Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Tetesi zipo hivi;

United walikataa kuweka kipengele cha kumuuza Lingard kwenye mkataba wake wa mkopo ambayo ilikuwa ni kwa £15M kwa makusudi akipata form yake wapige cha juu, kwa sasa Lingard thamani yake ni £20M.

Inasemekana United wanataka kumshusha Declan Rice mwenye thamani isiyopungua £50M na ikiwezekana kufanya swap deal na West Ham United kukamilisha usajili huo. Wakimuacha Lingard West Ham na kuna uwezekano akaongezwa Matic na Jones kwenye dili hilo.

Anthony Martial huenda huu ukawa msimu wake wa mwisho akiwa United, ni wazi akiuzwa United watakamilisha dili la Sancho kwa ada ya uhamisho isiyopungua £50M wala kuzidi £80M.

United pia wanataka kununua CB kutoka Sevilla, Jules Kounde. Pia RB kutoka Norwich City, Max Aarons mwenye thamani ya £35M anafukuziwa na United pamoja na Everton na Bayern Munich.

Msimu huu tunaweza kutoka hivi:

Buy
RICE - DM
SANCHO - RW
KOUNDE - CB
AARONS - RB

Sell
LINGARD
MATA
POGBA
MATIC
JONES

Siioni United ikimuuza Fred ambaye yupo on form na muhimu katika maslahi ya kikosi kipana cha United, zaidi naona Pogba akiondoka na kuachia nafasi kwa watu kama VDB. Kuondoka kwa Pogba hakutaathiri sana kikosi chetu kama tukikamilisha usajili wa DM.
Tukimpata Kounde na Aarons itakuwa tumefanya sajili muhimu sana katika eneo la ulinzi, Kounde siyo mwenye kimo kirefu wala kasi kubwa sana ila ni moja ya mabeki wa kati hatari.
Aarons ni one of the best attacking RB, huyu jamaa ataleta challenge kwa Bissaka. Jamaa anajua kupandisha mashumbulizi vizuri na kumwaga maji vizuri bila kusahau defending skills nzuri.

Mpaka hapo tukiongezea na Sancho tutakuwa tumemaliza kazi, Siioni United ikinunua striker kwa sasa kutokana mahitaji yetu muhimu. Cavani akiongeza mkataba tutakuwa vizuri bila Martial huku tukiwa na options za Rashford na Sancho kwenye wings pamoja na Greenwood kama ST nikiamini msimu ujao utakuwa wa kuanza kuitetea namba hiyo endapo Martial atauzwa.
Pogba mngefanya swap mkapewa mkokotonombe.
 
Manchester City projected to win the EPL six points above Manchester United so pathetic View attachment 1703259
Umejaribu ila city na united watakuwa na gape kubwa la sio chini ya pts 15 mshinbdi wa pili hadi 7 wataachana na tofauti ndogo ya pt moja au mbili na wengine GD tu. Burnley na Fulam hazitashuka daraja badala yake Shefield United, Newcastle na West Brom ndizo zitakazokushuka daraja. Arsenal hatashika namba 11 over my dead body, bali namba 9 au 10. Liverpool hatamaliza top 4, hii ni uhakika kabisa, badala yake hiyo nafasi atachukua aidha Leicester city au Westham au Chelsea
 
Msimu huu tumefunga magoli mengi licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga ,wachezaji/timu haina progress wala consistency only Bruno ndio mchezaji mwenye consistency while Martial amedrop sana at least Rashford licha ya kukosa magoli mengi still amejitahidi

Our main problem this season ni defence ,tumekuwa tunaruhusu magoli mengi sana kizembe kwenye mechi 14 za EPL tumeshafungwa magoli 23 last season tulifungwa magoli 36 kwenye mechi 38 kwenye Champions league tumefungwa magoli 10 kwenye mechi 6
Last season tulifungwa magoli 36 msimu huu mpaka sasa mechi 25 tumeshafungwa magoli 32

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Nyie Manure mnajua hizi majeruhi zitawaadhiri leo?
  1. Edinson Cavani Gomez - Katoka kwenye majeruhi ya Misuli - bado fitness yake iko mashakani
  2. Paul Pogba - Majeruhi ya paja
  3. Donny van de Beek - Katoka kwenye majeruhi yaMisuli - bado fitness yake iko mashakani
  4. Scott McTominay - Katoka kwenye tatizo la Kugongwa - bado fitness yake iko mashakani
  5. Daniel James - Haijulikani
  6. Juan Mata Haijulikani
  7. Phil Jones - Majeruhi ya kichwa
 
Tuchel tangu achukue timu hajafungwa, katika jumla ya mechi 8, kashinda 6 na kutoa droo 2
Katika mechi na Atletico Madrid hawakupata hata on target moja, ball possesion ilikuwa 64% kwa 36% ya Atletico
Chelsea ni timu ya pili nyuma ya Mancity kwa kufungwa, Mancity kafungwa 16 Chelsea 25.

Karibuni Darajani
 
Nashukuru leo hawakumuweka yule mwendawazimu wa Manure anayeitwa Anthony Taylor

MATCH OFFICIALS

Referee
: Stuart Attwell
Assistants: Constantine Hatzidakis & Simon Long
Fourth Official: Andre Marriner
VAR: Chris Kavanagh
Assistant VAR: Sian Massey-Ellis
 
My Starting XI vs Chelsea

======

Henderson

Bailly Lindelof Shaw

Fred Matic Bruno Telles

James Greenwood Rashford

=======

Lazima tuwe compact na clinical sana ili tuweze kushinda hii game..

Sema najua Ole atakuja tofauti na ninavyowaza na itakuwa easy draw or lose..

GGMU.
 
My Starting XI vs Chelsea

======

Henderson

Bailly Lindelof Shaw

Fred Matic Bruno Telles

James Greenwood Rashford

=======

Lazima tuwe compact na clinical sana ili tuweze kushinda hii game..

Sema najua Ole atakuja tofauti na ninavyowaza na itakuwa easy draw or lose..

GGMU.
James hawezi cheza yuko majeruhi au fitness hana
 
Watani wangu vijana wa Ed Woodwork, fanyeni hima leo mhitimishe honeymoon ya huyo mjerumani wa Abromovich. Najua mnaweza kumpiga. Mpigeni ili angalau mmalize wa pili msimu huu japo it's sad mtamaliza msimu bila kikombe hata cha chai.
 
Nyie Manure mnajua hizi majeruhi zitawaadhiri leo?
  1. Edinson Cavani Gomez - Katoka kwenye majeruhi ya Misuli - bado fitness yake iko mashakani
  2. Paul Pogba - Majeruhi ya paja
  3. Donny van de Beek - Katoka kwenye majeruhi yaMisuli - bado fitness yake iko mashakani
  4. Scott McTominay - Katoka kwenye tatizo la Kugongwa - bado fitness yake iko mashakani
  5. Daniel James - Haijulikani
  6. Juan Mata Haijulikani
  7. Phil Jones - Majeruhi ya kichwa
Katika orodha hiyo regular starter ni Scot alone.
By the way mechi ya leo tutashinda.
 
Watani wangu vijana wa Ed Woodwork, fanyeni hima leo mhitimishe honeymoon ya huyo mjerumani wa Abromovich. Najua mnaweza kumpiga. Mpigeni ili angalau mmalize wa pili msimu huu japo it's sad mtamaliza msimu bila kikombe hata cha chai.
Mkuu wewe hapo Spurs unajilazisha tu, kwanini usirudi nyumbani kumenoga?
 
Back
Top Bottom