Net spending, ulichonunua toa ulichouza
Mimi si mtaalamu wa Biashara coz sijasomea shule za Biashra.
Lakana Tukizungumzia Bajeti tunazungumzia kilichotengwa ambacho ndiyo kinachotumika kazi tayari kipo katika Mpango kazi.
Kwahiyo kinachoingia kwa kuuza wachezaji kinaingia moja kwa moja katika Account kwa ajili ya New Financial year!
Haimaanishi kiwa akiuzwa Pogba leo hela itaingizwa moja kwa moja kwa kuchanganywa na ile iliyobajetiwa £100m katika mfuko wa manunuzi bila ya kupita kwenye bodi ya Wakurugenzi kuidhinisha Matumizi.
Kwahiyo kilichobajetiwa ndiyo kinachotumika hata kama mutaingiza £200m.
Hakuna Kampuni/Taasisi/System yoyote inayotumia zaidi ya kilichobajetiwa kwenye Mfumo, lakini inaweza kutumia bila ya kufikia kilichobajetiwa.
Na habari za kuwa bajeti ni £100m hiyo sio kweli bali ni Rumours za twitter tu kwani Timu yoyote haitangazi Bajeti yake halisi kama vile Arsenal walipovumisha bajeti ya £45m.
Ukitangaza kuwa unabajeti ya £300m mawakala wanachangamkia Fursa kwani hata yule AWB wangetaka kumuuza kwa £80m, Maguire wangetaka £120m si time zitakuwa zinajua kuwa bajeti yenu ni kubwa!!
Lakini kitendo cha kuvumisha bajeti ya £100m timu zinajuwa wazi kiwa Hatakama nyinyi ni matajiri wakubwa lakini Hamuwezi kutumia nje ya Bajeti so, Wataishia kudai hela Ndefu huku wakitegeshea kwani wanajua kuwa Bajeti yenu sio £100m lakini hawajui ni ngapi.
Kwahiyo kulingana na Matumizi Bajeti yetu ni zaidi ya £150m au zaidi ya £200m.
Net spending haikalkuletiwi na mashabiki bali ni Mhasibu wa timu ndiye anayecalculate na kuiwasilisha kwa Bodi ya Wakurugenzi kila ifikapo new financial year ambapo ndiyo hutangazwa.
Kwahiyo mumeshazidi £100m katika hiyo bajeti yenu.