Magwaya amekuwa wamoto hivi karibuni lakini. Bruno naye ni hatari. Lile shuti lake jana, daaah, Manyumbu watuuzie yule mhuni aisee. Kale ka Garnacho nako si haba. Onana aliharibu ila najiuliza mbona hata Manyumbu walivyotangulia, game ilikuwa wazi mno? Kwa nini 7hag hakurejea mbinu zake za premier league za kupaki basi na kuvizia counter? Badala yake wakawa wanapishana mashambulizi, mido kuko wazi mtu anakimbia bila kukabwa utadhani mchezo wa riadha na siyo mpira. Ile game hata ingeisha 7-7 nisingeshangaa.