Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,382
- 10,951
Kwanza niliwaambia ManU it was a big mistake kumuweka Moyes kurithi mikoba ya SAF, aliyefaa kurithi mikoba ya SAF ni Harry Redknap.
Kwanza, ina maana wewe unaufahamu mpira wa Uingereza kuliko SAF? Unafahamu sababu za SAF kumpendekeza Moyes? Wewe una uelewa zaidi ya bodi nzima ya United waliokubali pendekezo la SAF?
Pili, Harry angefaa kwa sababu zipi? Ana kipi cha ziada kuliko David? Amefanya nini England ambacho kinamweka kuwa ndiye angefaa kuvaa viatu vya SAF?
Moyes yeye kaingia na kuondoa back management karibu yote ya SAF na kuweka yake.
Hii ni kawaida ya mameneja. Jose uwa anahama na coaching staffs wake; alipoondoka Graham Arsenal na kisha kuja Wenger kutoka kusikojulikana, aliweka majeshi yake miezi michache tu baada ya kuwa meneja.
Mameneja wanapoenda kwenye timu mpya, upenda kujenga legacy zao. Sasa huwezi kujenga legacy kwa kutumia majeshi ya aliyekutangulia. Lazima baadhi watatemwa na wengine kuachwa; lakini wale waliokuwa vigogo katika coaching staffs, ndiyo uachwa na meneja mpya kuleta wake.
Kwa mfano, pale United coaching backroom staff waliobaki na Moyes hadi sasa ni:
1. Richard Hawkins (PhD)---huyu ni mkuu wa kitengo cha human performance. Amekuja United mwaka 2008.
2. Brian Mcclair--huyu ni director wa academy, aliyejiunga United mwaka 2002.
3. Paul Mcguiness--huyu ni kocha wa under 18, aliyejiunga na United toka mwaka 1992.
4. Rob Swire---huyu ni physiotherapist, aliyejiunga United toka mwaka 1991.
Moyes kaja na:
1. Steve Round---huyu ndiye assistant manager sasa badala ya Mike Phelan.
2. Chris Woods---huyu ni kocha mpya wa makipa anayechukua mikoba ya Eric Steele. Pia ni kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Marekani chini ya Jurgen Klinsman.
3. Jimmy Lumsden--huyu ni kocha wa timu ya kwanza, anachukua nafasi ya Rene Meulensteen. Rene angeweza kubaki kwani David alimpatia ofa ya kazi nyingine tofauti na first team coach, lakini akakataa.
4. Robbie Cooke--huyu ni chief scout akichukua mikoba ya Martin Ferguson.
5. Phil Neville---huyu ni naye ni first team coach akisaidiana na Jimmy.
Pili alitambua kuwa anahitajika kiungo mahiri kusaidiana na Carrick....mwishowe akishia kuchukua garasha Fellaini......defenders are too soft and sloppy......
Sidhani kama meneja aliyeshinda tuzo za meneja bora wa ligi mara 3, anaweza akawa kamwona Fellaini mzuri, halafu wewe umwone galasha. Kumbuka tuzo hizo upigiww kura na mameneja wa timu za ligi. Ni SAF tu ndiye ameshinda mara nyingi zaidi yake, mara 4!
Fellaini ni mchezaji mzuri, atafit tu katika mfumo wa United.
mwaka huu ManU sidhani hata kwenye top 4 kama mtakuwepo......
Sawa..naona bongo pundits mmeng'ang'ana kweli na United kutokuwepo top 4!! Hayo uwa siyo malengo ya Man United! Eti kuwa top 4!! Man United uwa na lengo moja tu, nalo kushinda taji la ligi.
Sasa kama unafikiri kushinda taji kunahitaji sprinting start after 6 games, then you are very right on your own terms.
Ligi ni marathon running...so keep calm and enjoy the league.