa wawili kuondoka sehemu ya sherehe na kwenda nyumbani wakiwa wanandoa rasmi, ilikuwa ndiyo wakati ambao Namouih alijihisi vizuri zaidi kihisia kiasi kwamba alijua utayari wa kumpa Efraim Donald haki yake alikuwa nao. Mapambo aliyowekewa mwilini mwake yalimfanya aonekane kama mhindi kabisa, hasa jinsi mikono yake ilivyopakwa yna na nguo nyekundu kama sari yenye urembo mwingi wa dhahabu kuizunguka. Efraim Donald hata akambeba kabisa mpaka chumbani ingawa ngazi zilikuwa ndefu na Namouih kuwa na uzito kiasi, na baada ya kufika chumbani akamweka kitandani taratibu ili waanze kupeana mahaba waliyosubirishiana kwa muda fulani sasa.

Efraim Donald alipoonyesha wazi kutaka kuanza kumpa bibie mapenzi, simu yake ikaita. Namouih akatabasamu kwa hisia baada ya Efraim kusema hiyo huwa ni lazima itokee kama kwenye tamthilia za wahindi, lakini kwake isingemzuia hata kidogo kusonga mbele. Akaichukua simu akiwa na lengo la kukata kisha aizime, lakini akatulia kwanza baada ya kuona aliyekuwa anapiga ni daktari wa huko London; mmoja wa madaktari wake mzee Masoud, akipiga kwa kutumia mfumo fulani wa simu kama "application." Efraim akamwonyesha mke wake, naye Namouih akasema aipokee ili kujua daktari alitaka nini.

Efraim Donald akapokea na kuongea na kumsikiliza, kisha akamtazama Namouih kwa njia iliyoonyesha kwamba kuna tatizo. Namouih akiwa haelewi kinachoendelea akamuuliza shida ni nini, naye Efraim akaishusha simu na kumwambia sasa alikuwa ametumiwa taarifa kwamba mzee Masoud alipoteza maisha. Namouih alibaki kumtazama Efraim kama vile hajasikia alichoambiwa. Mume wake akaanza kumfariji na kumsogelea karibu zaidi huku anamwongelesha kwa huruma, lakini Namouih hakusema lolote lile na kubaki anadondosha machozi. Jamani, si mzee alikuwa sawa kabisa mpaka wamemaliza sherehe? Nini kilikuwa kimetokea? Jambo hili liliwafanya wanandoa hawa washindwe hata kuonyeshana upendo baada ya kuingiwa na majonzi mengi.

Taarifa zaidi zilipoanza kuja kutoka London zilionyesha kwamba mzee Masoud alifanikiwa ndiyo kuokoka saratani na angerudi kuwa na afya nzuri kabisa, lakini kulikuwa na maumivu ya ndani yaliyosababisha kifo chake. Ilieleweka kwamba hiyo ilitokana na upasuaji wa kitaalamu aliofanyiwa, labda mwili wake haukuwa imara vya kutosha kuendelea kuvumilia ingawa yeye Masoud alifanya ionekane kwamba yuko sawa. Iliwaumiza sana wanafamilia wake wote, lakini mwishowe wangepaswa tu kukubali kwamba hawakuwa naye tena.

Kwa hiyo baada ya siku chache mwili wake ukawa umerudishwa nchini, naye akazikwa mkoani kwao. Ilipokuwa imeanza kuonekana kwamba furaha mpya imempata Namouih, jambo lenye kusikitisha likawa limetokea. Kwa muda fulani alikuwa kwenye huzuni sana, na Efraim Donald aliona ampe muda tu wa kutuliza hisia zake huku akiendelea kumfariji na kumwonyesha upendo wake mwingi, hivyo mwisho wa siku mwanamke huyu akaendelea tu kuchapa kazi kwa bidii. Na ilikuwa bidii yenye nguvu kweli kweli maana hakuwahi kupoteza kesi yoyote ile aliyochukua kushughulika nayo.

Ndiyo kutokea wakati huo mpaka ndoa yao inamaliza mwaka na miezi michache, wanandoa hawa hawakuwa wamewahi kupeana mahaba kabisa.......


★★★★


WAKATI ULIOPO....


Ikiwa ndiyo usiku wa siku ambayo Efraim Donald alikuwa amerudi nyumbani baada ya kutoka safarini, haikuwa imechukua muda mrefu vya kutosha kumkwaza mke wake baada ya yeye kutotaka wapeane mahaba kwa kusema amechoka. Namouih alikuwa amejifungia bafuni kwa kukasirishwa na jinsi Efraim alivyomkwepa, na mwanaume huyu akasogea mpaka mlangoni kuingilia bafuni akijaribu kumwambia kwa upole atoke ili waweze kujipumzisha; akisisitiza kwamba ni kweli alikuwa amechoka.

Namouih kiukweli hakuweza kumwelewa Efraim vizuri. Tabia hii ilikuwa imeendelea kwa muda mrefu sasa, na mwanzoni ni kweli alihitaji muda kutokana na mambo mengi magumu aliyopitia kihisia, lakini kwa wakati huu alikuwa anamwonyesha wazi kabisa kwamba anataka kumpatia mapenzi kwa kuwa vidonda vyake vimepona, ila Efraim Donald akawa anampiga chini. Ndiyo sababu alimuuliza ikiwa labda hali hii ilisababishwa na yeye kutofanya naye mapenzi kabla hawajaoana, akifikiri labda Efraim alikwazwa kipindi hicho na sasa hii ndiyo ilikuwa adhabu yake, lakini kiukweli hiyo haikuwa sababu.

Sasa hili jambo lingeendelea kuwa hivi mpaka wakati gani? Blandina alikuwa amemshauri azungumze naye endapo angezingua kama hivi, na ndicho Namouih alichokifanya, lakini ilikuwa ni kama masikio ya mume wake hayasikii maana ilipokuja tu kwenye suala hilo alijali zaidi kazi, safari, kupumzika. Mwanamke akaendelea tu kukaa bafuni mpaka inafika saa nane, ndiyo akatoka na kukuta Efraim akiwa ameshalala. Akamwangalia sana, sana, kisha naye akaenda taratibu kitandani na kujilaza upande wake, kukiwa na nafasi kubwa iliyowatenganisha kitandani hapo, na mioyoni mwao.


★★★


Asubuhi ikafika. Namouih kama kawaida aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kazi, na wakati huu hakuwa amesumbuliwa na ndoto mbaya kama ile ya siku iliyotangulia. Alimwacha Efraim Donald akiwa amelala mpaka yeye alipomaliza kuvaa suti yake ya kike yenye sketi iliyoishia magotini, yenye rangi ya zambarau, viatu vyeusi na virefu chini, huku nywele zake akizibana kwa nyuma. Akashuka chini na kwenda kupata kiamsha kinywa huku akiwa na Angelo, yule paka wake, naye Esma alikuwa jikoni kushughulikia mambo mengine yaliyohitajika kwa baadaye.

Ndipo Efraim Donald akatokea huko juu chumbani Namouih alipokuwa mbioni kumalizia chai. Akafika karibu yake na kumbusu shavuni huku ameyashika mabega yake na kumsemesha kwa salamu, naye Namouih akatikisa kichwa tu kuitikia lakini akionyesha wazi kwamba bado alikuwa amekwazika. Mwanaume akakaa kwenye kiti chake mezani hapo, huku akiuliza ni mambo gani ambayo Namouih angeshughulikia leo. Yaani alifanya ionekane ni kama hakukuwa na tatizo kabisa, na kwa sababu Esma alikuwa amefika hapo kumwekea vyombo kwa ajili ya chai, Namouih akaona amjibu tu kwa ufupi, akisema anaenda kumtetea msichana kwenye kesi ya ubakaji akiwa na Blandina.

Efraim Donald akampongeza na kupendekeza kwamba wamwalike Blandina leo jioni, aje kupata chakula pamoja nao kwa kuwa alimkumbuka sana rafiki yake huyo. Angalau hii ilifanikiwa kumfanya Namouih atabasamu, naye akasema angemwambia. Mume wake akasema angekwenda mjini kutafuta mambo mengi mazuri ili Namouih akirudi atengeneze msosi wa nguvu, naye Namouih akakubali na kuaga hatimaye. Aliondoka akiwa hajihisi vizuri sana kwa sababu kuna upande wake mmoja uliofurahia sana utu wa Efraim lakini mwingine ulichukizwa na mambo kama yale yaliyotokea usiku wa jana yaliyofanya aina yao ya maisha iwe kama maigizo, lakini hakuwa na jinsi ila kubaki mtulivu; na hasa kwa sasa aelekeze nguvu zake zote kwenye kesi ya Agnes.

Akachukua gari lake aina ya Premo lenye rangi ya shaba iliyong'aa (silver) na kuanza kuelekea kwenye mahakama ambapo kesi ingesikilizwa, ikiwa imepangwa kuanza saa nne kamili asubuhi.

★★

Namouih alifika eneo la mahakama na kukuta watu kadha wa kadha wakiwa wameshafika, na Blandina tayari alikuwa hapo pia. Akamlaki rafiki yake na kuuliza ikiwa gari lake lilikuwa limepona kabisa ile sehemu iliyokunjika, naye Blandina akasema lilikuwa kwa mafundi bado likinyooshwa vyema na kupigwa rangi ili liwe kama jipya kabisa, kwa hiyo asubuhi hiyo alifika hapo kwa usafiri wa kulipia. Blandina alikuwa ameshikilia kablasha lenye karatasi za mambo kadhaa kuhusiana na kesi ya Agnes, akimwambia Namouih pia kwamba alikuwa ameshazungumza naye na mama yake kwa kuwa walifika hapo mapema, na hivyo walikuwa ndani wakimsubiri yeye Namouih.

Namouih akaanza kuvaa joho jeusi la mwanasheria alilokuwa ameliweka ndani ya gari lake, na Blandina akawa ametambua kwamba uso wake ulificha hisia ya huzuni. Akamuuliza shida ni nini, naye Namouih akasema hakukuwa na shida kabisa. Blandina akakisia kwamba mambo hayakwenda vizuri baina ya Namouih na Efraim Donald, naye akauliza ikiwa jaribio lake lilifanikiwa, na ndipo Namouih akafunguka kwa ufupi akisema alijitahidi sana lakini bado mume wake hakutaka kushiriki naye tendo la ndoa. Hii ilimshangaza Blandina kiasi, hata akauliza ikiwa labda Efraim alikuwa anatoka na mwanamke mwingine au ni shoga, lakini Namouih akasema angetakiwa tu kuliweka hilo pembeni kwanza. Akamwambia rafiki yake kuwa leo jioni anapanga kumkaribisha nyumbani kwake kwa ajili ya mlo, na lilikuwa ni wazo la Efraim, naye Blandina akafurahi na kukubali mwaliko huo.

Wawili hawa wakaanza kuelekea kule ndani ya jengo la mahakama. Lilikuwa jengo jeupe na kubwa, lenye muundo wa ghorofa pana likiwa na kumbi kadhaa, nao wakaingia moja kwa moja mpaka kule ambako kesi ingesikilizwa. Kulikuwa na mabenchi marefu yenye sehemu za kuegamia, kwa ajili ya wasikilizaji, kizimba kilichokuwa upande wa kulia kutoka pale ambapo hakimu (judge) angekaa huko mbele, upande wa kushoto kulikuwa na sehemu ambayo wangekaa waamuzi maalumu wa kesi (jury/jurors), na kulikuwa na watu wengi kiasi pande zote za kusikiliza.

Upande wa mtoa mashtaka, yaani Agnes, msichana ambaye Namouih angemtetea, ndiyo upande uliokuwa na watu wengi zaidi ya upande wa mtuhumiwa, yule kijana aliyeitwa Japheth, mwenye kesi ya kubaka. Mama yake Agnes alipomwona Namouih alianza kuongea naye, kisha akamwacha aende mpaka pale mbele kwenye meza ya kukaa mwanasheria na mtu wake wa kesi; ambako Agnes aliketi. Wakasalimiana vizuri, na Blandina alikuwa amekaa benchi la kwanza usawa wa sehemu aliyokaa Namouih pale mbele. Baadhi ya watu waliokuwepo walimwongelea sana Namouih, wakijua alisifika sana kwa kushinda kesi zote alizowahi kushughulika nazo, lakini wengine walikuwa wanaongelea zaidi urembo wake na jinsi alivyoonekana kuwa wa gharama na makini sana.

Baada ya muda fulani, Japheth akawa ameletwa hapo pamoja na mlinzi wake, yaani askari aliyetakiwa kumlinda alipokuwa amewekwa kwenye kifungo cha nyumbani, ingawa siyo nyumbani kabisa alikoishi (wanajua wenyewe wanakowapelekaga). Hii ilikuwa ni kwa sababu mwanasheria wake aliyepita aliomba apewe kifungo cha namna hiyo badala ya kumweka rumande, kwa hiyo hapo akawa amefika na kuwakuta wengine wameshatulia. Kwenye upande wake alikuwepo baba mkubwa wake, dada yake, mdogo wake wa kike, na marafiki wachache pia. Akakalishwa upande huo kwenye meza ya mbele, na askari wake akasimama pembeni. Bado, mpaka kufikia wakati huo, mwanasheria aliyetakiwa kumsimamia hakuwa amefika.

Namouih akamgeukia Blandina na kumuuliza ikiwa alikuwa ana taarifa yoyote kuhusu mwanasheria mpya wa Japheth, lakini rafiki yake akakanusha. Hivyo wakaendelea kusubiri tu mpaka wakati ambao hakimu aliingia hapo na kwenda kuketi kwenye kiti chake kule mbele, na watu wote walikuwa wamesimama mpaka alipokaa ndiyo nao wakakaa. Sasa msomaji wa kauli za mahakama (clerk) akawa amemwambia hakimu kwamba mwanasheria wa Japheth hakuwa amefika bado, na hakimu huyo akamuuliza Japheth mwanasheria wake alikuwa wapi.

Kijana huyo akasema mwanasheria wake alikuwa anakuja, hivyo wasubiri tu kidogo. Hakimu akaeleza wazi kwamba muda uliokuwa umepangwa ulitakiwa kufuatwa kwa sababu kuna kesi zingine zilihitaji kuendeshwa hapo kwa hiyo hawakuwa na muda wa kupoteza. Japheth hangeweza kujisimamia mwenyewe, kwa hiyo kama mwanasheria wake asingekuja inamaanisha kesi hii ingeamuliwa kwa kumpa hukumu kwamba ana hatia ya kubaka. Haya yote yangeepukwa kama angekuwa amekubali mwanasheria mwingine ambaye angeteuliwa mapema kwa ajili yake baada ya yule wa mara ya kwanza kupatwa na dharura, kwa hiyo huo ndiyo ungekuwa mwisho wa mambo haya yote.

Namouih akawa amekerwa sana na usumbufu wote huo alioona tokea mwanzo kabisa kwamba ungewafikisha huku. Kujiandaa kote halafu mtu anashindwa kuonyesha msimamo ni jambo lililomfanya akerwe sana, lakini mwisho wa siku ushindi ungebaki kuwa wao kwa hiyo....

"Samahani mheshimiwa... samahani kwa kuchelewa..."

Wote waliokuwa hapo wakageuka nyuma baada ya kusikia maneno hayo yakisemwa kwa sauti ya juu. Milango ya kuingilia ndani hapo ilikuwa wazi, na hapo aliingia mwanaume aliyevalia suti nyeusi huku akiwa ameshikilia begi dogo la mkononi, siyo la mgongoni. Blandina aligeuka vizuri zaidi na kubaki amemwangalia kwa umakini sana, naye Namouih alipogeuka na kumwona, akabaki kumtazama kwa umakini pia kadiri alivyoendelea kupiga hatua kuelekea mbele. Walimfahamu. Alikuwa ndiyo yule yule kijana ambaye asubuhi ya siku ya Jumapili wakati wawili hao walipotaka kwenda kumpa pole rafiki yao, yule Mwantum, Blandina alijigonga kwake na kupasua chupa, kisha mwanaume huyo akamnunulia nyingine na kuchukua namba zake; yaani Draxton!



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 787 604 893

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
Back
Top Bottom