OllaChuga Oc
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 21,933
- 25,245
Mzee bab umeandika kitu chenye maana sana..jambo moja kubwa ambalo washabiki na wapenzi wa manchester united tunapaswa kushukuru ni kushuhudia timu yetu imewahi kufundishwa na mwanadamu ambaye si mnafiki linapokuja suala lenye maslahi na kazi yake.
achana na madhaifu yake ya kujifanya ni msafi kwa kila jambo analoliamini lakini jamaa kwa kutumia mdomo wake usio ishiwa maneno ndiye aliyetuwezesha kufahamu kiundani madhaifu ya uongozi mzima wa manchester united.
huwa napenda kuzipitia comment zote za wachangiaji ili nipate kujifunza kwa sababu sijakamilika lakini ukizisoma hizi comment wengi wao wanarudi pale pale kwenye msimamo wa jose mourinho ambaye tulimuona shetani hata kwa lile ambalo lipo sahihi.
- kuna baadhi ya wachangiaji wanasema hatujawahi kusajili winga wa kulia kwa miaka 5, nadhani watakuwa wamepitikiwa kibinadamu kwa sababu chini ya david moyes tulimsajili wilfred zaha, chini ya LVG tulimsajili memphis depay, dimaria baada ya kumuona wilfred zaha hafai. Ukiifuatilia hii cinema kwa umakini ndio tunarudi pale pale kwenye mijadala yetu ya kila siku ya kwamba tulikuwa tunasajili na kuuza kwa kusikiliza zaidi porojo za walimu hata kama hawapo sahihi.
- alipokuja msema ukweli jose mourinho baada ya miezi kupita akamwambia ed woodward ya kwamba memphis depay bado hajawa na uwezo wa kucheza ligi ya uingereza kila wiki hivyo namhitaji ivan perisic wa inter milan, mpaka jose anaondoka hakuwahi kuletewa winga wa kulia.
- katika harakati zake za kujenga timu jose mourinho hakuvutiwa kabisa na juan mata lakini bodi ya klabu ilikataa kumtafutia mbadala, cha ajabu leo hii ndio kuna mashabiki ndio wanagundua udhaifu wa juan mata na wenzake.
- sitaki kuzungumzia ishu ya martial na jose mourinho kwa sababu sote tunafahamu jamaa alikuwa tayari hata kufanya swap deal dhidi ya willian wa chelsea, baada ya kumshuhudia jana martial akicheza ndio nimegundua jamaa alikuwa sahihi kumweka benchi antony martial na hata kumuondoa.
- sitaki kuzungumzia ishu ya walinzi wa kati ili nisiwachoshe, kwa sababu bado tunaendelea kuteseka licha ya jose kutokuwepo.
kama kweli united wana fedha kama wanavyojisifia zinapotolewa repoti za mapato mbona tunakimbilia kuwapa mikataba kina ashley young, jones, mata wakati wenzetu wanawatafuta mahrez, walker, sterling n.k.
Yote hayo jose alishayazungumza mara kwa mara lakini hatukumuelewa wengi wetu.
Tumuombe mungu kocha ajaye asiwe mnafiki ili aweze kuyapigania maslahi ya ukweli ya klabu la si hivyo tutashihudia tena dhoruba yenye maumivu.
mara paaaap matteo darmian, valencia wanapewa mikataba mipya huku man city wanamsajili ndombele na wanamrudisha jordan sancho.
Sent using Jamii Forums mobile app
, Chelsea na Liverpool wote chini ya 500 milion
...
