Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Ila kusema ukweli, dogo janja ametokota vibaya sana. Japo siipendi CCM lakini dogo janja ndiye aliyetengeneza mazingira yanayohalalisha yeye kuvuliwa ubunge. Walichokifanya mahasimu wake ni kutumia tu fursa hiyo ya kumvua ubunge kama ilivyojitokeza. Ushauri wangu kwa chadema ni kuwa, kwenye uchaguzi wa marudio wasimamishe mtu mwingine. Kama dongo janja atachukia na kwenda kuunga mkono juhudi za mkuu basi aachwe tu aende maana impact yake ni ndogo sana hata hivyo.
Thanks. Nassari nilipomsikiliza na machozi yake ya kijinga nilimdharau sana. Kwahiyo sasa hivi ndo anajua umuhimu wa ubunge. Chadema wala wasihangaike naye
 
Kama kawaida yenu tatizo sheria zinabagua watu na malengo na matendo ya Spika kama kweli mnafata sheria kwa kiwango hiki Spika alitakiwa kuwa mtu mwingine sababu huyu mwenyewe alianzia hospital na hakupumzishwa mpaka amerudi lakini yeye ndio amekuwa na matamshi na maamuzi yasiyo na hekima, utu na hila.

Narudia tena yeye ni captain sio kocha, yaani wenzie aliwakuta wabunge kabla ya yeye kuwa spika. Spika anatoka miongoni mwa wabunge. Alipashwa kumwita na kumpa nafasi ya kujieleza kuiga kwa mtu asiyekuwa manager ni makosa na tunataka kuona weledi katika mihimili na sio hizi sarakasi.

Watanzania tunataka haki, hawa sio tu hawatendi bali hata nia ya kutenda haki inamashaka. Ndio maana kila maamuzi yao ni kama hawajiamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo Nassari alikuwa anaumwa? Mbona Lissu hajavuliwa ubunge? Tuachane na madhambi ya spika kumnyima mshahara maana hata yeye hapo hajui afanyalo. Kwa hili la Nassari wala sioni shida maana alikuwa haumwi wala nini. Ni kiburi tu.
 
Kwanza nakupa pole kwakua hoja zako zimejaa utoto wenye fikra fupi.Kwanini unabeza matatizo ya mwenzio?Nilitegemea hoja ya msingi iwe kwenye uhalali wa taarifa alizotoa kwa speaker kutohudhuria bungeni ndio tuanzie hapo.Naamini ukikua utakuja kutambua utoto huu wa hoja otherwise naheshimu maoni yako.
Hivi kanuni na taratibu za bunge zinasemaje kabla ya kumfukuza MTU ubunge? Spika hapaswi hata kumuuliza mhusika? Kumpa onyo mhusika? Spika anamvizia mkosaji halafu anarusha taarifa za kumfukuza tweeter na siyo kumpa taarifa mhusika?

Na kwann spika anakwepa kupokea simu za Nassari?
Mkuu taratibu ziko wazi,kabla kikao Cha bunge,wabunge wote hutakiwa kuwahi bungeni kwenda ku report kimaandishi.
Kwa mbunge ambaye anaudhuru hutakiwa kumtaarifu speaker,na speaker akijirisha na hoja ya mtoa udhuru,atamruhusu kwa maandishi.kinyume Cha hapo utakuwa mtoro.
Sasa vikao hivyo vikifanyika Mara tatu mfululizo,kwa mujibu wa katiba,sheria na miongozo ya kibunge,utakua unepoteza sifa ya kuwa mbunge,kea hiyo,speaker ataialifu tune ya uchaguzi juu ya nafasi kuwa wazi.
Watanzania LAZIMA tujue ya kwamba ofisi ya bunge inawatumishii wengi,wa nyanja mbalimbali ambao uhudumu pale bungeni.
Karibu was bunge ndiye accounting officer.Hivyo wenyejazi zao humpelekea speaker taarifa mbalimbali,zikiwepo zinazohusu maudhururio ya kila mbunge,vikao vingapi hakuudhuria na Kama Kuna taarifa ya maandishi ya ruksa.
Sasa twende kea akiyekuwa mbunge.
Mosi mimva Sio Siri Ni mchakato,wa miezi Tisa.Hivyo mimba ikiingia Leo,tarehe ya kujifungua itajulikana.
Pili,akiyekuwa mbunge Ana wakubwa wake kwenye chama kwa ninii hakutoa taarifa kwao?
Hivi vijana wasomi,mnataka kutuaminisha kwamba unaweza kutoka nje ya kituo chako Cha bila kumtaarifu bosi wako?
Mbona hata watoto wetu wanapokwenda shule hutuaga kea kusema bye bye mom/dad.?
 
Mh. Nassari alikumbwa na mtihani wa uzazi,mpaka sasa more 80% huku Marekani walienda kufanyà IVF,kwa natur,risk and cost ya IVF hukustahiki kumbeza hivi. Omba Mungu akuepushe na mtihani wa uzazi
IVF NDO UMEONA NENO KUBWA SANA.RUDIA KUSOMA ULICHOANDIKA.

HAWA WABUNGE WANAPEWA M NGAP KWA MWEZI???. WATU HAWANA HATA MIA UNASIKIA "NILIKUA KWA TIRAMPUUUUU KUMUUGUZA MAAMAAA ENUUU"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nassari anatafuta huruma kwa kulia machozi.
Nassari ametuambia hawezi kuacha mke wake,kwa kufuata posho ya laki tatu kwa siku
Nassari ametuambia anakwenda mahakamani
Mkapa alikua sahihi sana kuwapa lile jina
Nassari unakwenda mahakamani kutafuta nini ikiwa umesema huwezi kumuacha mkeo kwa kufuata bunge
Ulipokua unaona hukujua kwamba wewe ni muwakilishi wa maelfu ya watu,wanahitaji uwakilishi wako?
Ungekubali yaishe ukalee mtoto wenu,mkeo anajifungulia marekani,wananchi waliokuchagua wanajifungulia kwenye baiskeli wakati wa kuwahi zahanati ilio mbali
 
Kwani mbunge mpaka anafukuzwa bungeni anatakiwa asiwe ameudhuria vikao wangapi?? Kama sikosei ni mitano mfululizo. Inamaana 2017 na 2018 Nassari hakuudhuria vikao vya bunge. Kama hakuudhuria inamaana akutoa taarifa. Halafu yeye baada ya kwenda Marekani kumuuguza mkewe, kwavyovyote alijua vikao vinaanza lini. Alishindwaje kuandika barua kabla. Kwa mawazo yangu hii issue Nasari anaijua maybe ameshalipwa kiinua mgongo wake kabisa wa kumaliza ubunge 2020. Uku akijua kuwa hawezi kurudi 2020. Kwa mwenye akili timamu kama Nasari haiwezekani asiudhurie bungeni mikutano minne mfululizo na huku akijua kabisa kuwa hiki kikao inayoanza nikiudhuria nitakuwa nimefuta makosa yote ya kutoudhuria mikutano minne. Alishindwa kupanda ndege akaudhuria kwenye kikao cha mbunge na kuomba ruhusa na kurudi tena marekani. Sidhani kama Nasari angeshindwa nauli ya ndege. Ilikuwa safari ya siku moja na kurudi, halafu hospital za wenzetu hakuna chochote ambayo nasari angesaidia hata kama asingelikuwepo pale. Sana sana mke wake angemmiss kwa maybe two days na angerudi. Na mkewe angemwelewa kwasababu ilikuwa ni muhimu kutokana na utoro wake wa nyuma. NASSARI KAUZA JIMBO HATA KAMA LITARUDI LKN NDIO UKWELI. KAMA SIO HIVYO BAC SPIKA AMETEGESHEWA NGOMA ILI AONEKANE KWA JAMII ANAVYOWAONEA OPPOSITION
JIMBO HALIRUDI REJEA "NATAMANI NIWE MBUNGE WA ARUMERU". PLANNED EVENT NA MBUNGE HUSIKA HAKUJA FUNUNU NI AMA ALIJUA AMA DHARAU AS USUAL

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbona Spika alikaa nje ya nchi muda mrefu akijiuguza?
hoja dhaifu hii
spika alipewa ruhusa hakupotea kama Nassari,halafu spika hakua mjamzito
Nassari alitakiwa kujua ujauzito sio ugonjwa
 
Hata najiuliza hili lichama linaendeshwaje? Hakuna hata social life yaani, hata group la WhatsApp la viongozi basi! Yaani mikutano mitatu inapita mtu hahudhurii and nobody notices. Wote wanakuja kushtuliwa na barua ya spika!
Hivi Chadema hawawezi kufanya vizuri hata kitu kimoja jamani, kimoja tu
Hili jambo linafunua udhaifu wa cdm na wote wanaomtetea mpokwaji wana matatizo yasiyopimika
 
Nachojiuliza ni kwamba yaan miaka yote majukwaani wanatuambia CCM Ni mashetani hawafai halafu tena wanajiingiza wenyewe kwenye 18 za mashetani na kutaka huruma eti spika hakuniita kuniuliza kinachonisibu or nilishauriwa na msaidizi wa spika, sympathy from an enemy? Ngoja niandike kitabu chenye hiyo title
 
Nianze kwa kusema kua,nimekua nikimfuatilia sana na kwa ukaribu Joshua Nasari,akiwa bungeni na Jimboni. Joshua anajua kujenga hoja,anajua kuipangilia hoja yake na akaeleweka na wenye akili. Kwale wakuunga mkono kila kitu huwa inakua ngumu kidogo kumuelewa Nasari.

Jimboni kwake nimepita mara nyingi,huwezi kumsema vibaya ukaeleweka. Anasifika kwa uchapakazi wake,na kuhudumia wananchi wake,na alikua kiongozi anayeongoza na kufuatwa na anaowaongoza siyo kwakua walimuogopa,hapa,kwakua tu walimkubali na kumuamini.

Nasari alikosea hapa,1.kulewa sifa,akadhani tupo kwenye zama zile.,2.kujisahau,na hili ni tatizo la wabunge karibu wote,wanakujaga kugutuka yakiwakuta kama hili la Nasari au kuanza kukataliwa majimboni kabla hata ya uchaguzi.
Mfano mzuri ni mkuu mmoja wa mkoa sasahivi,alienda msibani mwaka 2015,alikua hajawahi kufika eneo hilo tangu uchaguzi wa 2010,alichoambiwa na wafiwa ni"ondoka tuzike,maiti imegoma kutoka ndani mpaka uondoke",aliondoka kwa aibu mno.
3.Nasari alijawa na kiburi na dharau. Kwa mtu yoyote aliyeajiriwa,ukiomba ruhusa huondoki eneo la kazi bila kuhakikisha umeruhusiwa,vinginevyo utakua umejiruhusu.

Eneo lingine aililokosea Nasari,ni kudhani kuna huruma kwenye sheria,Ndugai anaweza kuwa na huruma,ila siyo sheria anazozisimamia. Nimesoma posts nyingi na comments nyingi humu JF,wengi wanamtukana Ndugai na kusahau kuwa siyo yeye,ni sheria.
Wanasema za mwizi ni 40,jitahidi kuhesabu,zikifika 38 tulia kidogo,kwamaana Nasari alipaswa kuwa anaenda bungeni japo mara mojamoja.

Alipokosea tena ni kubase tatizo lake na tatizo la mkewe,alokua anajifungua na mke,siyo yeye,ana dada zake,ana mama yake,mke ana ndugu zake wa kike,walitosha sana kuwa watu wa karibu mke wake,yeye alitakiwa awe kuhenya kutafuta nguo za mtoto na chakula cha mzazi. Sawa,ndoa inakiapo chake,sikatai,ila sometimes hawa tunaoapa nao ndo wasaliti wakubwa wa viapo hivyo,mwanaume uchague sahihi.

Lingine ni kulia mbele za kamera. Mwanaume halii hata sikumoja chozi likaonekana,labda msibani,nako kuna watu wa kukuambia"vumilia,jikaze,wewe ni mwanaume". Huambiwi haya kwa bahati mbaya,ni kukumbusha kuwa,uwe na ngozi ngumu. Unaanguka,unasimama tena.

Mwisho,sioni logic ya yeye kwenda mahakamani. Kufanya nini?,kumshtaki nani?,ili iweje?,katiba inasemaje?,ana barua ipi iliyomruhusu kutokuhudhuria vikao?,anataka kumfurahisha nani kuwa ameenda kuitafuta haki ila imeshindikana?

Yote haya,jibu lake ni kujisumbua,bunge ni muhimili mwingine,mahakama na serikali ni muhimili mwingine.
Pia,asome tu alama za nyakati.



WAASALAM.
Huwa ana hoja makini sana bungeni.. kichwa smart...
Nadhani akina Mbowe, Lijuakali na Lissu wasimpe kiburi na kwenda mahakamani .... Ni miezi 9 hajakatiza Dodoma

Anayo nafasi ya kuomba radhi kwa spika na pengine spika anaweza kumwachia kwa onyo kali
Sifurahii kupoteza kwake hivyo namuombea apewe huruma na kurudishwa bungeni.
 
ati nini?.....hawezi kuacha mke ili aende bungeni?,haya sasa ni madharau
Ndio vimemgharim sasa, ila mi naona ni halali tu alivyoliwa kichwa kwsbb kuna wabunge wengi tu wanawake wanajifungua na baada ya muda wanaendelea na majukum yao.
Kuna wabunge wa kiume wengi tu ambao wake zao wamejifungua still haikuathiri kazi zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachojiuliza ni kwamba yaan miaka yote majukwaani wanatuambia CCM Ni mashetani hawafai halafu tena wanajiingiza wenyewe kwenye 18 za mashetani na kutaka huruma eti spika hakuniita kuniuliza kinachonisibu or nilishauriwa na msaidizi wa spika, sympathy from an enemy? Ngoja niandike kitabu chenye hiyo title
Hv ni jukum la spika kumuita au yy ndio alitakiwa kutoa taarifa ya kwnn amekuwa mtoro?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa ana hoja makini sana bungeni.. kichwa smart...
Nadhani akina Mbowe, Lijuakali na Lissu wasimpe kiburi na kwenda mahakamani .... Ni miezi 9 hajakatiza Dodoma

Anayo nafasi ya kuomba radhi kwa spika na pengine spika anaweza kumwachia kwa onyo kali
Sifurahii kupoteza kwake hivyo namuombea apewe huruma na kurudishwa bungeni.
Ila jmn ht km ndio mambo ya mimba, miezi tisa ya utoro kazini ni mingi sana unless labda km yy ndio angekuwa anaumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...hivi hakuna mbinu nyingine ya kuifufua ccm.
 
Back
Top Bottom