Belo
JF-Expert Member
- Jun 11, 2007
- 12,913
- 10,263
Again Jose hawezi kuwa Klopp/PepHakika una hoja mujarabu kabisa. Hongera sana ndugu yangu.
Nimekuwa nikipiga kelele humu miaka sasa kuhusu mourinho na uwezo wake kimbinu ambavyo hauendani na soka la kisasa. Mpira wa kisasa kujilinda ni wewe kumiliki mpira. Huwezi kujilinda "Defend" kwa kuwa na "Poor Possession".
Bahati mbaya au nzuri Ni mashabiki wachache tulifanikiwa kuona gap la Mourinho kuwa haendani na soka tulilolizoea la manchester united; na ndio sababu hata Sir Alex Furguson hakumuweka Mourinho kwenye hata top 3 ya makocha wa kumrithi. Ukisoma kitabu cha furguson Cha "MY AUTOBIOGRAPHY" utaona haya niliyosema. Mzee Boby Charlton yeye ndio aliongoza jopo la wanamanchester united kumkataa Mourinho asitue Klabuni. Hapo sijawazungumzia wachezaji manguli wa Manchester united waliopinga ujio wa Mourinho. Gigs mpaka leo hapatani na mbinu za kocha wetu.
Hawa wote ni watu waandamizi kwenye club. Ni watu wazito.
Hoja kubwa ya wanaomtetea mourinho wanajiegemeza kwenye mafanikio ya kutwaa kombe la Europa na kikombe cha FA. This doesn't justify his collapse. Huwa nawashangaa sana sijui ni ukichaaa!!!!!
Wanasahau ni mourinho huyu huyu alitolewa Chelsea akiwa katoka kuwapa Kombe la ligi. Wamesahau. Kama ni suala la uvumilivu wangeanza kuwa nao chelsea.
Mbaya zaidi hata ukiangalia mpango kazi wa mourinho huoni future ya team. Kwa ligi yenye kocha kama Guardiola, na Klop inabidi uwe na kocha mwenye mbinu bobezi na za kisasa kupambana nao.
Niliwahi kuandika hapa na ninarudia tena ili upime uwezo wa Mourinho angalia opponents wake wakubwa katika ligi ambao kwa sasa ni Guardiola na Klop. Tangu klop katua Liverpool unaona kabisa ni suala la muda tu team ianze kula matunda. Tayari ameshaifikisha team fainal mbili za Europa na Uefa.
Guardiola nae kila mtu anajua alichofanya last season. Kapoteza game moja ya Ligi. Timu yake imefunga zaidi ya magoli 100. Huitaji elimu ya kiwango cha masters kuona utofauti.
Mbaya zaidi mourinho hajawahi kufurukuta mbele ya Guardiola. Huu ndio wasiwasi wangu mkubwa. Wote tunajua alichokuwa akifanywa alivyokuwa Madrid. Na record ziko wazi.
Mbinu za kizamani za mourinho za kumfunga Arse wenger nje ya uwanja kwa maneno ya shombo hawezi kufanya kwa Guardiola au Klop kwasababu hawa ni Disminders. Ndio maana hata kijembe alichomtupia Guardiola kuwa anamwaga pesa kununua kikombe Guardiola aliishia kucheka tu.
Wengine wanasema mourinho apewe muda. Timu inayoandaa zaidi ya poundi milion 300+ kwa usajili sio ya kupeana muda. Ni taeam inayohitaji instant Results.
Kwa aina ya usajili wanayofanya Klop na Guardiola sioni mourinho akitusua mbele ya hawa watu. Kwasababu yote kwa yote na vyovyote iwavyo destination ya mafanikio ya team ni lazima tutakuwa kwenye chungu kimoja na Mancity,Liver,Chelsea au Arsenal. Chelsea na Arsenal sizipi uhakika sana ya kuwa wapinzani wakubwa msimu huu kwa sababu ya mabadiriko ya makocha. Liver na Mancity ndio team inabidi tujipime nazo na kwa kumlinganisha mwalimu wetu kwa kupima uwezo wake dhidi ya makocha wa hizi team.
Siioni Mancheater. Tunasubiri Ngekewa. Itakuwa team yenye inconsistency.
Klopp/Pep hawezi kuwa Mourinho
Hata waliompa hiyo kazi wanafahamu hilo
Mpira wa kisasa ni kufunga magoli zaidi ya mpinzani wako I think umeangalia WC why Brazil,Spain mabingwa wa possesion wameshindwa na na timu kama France,Croatia
Last edited: