Nini kimewakumba Maswahiba wa Lowassa; Yusuph Manji na Rostam Aziz? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kimewakumba Maswahiba wa Lowassa; Yusuph Manji na Rostam Aziz?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lizaboni, Aug 19, 2016.

 1. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Wadau, amani iwe kwenu.

  Mtakumbuka kuwa, katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, Waziri Mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu kutokana na kashfa za ufisadi wa Richmond, Edward Lowasa, alitengeneza mtandao wa wafanyabiashara ambao ndio waliokuwa wanamfadhili kwenye harakati zake za kisiasa. Maswahiba hao walikuwa wanampa mabilioni ya fedha Edward Lowasa akiwa ndani ya CCM na hata baada ya kuhamia CHADEMA. Hawa ndio walioratibu kauli mbiu ya ULIPO TUPO.

  Hata hivyo, baada ya Uchaguzi wa Oktoba 2015, maswahiba hawa inaelekea hesabu zao hazipangiki. Rostam Aziz inadaiwa kuwa amekimbia nchi tangu Septemba 2015 na haijulikani yupo wapi kwa sasa ingawa baadhi ya taarifa zinadai kuwa yupo Uingereza na wengine wakisema yupo Uarabuni na wengine wakisema yupo Marekani. Wengine wanadai kuwa Rostam bado yupo nchini isipokuwa kwa sasa ameamua kujifungia tani kwa vile mambo yake kibiashara yanaenda hovyo. kafulia.

  Yusuph Manji, Diwani wa Mbagala Kuu, aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga kabla ya kuachia ngazi hivi majuzi baada ya wazee wa Yanga kushtuka dili la kumkodisha timu kwa miaka 10, inadaiwa kuwa hayupo Tanzania kwa sasa. Manji amelazimika kuondoka nchini kutokana na msuguano ulioibuka ndani ya klabu ya Yanga. Aidha, kabla ya hali hiyo, Yusuph Manji aliamua kujitoa kuongoza Quality Group, kampuni ambayo inadaiwa kutumia mwanya wa Manji kuongoza Yanga kuikopesha timu hiyo mabilioni ya fedha ambapo mpaka sasa timu hiyo inadaiwa Bilioni 5. Baadhi ya wana Yanga wanahoji, inakuwaje mtu ambaye aliahidi kuisaidia Yanga aidai fedha zote hizo? Ina maana kwa miaka yote Manji aliyoongoza yanga, timu haikuwa na mapato yoyote hadi deni limefikia kiasi hicho? Je hilo deni limetokana na nini? Wanachama wengine wameomba TAKUKURU kuchunguza deni hilo.

  Kwa ujumla, hawa marafiki wa Lowasa ni dhahiri kwamba walikuwa wanafanya biashara kijanja ujanja na ndio maana walikuwa wanatumia fedha zao hovyo hovyo kufadhili kampeni za fisadi Lowasa.

  Kutoweka kwa Manji, Rostam pamoja na akina Karamagi kumeenda sambamba na kufunga mdomo Edward Lowasa. Kwa sasa mwanasiasa huyo hayupo kabisa kwenye ulimwengu wa siasa na hata hizi harakati za CHADEMA za UKUTA Septemba Mosi ameamua kujiweka kando.

  Ni wakati sasa wa Lowassa kujitokeza hadharani na kuwaeleza Watanzania nini kimewasibu Maswahiba wake. Maana kule Mbagala Kuu wametapeliwa kwa kumpa Manji Udiwani kwa ahadi hewa. Yanga nao wametapeliwa. Na inawezekana na Lowasa naye katapeliwa.
   
 2. Sky Eclat

  Sky Eclat JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2016
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 24,662
  Likes Received: 65,316
  Trophy Points: 280
  Mzee Makamba alisema "Anamwaga mapesa makanisani, misikitini, akiulizwa mapesa unayatoa wapi, anadai marafiki zake wanampa, hawa marafiki wakupe pesa wewe ni shemeji yao umewaolea dada yao".
   
 3. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2016
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,856
  Likes Received: 10,502
  Trophy Points: 280
  Kila siku nakuambia mambo usoyajua usikimbilie kubwatuka!! Rostam Aziz alihamishia biashara zake nyingi Kenya!! Rostam aliuza shares vodacom ktk mpango wake wa kuhamishia uwekezaji Kenya na hawezi kufulia kijinga!!!
   
 4. Dwaso

  Dwaso Member

  #4
  Aug 19, 2016
  Joined: Jul 6, 2016
  Messages: 44
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  IMG-20160818-WA0025.jpeg
   
 5. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Mzee Makamba alikuwa sahihi kabisa
   
 6. Akasankara

  Akasankara JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 28, 2015
  Messages: 1,848
  Likes Received: 1,884
  Trophy Points: 280
  Wengine wanaukwaa Ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa wewe kutwa majungu mtandaaoni!
   
 7. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Na Yusuph Manji kahamishia biashara zake wapi?
   
 8. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaaaaaa! Sina haja ya kupata madaraka. Nafanya haya kwa mapenzi mema na chama changu
   
 9. T

  TRUVADA JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2016
  Joined: Jan 6, 2014
  Messages: 4,528
  Likes Received: 1,187
  Trophy Points: 280
  hivi KARAMAI mzee wa tics bado anamiliki 35 % za pale ticks au amesha toka
  , rostama kufilisika sio rahis mzee lizabon maana ana hisa na matenda mengi ya kifisadi kwenye migodi mingi sana kama buzwagi na buliynku, na pia kwenye vodacom ana superdealer kama SHIVACOM kupitia kwa akina FRED lowasa
   
 10. Dwaso

  Dwaso Member

  #10
  Aug 19, 2016
  Joined: Jul 6, 2016
  Messages: 44
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  Pole kwa kazi japo hawakukumbuki.
   
 11. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kufilisika kwa hawa mataikuni si sawa na kufilisika kwa TRUVADA.
   
 12. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Unataka nikumbukwe mara ngapi?
   
 13. The Businessman

  The Businessman JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2016
  Joined: Jan 9, 2014
  Messages: 7,236
  Likes Received: 6,880
  Trophy Points: 280
  Lowasa anawaumiza sana vichwa!!
   
 14. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Huo ni mtazamo wako Mkuu
   
 15. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2016
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 11,007
  Likes Received: 3,271
  Trophy Points: 280
  Aisee! Ina maana mgombea udiwani wa CCM alikuwa anatoa ufadhili wa hela kwa mgombea wa CHADEMA?
   
 16. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2016
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,702
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 280
  Lizaboni, amechanganyikiwa kama walivyo wanaCCM wenzake , akilala anamuwaza Lowassa tu.......Manji ni Diwani wa CCM so kama ni tapeli basi anawakilisha utapeli wa CCM ........
   
 17. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Urafiki hauna mipaka. Alianza hivyo wakati Lowasa akiwa CCM
   
 18. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2016
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Sijachanganyikiwa. Mimi ni msema kweli
   
 19. chuma cha mjerumani

  chuma cha mjerumani JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2016
  Joined: Dec 4, 2013
  Messages: 6,095
  Likes Received: 9,544
  Trophy Points: 280

  Ingekuwa mapenzi mema ungekuwa unamshauri rais awatumbue hao mafisadi wa ccm waliotufikisha hapa.
   
 20. nankumene

  nankumene JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2016
  Joined: Nov 12, 2015
  Messages: 4,935
  Likes Received: 4,207
  Trophy Points: 280
  mkuu hivi bado hujapata ukuu wa wilaya tu?au bado unaendelea na kazi yako ile ya ujumbe wa nyumba kumi
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...