Manji: Nchi yangu hainithamini

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,410
7,318
Kuna tangazo linarushwa Clouds, Manji Diwani wa Mbagala kuu ameonekana akilalamika sana juu moja ya kampuni yake kuhusu uendelezaji wa ufukwe Coco Beach. Ameeleza mengi mpaka suala la Magomeni.

Ameeleza mafanikio yake kupitia kampuni yake ya Quality Plaza na dunia inavyomthamini. Ila amesema nchi yake haimthamini.. Sijajua nini maana ya Manji kusema nchi haimthamini, anakusudia nini Maana nchi ni watu na viumbe..

Anasemaje sisi watanzania hatumthamini wakati tumempa udiwani Mbagala na tumempa uenyekiti Yanga.

Naomba Manji atupe ufafanuzi ni nchi haimthamini au viongozi ndio hawamthamini?

Atueleze vizuri..
 
Ahame inchi,namjua kama mpigaji na mdhulumati ukifuatilia apeech ya mengi JPM hawezi muonea ivi ivi tuu kuna rafu apo.
Maana utajiri wote alionao ukiuliza kodi alipayo sasa ndo unaweza zimia
 
Siwi mbaguzi, lakini suala hili lazima serikali ya Magufuli iliangalie kwa umakini: Sehemu kubwa ya Utajiri wa Tanzania imeshikwa na Wahindi.
 
Dhulma na ufisadi alioufanya kwa Taifa hili halafu bado anakula pilipili za kihindi uraiani anahisi taifa lote ni jinsia ya kike kasoro yeye ndio sababu ana kebehi eti Taifa halimthamini. Kwanza yeye si Mtanzania aseme tu ana hati ya kusafiria ya Tanzania. HATA BAba yake Marehemu Mzee Ghulum alikuwa na pesa maarifa mengi ya kibiashara lakin hakuwa Mshenzi kama Mwanae. Kamdhulumu mpaka Dada yake wa Pekee mirathi ya Baba yake itakuwa Hohe hahe wa Mitaani!!
 
Ahame inchi,namjua kama mpigaji na mdhulumati ukifuatilia apeech ya mengi JPM hawezi muonea ivi ivi tuu kuna rafu apo.
Maana utajiri wote alionao ukiuliza kodi alipayo sasa ndo unaweza zimia
Ni kweli anaweza kuhama nchi ila tujue tu atahama na ajira za watu kibao ambao mpaka sasa serikali bado haijajipanga kuwapa ajira wala kuwawezesha kujiajiri.

Siungi mkono ufisadi ila nawakubusha tujadili haya mambo kwa kuangali pande zote ili watu waweze kujipanga.
 
Mwambieni kuwa Yanga ni club tu ka Simba na Azam hata Toto Afr. Kuukwaa uongozi yanga si fagio la kuwafanya Watanzania wamthamini.
Wapo wanaotoa misaada mingi tu kwa ajili ya wenye shida mbali mbali, na bado hawajaomba hata ujumbe wa nyumba kumi. Yeye kuwa mfadhili wa Yanga tu ndo nchi yake imthamini?
Maji, jiulize umeifanyia nini nchi yako, si watu wamekufanyia nini. Mwaga misaada kila mkoa, Wekeza kwenye vyama vya kuondoa umasikini hata tubilioni tuwili hivi, kwani utafilisika? Mbona umeenda kuwabania wenzako kwenye udiwani hutaki watoto wa wengine wende chooni?? Manji, weye si wa kugombea udiwani tafadhali. Ungeomba Urais au ukishuka kidogo, uwe mbunge ka wenzaki kina Abood.
Ukitaka tukuthamini, kwanza jithaminishe kwetu
 
Kuna tangazo linarushwa Clouds, Manji Diwani wa Magala kuu ameonekana akilalamika sana juu moja ya kampuni yake kuhusu uendelezaji wa ufukwe Coco Beach. Ameeleza mengi mpaka swala la Magomeni.

Ameeleza mafanikio yake kupitia kampuni yake ya Quality Plaza na dunia inavyomthamini. ila amesema nchi yake haimthamini.. Sijajua nini maana ya Manji kusema nchi haimthamini, anakusudia nini? Maana nchi ni watu na viumbe..

Anasemaje sisi watanzania hatumthamini wakati tumempa udiwani Mbagala na tumempa uenyekiti Yanga? Naomba Manji atupe ufafanuzi ni nchi haimthamini au viongozi ndio hawamthamini?

Atueleze vizuri..
manji ni mwekezaji bepari, tena mlanguzi. mtindo wake wa kuwaza ni wa kibepari. sio kama bepari hana faida na maendeleo ya nchi ila mukimuendekeza atawanyonya hadi kubakia mifupa. bepari lazima kumdhibiti ili mwananchi aweze kufaidika na uwekezaji wake.
 
Back
Top Bottom