Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

tuchukulie hivyo hivyo unavyotaka wewe ya kwamba leicester city ni upepo wa kisulisuli,

timu bora haijengwi kwa mwaka mmoja kama tutatumia reference za team nyenginezo kama liverpool ya klopp (kwa siku ya leo sipo kabisa kwenye huu mjadala wa kujenga timu imara ya muda mrefu itakayoturudishia nyakati za furaha kwa sababu nafahamu fika tumekosa football heritage hivyo basi tutahitaji uwekezaji mzuri wa wachezaji wenye kuendana na mfumo wa mwalimu aliepo pamoja na muda kama ulivyozungumza na hilo tumeshaanza kuliona baada ya kushuhudia uwekezaji wa wachezaji wote watatu walioletwa na mwalimu wanafanya vizuri sana na baadhi yao pia wakiondolewa mfano fellaini ambaye si mchezaji anayeendana na philosophy tulioizoea pale carrington na wengineo wataondolewa)

lakini huo ujengaji wa timu bora isiwe sababu kuu ya kuamua kujitoa ufahamu kwa makusudi pale timu inapofanya vibaya, wewe jenga timu yako lakini hakikisha timu inaendelea kupata matokeo yenye kuridhisha na ndio maana kwa kulifahamu hilo uongozi wa man utd kwa kiasi kikubwa sana japokuwa hawajaliweka hadharani wamewawekea makocha kipaombele kikuu cha kuhakikisha timu angalau inapata tiketi ya kushiriki UEFA kila msimu (hatuna uwezo wa kushinda ubingwa basi hata UEFA ndio itushinde licha kufanya uwekezaji mkubwa kila mwaka)

achana na mlango wa europe league na utapataje tiketi ya uefa kama utashindwa kuzifunga timu ndogo ambazo ndio nyingi?

kama nipo sahihi
tumepata alama 14/18 dhidi ya timu kubwa (well done)
tumepata alama 10/30 dhidi ya timu ndogo (poor, poor, poor)

tunachohitaji ni kuiona nguvu ile ile yenye kuambatana na nidhamu ya uchezaji kwenye mechi kubwa pia tunaitumia kwenye mechi ndogo na mwenye wajibu wa kulisimamia hilo ni mwalimu hata kama yeye si mchezaji wa uwanjani ila kumbuka mtoto anapokosa nidhamu mtu wa kwanza anayepaswa kuangushiwa lawama ni mzee ndio maana mwisho wa siku anayetimuliwa kazi ni mwalimu na si wachezaji.

=============================================
brendan rodgers ameanza kufanya kazi february 2019 pale leicester city.
ole gunnar solksjaer ameanza kufanya kazi december 2018 pale man utd

kwa nini leicester city wanacheza vizuri zaidi ya man utd
kwa nini leicester city wanapata matokeo mazuri zaidi ya man utd.

tunapaswa tujitofautishe na blackburn rovers ya damien duff (wazee wa kukamia mechi kubwa)
Umenena vema bro
 
Yope remix ndani ya Etihad Stadium
tapatalk_1575825680290.jpeg
 
Back
Top Bottom