Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mimi nilisema toka wiki mbili zilizopita kuwa man u haitasajili mtu mwingine zaidi ya Maguire.

Katika kipindi cha Woodward ni msimu mmoja tu man u iliweza kusajili wachezaji zaidi ya watatu msimu mmoja
Dirisha la July 2014, tulimsajili. Daley Blind, Morgan Shenerndalin, Dimaria, Memphis Depay, Marcos Rojo,,Ander Herera Victor Valdez.
Official we will not sign anyone now maybe january
 
tetesi:
Man Utd wapo kwenye mazungumzo ya kumnasa Mario Mandzukic kutoka Juventus kuziba pengo la Romelu Lukaku aliyetimkia Inter Milan.

baadhi ya wadau walitwambia ya kwamba bwana ole gunnar havutiwi na style ya uchezaji ya lukaku, swali la kujiuliza mario mandzukic ana utofauti gani na lukaku?
Mandzukic yupo Menopause ya mpira. Ila tuliambiwa anatafuta vijana asuke kikosi.
 
Mkuu mandzukic akija Ni aina ya mchezaji ambae hatachukia kukaa benchi, amebeba makombe yote club level, kacheza ligi mbalimbali, na ana fainali ya world cup, experience yake itawasaidia chipukizi kujifunza zaidi. Akija atakuwa tu impact sub na kucheza makombe ya mbuzi.
Zlatan ni bora mara mia kuliko Mandzukic.

Unanunua mchezaji atakaekaa benchi??
 
Hapa nakubali mkuu, tunamiss midfield ya kufanya tumchezeshe pogba Kama 10, Kuna sehemu niliona stats za pogba ana contribution 1.4 ya Goli Kama no 10, Ina maana either anafunga ama anatoa pasi ya goli Kila mechi.

Labda Fred atafufuka mkuu, acheze na McTominay chini na pogba apande.
Labda Fred atafufuka..

Bro, dunia ya leo unaishi kwa labda?

It's either aoneshe kiwango au aoneshwe mlango wa kutokea.

Ndio maana tunajaza deadwoods kwenye timu.
 
Chelsea munaichukulia dhaifu lakini Man united wanajua wanaenda kukutana na kigongo cha chuma mziki mnene, kipigo kipo pale pale..
 
Labda Fred atafufuka..

Bro, dunia ya leo unaishi kwa labda?

It's either aoneshe kiwango au aoneshwe mlango wa kutokea.

Ndio maana tunajaza deadwoods kwenye timu.
Kuna wachezaji wanadeserve second chance mkuu, lindelof msimu wa Kwanza alizingua pia ila Sasa Hivi amekaa vizuri, Fred msimu huu ana nafasi ya mwisho kuprove, maana msimu wa kwanza tunasema anazoea ligi.

Mwisho wa msimu uliopita pia alijitahidi mechi alizopangwa. Naamini mtu ambae amewahi kucheza timu ya Taifa Brazil sio Garasa Kama tunavyoaminishwa.
 
So far Arsenal wamesajili vizuri sana msimu huu.
Nawapa Arsenal heko kwa usajili wa Pepe na Tierney lakini sio David Luis

Bado beki yao (kati) sio nzuri. Pia midfielder yao bado ni kupigania top six

Mbele ndio wapo vizuri especially central attackers
 
Mwaka Jana Fulham wali tu outspend na mwaka Huu Aston Villa, rekodi yetu inaendelea, Timu zinazopanda daraja Zina ambition kuliko sisi.
Kwa jicho Kali kabisa na hiyo Sio dalili njema kwa timu inayojipambanua kutafuta makombe.

Unless tukubalie kwamba na sisi now days tumeyaishi na kuyazoea maisha ya mid-table clubs Kama hizo Kina Fulham.

Kikosi chetu hakitakua na miujiza yoyote huu Ni ukweli tuukubali na kujiandaa kisaikolojia ili tusiumie.

Eneo la katikati na eneo la ushambuliaji bado sisi Ni wakaida mnoo.
 
Zlatan ni bora mara mia kuliko Mandzukic.

Unanunua mchezaji atakaekaa benchi??
Yes Ni kawaida mkuu kwa timu kununua impact sub/ mchezaji wa bench, mifano halisi kwenye timu yetu Ni kocha wetu wa Sasa ambae hajawahi kuwa na namba ya kudumu kikosi chetu, Pia Tedy sherigham alikuwa Hivi Hivi wote walikuwa wanasubiria kwa Andy Cole na Yorke, Alikuwepo Chicharito, Henrik Larson, Saha (sio wakati wote) etc

Henrik Larson alikuja tu kwa mkopo toka Barca Tena kizee Cha miaka 36, kacheza Kama mechi 10 tu na kufunga goli 3, lakini Kila goli Ni muhimu kupita maelezo na anakuwa regarded Kama mchezaji muhimu zaidi kutupa kombe, ikumbukwe kabla yake UTD ilipotea kwa Arsenal Invicible na Chelsea ya Mou.

Hawa wazee wenye experience ambao hata wakikaa benchi hawalalamiki sababu wameshashinda Kila kitu maishani mwao Wana umuhimu wake mkuu, na Wala wakija hawavunji philosophy, starting XI ya man U Sasa Hivi mkubwa Ni De Gea na ana miaka 28.
 
Back
Top Bottom