Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Pia Serikali ijiandae kununua chakula na kuhifadhi katika ghala za taifa kukitokea upungufu wa chakula. Mabadiliko ya tabia nchi yameleta balaa kwa wakulima, mvua hazijajesha kwenye maeneo mengi, waliopanda mazao kwa kutegemea ‘mzimu’ wa mvua, baadhi ya sehemu yameanza kukauka.
Kweli kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeipanda busara hii na kuelewa kinagaubaga. Ukweli ni kwamba X-MP kauaibisha upinzani, wasomi na viongozi vijana. Anataka ithibitike kweli waTz ni wavivu na janjajanja kumbe ni yeye tu. Si busara kujiruhusu baadae ukatoa taarifa hata kama boss wako unamdharau! Watumishi wa namna hii ni mizigo, heri spika kautua.
Spika hana tatizo mkuu, amepata mpenyo (kama X-MP hakununuliwa), basi alijilengesha mwenyewe kwenye Ranging Scale ya Mh. Spika na akajaa as a target. Then kuna watu walitaka Mh. Spika asi-pull the trigger to hit the target.
Ameaibisha sana umma wa vijana huyu, umma wa wapinzani na wapenda Demokrasia.
Vijana wajanja wajanja kama huyu HAWAFAI kutetewa hata Mahakama Kuu
 
JE! MBUNGE ANAHUDHURIA BUNGENI KWA AJILI YA POSHO YA LAKI TATU AU KUTEKELEZA MAJUKUMU MAKUU MATATU YA BUNGE?

Nimesikiliza kwa makini hotuba fupi ya ndugu Nassari iliyojaa mambo mengi ya kujadili na yenye kuacha maswali.

Binafsi namfahamu ndg. Nassari tangu tukiwa wote wanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaam. Hivyo nampa pole kwa yanayoendelea. Hii historia ya kujirudia kwake. Mwaka 2008 akiwa naibu spika wa bunge la wanafunzi alivuliwa unaibu spika kwa mizaha tuu ya kutokufuata kanuni za bunge na DARUSO by-laws spika akiwa ndg. Mgeta.

Ninafahamu Nassari akiwa na rafiki yake ambaye ni rafiki yangu pia Jaccob Mlikuza hawakuwa wazembe darasani, hivyo Nassari alihudhuria vyema somo la filosofia ya ujenzi wa hoja, "critical thinking and argumentation" chini ya wahadhiri mahili kama Dk. Mihanjo, Dk. Lwaitama, n.k

Nilivyo msikia akilinganisha kati ya " KUHUDHURIA BUNGENI KWA AJILI YA POSHO YA LAKI TATU AU KUBAKI AKIHUDUMIA MKEWE ANGECHAGUA NINI!" binafsi nilishtuka.

Ninajua bunge lina shughuli kuu tatu. 1. kuisimamia serikali, (oversight function) 2. Kutunga sheria (Legislative function) na 3. Uwakilishi (representative function). Katika majukumu hayo, hakuna sehemu nimeona kuwa mbunge anahudhuria bungeni kwa ajili ya kupokea posho ya laki tatu bali kutimiza majukumuhayo ya bunge. Hapa pana maswali ya kujiuliza:-
1. Je! Nassari amekuwa akihudhuria bungeni kwa ajili ya posho?
2. Je! Kauli yake hiyo inawakilisha tabia na lengo la wabunge wetu kwa ujumla wakiwa bungeni?

Hotuba ya nasari ina mengi. Badaye tutajadili ile ya kupewa Ndafu Ndugai kuitumia kama sehemu ya kuomba huruma. " argumentum ad pitium"
Maji yamezidi unga!
 
Pesa ya mkopo haina tofauti na nguo ya kuazimwa isivyositili uchi, mwenye nguo akichukua lazima nyeti zako zionekane hadharani.
Mfanyabiashara au tajiri yeyote kukopa ni kawaida,tatizo linakuja pale mauzo au uzalishaji alioutegemea umeenda tofauti kwa sababu ambazo ziko nje ya uwezo wake.
 
HAKI GANI WATU WANAITAKA ZAIDI? NASSAR NI MSOMI NA MWELEWA SANA/ ANAJUA TAARIBU ZOTE. HATUA ILIYOCHUKULIWA NA SPIKA NI NDO HAKI YENYEWE YA WANANCHI WA ARUMERU. WANANCHI WA ARUMERU WANA HAKI ZAIDI YA KUWAKILISHWA MATATIZO YAO BUNGENI KULIKO HAKI YA MTU MOJA (NASSARI).
Uitishwe uchaguzi mwingine.Tunataka mbunge mpya
 
Mie najiuliza tu, makosa madogo kama haya,(kama ni kweli) ni uzembe .... sasa unawezaje kufanywa na vijana wanaoitwa wasomi na pengine chama kikishika hatamu wawe viongozi wa juu serikalini, watatufikisha kweli?
Hakuna umakini wowote, ni walaghai tu hao. Hawafai kuongoza nchi.
 
Mimi UTETEZI wake siuelewi kabisa.

Yaani miezi Tisa mtoro.

Juzi ndo anaandika barua, Siku zote alikuwa wapi?
Aliwezaje kusafiri bila kibali Cha Spika?
utoro miezi tisa yani toka mimba inatungwa yeye yupo busy tumsamehe bure ukute yeye ndio alipewa mimba..
 
Then kuna watu walitaka Mh. Spika asi-pull the trigger to hit the target.
So, he pulled the Trigger to hit the Target..... I like that. Ninalaani uzembe wa namna hii na ninafikiri liwe funzo kwa wengine wasije kutuaibisha tena.
 
..tatizo lako ni CHUKI.

..UVCCM mmeambukizwa chuki na wazee wenu ktk chama.

..wakiondoka hao, na mtakapobaki peke yenu mtaangamizana.

..hamjafundishwa kabisa ku-reason na ku-accomodate mawazo mbadala.
Nawe naona kama unapungua kiwango! senility? Sasa hao UVCCM wanamuonea wivu gani? Wivu wa kufukuzwa Ubunge? au wivu wa mkewe kujifungulia America hadi kupoteza ubunge? Tunajadili kilichotokea na maelezo yake. Wivu umetoka wapi boss?

Tusaidie kuwaomba wabunge waonyeshe kiwango badala ya ujinga (ignorance) juu ya kazi yao.
 
Hata aende wapi Hashindi TTakwimu zinaonyesha hajasingiziwa ingekua ni ghafla tuuu hapo sawa ila alishawahi kuwa ktk list ya WATORO leo utashinda kwa point ipi?? Ajiongeze tu
 
Kwako Mh.Joshua Nassar ,

Pole kaka yangu kwa changamoto zote ambazo umepitia na hongera kwa kupata mtoto Mungu ampe afya njema na amkuze.

Pia pole kwa kuvuliwa ubunge najua namna unavyojisikia vibaya ,inauma sana .

Ila nimesikia mkutano wako wa vyombo vya habari (Press conference), umeongea vizuri sana hasa ulipojishusha na kuomba Mh.Spika arejee maamuzi yake kwa busara kama mlezi.

Mh.Nassar najua sio muda huu wa kukulaumu ila ni muda wa kuambiana kuwa wapi ulijisahau kidogo na wapi uliteleza kidogo ,kwani kupitia kujua ulipoteleza ndio mwanzo wa kufahamu wapi pakutokea na kujifunza kwa wabunge wengine na kuishi kwa tahadhari.

Ni kweli kabisa ,Mh.Spika Ndugai alipaswa atumie busara kama mzazi na mlezi wa Bunge ,ila na wewe pia Mh.Nassari ulipaswa kuwa na tahadhari kwa kuangalia namna ulivyokuwa vocal critics bungeni ,kwa kuangalia aina ya spika na kalba yake,kwa kujiangalia wewe ni mbunge wa chama gani mpinzani au Chama tawala ,kwa kuangalia pia namna upinzani unavyokumbana na changamoto .Hayo yote yangekupa fahmu ya kujua tahadhari ipi ulipaswa kuchukua.

Mkutano wako na vyombo vya habari uliacha maswali kadhaa ambayo hayakujibika hasa ulipokataa maswali ,labda ni kwa sababu zako muhimu.

Mh.Nassar uongozi au kazi ya kuhudumia wananchi haina maana ya kuacha kuhudumia au kuuguza familia hapana hata kidogo,ila kuna taratibu zake za kufuata ,huku wajibu wa msingi wa kuhudumia au kuuguza familia ukabaki nao na usiathiriwe.

Mh.Nassar ,Spika labda na yeye hakutumia busara ila hata na wewe kuna majukumu fulani uliyaruka ,ukasau kuyafanya aidha kwa mawazo ya kuuguza shemeji yetu au kwa kusahau.

1. Mh.Nassar wewe ofisi yako ni Bunge la jamhuri katika taratibu mlezi na bosi wako ni spika wa bunge ,ulipaswa kuandika barua ukaipeleka au ikapelekwa na mtu kwaniaba yako kwa despatch book ,sababu kutokuhudhuria vikao sio jambo dogo ni swala nyeti ,Mh.Lema angekupelekea bungeni kwa despatch au mbunge yeyote unaye muamini hivyo ungekuwa na ushahidi wa kutosha leo.

Ila Mh.Nassar unasema ulimuomba msaidizi wa spika email ya spika ,Mh.Nassar ni kweli email au barua pepe iko kundi moja na registered mail, DHL, EMS n.k. Kwenye zote hizi, proof ya kupokea ni utumaji. Once sent, it's deemed to have been delivered.

Ila hofu yetu ni kuwa vipi kama aliyekupa email ya spika alitoa email ambayo sio active kwa makusudi ? ,vipi kama Mh.Spika aliona email yako ila akasema hajaona kwa makusudi au hajaiona kweli ? ,vipi kama mh.spika akiikana kwa makusudi email uliyotumia kuwa sio yake na akadai aliyekupa amekudanganya ?.

Turudi kwa hoja ya awali kuwa ulipaswa kupeleka au mtu akakupelekea barua ofisi ya spika kwa despatch book leo ungekuwa unatuonesha saini ya kupokea barua sio texts za whaatsp za msaidizi wa spika.

Pia ulisema Bunge la mwanzo wa January mwaka jana na Novemba mwishoni 2018 ,hukuwepo ,huku ukisema uliandika barua January hii ya 2019 ila hujasema huko nyuma ,kama ulitoa taarifa kwa spika au laa .

2.Mh.Nassar wewe ulikuwa unawakilisha wananchi wa Arumeru mashariki waliokuchagua kwenda bungeni ,hivyo wewe ulikuwa Agent kwao na wao kwako ni principal, hivyo wewe ulikuwa unawajibika kwao, sababu bungeni haukuwa unaenda chukua posho ila kuwawakilisha wao ,ulipaswa kutoa taarifa ya kiofisi (Ofisi ya Mbunge ) kwenda kwa wananchi kuwa hautakuwepo bungeni kutokana na changamoto za kuuguza ,hakika matatizo yameumbiwa binadamu ,wananchi wako wangekuelewa na wangekuwa wanakuombea dua na baraka kwa Mungu.

3.Mh.Nassar ,wewe ulipita kupata uwakilishi kupitia Chama chako ,Bungeni kuna ofisi ya Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani (KUB) ,ofisi ya party whip ambaye kaimu ni Mh.Selasini pia katika chama chako kuna uongozi Katibu au ofisi ya mwenyekiti .Hawa walipaswa kupata barua yako ya kutohudhuria bungeni kutokana na changamoto za afya ya shemeji yetu (Mke wako) na Afya ya shemeji yetu ilikuwa na uzito mkubwa hakuna ambaye angekataa ,ungepata pia baraka za chama chako na viongozi wako ,hata nakala ya barua ambayo ungetuma kwa spika ingetosha tuu kuwatumia na wao.

Leo Kaka yangu Nassar ungekuwa na utetezi kutoka pande zote ,watu wameumia na wanasikitika ila kuna sehemu nyingi uliteleza ukajisahau ndio maana wanashindwa wasimame kutetea namna gani.

Ushauri wangu kwako kaka yangu.

1.kaa pamoja na wanasheria wako uwasilikize kama kuna ushihidi wa kutosha (Evidences ) na (Vithibitisho) exhibits vya msingi ambavyo vitasaidia kama ukifungua kesi kupinga haya maamuzi ,simama imara pinga bila kuvunjika moyo kutafuta haki yako na ya wananchi wako.

2.Ila kama kweli wanasheria wameona hakuna ushahidi na vithibiti vya kutosha ,Nakuomba ujadiliane na viongozi wako kwenda kuongea na ofisi ya spika ,busara yake itumike hapa kama mzazi na mlezi wa wabunge wote .

Aguswe na afya ya shemeji yetu ,aguswe na changamoto ulizopitia na ukiri kuwa kweli ulikosea kutokana na changamoto za kuuguza shemeji yetu (Mke wako ) ,na usiache pia kumuomba Mungu akuvushe katika kipindi hiki kigumu hakika Mungu atakujalia ,na hakika Mungu atampa busara zaidi Mh.Spika katika kuangalia maamuzi yake upya .

Pole sana kaka yangu,Mungu ampe afya njema mdogo wetu na mama huko nyumbani ,awape uvumilivu wa kutosha katika kipindi hiki kigumu.



Abdul Nondo.


abdulnondo10@gmail.come

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mtoto kawadharau sana wananchi wake yaani asingeenda kupokea posho kwani ametumwa bungeni kwenda kusaini posho ?

Huenda kachoka siasa huyu mjinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom