Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Nianze kwa kusema kua,nimekua nikimfuatilia sana na kwa ukaribu Joshua Nasari,akiwa bungeni na Jimboni. Joshua anajua kujenga hoja,anajua kuipangilia hoja yake na akaeleweka na wenye akili. Kwale wakuunga mkono kila kitu huwa inakua ngumu kidogo kumuelewa Nasari.

Jimboni kwake nimepita mara nyingi,huwezi kumsema vibaya ukaeleweka. Anasifika kwa uchapakazi wake,na kuhudumia wananchi wake,na alikua kiongozi anayeongoza na kufuatwa na anaowaongoza siyo kwakua walimuogopa,hapa,kwakua tu walimkubali na kumuamini.

Nasari alikosea hapa,1.kulewa sifa,akadhani tupo kwenye zama zile.,2.kujisahau,na hili ni tatizo la wabunge karibu wote,wanakujaga kugutuka yakiwakuta kama hili la Nasari au kuanza kukataliwa majimboni kabla hata ya uchaguzi.
Mfano mzuri ni mkuu mmoja wa mkoa sasahivi,alienda msibani mwaka 2015,alikua hajawahi kufika eneo hilo tangu uchaguzi wa 2010,alichoambiwa na wafiwa ni"ondoka tuzike,maiti imegoma kutoka ndani mpaka uondoke",aliondoka kwa aibu mno.
3.Nasari alijawa na kiburi na dharau. Kwa mtu yoyote aliyeajiriwa,ukiomba ruhusa huondoki eneo la kazi bila kuhakikisha umeruhusiwa,vinginevyo utakua umejiruhusu.

Eneo lingine aililokosea Nasari,ni kudhani kuna huruma kwenye sheria,Ndugai anaweza kuwa na huruma,ila siyo sheria anazozisimamia. Nimesoma posts nyingi na comments nyingi humu JF,wengi wanamtukana Ndugai na kusahau kuwa siyo yeye,ni sheria.
Wanasema za mwizi ni 40,jitahidi kuhesabu,zikifika 38 tulia kidogo,kwamaana Nasari alipaswa kuwa anaenda bungeni japo mara mojamoja.

Alipokosea tena ni kubase tatizo lake na tatizo la mkewe,alokua anajifungua na mke,siyo yeye,ana dada zake,ana mama yake,mke ana ndugu zake wa kike,walitosha sana kuwa watu wa karibu mke wake,yeye alitakiwa awe kuhenya kutafuta nguo za mtoto na chakula cha mzazi. Sawa,ndoa inakiapo chake,sikatai,ila sometimes hawa tunaoapa nao ndo wasaliti wakubwa wa viapo hivyo,mwanaume uchague sahihi.

Lingine ni kulia mbele za kamera. Mwanaume halii hata sikumoja chozi likaonekana,labda msibani,nako kuna watu wa kukuambia"vumilia,jikaze,wewe ni mwanaume". Huambiwi haya kwa bahati mbaya,ni kukumbusha kuwa,uwe na ngozi ngumu. Unaanguka,unasimama tena.

Mwisho,sioni logic ya yeye kwenda mahakamani. Kufanya nini?,kumshtaki nani?,ili iweje?,katiba inasemaje?,ana barua ipi iliyomruhusu kutokuhudhuria vikao?,anataka kumfurahisha nani kuwa ameenda kuitafuta haki ila imeshindikana?

Yote haya,jibu lake ni kujisumbua,bunge ni muhimili mwingine,mahakama na serikali ni muhimili mwingine.
Pia,asome tu alama za nyakati.

WAASALAM.
 
Ninachojua tu na nina uhakika nacho ni kwamba Spika Ndugai ' hajakurupuka ' katika hili na kwamba Vigezo vyote na Masharti yote vilizingatiwa katika ' Kumpoka ' Jimbo Mbunge ' Mpokwaji ' Joshua Nassari. Sheria ni Msumeno na si kila akifanyacho Spika Job Ndugai ni Kibaya kwakuwa tu kuna Watu wana Chuki nae ambazo nyingi zimetawaliwa na kuchochewa na Siasa na Itikadi zetu. Binafsi nimeshawahi Kuanzisha ' Threads ' kadhaa hapa za ' Kumchana / Kumnanga / Kumsiliba / Kumsema ' Spika Ndugai kwa baadhi ya mambo katika ' Utendaji ' wake ila kwa hili naungana nae tena kwa 100% na hata huyo Mbunge ' Mpokwaji ' sina uhakika kwamba hata akienda / akikimbilia huko Mahakamani kuna atakachokipata kwani Watu walishachungulia mbali kwa marefu na mapana yake hadi ndiyo wakaamua Kumla Mtu Kichwa tena mapema ( asubuhi ) tu.
 
Ka-mtu kenu kajinga tu! Nahisi kalilengesha azaliwe huko kwa matumaini kwamba akikuwa, ataomba awe raia wa US. Hapo ndo utaona kwamba tuna wasio na akili ndani ya Bunge. Analipwa mshahara kwa kazi ya ubunge. Hiyo ndo ajira yake. Ni ajira ya kiapo cha kuwatumikia wananchi. Sasa yeye anakuja na hadithi za kusema eti familia yake ni bora kuliko ajira! Kwa maana nyingine familia yake ni bora kuliko wananchi anaowawakilisha. Soo low!

Ni mmoja wa vijana walsiojitambua kama wewe unayelinganisha Mbunge Ndugai na mke wa Nasari. MKe wa Nasari ni mbunge?

..tatizo lako ni CHUKI.

..UVCCM mmeambukizwa chuki na wazee wenu ktk chama.

..wakiondoka hao, na mtakapobaki peke yenu mtaangamizana.

..hamjafundishwa kabisa ku-reason na ku-accomodate mawazo mbadala.
 
Hata najiuliza hili lichama linaendeshwaje? Hakuna hata social life yaani, hata group la WhatsApp la viongozi basi! Yaani mikutano mitatu inapita mtu hahudhurii and nobody notices. Wote wanakuja kushtuliwa na barua ya spika!
Hivi Chadema hawawezi kufanya vizuri hata kitu kimoja jamani, kimoja tu
 
Nianze kwa kusema kua,nimekua nikimfuatilia sana na kwa ukaribu Joshua Nasari,akiwa bungeni na Jimboni. Joshua anajua kujenga hoja,anajua kuipangilia hoja yake na akaeleweka na wenye akili. Kwale wakuunga mkono kila kitu huwa inakua ngumu kidogo kumuelewa Nasari.

Jimboni kwake nimepita mara nyingi,huwezi kumsema vibaya ukaeleweka. Anasifika kwa uchapakazi wake,na kuhudumia wananchi wake,na alikua kiongozi anayeongoza na kufuatwa na anaowaongoza siyo kwakua walimuogopa,hapa,kwakua tu walimkubali na kumuamini.

Nasari alikosea hapa,1.kulewa sifa,akadhani tupo kwenye zama zile.,2.kujisahau,na hili ni tatizo la wabunge karibu wote,wanakujaga kugutuka yakiwakuta kama hili la Nasari au kuanza kukataliwa majimboni kabla hata ya uchaguzi.
Mfano mzuri ni mkuu mmoja wa mkoa sasahivi,alienda msibani mwaka 2015,alikua hajawahi kufika eneo hilo tangu uchaguzi wa 2010,alichoambiwa na wafiwa ni"ondoka tuzike,maiti imegoma kutoka ndani mpaka uondoke",aliondoka kwa aibu mno.
3.Nasari alijawa na kiburi na dharau. Kwa mtu yoyote aliyeajiriwa,ukiomba ruhusa huondoki eneo la kazi bila kuhakikisha umeruhusiwa,vinginevyo utakua umejiruhusu.

Eneo lingine aililokosea Nasari,ni kudhani kuna huruma kwenye sheria,Ndugai anaweza kuwa na huruma,ila siyo sheria anazozisimamia. Nimesoma posts nyingi na comments nyingi humu JF,wengi wanamtukana Ndugai na kusahau kuwa siyo yeye,ni sheria.
Wanasema za mwizi ni 40,jitahidi kuhesabu,zikifika 38 tulia kidogo,kwamaana Nasari alipaswa kuwa anaenda bungeni japo mara mojamoja.

Alipokosea tena ni kubase tatizo lake na tatizo la mkewe,alokua anajifungua na mke,siyo yeye,ana dada zake,ana mama yake,mke ana ndugu zake wa kike,walitosha sana kuwa watu wa karibu mke wake,yeye alitakiwa awe kuhenya kutafuta nguo za mtoto na chakula cha mzazi. Sawa,ndoa inakiapo chake,sikatai,ila sometimes hawa tunaoapa nao ndo wasaliti wakubwa wa viapo hivyo,mwanaume uchague sahihi.

Lingine ni kulia mbele za kamera. Mwanaume halii hata sikumoja chozi likaonekana,labda msibani,nako kuna watu wa kukuambia"vumilia,jikaze,wewe ni mwanaume". Huambiwi haya kwa bahati mbaya,ni kukumbusha kuwa,uwe na ngozi ngumu. Unaanguka,unasimama tena.

Mwisho,sioni logic ya yeye kwenda mahakamani. Kufanya nini?,kumshtaki nani?,ili iweje?,katiba inasemaje?,ana barua ipi iliyomruhusu kutokuhudhuria vikao?,anataka kumfurahisha nani kuwa ameenda kuitafuta haki ila imeshindikana?

Yote haya,jibu lake ni kujisumbua,bunge ni muhimili mwingine,mahakama na serikali ni muhimili mwingine.
Pia,asome tu alama za nyakati.

WAASALAM.
MTU nambariwani anayelia hadharani (kanisani) ni mkuu wa Mkoa wa Dar siyo Nassari.
 
Kama kawaida yenu tatizo sheria zinabagua watu na malengo na matendo ya Spika kama kweli mnafata sheria kwa kiwango hiki Spika alitakiwa kuwa mtu mwingine sababu huyu mwenyewe alianzia hospital na hakupumzishwa mpaka amerudi lakini yeye ndio amekuwa na matamshi na maamuzi yasiyo na hekima, utu na hila.

Narudia tena yeye ni captain sio kocha, yaani wenzie aliwakuta wabunge kabla ya yeye kuwa spika. Spika anatoka miongoni mwa wabunge. Alipashwa kumwita na kumpa nafasi ya kujieleza kuiga kwa mtu asiyekuwa manager ni makosa na tunataka kuona weledi katika mihimili na sio hizi sarakasi.

Watanzania tunataka haki, hawa sio tu hawatendi bali hata nia ya kutenda haki inamashaka. Ndio maana kila maamuzi yao ni kama hawajiamini.
Wasalaam!! Kwa mara ya kwanza naomba nimpongeze Spika Ndugui na uongozi wote wa bunge kwa hatui hii waliyochukua. Baada ya kumsikiliza Nassari na sababu zake za kitoto za kutokuhudhuria vikao vitatu mfululizo nimemdharau sana. Sisi ni watanzania na wengi tumeajiriwa au tumejiajiri.

Ni boss gani atakayekuvumilia zaidi ya miezi mitatu eti mwanaume unasubiri mkeo ajifungue? Huwezi angalau kwenda kwazini hata siku mbili kwa mwezi kisa unasubiri mkeo ajifungue? Nassari ni daktari?

Nassari alishindwa nini hata kumtuma mama mkwe wake kumuangalizia mkewe wakati akiwa kalazwa ili angalau atimize sehemu ya majukumu yake? (Kwatamaduni zetu za kiafrica inakubaliwa). Hata Magufuli mama yake yuko ICU lakini anafanya kazi. Watanzania tuache kulea ujinga kama wa huyu anayejiita dogo janja.

Nassari angekuwa mfanyabiashara angekaa hosipitali miezi zaidi ya mitatu kisa mke anasubiri kujifungua mtoto? Ungekuta hizo biashara? Mbona tunajipa majukumu ambayo sio yakwetu? Spika Ndugai nakupa Kongole uko sahihi. Watanzania tuache kuendekeza upuuzi kisa mazoea ya kujiona sisi tu na kwasababu tuna machozi basi tuishi kwa mazoea. Nasema Noooooo!!!!

Juzi walikutana msibani na Mh. DC na Mzee Sarakikya bila aibu akatamka yuko nje kuwatafutia wananchi wake misaada. Sasa leo hizo sababu kazitoa wapi? Naomba afuatilie suala la Makonda na makontena yake. Na pia sio kazi yake kuomba misaada ya hii nchi kwa wahisani. Yeye anatakiwa kuiambia serikali matatizo ya wananchi wake serikali itekeleze na sio kuzurura na kupiga picha nje kwa matanuo yake.
Naomba hili liwe fundisho kwa wawakilishi ngazi zote.
Na sisi watanzania tuache kuwaonea huruma wapinzani kwa baadhi ya mambo yao ya kipuuzi ambayo yatatutia aibu. Kama wapinzania wanapigania sheria na wawe tayari kuhakikisha hata wao na wafuasi wao wanafuata sheria na taratibu nyingine za nchi ambazo zimetungwa kwa mujibu wa sheria na katiba yetu.
Asanteni Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata najiuliza hili lichama linaendeshwaje? Hakuna hata social life yaani, hata group la WhatsApp la viongozi basi! Yaani mikutano mitatu inapita mtu hahudhurii and nobody notices. Wote wanakuja kushtuliwa na barua ya spika!
Hivi Chadema hawawezi kufanya vizuri hata kitu kimoja jamani, kimoja tu
Katibu mkuu wa chama yupo kama pambo, viongozi wamepoteana, wabunge kama wamepigwa ganzi.Waweza kuhisi wana mabifu ya chini chini.Ila huyu dogo kalewa mafanikio mapema.Kakamata vimilioni akiwa mdogo na route za nje mara kwa mara akasahau alikotoka.Ndo maana zamani Ubunge ilikuwa ni kazi za watu wazima kidogo, ingawa siku hizi na wazee wengine busara ni ZERO.
 
..wewe inawezekana huna mke.

..au kama una mke, haujapitia MTIHANI wa kujaribu kupata mtoto na ikashindikana kwa muda mrefu.

..unazungumzia biashara?!! Kuna watu wanafilisika kwa mtihani wa kupata mtoto.

..mbona Spika alikaa nje ya nchi muda mrefu akijiuguza?

Pointless dogo kachemka!
 
Tatizo sio kukaa nje ya nchi je umefuata taratibu za kutokuwepo kazini kwako.
 
Paternity leave ingemtosha
Huyu jamaa akubali kosa tu na akatafute kazi nyingine
Unashindwa kujua masharti ya kazi yako

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Nadhani cha kufanya ni yeye ajipange kugombea tena ubunge tu. Kwenye kampeni kama wapiga kura wataelewa hoja zake haitakuwa tabu kushinda
Kuna jimbo walipoteza wapinzani wakalichukua tena kwa siku za karibuni? Na umewasikikiza wazee wa kimeru walichokisema?
Hicho kitu hakipo, kwa kifupi tu
 
Tatizo sio kukaa nje ya nchi je umefuata taratibu za kutokuwepo kazini kwako.

..Nassari amejitetea kwamba alihudhuria vikao vya bunge vya September.

..vikao vya November hajavizungumzia, hivyo huenda hakuhudhuria.

..vikao vya Januari, alimtaarifu Spika kuwa ana udhuru wa dharura ya matatizo ya mke wake nje ya nchi.

..katika mazingira hayo, kwanini Spika amfukuze. Sheria inaelekeza afukuzwe baada ya kutohudhuria vikao vitatu.
 
Huo ushahidi wa kuhudhuria vikao upo wapi?yani hata wabunge wenzie washindwe kusema tarehe fulani alihudhuria kikao maana hata kwny kamati kuna zaidi ya watu 10.

Hilo suala la barua tunajua utaratibu ulivyo wa kupeleka barua kwny idara ya serikali lazima ubaki na copy iliyogongwa muhuri na sahihi ya mtu aliyeipokea.

Kama ni email alituma atuonyeshe copy iliyobaki kwny sent items zake za email maana inakuwa na saa na tarehe uliyotuma,teknolojia haidanganyi kama aliingia bungeni hata kamera za cctv zitaonyesha.
 
Ka-mtu kenu kajinga tu! Nahisi kalilengesha azaliwe huko kwa matumaini kwamba akikuwa, ataomba awe raia wa US. Hapo ndo utaona kwamba tuna wasio na akili ndani ya Bunge. Analipwa mshahara kwa kazi ya ubunge. Hiyo ndo ajira yake. Ni ajira ya kiapo cha kuwatumikia wananchi. Sasa yeye anakuja na hadithi za kusema eti familia yake ni bora kuliko ajira! Kwa maana nyingine familia yake ni bora kuliko wananchi anaowawakilisha. Soo low!

Ni mmoja wa vijana walsiojitambua kama wewe unayelinganisha Mbunge Ndugai na mke wa Nasari. MKe wa Nasari ni mbunge?
Kiongozi achana nao utaumiza kichwa bure. Haingii akilini hata sekunde moja. Nassari ni mpuuzi tu na akili za kitoto zunamsumbua
 
Kinacho nifurahisha sana ni kwamba upinzani wanajua uongozi tulionao awamu hii ni mzuri sana kuwahi kutokea nchini..

Nyerere ukweli usemwe watu walipanga foleni kununua mahitaji muhimu ya nyumbani.. kila mtu kimoja tu.. familia zilibebana hata kukaribisha ndugu wasaidie kununua hayo. Kwa JPM though upinzani wanamkubali kuwa ni kiongozi wanayemtamani hata awape vyeo ni hivyo tu wafanyaje sasa.. uoga, kuoneana aibu etc umewajaa

Mnavyomsema Nassari ni wivu tu juu yake umewajaa.. kama kweli anatamani kuwa chini ya JPM si mumuache aamue yake bila hata kumsemasema na wivu wenu. Hamkuwahi hata kumuongelea kama wakati wa Dr. Slaa akiwepo.. now midomo mnairefusha pioooooo..

Magufuli oyeeeeee
 
Back
Top Bottom