1. Lvg hakupewa hela za usajili wa kuimarisha Timu bali za kureplace wachezaji, anapewa timu hali ya kuwa mabeki watatu wa kutegemewa ndani ya club wanaondoka kwa mpigo, Vidic, Rio na Evra, midfield nao wanaondoka kina scholes, fletcher etc alibaki carrick, Giggs kastaafu, timu haina quality kabisa, ukiangalia usajili wa LVG alileta tu squad players kina shaw, Herrera, blind etc hao kina Di maria, Falcao etc waliletwa tu na timu kocha alikuwa na Target zake Muller, Robben Etc.
2.Hio 600 unayoitaja ina double counting kibao, mfano Di maria kanunuliwa kwa 60m kisha kauzwa kwa 45m hela yake ikanunuliwa mtu kama Depay na martial kwa around 60m again, huwezi kusema eti tumespend 120m kununua wachezaji watatu, ni hela ile ile imezungushwa.
3. Huu ni ushahidi wa uhuni wa Glazer na Woodward.
-miaka 10 iliopita Man U ndio timu ilioingiza hela nyingi zaidi ligi ya Uingereza kutokana na Activities mbalimbali. 1.3B pounds, kwa comparison timu ya pili ni Arsenal around 700m pounds, hivyo uone gap la hela baina ya Man U na timu nyengine, Man city ni around 140m tu.
-pamoja na kuingiza hela nyingi hawa jamaa wanazichota zote na kulipia Madeni ya Mmiliki, ikumbukwe kabla ya Glazer Man U ilikaa miaka zaidi ya 70 bila deni, ilikuwa ni Timu ya kuigwa Ila jamaa walivyofika na kuinunua Club wakahamishia Deni lao Binafsi kwenye Timu na kisha Wanatumia Hela zetu kulipia Deni lao.
Ukiangalia hizo data utaona kati ya 1.3B ilioingia almost 800m inalipa madeni na Riba.
-Hili graph linaelezea zaidi
Ukitoa spurs na arsenal, Man U ni timu ya tatu kutoka mwisho kwenye kutoa hela zake inazoingiza kwenye usajili. Imagine mkuu club tajiri zaidi duniani inashika nafasi ya tau toka mwisho kwenye kutoa hela za usajili unategemea nini?
Na bora hata hizo hela za timu wangeziweka kwenye cash ungesema labda wanasave for future na kuweka reserve kubwa,
Kiufupi mkuu tumepatikana sana, na sijui nani wa kututoa hapa, matajiri wengi wana Approach kuirudisha Man u ila jamaa wanatoa Unrealistic figures ili timu iendelee kuwa yao.