Nilichoona
Fred na Mc Terminator walitisha sana kati kati, kwa Scoty tuna mtu wa maana kweli kweli
Rashy anaweza ku score goli, lakini sio aina ya namba tisa wale tunaowajua (niliwahi kusema, Rashy anaweza kukupatia goli kati ya 15 na 25 kwa msimu)
Kwa namna United inavyocheza sasa na aina ya wachezaji waliopo, itaendelea kupata penati za kutosha. Wachezaji wa mbele wana pace ya kulazimisha beki ya upinzani kucheza faulo. DJ atatuletea penati nyingi sana.
Kuna watu humu (kutoka vitimu vidogo vidogo) wanataka kutuaminisha kwa kuwa United anafunga kwa penati, basi penati zimefutwa kwenye mchezo wa soka. Hawa hawa watu walimsifia sana Hazard, Salah, Kane, Aguero n.k. walipoongoza kwa ufungaji wa magoli yakiwemo mengi ya penati.
Goli la Chelsea limepatikana sababu ya makosa ya mabeki kwa sehemu flani, hivyo beki ya kati kwa sehemu inahusika. Hata hivyo lazima tuisifu beki na kiungo yetu, kwani goli moja walilopata Chelsix ndio shot on target pekee waliyopiga
Good morning kwa hisani ya Scot Mc-terminator