hivi wewe unajua màana ya neno takatifu au unalopoka tu.. Mahala patakatifu angeingia huyu mzinzi,mshirikina,mwizi,mnafiki...ikulu si mahala patakatifu tena bali ni mahala wanapokutana wahuni kupanga dili za kutekeleza mauwaji,kung'oa watu meno na kucha,kupiga picha na wabwia uga...
Kwanza hapo tukishapachukua itabidi kufanya maombi ya kung'oa viti vya enzi vya JOKA na mashujaa wake (majini na mizimu) iliyoweka kambi ili kuifunga Tanzania katika vifungo vya giza.
Itabidi kuvunja maagano yote na matambiko yote yaliyofanyika na kulifanya Taifa kukabidhiwa kwa Lucifer...tutang'oa misingi yote ya uovu ambayo imelifanya taifa liwaneemeshe wezi na waovu na kuwafukarisha wasio wezi na wapenda haki.
Tutafanya maombi yakuwateketeza kwa moto wa Yesu na radi wachawi wote, wasoma nyota na waganga wa kienyeji walioshirikiana na viongozi kutoa kafara kwa shetani ili kulikabidhi taifa hili kwa JOKA lililotupwa kutoka mbinguni.
Tutaikabidhi hii nchi kwa Mungu wa Abraham, Isaka na Yakobo (Israel). Na immediately tutarejesha uhusiano wetu na taifa la Israel maana moja ya laana ya nchi ya Tanzania ni kulikataa taifa la Israel. Kutoka 23:22 inasema nitakuwa adui wa adui zako na mtesi wa hao wakutesao. Taifa lolote linalokuwa na uadui na Israel linalaaniwa na Taifa linalokuwa na urafiki na Israel linabarikiwa, Marekani wanaijua siri hiyo ndio maana wanabarikiwa sana.