Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu uliyosema Ni sahihi lakini hoja Ni je unawezaje kuuza mfungaji aliyekua tegemezi kwako Kisha ukam replace kwa mchezaji atakayekuwa "impact sub na kucheza kombe la mbuzi"?!

Hivi kweli tunaanza league kwa kutegemea Rashford kuwa ndiye mfungaji wetu????
Kabla match kuanza tumeshafungwq na Chelsea , Rashford ndio forward namba moja united
 
Marcos Rojo amewasili Carrington training complex na wakala wake tayari kwa mazungumzo ya kuondoka Manchester united...

Sababu kubwa ni kutopewa uhakika wa dakika za kutosha kucheza uwanjani katika mpango wa msimu unaotarajiwa kuanza. View attachment 1175468
kuondoka kwa marcos rojo itakuwa ni faida kubwa sana kwa klabu, nampenda marcos anapokuwa fiti kiafya kuliko mlinzi yeyote wa kati tulionao ila tatizo la majeruhi limemfanya apoteze muelekeo wake kisoka

everton mwaka uliopita walikuwa tayari kulipa paundi millioni 25 ili wapate huduma yake sijui msimu huu wameweka kiwango gani cha fedha ili wamsajili, bila ya shaka kuondoka kwa kourt zouma itawalazimu watafute mlinzi mwengine mwenye uzoefu.
 
1. Kuna tier system kwenye uvumi/taarifa na Kuna waandishi ambao Ni official wa club wanapata taarifa direct toka kwenye club, mfano Ni huyo Cooper niliemtaja kuhusu issue ya ole, hivyo si Kila mwandishi Ni uvumi wa Twitter wengine maneno Yao yana uzito zaidi.

2. Tuje kwenye budget ya timu.

Club za mpira wa miguu haziendeshwi Kama serikali ama kampuni nyengine, ukipewa budget kiasi kadhaa unaweza ukaiongeza hio budget kwa kuuza wachezaji, kusema kwamba hela ya mchezaji ulioiuza inaingia mwaka mwengine si kweli. Club za mpira Zina wachezaji fixed hawazidi 30 hivyo unapopewa let's say 50M kuspend inamaanisha unatakiwa kuongeza hio value on top of current value, inapotokea current value imepungua inabidi uiongeze.

Chukulia mfano wa duka, una duka lenye bidhaa za milioni 5, na ukauza bidhaa za milioni 2, bosi wako akakuongeza milioni 1 ya kununua bidhaa zaidi,

Je utarudisha milioni 2 kwa bosi na kuchukua ile milioni na kushusha thamani ya duka hadi milioni 4, ama utarudisha zile milioni 2 dukani na ile milioni 1 na kupandisha thamani ya duka?

Unapoona hizi deals sijui Adidas, Mara Chevrolet, na wengineo, nyingi thamani ya hizi deals zinazotokana na thamani ya club, hivyo Kila mchezaji anapoondoka thamani ya club inapungua, na inabidi hio hela itumike kuiongeza thamani iliopungua.

Kuhusu Arsenal nisiwaongelee Sana sababu sifuatilii habari zao ila usisahau Peter cech, Ramsey, beki wao sijui ndio koscienly, welbeck, Denis suarez, etc Kuna wachezaji takriban 10 wameondoka, hao wote sitashangaa Kama Arsenal wamefree zaidi ya 50M kuspend kwenye wachezaji wapya, ambao watakuwa na values kubwa Huku wakilipwa mishahara midogo.
"Kuhusu Arsenal nisiwaongelee Sana sababu sifuatilii habari zao ila usisahau Peter cech, Ramsey, beki wao sijui ndio koscienly, welbeck, Denis suarez, etc Kuna wachezaji takriban 10 wameondoka,"

Mkuu wewe ni muhaya nini?maana unadai timu uifuatilii na wachezaji wake huwajui ila unawataja vizuri kabisa bila ya kukosea hata spelling duh........

Ila umejitahidi kueleza vizuri suala la kibiashara ,doa pekee ni hiyo dharau/nyodo tu
 
Marcos Rojo amewasili Carrington training complex na wakala wake tayari kwa mazungumzo ya kuondoka Manchester united...

Sababu kubwa ni kutopewa uhakika wa dakika za kutosha kucheza uwanjani katika mpango wa msimu unaotarajiwa kuanza. View attachment 1175468
Kiwango kibovu,majeraha kila siku..dakika za kucheza atazipataje??

Atafute timu haraka kabla ya 00.00Am
 
Kabla match kuanza tumeshafungwq na Chelsea , Rashford ndio forward namba moja united
Huyo huyo Rashford ameshaifunga Chelsea na Arsenal.

Simbezi kwamba Hana kiwango lakini bado hastahili kuwa ndio forward tegemezi letu.
 
Aman iwe nanyi

Endapo kesho kutwa man united akikubali kupokea kichapo cha haja mbele ya wababe wa Stanford basi ajiandae kushuka daraja

Hakuna asiyejua kuwa Chelsea ndo team yenye hali mbaya zaid ulimwengun kwa sasa, ndo team ambayo imeuza mchezaji tegemeo na imezuiwa kusajili

Ndo team ambayo imeamua tu liwalo liwe baada ya kocha wake kutimukia juventus na kumuita kocha ambaye hana uzoef kabisa Frank lampard

Ndo team ambayo imeita madogo ambao walikuwa wanakipiga huko ndondo kama akina mason mont na akina tamy Abraham na akina batshway ambao hata hawajulikan walikuwa wanacheza wapi

Ndo team ambayo wachezaji wake wote ni majeruh kama akina rudiger, wiliam,odoi,ngolo kante na cheek

Endapo man united aki suluhu au kufungwa bas ajiandae kushuka daraja

LONDON BOY
mkuu,

kwa upande wangu nona chelsea iko katika mikono salama zaidi ya mani united

ni kweli ktk kumuuza hazard chelsea wamepoteza mtu mzito lkn sio kama unavyo fikiri..ni wazi kuwa kumpoteza kama hazard ni pengo kubwa lkn bado kuna mikono salama ya watu kama willian na pedro..japo kiuhalisia hazard ni next level compared to these guys... uwepo wa CHO na pulisic ni hazina kubwa...labda hapo kwenye striker .. tammy hana uzoefu wa kutosha wa premier.. mitchy sio yule aliyetoka france na giroud haamini..lakini huko kwingine safituu

david luiz anasepa bila kusahau

nafikiri lampard tafikisha timu salama

kwa upande wa united hadi sasa harry maguire ndio mpango mzima..eneo la ulinzi sasa limekamilika..lkn litakamilika vizuri endapo David De Gea atakuwa wa tofauti na msimu uliopita.. kwangu mimi shida ya united naiona kule mbele tuuu..wale watu watatu wa mbele wa OGS.. bado sina imani nao.. mata,martial na sanchez hawakuwa kwenye kiwango bora last season... james tumuweke kiporo.. anabaki Rashid makame ambaye ndio anaonekana kutumainiwa pale mbele

lets wait and see
 
mkuu umemzungumzia mandzukic kana kwamba anafanana kitabia na michael owen yule aliyesajiliwa na ferguson.
mkuu kiuhalisia unaweza kumweka nje mario mandzukic kwenye mechi muhimu na kuchukua maamuzi ya kumuanzisha marcus rashford yule wa msimu uliopita?
Pengine Mimi na wewe hatuwezi ila OLE anaweza mkuu, mfumo wa Sasa Ni Kama wa klop pale mbele, Rashford ana Role ya Firmino, Ni false 9 zaidi kuliko striker.
 
Pengine Mimi na wewe hatuwezi ila OLE anaweza mkuu, mfumo wa Sasa Ni Kama wa klop pale mbele, Rashford ana Role ya Firmino, Ni false 9 zaidi kuliko striker.
hapo kwenye namba 10 atakuwa bwana paul pogba au bwana lingard kwa mtazamo wako?
kama atakuwa pogba unadhani namba 8 atakaye deal zaidi na upande wa kulia atacheza nani?

msimu uliopita mechi alizokuwa anapewa andreas perreira alikuwa anachemsha sana eneo la ander herrera na ndiye pekee mwenye matumaini ya kuziba nafasi ya ander , hapa ndipo unapoukumbuka usajili wa bruno fernandez.
 
Mkuu CHD ndo nani na david luis anasepa wapi
mkuu,

kwa upande wangu nona chelsea iko katika mikono salama zaidi ya mani united

ni kweli ktk kumuuza hazard chelsea wamepoteza mtu mzito lkn sio kama unavyo fikiri..ni wazi kuwa kumpoteza kama hazard ni pengo kubwa lkn bado kuna mikono salama ya watu kama willian na pedro..japo kiuhalisia hazard ni next level compared to these guys... uwepo wa CHD na pulisic ni hazina kubwa...labda hapo kwenye striker .. tammy hana uzoefu wa kutosha wa premier.. mitchy sio yule aliyetoka france na giroud haamini..lakini huko kwingine safituu

david luiz anasepa bila kusahau

nafikiri lampard tafikisha timu salama

kwa upande wa united hadi sasa harry maguire ndio mpango mzima..eneo la ulinzi sasa limekamilika..lkn litakamilika vizuri endapo David De Gea atakuwa wa tofauti na msimu uliopita.. kwangu mimi shida ya united naiona kule mbele tuuu..wale watu watatu wa mbele wa OGS.. bado sina imani nao.. mata,martial na sanchez hawakuwa kwenye kiwango bora last season... james tumuweke kiporo.. anabaki Rashid makame ambaye ndio anaonekana kutumainiwa pale mbele

lets wait and see
 
"Kuhusu Arsenal nisiwaongelee Sana sababu sifuatilii habari zao ila usisahau Peter cech, Ramsey, beki wao sijui ndio koscienly, welbeck, Denis suarez, etc Kuna wachezaji takriban 10 wameondoka,"

Mkuu wewe ni muhaya nini?maana unadai timu uifuatilii na wachezaji wake huwajui ila unawataja vizuri kabisa bila ya kukosea hata spelling duh........

Ila umejitahidi kueleza vizuri suala la kibiashara ,doa pekee ni hiyo dharau/nyodo tu
Hapana mkuu huwa Mimi Sina dharau, na mwenyezi mungu aniepushie,

Hao wachezaji niliowataja Ni maarufu sidhani Kama Kuna mtu mpenzi wa mpira asiewajua, mshabiki wa arsenal anaefuatilia anawajua zaidi ya hao.
 
hapo kwenye namba 10 atakuwa bwana paul pogba au bwana lingard kwa mtazamo wako?
kama atakuwa pogba unadhani namba 8 atakaye deal zaidi na upande wa kulia atacheza nani?

msimu uliopita mechi alizokuwa anapewa andreas perreira alikuwa anachemsha sana eneo la ander herrera na ndiye pekee mwenye matumaini ya kuziba nafasi ya ander , hapa ndipo unapoukumbuka usajili wa bruno fernandez.
Hapa nakubali mkuu, tunamiss midfield ya kufanya tumchezeshe pogba Kama 10, Kuna sehemu niliona stats za pogba ana contribution 1.4 ya Goli Kama no 10, Ina maana either anafunga ama anatoa pasi ya goli Kila mechi.

Labda Fred atafufuka mkuu, acheze na McTominay chini na pogba apande.
 
Mkuu uliyosema Ni sahihi lakini hoja Ni je unawezaje kuuza mfungaji aliyekua tegemezi kwako Kisha ukam replace kwa mchezaji atakayekuwa "impact sub na kucheza kombe la mbuzi"?!

Hivi kweli tunaanza league kwa kutegemea Rashford kuwa ndiye mfungaji wetu????
Ngoja ligi ianze mkuu, tutajua Ole alimaanisha Nini, ila ninavyoelewa Mimi hatuchezi Tena na striker,
 
Timu ya Chelsea sio dhaifu mbona still inawachezaji wazuri tu wanaweza kuleta competition kwangu sioni ajabu kwa Chelsea kumfunga man united.
 
Back
Top Bottom