Mkuu hapo tunaongelea in general context
Angalia mfano Mou timu alizofundisha na kupata mafanikio, Porto, Chelsea mara 2, Real Madrid na Inter
Porto kachukua UCL, je Guardiola anaweza beba UCL na Porto au timu yenye profile sawa na Porto?
Angalia alichokifanya akiwa Inter, kocha wa kwanza kushinda makombe 3 ndani ya msimu mmoja tena akiwa na Inter ya kawaida tu
Ameenda Uingereza wababe wakiwa ni United na Arsenal, tangu aingie pale Premier imekuwa ya yoyote, hakuna wenye haki miliki
Madrid amechukua Segunda na kombe la ligi huku akiwa anapambana pengine dhidi ya timu bora kuliko zote kwa wakati wote duniani. Hapa naongelea Barcelona ya Lio at his prime, Iniesta, Xavier, Bosquet, Puyol n.k
Rudi kwa Guardiola, kwanza nakubali kwamba Guardiola ni moja kati ya makocha bora duniani
Lakini lazima tukubali kwamba mafanikio yake kwa sehemu kubwa yamebebwa na ubora wa individual players aliowahi kuwafundisha, udhaifu wa ligi alizopitia na support anayoipata kwa wamiliki wa club zake. Hii inajidhihirisha pale Barcelona, Bayern Munich na City anapondisha kwa sasa
Na ndio maana sitashangaa siku za usoni, nikimuona Guardiola anaenda PSG au Juventus