media zao pamoja na wachambuzi wao wa soka wenye ufahamu na wale wanaojitoa ufahamu kwa mapenzi yao binafsi ya timu zao walizowahi kuzichezea pamoja na utaifa wao kwa kiasi kikubwa wanawafanya raia wao wawe na sifa takribani tatu.
- wawe na gharama kubwa unapowahitaji hususani timu kubwa.(overpriced)
- wengi wao wanawapa sifa nyingi pasina ukweli wa sifa hizo.(overrated)
- wanawatangaza sana japo hili si vibaya kwa sababu ni wachezaji wa nyumbani (overhyped)
mchezaji wa kiingereza akiwa na kipaji kidogo cha soka bei yake inakuwa kubwa sana kwa sababu vijana wengi wa kiingereza hawana vipaji halisi vya soka, inamaana kama uzalishaji wa vipaji ni mdogo na mahitaji ni makubwa lazima bei iwe kubwa halafu kwa mujibu wa sheria ni lazima uwe na wachezaji 8 waliokulia uingereza kama nitakuwa nipo sahihi.
naamini kama utawakusanya wachezaji 20 wa kiingereza wanaochipukia ambao wanacheza eneo la kiungo basi utapata mchezaji mmoja tu mwenye skills, intelijensi ya soka na kwa taifa kubwa huu ni udhaifu mkubwa wa kimfumo.
lakini ukienda nchi kama spain, brazil, germany, netherland na nchi nyenginezo wanazalisha vipaji mara kwa mara na si kwamba eti hawana media za kuwapa promo wachezaji wao wawe ghali bali wanafanya hivyo kupunguza mzigo wa wachezaji wasiokuwa na timu za uhakika za kuchezea, hivi jamani utawasifu akina neymar wangapi nchini brazil kila baada ya muda mchache?
tukija kwenye ishu ya man united binafsi sichukizwi na wachezaji wa kiingereza wenye vipaji (technically gifted or talented) ambao wana kitu muhimu zaidi wanachoweza kukupa ndio maana sijawahi kuwaponda
wayne rooney, paul scholes, steven gerrard, frank lampard, joe cole, ferdinand, terry, robbie fowler, michael owen, shearer, andy cole na wote hao nimewashuhudia wakicheza tokea mwaka 2001.
nachukizwa na wale wasiokuwa na maajabu makubwa ya kisoka either technically or talent , ni ujinga kulipa hela nyingi sana kwa mchezaji wa kiingereza ambaye uwezo wake wa kisoka hauna tofauti na mchezaji wa nchi za dunia ya tatu, ni lazima kama tunataka tuondoke kwenye huu mkwamo tunahitaji kuacha huu utamaduni wetu wa kukumbatia wenye underdog mentality kwa sababu ya utaifa na man united utaifa upo tokea nyakati za fergie japokuwa mwenyewe hajawahi kukiri hadharani.
jaribu kuangalia timu kama
barcelona, bayern munich zote hizi zimejaza wachezaji wazawa wenye uwezo wa kujisimamia bila ya kutegemea msaada mkubwa kutoka kwa wageni tofauti na wachezaji wengi wa kiingereza ambao wengi wao wanasukumwa zaidi na wachezaji wa kigeni.
wakati wewe unalipa paundi millioni 35 kwa ajili ya mpuuzi
andy carroll mwenzako analipa paundi millioni 27 kwa ajili ya
robert lewandowski yule mwenye miaka 24 je nani ameramba dume?
wakati wewe unahangaika kumsajili declan rice or eric dyer kwa pound millioni 40 haliyakuwa hawana utofauti wowote na
scott mctominay kimpira mwenzako anakwenda kumsajili
ndombele, pjanic, koke, matuidi, de jong je yupi amepata zaidi?
ashley young, phil jones, smalling, luke shaw, scott mctominay, jesse lingard, marcus rashford, angel gomez na gardner jamani tayari tushatimiza wachezaji 8 wa kiingereza na wameshatosha kwenye kikosi chetu cha kwanza tusitafute wengineo waliojaaliwa zaidi kipaji cha kupiga square pass kama mchezaji wa uswahilini kwetu labda awe
jadon sancho kidogo ana muelekeo ikiwa hatovimba kichwa hapo mbeleni.
wakati wenzetu liverpool wameshachoshwa na
captain henderson cha ajabu sisi bwana phil neville anatuvumishia stori za
eric dyer, kadri tutakavyowakumbatia wachezaji aina ya
dyer, rice ndivyo tutakavyozidi kudhalilishwa na timu zinazoweza kumiliki mpira na pressing ya hali ya juu kama liver, city, psg,barcelona.
tujisahihishe bado hatujachelewa naamini sheria bado hazijalazimisha wachezaji wa kiingereza wacheze kikosi cha kwanza kwa takwimu maalum.
wakuu munakumbuka kipindi kile sheikh
rio ferdinand mnamo mwaka 2004 amefungiwa miezi 8 nafasi yake ikawa inazibwa na
wes brown, neville brother😛😛😛(flashback)