HABARI ZILITOKA HIVI PUNDE.
KIPIGO CHA MAN CITY, CHAMFUKUZISHA OLE
HABARI zilizotoka asubuhi hii, ni Ole kutupiwa vilago vyake baada ya Manchester City kumpiga Manchester United magoli ma3 kwa moja pale Old Trafford.
Ulikuwa ni usiku mbaya sana kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kutolewa kwenye FA Cup na timu hasimu wanayotoka Jiji moja la Manchester. Goli pekee la United lilifungwa na kinda M-Brazil; Pereirra huku Man City tukiona wakimiliki mchezo mzima kwa kipindi cha kwanza ambapo KDB au De Bruyne akiwa mwiba mkali langoni mwa Manchester United.
Manchester United iliwakosa watu wake muhimu kama vile Scott McTominay na Paul Pogba ambao wote ni majeruhi. Pia Tony Martial alikuwa anatoka kuuguza vijeraha vidogo alivyovipata siku za nyuma hivyo hakuonyesha cheche zake. Meneja wa Manchester United alijitetea hivi mbele ya waandishi wa habari.
Mbali na hapo, Fred Boy mapafu ya Mbwa, yeye alibahatika kucheza nafasi ya DM au tuseme Defensive Midfield (Namba 6) huku Perreira akiua AM - Attacking Midfield na Lingardinho akimaliza CAM as namba 10. Kwa hali halisi unaweza kuona hizi Middle zinaweza kufanywa nini zinapokutana na wababe kama KDB, Fernadinho, Silva nk. Na wakati huo Phil naye alikuwepo uwanjani akizungushwa na kugeuzwa kama chapati na KDBizo.
Baada ya matokeo haya, ndipo uongozi wa familia moja ya Kimasai huko Arusha vijijini uliamua kumtupia vilago vyake ndugu Ole Sendeka baada ya kukataa kumuoa mtoto wa tajiri ng'ombe mmoja wa kijiji kinachopatikana huko Arusha. Ole alichukua vilago vyake viwili alivyoshonewa na mama yake pamoja na begi lake la nguo na kisha kwa masikitiko aliiambia familia yake kuwa watamkumbuka sana.
Tukio hili lilitokea saa sita ya usiku punde tu mechi ya Man U na Man City kuisha. Ole Sendeka ambaye alifika studio za
Upepo wa Pesa zilizopo Chato, alikutana na akina
Mshana Jr na kumpa mkasa mzima na mimi nikaamua kuuleta mkasa huu hapa
JamiiForums.
Asante.