Siyo wote mkuu Reguillon ni fullback wa kawaida tu siyo upgrade ya Brandon wala Luke Shaw.
Fullbacks za Real Madrid za sasa ni za kawaida tu na Marcello alikuwa na majeraha ya muda mrefu kwanini Reguillon hakuchukua nafasi.
kama pesa ipo ya kutafuta mlinzi mwengine wa kushoto mwenye kuvuka ubora wa hawa tulionao basi si vibaya kama tutasajili tena mlinzi wa pembeni kwa mara nyengine (dalot, wan bissaka, luke shaw, rojo, darmian)
nikimuangalia brandon williams anavyocheza inaniwia vigumu sana kuamini ya kwamba siku moja ataweza kufikia level ya ubora waliokuwa nao walinzi wengine wa kushoto waliokuwa wanatumia mguu wa kulia kwa kiwango kikubwa sana (mfano phillip lahm na javier zanetti).
kwa ufupi
brandon williams anateseka sana pindi anapocheza upande wa kushoto na kuteseka kwake kunapelekea timu yetu iwe dhaifu sana pindi tunapokwenda mbele kushambulia (kiwango kibovu cha rashford na kuumia kwa luke shaw kulipelekea kwa kiasi kikubwa upande wetu wa kushoto kuwa butu mwishoni mwa msimu)
brandon williams hana msaada mkubwa sana tunaposhambulia (si hodari wa kuoverlap, passing accuracy bado ni tatizo, hawezi kumzidi mpinzani akiwa outside, hawezi kupiga krosi ya uhakika kwa kutumia mguu wa kushoto) ukimlinganisha na luke shaw (japokuwa shaw hana maamuzi bora tunapofika eneo la hatari lakini bado analeta faida kubwa sana, link-up na uhuru kwa winga wa kushoto).
kama ni kweli tunahitaji kufanikiwa kupitia huu mfumo wa 4-3-3 basi tunapaswa tuongeze nguvu kubwa sana eneo la pembeni, ni lazima tuwe na wachezaji wenye uwezo wa kupenetrate, break low blocks and provide natural width, kwa sasa hatuna traditional wingbacks wa uhakika lakini kufidia tatizo hili hatukupaswa pia kukosa attack-minded fullbacks ((nimeumizwa sana na usajili wa mchezaji aina ya
wan bissaka kwa gharama, huyu hana kisingizio cha kutumia mguu wa kushoto akiwa ni mlinzi wa kulia kama ilivyo kwa brandon williams)
angalia timu kama real madrid wanamtumia marcelo wa zamani, juventus (alexsandro), barcelona (jordi alba wa zamani), robertson (liverpool), davies (bayern munich) na wote hawa wanatumia miguu ya kushoto ya asili.
ikiwa ole hana imani na
diogo dalot basi ni bora auzwe halafu brandon williams arudishwe upande wa kulia apambane na wan bissaka.
uzuri ni kwamba wan bissaka na brandon wana takwimu nzuri sana za kiafya,
ningeliitumia nafasi hiyo kwa kumtoa kwa mkopo
ethan laird akapate uzoefu. Kuendelea kumtegemea brandon williams upande wa kushoto kama ni backup ya mgonjwa luke shaw itakuwa tunazidi kutengeneza tatizo (kwa sababu kiwango cha rashford hakieleweki)