Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Man u 3 Chelsea 0

Nitakuja kufukua kaburi
Kwa mara ya kwanza naona shabiki wa aseno anataka man u ishinde...

Navyowajua shabiki wa aseno kindaki ndaki hata man u acheze na ndanda huwa wanaside na ndanda hata kama man u atashinda 10, umenishangaza sana
 
Mkuu Chief,wakati huo akina Larsson wanakuja kama sub ndani una Rooney,ole anakuwa supa sub lakini ndani yuko Andy Cole na Yorke. Chicharito anatokea bench lakini pembeni kuna van persie,rooney. Tofauti na sasa una mandzukic bench halafu ndani yumo rashford,lingard na Mason.
 
Nyie Timu yenu Haina pressure kivile, mmezoea kutochukua makombe,
Mpira wa ujanja ujanja hauna nafasi tena kwenye Modern Football ya sasa,kila timu ina pesa ya kufanya chochote inachotaka,na kwa timu yenu hii mtaishia kubeba makombe ya kombolela tu Epl na UEFA tena mpaka Yesu arudi.
 
UKWELI MCHUNGU
Forward ya kutegemewa man u kwa sasa ni rashford na lingard... Kidogo na Martiall. Sanchez wala hana lolote....
Sasa ukiangalia kwa misimu karibu mitatu iliyopita hao wote (rash+ling+martial) hakuna hata mmoja alieweza kufikisha walau magoli 13 tu kwenye E.P.L. sasa najiuliza nani atafunga hayo magoli ili hawa Man U waingie top 4??
Maana liver wao mane+salah+firmino nauhakika kilammoja lazima atafikisha goli13+, hivyohivyo lacazette na aubameyang , hivyohivyo Son+harry kane nao watafikisha pia. Sasa kama hamna bull striker mnataka big 4 muingilie dirishani au? Kwamba timu nzima mnaishia kuwaamini watu ambao hata goli13 kufikisha kwa msimu hawawezi!!!!
 
Mkuu Chief,wakati huo akina Larsson wanakuja kama sub ndani una Rooney,ole anakuwa supa sub lakini ndani yuko Andy Cole na Yorke. Chicharito anatokea bench lakini pembeni kuna van persie,rooney. Tofauti na sasa una mandzukic bench halafu ndani yumo rashford,lingard na Mason.
Mkuu wakati Larson anakuja RVN ndio kaondoka, Rooney na Ronaldo ndio vitoto vinachipukia, wote Rooney na Ronaldo walikuwa bado hawajaanza kufunga Goli 20 kwa msimu kwenye ligi Ila walikuwa wanapita goli 10 kwa msimu. Ilikuwa mwaka 2006, Mwaka uliofuatia ndio Ronaldo akaanza kukiwasha 2007 mpaka 2009 ndio alipeak Man UTD.

Mimi naamini Kama Martial na Rashford wata step up na kutupa goli 15 Kila mtu, tutafanya vizuri,
 
Back
Top Bottom