Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Tumecheza kama tulivyocheza game ya Watford na West Ham,

Tofauti ni kwamba leo Everton hajapoteza nafasi za kufunga

Poor United, don't deserve to play UCL next season

Will regret to sign OGS instead of Poch
OGS tayari ana cheque yake, mkivunja tu mkataba mnamlipa ndefu!
 
Hilo ni tatizo kubwa kweli kweli team imekosa mipango na kibaya zaidi nadhani Ole anatupeleka kubaya sana.

Ole anamwabudu Pogba Hii ni hatari sana,afadhali Jose alikuwa guts za kumpiga bench huyu mshenzi wa viwango vyote.
Naona unaanza kuja taratibu,our next game Vs City unafikiri hali itakuwaje ?
 
Ndugu yangu hakuna ambaye yupo ndani ya club kati yetu, lakini ni mambo mangapi ya ndani tunaongea kuhusu kinachoondelea pale United? Sources zetu za info ni zile zile, Tv kubwa na article kubwa kutoka kwa vyombo kama BBC, Sky n.k. Pia kupitia akaunti za social media za watu maarufu wanaojihusisha na soka.

Vinginevyo tungekuwa hatuongei mpaka tusubiri club i confirm flani kasajiliwa au flani kaachwa. Kwa hiyo sio pale zinapotajwa habari zinazopendwa ndio tujidai tunajua habari za nyuma ya pazia na details nyingine, ila kama habari hatuipendi ndio tujidai kwamba hatuwezi kujua habari zilizopo nyuma ya pazia.

Kuhusu kutoa hela hovyo bila kujali wage structure si jambo la busara lakini si ndio Ed alitoa £500,000 kwa Alexis? Au hiyo ipo kwenye structure ya wage bill ya United?

Lakini labda nikuulize je unajua kwanini sasa hivi Mata, Herrera na Degea wataka dau kubwa katika mkataba wao. Sababu ni simple tu, katika negotiation wana upper hand dhidi ya United, yaani kwa kuchelewa kuwapa mkataba United amekuwa kwenye upande wa kubanwa katika mazungumzo.

Ina maana mazungumzo yangefanywa hata miaka 2 kabla ya mkataba kuisha wasingetaka dau kubwa kama sasa na wangetaka dau kubwa United angekuwa na options zaidi tofauti na sasa (mfano kuwauza kwa bei nzuri na kutafuta mbadala).

Na kwa mtazamo wako kwamba kitakachofuata ni nini? Ni kumuaza Degea kwa hasara (maana mkataba utakuwa umebaki chini ya Mwaka) au kumpa mkataba anaotaka (kitu ambacho Ed anagomea sasa hivi). Kwa Herrera na Mata itakuwa either kuwapa mkataba wanaotaka au waondoke bure na Man United atafute £ 80+ kuziba nafasi zao hao jamaa wawili na kuwapa mshahara mnono hao wachezaji wageni.

Anacholaumiwa Ed ni kuchelewa ku settle mambo ya mikataba mapema kiasi cha kwamba wachezaji wanaweza kuondoka bure na kuziba nafasi zao kuwa tabu.

Kumbuka kwa sasa Man anahitaji almost £250 million kuimarisha kikosi (bila akina Herrera kuondoka) lakini hao jamaa wakiondoka itawalizimu kutumia zaidi ya £300 ili kuziba mapengo na kuimarisha kikosi, je huyo Ed yupo tayari kutoa huo mpunga? Na akitoa huoni kama gharama waliyoikwepa kwa mlango huu wanaikubali kwa mlango mwingine?

Halafu mfano wa Arsenal ni mfano wa ajabu sana. Yaani kwa kuwa Ramsey anaondoka bure na sisi tuige kwao. Arsenal walifanya makosa kwa Sanchez akaondoka, kwa Ozil (bahati nzuri wakamsainisha mwishoni, lakini kwa hela aliyotaka) na sasa kosa limejirudia kwa Ramsey. Kosa ni lile lile la kusubiri mkataba upo mwishoni ndio mnaanza kukimbizana kwenye mazungumzo.

Ed ni mzigo kwenye football side japo anajitahidi kwenye biashara na tukumbuke yeye na Glazers siblings wanachotaka ni timu kuingia top four tu ili timu itinge UCL kwa ajili ya biashara, sasa sisi tunaopenda kuchukua vikombe kazi kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Plz naomba mwenye groups za Man u aweke link hapa
 
Kwa upande wa Jose nakubaliana na Woodward nadhani tulifanya haraka kumfukuza Van Gaal kwasababu kipindi chake team ilianza kushambulia na pia aliwapa nafasi makinda.

Kumbuka Jose alipewa nafasi ya kusajili Baily na Leondof bado akataka asajili CB mwingine !.
Lindelof ndio our best CB this season ,Kama Woodward angekubali Jose asajili new defender sidhani kama Jones/Rojo bado wangekuwa bado wanachezea United
Tayari msimu huu tumeweka rekodi ya kufungwa magoli mengi kwenye EPL but Jose alimwambia Woodward timu inahitaji new defenders akamgomea
 
Ndio mpira bwana. Leo Everton walikuwa na hali ya ushindi kwa 70% kutokana na ubovu wa timu yetu, mimi wala sishangai matokeo haya kipigo kilikuwa lazima.
 
√KIMSINGI wachezaji na kocha they are not good enough..

√Sioni tukiprogress

√Timu imejaza waingereza wengi wasioweza mpira..Hivi huyu bernard wa everton si anamzidi Lingard mchana kweupe??

√KIMSINGI tuna timu mbovu kuanzia juu kwenye uongozi mpaka kwenye benchi la ufundi..

√Next season tupo Europa so hao masharobaro wakitaka kusepa wasepe..i don't even care anymore

√Fu.cking disgusting
 
Lindelof ndio our best CB this season ,Kama Woodward angekubali Jose asajili new defender sidhani kama Jones/Rojo bado wangekuwa bado wanachezea United
Tayari msimu huu tumeweka rekodi ya kufungwa magoli mengi kwenye EPL but Jose alimwambia Woodward timu inahitaji new defenders akamgomea
Kweli jamaa anajituma sana kuliko hiyo michezaji mingine
 
Back
Top Bottom