mkuu utakuwa umesahau
- unafahamu ya kwamba mauricio pochettino misimu yake mitatu ya mwisho hajawahi kushuka kwenye top 3?
- msimu wa 2017/2018 licha ya kwamba manchester united wamefanya usajili wa gharama sana kwa kisingizio cha kujenga timu lakini tumetofautiana kwa point 4 na tottenham hotspurs?
- msimu wa 2016–17 unafahamu ya kwamba tottenham walitupita kwa point 17 ambapo wao walishika nafasi ya pili nyuma ya chelsea na sisi tuliishia nafasi ya 6 chini ya jose mourinho.
tunasahau ya kwamba ni mourinho huyu ndiye aliyesema msimu uliopita yupo on fire kwa sababu ya upana wa kikosi alichonacho hususan baada ya kusajiliwa nemanja matic.
"I want to play West Ham a difficult match, then go to Swansea for another difficult match. I want the Champions League to start. I want, I want, I'm on fire. But I will behave on the touchline, even if goals are offside,"
sasa mtu kama huyu unamtafsiri vipi pindi anapokwambia hana timu ya ushindani?
ed woodward inawezekana hakucheza mpira ila nayeye mpira anaufahamu ndio maana msimu huu baada ya kumsajili fred na diogo dalot akaachana na habari za usajili kwa sababu ujio wa fred ni kwa ajili ya carrick na ujio wa diogo dalot ni kwa ajili ya antonio valencia ambaye hata woodward naye anajua fika valencia hakuwa na msimu mzuri ndio maana akatafuta mbadala wake kwa haraka.
ed woodward naye anafahamu fika ya kwamba haiingii akilini nimekuletea martial, sanchez, mata, matic, pogba, lukaku,fred,bailly,lindeloaf, shaw, dalot, mkhitaryan, rojo, ibrahimovic na bado unasema ni timu dhaifu.
timu imekosa muunganiko mzuri wa kimfumo jambo linalopekea wachezaji wanatembea kama
bata mzinga