Nafsi imamsuta huyo! Aachane na uwekezaji wa hila hila, akome kurubuni watumishi wa umma kupora haki za wanyonge, tunamthamini kama mwanadamu mwenyeji wa Tanzania lakini tunachukia sana baadhi ya vitendo vyake! Ajirudi
Well said mkuu, kwani unafikiri Manji ni mtu wa kupoteza muda wake katika mambo ya Udiwani au Masuala ya Mpira? Anachota watu akili kuendeleza uwekezaji wake wa hila hila tu, hana Uchungu wa kweli kwa Taifa letu na ana jeuri sana - anatoa wapi ubavu wa kutaka kulumbana kwa mbali na Rais wetu - kama anaona anaonewa kwa nini aombi fulsa ya kukutana na JPM akajieleza - sasa mbinu zake za kutumia media kufikisha ujumbe utamsaidia nini - si ataonekana ni mkorofi tu anasumbuliwa na jeuri ya pesa - kwa hiyo as far as is concern kila mtu ni fair game kwanke na bila shaka alikuwa amezoea kufanya apendalo bila ya kushtukiwa au kuchukuliwa hatua yoyote.
Hivi anaweza kutuangalia usoni akatuthibitishia kwamba is so smart kibiashara kuliko Watanzania wengine in otherwords ana business acumen ya kushida tender zote za kumiliki Coco Beach, kuvunja nyumba zote Magomeni sijui kuwekeza kitu gani, sina hakika kama naye hana ubia kwenye project zinazo endelea eneo la Oyster bay Polisi ya zamani, kama hayo hayatoshi kakimbilia tena Mbagala kwa kutumia mgongo wa Udiwani kutaka kuteka viwanja/aridhi kubwa kwa malengo yake mwenyewe kwa kuwarubuni Manispaa eti atafanya ubia nao lakini mwisho wa siku manispaa ingevuna fedha kiduchu tu, hawawezi kuwa na ubavu wa kukagua vitabu vyake vya mahesabu - tusisahau kwamba watu hawa wana mbinu nyingi sana, siwasemi vibaya lakini ukweli ndio huo.
Watu wenye busara wakisikia Head of State anasema kitu fulani hakifahi basi muhusika una throw in towel kwa kutambua kwamba Serikali/Rais ana vyombo vya kung'amua ulaghai na ujaja janja husio na tija, badala ya kuheshimu ushauri wa Rais yeye anakuja na makaratasi sijui na viambatanisho gani na visingizio chungu mzima anagharimia Airtime na media nyingine kuendeleza malumbano yasiyo na tija kwa Taifa - all is interested in ni ku-get EVEN - 4 what if I may ask?- Si hilo tu anakwenda mbali zaidi kwa kutaka kulazimisha Watanzania wamuheshimu - kasahau kwamba heshima inakuwa earned hainunuliwi au kulazimishwa.
Watu wengi wamemshauri humu kwamba kama shida yake ni kuwekeza karibu na Beach basi atafute sehemu nyingine, yeye hataki - mbona kuna sehemu karibu na Hotel ya Bahari Beach kuanzia makutano ya barabara inayo kwenda Ras Kilomoni na barabara ya Ununio ukifuata barabara ya Ununio kuna sehemu kubwa wanaprocess chumvi ukienda mbele kidogo kuna Mradi uliyo kuwa wa Wasomali au Gadddafi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba naona mradi huo ulikuwa abandoned siku nyingi tu - sasa sehemu hiyo ni kubwa sana kuliko ya Coco Beach, kwa nini haendi kuwekeza huko.