Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Enzi hizo damu ya Kabumbu Imetamalaki Mwilini,
Club Chelsea Nilikuwa nafuraha sana ikichezea kipigo toka kwa Man u.

Oles At The Wheel,Hongera Ole kwa kumdhibiti Chelsea Sugar dady...Japo naimini Hii kazi Man U imekuzidi Uwezo.


Jose Chelsea alimsumbua sana Mzee Alex.



"You Can Change Your Wife,
Your Politics,
Your Religion,
But never,Never Can You Change Your Favourite Football Team."
 
Brandon william ni hatar sana hao madogo watatu watatupa msaada sana siku zijazo
Instagram%20media%20-%20B4QZrARlKet%20(%201350%20X%201080%20).jpeg
 
Yamekuwa haya tena?
Kabla ya kugegedwa na Man United kwanini hukuwahi kusema kauli hii?
City hawezi kuacha vikombe FA EPL EFL wazo langu ni mashabiki wa city agenda yao ni kujilimbikizia vikombe kama nyinyi na utd wakati wa ubora wenu
 
City hawezi kuacha vikombe FA EPL EFL wazo langu ni mashabiki wa city agenda yao ni kujilimbikizia vikombe kama nyinyi na utd wakati wa ubora wenu

Nyinyi Chelsea hamutaki vikombe?
Umeona EPL huna ubavu!
Umeona CL ni msindikizaji!
Carabao ndiyo huyo umetandikwa nyumbani!
FA unaona kunawaka moto!
Sasa unaishia kumsifia jirani!

Bado na UCL pia mpe Man City
 
Nyinyi Chelsea hamutaki vikombe?
Umeona EPL huna ubavu!
Umeona CL ni msindikizaji!
Carabao ndiyo huyo umetandikwa nyumbani!
FA unaona kunawaka moto!
Sasa unaishia kumsifia jirani!

Bado na UCL pia mpe Man City
Wasiwasi wako tu Chelsea hatutoki patupu mark my word walisema Sarri hajawahi kushinda chochote lakini mwaka wake wa kwanza akashinda Europa siwezi shangaa Chelsea kushinda kombe kwa miaka hii 15 ni kawaida ila nitashangaa city kukosa trophies 2 kwa uwekezaji wao
 
Hizi picha zimenikumbusha ugomvi uliokua ukizuka kati ya Keane na Vieira.Ugomvi usioisha
Roy Alikuwa Mtata sana,Baada ya Eric Cantona Kuondoka Jamaa akawa zaiidi ya Mtata,Anakemea Uzembe na uvivu dimbabi kwa kila njia iwe ngumi au Mateke na sentensi za Makaripio lukuki.

Ferguson aliwahi kuelezea njisi alivyo Muondoa Old Trafford,Ilifika kipindi Roy aliingia Mutv kisha akawapa Makavu/Maneno mazito karibia kila Mchezaji,

Mfano Fletcher aliambiwa kurukaruka kwakwe uwanjani tayari kashajiona superstar akirudi Taifa basi bichwa hilo.

Wachezaji waliokuwa na uwezo walau kidogo wa kusimama naye hata kwa kujibu vijineno viwili vitatu walikuwa Van N & Edwin Van D,Wengine Wote kama kondoo.

Ferguson alivyoona hivyo akamuita kisha akamwambia shukrani kwa kazi iliyofanya klabuni,Nadhani ni Wakati wa Kuagana kwa Amani.

Roy Akasema Mzee hukuwa hivi Umebadilika haya si maneno yako,Mzee akijibu haya mabadoliko ndio yanifanya niwepo hapa..

Roy Keane alikuwa anamgwaya sana Eric Cantona,Eric alikuwa ni chuma cha Pua mbaya zaiidi Jamaa alikuwa msomaji mzuri wa vitabu na Falsafa lukuki za akina Hegel mpaka Kwa mbabe wa Alexander The Great bwaana Diogenes of snope..

Kuna picha nimeiweka ya Eric Cantona akitoka Uwanjani akiwa na polisi huko Uturuki mechi ilikuwa ya vurugu Uefa,Walivyoingia vyumbani wachezaji Wote Jamaa akataka arudi uwanjani amtafute moja wa askari aliyemzongazonga amgawie dozi kamili,

Wachezaji Wote, wengine wakipiga magoti wakimuomba asirudi uwanjani itakuwa balaaaa sana,Jamaa Mzuka Ukopoa.



Roy & Vieira Wameacha Alama na burudani Epl.....Great Captains.
 
Back
Top Bottom