"kwetu sisi matokeo ya ndani uwanja hayana athari kubwa sana kwenye soko letu la biashara." (ed woodward)
mashabiki wa manchester united waliodhamiria kukodi ndege kwa ajili ya kumdhihaki ed woodward wakae wakijua hawatabadilisha upepo na hizo gharama za kukodi ndege ni bora wangelitoa sadaka kwa wanaohitaji msaada.
ni rahisi sana kwa familia ya glazer kuiuza manchester united kuliko kumruhusu ed woodward aondoke manchester united kwa kutumia hoja dhaifu za jose mourinho na walimu wengine waliotangulia.
- ed woodward amelipa pound million 30 kwa ajili ya luke shaw wakati wa van gaal halafu anatokezea mshabiki anamlazimisha ed woodward alipe tena pound millioni 60 kwa ajili ya alex sandro, inamaana kama alex sandro naye hakuendana na falsafa ya mwalimu mourinho ed woodward atoe tena pound millioni 80 kwa ajili ya usajili wa marcelo?
- ed woodward amelipa pound millioni 80 kwa ajili ya victor lindeloaf, bailly na marcos rojo na halafu anatokezea mshabiki anamtaka ed woodward alipe tena pound millioni 60 kwa ajili ya maguire au toby alderweired, kama hawajendana na falsafa ya mwalimu atoe tena pound millioni 80 kwa ajili ya sergio ramos?
- ed woodward alilipa pound million 60 kwa ajili ya di maria na mwisho wa siku van gaal alishindwa kumtumia ipasavyo dimaria ndipo akamuuza, ed woodward akatoa tena pound millioni 45 kwa ajili ya antonio martial, mourinho ameshindwa kumtumia ipasavyo , bado ed woodward akatoa tena pesa kumsajili alex sanchez, ina maana tunataka ed woodward alipe pound millioni 100 kwa ajili ya bale na kama haendani na style ya mourinho muheshimiwa ed woodward alipe pound millioni 300 kwa ajili ya mbappe?
- ed woodward ametumia zaidi ya pound millioni 250 kwa ajili ya matic, schneiderlin, fred, fellaini, depay memphis, pogba na bado munataka ed woodward alipe pound millioni 50 kwa ajili ya luka modric, inamaana kama naye haendani na falsafa ya mourinho ed woodward alipe tena pound millioni 70 kwa ajili ya toni kroos?
- ed woodward amelipa pound millioni 75 kwa ajili ya romelu lukaku na huku upande wa pili wa majirani zetu wamelipa nusu ya pesa hiyo kwa ajili ya mfungaji bora wa msimu uliopita lakini bado kuna watu wanamtaka ed woodward atoe tena pesa kwa ajili ya usajili wa striker eti kwa sababu lukaku siyo top striker, hivi aliyetoa wazo la kusajiliwa lukaku ni ed woodward?
- hivi aliyetoa wazo la kuuzwa kagawa, van persie, chicharito, luis nani pia ni ed woodward?
kikosi cha tottenham hotspurs
hugo loris, kieran trippier, sergi aurier, vertonghen, alderweireld, wanyama, dembele, dier, eriksen, dele ali, sissoko, kane, rose.
hivi jamani tottenham hotspurs wanafanya vizuri ndani ya uwanja ni kwa sababu wana mwalimu bora au wana mwenyekiti bora?
tusisahau ya kwamba msimu huu totenham hotspurs hawajafanya usajili.
unapiga shoot target mbili kwenye mechi dhaifu dhidi ya brighton halafu unamlaumu ed woodward eti hajampa mourinho pesa ya usajili hii ni sawa?
msimu uliopita brighton alifungwa goli tano uwanjani kwake na liverpool na mlinzi wa kati alikuwa widjnaldum na lovren
unacheza na leicester city uwanjani kwako unapiga shoot on target nne halafu unamlaumu ed woodward je hii ni sawa?
unadhalilishwa na sevilla halafu unamlaumu ed woodward hajatoa pesa kwa ajili ya usajili wa messi hii ni sawa?
mourinho anapaswa ashukuru sana kufanya kazi na huyu jamaa asiyejali sana maokeo ya ndani ya uwanja kwa ajili ya kutimiza majukumu yake ya kazi.
abramovich akupe pound millioni 300 kwa misimu miwili halafu umletee ujinga na bado akupe mkataba mpya?