Dirisha la usajili ndio hilo limefungwa
Sasa club iangalie kupata Sporting/Technical Director na si lingine
Shabiki yoyote angependa kuona sura mpya kikosini, hiyo ndiyo hulka yetu.... Yaani hata Rojo angekuwa yupo Benfica juzi tungetamani sana jana atangazwe kuwa mchezaji wetu mpya. All fans are desperate for new faces
Kuna baadhi yetu Nimeona wanawatamani Arsenal kwenye usajili wao na wanauponda usajili wetu. Amin Amin nakwambia, hata Man Utd wasingesajili mwanzo wa dirisha (kama ilivyokuwa kwa Arsenal) halafu mwishoni tuje tusajili Daniel James, Wan Bissaka na Maquire na Arsenal wange fanya usajili huu walioufanya, mapema dirisha lilipofunguliwa, tungeona sisi tumesajili vizuri zaidi
Kiujumla kwa mujibu wa mahitaji yetu na mahitaji ya Arsenal, naona sisi tuna afadhali kuliko wao. NIMESEMA TUNA AFADHALI, SIJASEMA NIMEREDHIKA. Bado naamini tulimuhitaji sana BF asaidiane na Pogba, tulihitaji sana CDM na winger wa kulia, japo hizo nafasi mbili za mwanzo nilizozitaja ndio zilikuwa muhimu sana.
Ukiniambia mimi ni rank timu zipi zilizosajili vizuri (kwa top six) kulingana na mahitaji yao, wa kwanza nitampa Man City, wa pili Spurs na wa tatu atakuwa United kisha Arsenal na Liverpool. Chelsea wao hawakusajili kabisa
Kiukweli tulihitaji sana, beki wa kati na wa pembeni kulia, pia tulihitaji winger ambao watatoa nafasi kwa Martial na Rashford kucheza zaidi kwenye nafasi wanazozipendelea, na hilo ndilo lilifanyika. Huu usajili wa kuzingatia mahitaji ndio unanifanya niseme tumesajili afadhali. Lakini kiujumla usajili wetu msimu huu hauridhishi lakini utaifanya timu kuwa imara kuliko ilivyokuwa msimu ujao
City wameimarika zaidi. Liverpool wataendelea kuwa na changamoto ya depth ya kikosi, Arsenal pia wata improve beki yao ya kushoto na winger yao ya kulia na Spurs watatisha zaidi.
Kiujumla dirisha hili lilipita halitakumbukika sana vichwani mwetu washabiki wa United.
Ngoja tuwaangalie pia mazao kutoka academy akina Mc Tominay, Pereira, Tuanzebe, Greenwood, Gomes, Chong kama wataweza kutuongezea nguvu pale palipopungua.
EPL IS BACK