Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Tatizo sio martial . Timu trash United yote imeoza . Uzeni timu nzima hadi ole sendeka sosha msajili upya
CF ni Martial unategemea utafunga!! Mchezaji mvivu sana. Hajapiga hata shuti moja. Pereira leo alikuwa chini ya kiwango chake na amepiga shuti tatu na sio CF.
 
Poleni sana mashabiki wa ibilisi fc,Hawa Bournemouth wamewalaza mapema,muache kukamia mechi kubwa na kidondosha points kwa timu za kawaida.
Hao ndo Nyubuzi fc . Wanakamia karaghabao cup . Wananyooshwa na bounermoth
 
√Hiki kinachotokea ndo kile tunacholia nacho kila siku..consistency..Martial anacheza mechi moja vizuri nyingine hovyo..Tunahitaji No 9 wa kueleweka

√Sijawahi kumkubali Perreira..ni bora kwenye kitu gani??..Tunahitaji play marker ambaye pia anaweza kutoa key passes za uhakika

√Kuna watu wanamlaumu sana Fred ila mimi naona anapambana anapass foward,anatuliza timu n.k..anamiss kitu kwenye kukaba,anakuwa na Papara..

√Hii timu bila Pogba hatuwezi kabisa kutengeneza nafasi za kueleweka..Tunaomchukia huu ukweli lazima utuume

√On and Off that our mood this season..leo sherehe kesho msiba..inabidi tuzoee tu,no way
wan bissaka ameendelea kuwa useless kwenye kupandisha mashambulizi kama kawaida yake, siku tutakayopata mwalimu mwenye fikra za guardiola au klopp basi tutaingia tena sokoni kwa lengo la kutafuta mlinzi mwengine wa kulia, ina maana tutakuwa tunaendeleza tabia ile ile ya kusajili wachezaji kwa kuangalia zaidi mzuka wa mwalimu.
ndio maana tetesi zake za usajili sikuzifurahia kwa kiwango kikubwa sana.​

bora ashley young kuliko wan bissaka kimchango kwenye kupandisha mashambulizi, timu inasumbuliwa na tatizo la kukosa wachezaji viungo walio creative jambo linalopelekea utatu wetu wa mbele uonekane butu lakini cha kusikitisha jamaa pia na yeye wala haleti faida kutokea pembeni, waangalie liverpool wanavyofaidika na walinzi wao wa pembeni muda wote wa mchezo.
wan bissaka benchi, brandon williams on ili ashley young arudi upande wa kulia

hivi timu yetu inafanya mazoezi ya kumiliki mpira pindi wachezaji wanapokuwa kwenye presha, mbona tunabutua mipira ovyo kama vichaa?​
 
Poleni watani ngoja niende jukwaa pendwa la Arsenal maona huku lawama tu.
 
Back
Top Bottom