Mimi si mtaalamu wa Biashara coz sijasomea shule za Biashra.
Lakana Tukizungumzia Bajeti tunazungumzia kilichotengwa ambacho ndiyo kinachotumika kazi tayari kipo katika Mpango kazi.
Kwahiyo kinachoingia kwa kuuza wachezaji kinaingia moja kwa moja katika Account kwa ajili ya New Financial year!
Haimaanishi kiwa akiuzwa Pogba leo hela itaingizwa moja kwa moja kwa kuchanganywa na ile iliyobajetiwa £100m katika mfuko wa manunuzi bila ya kupita kwenye bodi ya Wakurugenzi kuidhinisha Matumizi.
Kwahiyo kilichobajetiwa ndiyo kinachotumika hata kama mutaingiza £200m.
Hakuna Kampuni/Taasisi/System yoyote inayotumia zaidi ya kilichobajetiwa kwenye Mfumo, lakini inaweza kutumia bila ya kufikia kilichobajetiwa.
Na habari za kuwa bajeti ni £100m hiyo sio kweli bali ni Rumours za twitter tu kwani Timu yoyote haitangazi Bajeti yake halisi kama vile Arsenal walipovumisha bajeti ya £45m.
Ukitangaza kuwa unabajeti ya £300m mawakala wanachangamkia Fursa kwani hata yule AWB wangetaka kumuuza kwa £80m, Maguire wangetaka £120m si time zitakuwa zinajua kuwa bajeti yenu ni kubwa!!
Lakini kitendo cha kuvumisha bajeti ya £100m timu zinajuwa wazi kiwa Hatakama nyinyi ni matajiri wakubwa lakini Hamuwezi kutumia nje ya Bajeti so, Wataishia kudai hela Ndefu huku wakitegeshea kwani wanajua kuwa Bajeti yenu sio £100m lakini hawajui ni ngapi.
Kwahiyo kulingana na Matumizi Bajeti yetu ni zaidi ya £150m au zaidi ya £200m.
Net spending haikalkuletiwi na mashabiki bali ni Mhasibu wa timu ndiye anayecalculate na kuiwasilisha kwa Bodi ya Wakurugenzi kila ifikapo new financial year ambapo ndiyo hutangazwa.
Kwahiyo mumeshazidi £100m katika hiyo bajeti yenu.
1. Kuna tier system kwenye uvumi/taarifa na Kuna waandishi ambao Ni official wa club wanapata taarifa direct toka kwenye club, mfano Ni huyo Cooper niliemtaja kuhusu issue ya ole, hivyo si Kila mwandishi Ni uvumi wa Twitter wengine maneno Yao yana uzito zaidi.
2. Tuje kwenye budget ya timu.
Club za mpira wa miguu haziendeshwi Kama serikali ama kampuni nyengine, ukipewa budget kiasi kadhaa unaweza ukaiongeza hio budget kwa kuuza wachezaji, kusema kwamba hela ya mchezaji ulioiuza inaingia mwaka mwengine si kweli. Club za mpira Zina wachezaji fixed hawazidi 30 hivyo unapopewa let's say 50M kuspend inamaanisha unatakiwa kuongeza hio value on top of current value, inapotokea current value imepungua inabidi uiongeze.
Chukulia mfano wa duka, una duka lenye bidhaa za milioni 5, na ukauza bidhaa za milioni 2, bosi wako akakuongeza milioni 1 ya kununua bidhaa zaidi,
Je utarudisha milioni 2 kwa bosi na kuchukua ile milioni na kushusha thamani ya duka hadi milioni 4, ama utarudisha zile milioni 2 dukani na ile milioni 1 na kupandisha thamani ya duka?
Unapoona hizi deals sijui Adidas, Mara Chevrolet, na wengineo, nyingi thamani ya hizi deals zinazotokana na thamani ya club, hivyo Kila mchezaji anapoondoka thamani ya club inapungua, na inabidi hio hela itumike kuiongeza thamani iliopungua.
Kuhusu Arsenal nisiwaongelee Sana sababu sifuatilii habari zao ila usisahau Peter cech, Ramsey, beki wao sijui ndio koscienly, welbeck, Denis suarez, etc Kuna wachezaji takriban 10 wameondoka, hao wote sitashangaa Kama Arsenal wamefree zaidi ya 50M kuspend kwenye wachezaji wapya, ambao watakuwa na values kubwa Huku wakilipwa mishahara midogo.