Mapendekezo: Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ifute matumizi ya fedha za sarafu na itengeneze noti mpya ya shilingi elfu 20 na elfu 50

Wakati dunia inahamia kwenye cashless, kuna watu wanawaza kuongeza noti. Mimi nashauri serikali iache kabisa kuingiza noti na sarafu kwenye mzunguko na iondoe tozo watu walipe kwa mitandao kuanzia supermarket, madukani mpaka kwa mama ntilie iwe mwendo wa mpesa tu.
 
Matumizi ya fedha za sarafu yanaakisi ni kiasi gani watanzania bado wapo nyuma kiuchumi,ni risk kuzihifadhi kwa maisha ya sasa kwasababu hata kuzihifadhi tu mifukoni au kweny bahasha ni usumbufu mkubwa,
Hivyo napendekeza watengeneze noti mpya ya elfu 20 na elfu 50 ili kuweza kupunguza idadi ya note hasa kwa wale wanaohifadhi fedha nyingi waweze kupunguza wingi wa note.
Napendekeza badala yake tuongeze uzalishaji ili pesa ipande thamani
 
Matumizi ya fedha za sarafu yanaakisi ni kiasi gani watanzania bado wapo nyuma kiuchumi,ni risk kuzihifadhi kwa maisha ya sasa kwasababu hata kuzihifadhi tu mifukoni au kweny bahasha ni usumbufu mkubwa,
Hivyo napendekeza watengeneze noti mpya ya elfu 20 na elfu 50 ili kuweza kupunguza idadi ya note hasa kwa wale wanaohifadhi fedha nyingi waweze kupunguza wingi wa note.
Mawazo ya Iddi Amin hayo. Pesa hawaprint kama karatasi za tuition.
Kuna sababu za kiuchumi hapo na siyo kwa ajili ya urahisi wa kutembea na hela nyingi.
 
Ishu ni kwamba fedha za sarafu zisitumike tena,yaani kuanzia shilingi mia tano ya note hadi elfu 50 sasa hapo utapata usumbufu upi wa kupata chenji
Kuna mtu mauzo yake kwa siku ni sh 10000, maana yake hawezi uza kwa mti wa 50000! Sijui wewe unafikiria mshahara wa mwisho wa mwezi tuu?
 
Mzunguko wa fedha mdogo sana ungekuwa mkubwa sana wangeprint

Lakini kwa sasa ninakushangaa wewe unaishi dunia ya wapi watu wenye pesa nyingi hawahifadhi nyumbani ni benki na miamala mingi huifanya kwa ki electronic hivyo kufanya washikaji pesa taslimu kupungua

Hizi sarafu zinahitajika sana kwa majority ya watanzania kulipa nauli za daladala,kununua mahitaji mitaani mfano magenge ya kuuza nyanya,vitunguu nk

Kununua maandazi,chapati nk
Pia kuna sekta imeingia ya kucheza kamari zinahitajika sana hizo sarafu
Kwa comment hii, mada umeifunga.
 
Ishu ni kwamba fedha za sarafu zisitumike tena,yaani kuanzia shilingi mia tano ya note hadi elfu 50 sasa hapo utapata usumbufu upi wa kupata chenji
Maliza shule kwanza ndo utajua hujui, dunia nzima huwezi epuka sarafu, nenda ulaya na Amerika. Usianzishe uzi bila kusoma kwanza
 
Wakati dunia inahamia kwenye cashless, kuna watu wanawaza kuongeza noti. Mimi nashauri serikali iache kabisa kuingiza noti na sarafu kwenye mzunguko na iondoe tozo watu walipe kwa mitandao kuanzia supermarket, madukani mpaka kwa mama ntilie iwe mwendo wa mpesa tu.
Unaishi sayari ya Mars
 
Shida wp hizi sarafu ndy shida,fedha zikiwa kwa mfumo wa note hapatakuwa na usumbufu wa chenji kama ilivyo sasa
Acha bangi wewe.... kwamba nampa konda noti ya elfu 20 au 50 akate 600.... au naenda kununua vucha ya 1000 nimpe noti ya elfu 50..... AU UNATAKA UPUUZI WA KWENDA DUKANI NA KIROBA CHA KUBEBEA CHENCHI...... jinga kabisa...
 
Umeshawaza unanunua vocha ya 1,000 halafu mtu kakupa note ya 50,000? Sitaki hata kuwaza daladala konda kapewa 50,000 akate 400.
Juzi nilikuta ugomvi mkubwa Sana kituo cha daladala baada ya konda kuvurugana na abiria wake kisa ni abiria kumpa konda elfu kumi kwa nauli ya mia nne tuu. Konda baada ya kukosa chenchi akamwambia abiria waende mpaka mwisho wa bus na atarudi naye mpaka anaposhukia kwani hana jinsi. Ikatokea abiria mmoja msamaria akamlipia huyo mama sh 400 ndo safari ikaendelea...
 
Yaani ukipoteza note 1 ya 50,000, umepoteza hela ya kulimia eka 1?? Au mshahara wa kibarua mara!
Aisee na umesomea wapi Econometrics??
 
Back
Top Bottom