Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kushabikia team ni maamuzi tu mkuu acha kuwa brain washed kuwa kuanza kushabikia mpira zamani ndyo kujua mpira
Wengi wa Man City fans huwa either ni MEMKWA (wamejua soka ukubwani) au Wahamiaji kutoka timu nyingine (ambao pia watahama timu ikishuka kiwango)

Ndio maana mimi huwa nawacheeeki.....
 
Ukitaka kuamini kuwa pep ni bonge la kocha mpeleke man u umpe wachezaji anaowataka uone kama hatonyanyasa EPL
Mkuu hapo tunaongelea in general context

Angalia mfano Mou timu alizofundisha na kupata mafanikio, Porto, Chelsea mara 2, Real Madrid na Inter

Porto kachukua UCL, je Guardiola anaweza beba UCL na Porto au timu yenye profile sawa na Porto?

Angalia alichokifanya akiwa Inter, kocha wa kwanza kushinda makombe 3 ndani ya msimu mmoja tena akiwa na Inter ya kawaida tu

Ameenda Uingereza wababe wakiwa ni United na Arsenal, tangu aingie pale Premier imekuwa ya yoyote, hakuna wenye haki miliki

Madrid amechukua Segunda na kombe la ligi huku akiwa anapambana pengine dhidi ya timu bora kuliko zote kwa wakati wote duniani. Hapa naongelea Barcelona ya Lio at his prime, Iniesta, Xavier, Bosquet, Puyol n.k

Rudi kwa Guardiola, kwanza nakubali kwamba Guardiola ni moja kati ya makocha bora duniani

Lakini lazima tukubali kwamba mafanikio yake kwa sehemu kubwa yamebebwa na ubora wa individual players aliowahi kuwafundisha, udhaifu wa ligi alizopitia na support anayoipata kwa wamiliki wa club zake. Hii inajidhihirisha pale Barcelona, Bayern Munich na City anapondisha kwa sasa

Na ndio maana sitashangaa siku za usoni, nikimuona Guardiola anaenda PSG au Juventus
 
Ukitaka kuamini kuwa pep ni bonge la kocha mpeleke man u umpe wachezaji anaowataka uone kama hatonyanyasa EPL
Kupewa wa Man U haitawezekana

Ila alikwishapewa akina Kolarov, Ihenacho, Kompany msimu wa kwanza, alifanya nini?

Ameonekana kocha wa maana baada ya kuanza kutumia 90% ya wachezaji alionunua yeye
 
Kwanini utumie wachezaji wabovu ukiwa kwenye mashindano huo ni ujinga
Mkuu usijali. Tujadili tu

Pep ni kweli ni miingoni kati ya makocha bora,lakini si bora kama tunavyataka kuaminishwa

Ukweli ni kwamba Pep hajawahi kujaribiwa uwezo wake akiwa na wachezaji wa kawaida ama waliochoka, mfano mzuri angalia wachezaji aliowakuta city, ukiondoa aguero , Silva na De Bruyne nani mwingine ambaye bado anayecheza pale chini ya Pep

Msimu wa kwanza wa Pep pale City ndio uliotupa picha kwamba Pep anaweza kushinda makombe akiwa na wachezaji wa kawaida ama la (Kumbuka pia wale wachezaji, akina Hart,Zabaleta, Kompany,Otamendi, Navas, Zeko n.k ndio walibeba kombe EPL mara kadhaa, hivyo hawakuwa wabovu kiivyo)

Kwahiyo mkuu Kagawa wa United ndio akina Navas wa City, pia Ihenacho wa City ndio Rashford wa United. De Maria wa United kwani kwa sasa anafanya nini kikubwa huko PSG? Lakini pia nakukumbusha hao wachezaji uliowataja wote waliondoka kabla ya Mourinho hajawa Mwalimu wa United
 
Best comment ever
Mkuu kuna 2 style za defense:-

1. Defending by offense
2. Defending by defense

Mou anatumia hiyo ya 2, na amekuwa analazimisha strikers, midfielders kurudi nyuma kuzuia (unaikumbuka kazi ya kina Etoo Inter), na mfano mwaka jana kuna scenarios Lukaku anajifunga kwa sababu ya kuja huku kwenye back line.

Kwa mpira wa sasa ambao wings hazipigi cross, bali zinakufata imekuwa ni kazi sana kuwa na mafanikio kwenye eneo la defense kama unarudisha timu yote nyuma na watu wanakushambulia muda wote, back then ungekuta wings zinabanwa kwenye crosses, strikers wanapigwa pini maisha yanarahisika, toka 2010 Mou achukue UEFA, then Chelsea 2012 (almost kwa kutumia schemes za Mou) hii mbinu ya ukabaji si rafiki tena kwenye soccer.

Pep anatumia mbinu zote mbili, anakaa na mpira katikati na mbele, muda mwingi nyuma kuna relax (offensive way of defending), na ikitokea mpira ukaja nyuma anarudisha wachezaji wachache kuja kusaidia back line ili wakirecover mpira kunakuwa na watu wa kuupokea. Na ndiyo maana ni wao waliofungwa goli chache EPL na wamefunga goli nyingi. Mfumo wa Mou wa ukabaji haukupi nafasi ya kufunga goli nyingi.

Pep na Barca yake walijikita kwenye mbinu ya kwanza pekee, walikuwa hawajali sana kwenye beki isipokuwa ushambuliaji, ila hii Man City jamaa kasuka beki nzuri, anasumbua kote.

Pep ni bora vs Mou; unapopewa timu, una identify mahitaji, unapewa hela unanunua wachezaji wanaokupa matokeo kama haya wewe ni bora.

Akiwa Bayern hakuwa na mandate kama aliyonayo leo Man City, ile timu Legends ambao ni wazawa wanaangalia pale, wana sauti, na ni timu almost ya Taifa, uhuru wa kufanya utakavyo ni ngumu.

Mou kashapewa wachezaji wengi na anasema hawafit, wrong choice of resources ni almost misuse, huwezi kuwa unanunua 5, moja ndo inafanya vyema tukasema wewe ni bora.

Mimi kwangu Mou was best up to 2010.
 
Hata wewe ukipewa u kocha lazima utafute watu ulio na uhitaji nao sio kukumbatia vituko kama bailly
Kupewa wa Man U haitawezekana

Ila alikwishapewa akina Kolarov, Ihenacho, Kompany msimu wa kwanza, alifanya nini?

Ameonekana kocha wa maana baada ya kuanza kutumia 90% ya wachezaji alionunua yeye
 
Mimi naomba unisaidie sababu ya morinho kutomtumia DM mtanisaidia jina, akampeleka timu ya vijana, kwa Nini aachane na zlatan? Alikuwa bora kuliko lukaku, tatizo la morinho anachuki binafsi. Na huyo hawezi kupata mafanikio ya maana. Unaona amewapa vikombe the blue lkn anahangaika nao, hakuna kuheshiniana kikazi, japo kibinadanu hakuna. Ferguson alisumbualiwa Sana ishu za usajili. Na ndio maana alimalizia na wachezaji ambao wasingeweza kutumiwa na kocha mwingine
Mkuu kuhusu Zlatan ukimlaumu Mou unamuonea

Unajua Zlatan aliomba mwenyewe kuondoka, tena anasema alimfuata Mou akamwambia baada ya majeruhi niliyoyapata najua siwezi kukupatia kile unachotegemea kutoka kwangu hivyo akaomba aruhusiwe aende USA
 
Mimi naomba unisaidie sababu ya morinho kutomtumia DM mtanisaidia jina, akampeleka timu ya vijana, kwa Nini aachane na zlatan? Alikuwa bora kuliko lukaku, tatizo la morinho anachuki binafsi. Na huyo hawezi kupata mafanikio ya maana. Unaona amewapa vikombe the blue lkn anahangaika nao, hakuna kuheshiniana kikazi, japo kibinadanu hakuna. Ferguson alisumbualiwa Sana ishu za usajili. Na ndio maana alimalizia na wachezaji ambao wasingeweza kutumiwa na kocha mwingine
Zlatan ulikuwa usajili bora sana kwa United (ndani na nje ya uwanja) na angeweza kuwa backup ya Lukaku tatizo ni alivyopata majeruhi na umri wake hata yeye mwenyewe alihisi anaweza asicheze tena ligi ya mikikimikiki ndio maana alienda US.Zlatan na Mourinho ni washkaji na kila kwenye interview Zlatan anamsifia Mourinho na hizi story za kina Pogba/Martial kugombana na kocha zisingeweza kutokea kama Zlatan angekuwepo
Kama unataka kushindana na Chelsea,Liverpool,Spurs,City huwezi kumtegemea DM kama McTomey kupambana na kina Fernandinho,Kante,Jorginho,Dembele,Dier na kibaya zaidi timu haiko kwenye kiwango kizuri dogo achemsha mechi moja mashabiki wangepiga kelele
 
Kuhusu suala la Mc Tomenay hawezi kuwa tegemeo pale Man U nakumbuka hata Van Gaal alikuwa akilaumiwa sana na hawa jobless wa man u kuwa anawapa wavulana kazi zinazotakiwa kufanywa na wanaume.

Ukweli ni kwamba wachezaji wa Man u wameyaamini magazeti kuwa hawana uwezo mkubwa kiasi cha kupoteza confidence.
 
Mkuu hapa umeongea point kubwa sana

Tatizo pale United ni kubwa kuliko Mou au Wachezaji

Tatizo linaanzia kwa Wamiliki (Glazers) na Ed. Unajua wamiliki sio watu wa soka kiviile, wenyewe wanachoangalia ni mwisho wa siku timu imeingiza kiasi gani cha mapato. Ndio maana timu isipofanya vizuri (lakini angalau ishiriki UEFA kocha hawezi guswa hata kidogo, ila ikijichanganya ikose nafasi kushiriki UEFA ujue kocha hana kazi, sababu UEFA ni pesa. Imeshamtokea Moyes na LVG.

Ed ni mzuri sana kwenye Biashara lakini si mzuri kwenye mafanikio ya timu kisoka. Kenyon alikuwa bora kwenye vyote lakini sanasana kwenye soka.

Halafu Ed hajui hata soka kivile lakini Mou akitaka mchezaji anamwambia huyo hatufai au huyo hayupo tofauti na wachezaji tulionao. Hii kazi angalau angetafutwa Director of Football ili awe anafanya maamuzi ya namna hiyo na si yeye Ed ambaye kwake mpira ni baishara tu.
So tusipopata nafasi ya kucheza UEFA next season una uhakika kuwa Mourinho atafurushwa pale OT??
 
Back
Top Bottom