Alafu mechi na Norwich Shaw anaanza pumbavu, Dogo Brandon Williams licha ya Jana kuteleza ila alikuwa poa na hata alipoteleza alikuwa anajaribu kuokoa sehemu ya Jones pumbavu.
Brandon hatabiriki mpira anapigaje anaweza kusogea golini letu na mpira mkamvamia akala kona mbio mbio na accurate pass kwa Fred tofauti na Shaw au Young.
Nataka Dogo aanze na Norwich.
Greenwood tusimuonee dogo ana roho safi hata pale alipompa assist Rashford angekuwa ni Rashford angebutua ovyo.
Kingine kampasia Lingard jamaa ovyo kisigino kurudisha.
Wan Bissaka afadhali anapandisha kidogo.
Hili suala la David James kupigwa Sub naomba ufafanuzi please.
Now tunajua umuhimu wa Maguire aseee!
Kuhusu Lingard aaah! Duh! OLE OLE OLE wewe kakupa nini huyu jamaa ovyo tu.
Kama Norwich Maguire asporudi wakuu mnaonaje tukawa na 3 backs 5 mids na two forward.
Mids za kupanda na za kusaidia defense maana Jones ujinga mtupu.
All in all hii timu siku hizi inatabirika. Kuna wachezaji wasiotabirika.
Greenwood, Williams, Matic, Fred hasa pass zao tatizo wakiwapoteza wapinzani sasa kimbembe pasi wampigie nani, mpira ukitua kwa lingard unaishia kuburuzwa, ukitua kwa Rashford ustaa mwingi, kwa Perreira shuti za ovyo mara chache assit ukitua kwa Greenwood kuna afadhali.
Rashford anaboa kitu kimoja hana teamwork ni uchoyo na kutaka sifa ona free kick inapigwa ovyo.
Na kocha mwe mwe mwe hawezi hata kujiwekea vitunguu machoni aonekane amekasirika dah jamaa kakunja nne madogo wanachomesha timu.