Tufike mahali tudadavue tatizo liko wapi? Wengi ni kulaumulaumu tu hakuna ujuzi wa kutambua shida iko wapi.
Kipindi cha kwanza nafasi za kufunga za Manutd zilikuwa nyingi kama za Liverpool lakini ukabaji wa Liverpool ni bora kuliko wa Manutd na pia umaliziaji uligoma leo.
Kushinda hii ligi, inabidi Solksier apunguze striker mmoja wabaki wawili kwa sababu left na right backs wanaweza kushambulia.
Jawabu ni kumchezesha Dalot amsaidie Luke Shaw upande wa kushoto na kumweka bench Rashford.
Mabao yote yamepitia kwa Luke Shaw kwa sababu Luke Shaw anapenda kucheza kama Central Midfielder wakati ni left back
Hii inamaanisha Manutd hujikuta na three central defenders na inapungukiwa na left back na hapo Atalanta na Liverpool wameliona hilo na nina uhakika Spurs na Manchester City wameliona.
Ukiona Dalot hajapangwa next mechi ujue fika Manutd watafungwa kupitia left back. Mipira itaelekezwa upande wa left back na Luke Shaw ataendelea kugongana na Maguire na pasi zitapelekwa left back Luke Shaw atakuwa hayupo bao litafungwa.
Leo angepanga five defenders Liverpool hata bao moja asingelipata na angefungwa.
Kikosi cha ushindi
Left back Dalot, right back Wan Bissaka na three central defenders yaani Luke Shaw, Maguire na Lindelof.
Kati Fred, McTominay na Fernández
Washambuliaji CR7 na Greenwood.
Pogba auzwe desemba hii anawavunja moyo wenzie. Ukiona timu kubwa inamwendekeza mchezaji ambaye hataki kuongeza mkataba ndani ya miaka miwili kabla ya mkataba kwisha huyo hana mapenzi na timu. Hivyo, kumuuza tu hata kwa dau la kutupa.
Pogba mkakati wake ni kuacha mkataba uishe halafu ajiunge na aidha Real Madrid au PSG na dau la usajili apewe yeye badala ya Manutd. Inasemekana atalipwa £25MILL akijiunga na PSG kama mchezaji huria.
Pogba kiwango kimeshuka kwa sababu yuko kibiashara zaidi kulikoni kiuchezaji.