(Essien, Obi),
(David Villa)
(kwa nini unakimbia category ya timu na unani-limit kwa makocha pekee?)
Chifu, unakumbuka umafia uliofanyika hadi Mikel akatinga London? Dogo alikuwa keshasajiliwa na United, hadi akapiga picha na jezi ya United, kama nakumbuka vizuri ilikuwa namba 21. Badae kasemekana kapotea; mara kuja kupatikana yupo London, anasema United hawakumshirikisha wakala wake na yeye anapenda kucheza Chelsea zaidi. Unakumbuka United na ile timu yake ya zamani waliifungulia kesi Chelsea, na hadi kwenda Chelsea, Chelsea ilibidi wafanye makubaliano na United na ile timu. Ina maana kuna pesa hapo ziliwatoka tena.
Kuhusu, Essien na Villa, United hawakuwahi kuweka ombi rasmi (na maana kuweka mezani ombi na pesa ya usajili), zaidi ya maneno ya vyombo vya habari.
Nimeweka makocha kwa vile katika post yako, awali ulisema timu na kisha ukasema makocha. Sasa, tunaelewa timu alizopita Jose, alizopita Pellegrini na hata Pep. Sasa yawezekana United ishashindana na Barcelona katika kusajili wakati Pep hayupo Barca. Vivyo hivyo kwa Pellegrini, pengine Shitty washashindana na United kipindi Pellegrini hayupo. Hata Jose, katika timu alizopita (Porto, Inter na Real), pengine timu hizo zilishashindina na United wakati Jose hayupo.
Sasa mimi nikasisitiza kwa makocha ili kuweza kueleza kwa muktadha huo.