Mkuu so it seems the board is looking at another options....so wanaona wasitumie hela kwa mtu alieshindwa o???
Definately Yes,
Moyes alirithi kikosi akijua atapata nacho mafanikio kwa sababu ni kikosi kilichokuwa kimetoka kubeba ndoo.
Robin Van Persie Alikuwa katoka kuwa top scorer bench kuna sub ya chicharito na welbeck. Hivi ni kocha gani angesajili kwa utatu huu. Nyuma yao alikuwepo Rooney akifanya mambo Van Persie kuchukua golden Boot.
Winger alikuwepo Ashley young + Luis Nani + Wilfred zaha alieletwa baada ya kuwa on loan crystal palace alipotumia one year on loan baada ya kusajiliwa na Ferguson. David Moyes imani yake ya kikosi Kilichoachwa na Ferguson ndio iliyomuangusha na sio suala la kutoletewa wachezaji. Mpaka anaondoka moyes hajawahi kusema alikuwa anabaniwa kwenye transfer.
Sasa unaona watu wanakuja na Hoja "Utumbo " eti moyes hakuletewa wachezaji Comeeeeeon. Uongo.
Watu wanashindwa kutofautisha Mchezaji kukataa kuja manchester United na Bodi kushindwa kusajili.
Kusema manchester united inashindwa kusajili huu ni uongo mzito. Baadhi ya Wachezaji ndio wanakataa kuja united. Kipindi cha David Moyes united Ilikuwa inamvizia Toni Kroos alipokuwa Bayern Munich, ila yeye binafsi Kroos aliamua kwenda Real Madrid. Maamuzi Binafsi na sio team kushindwa kumsajili.
Kipindi cha David Moyea pia team ilimtaka Muller wa Bayern Munich ila mchezaji mwenyewe aligoma kutoka Bayern. Sasa mtu haoni hizi scenario anasema timu inashindwa kusajili.
Bahati mbaya hili wimbi la wachezaji kuikataa united mpaka leo chini ya Mou lipo. Huyo Ivan Perisic kama angekuwa ana nia ya dhati kuja united asingesaini long term contract katika kipindi cha dirisha dogo la usajili united ilipokuwa ikimfukuzia.
Tutofautishe Timu kushindwa kusajili na Wachezaji kuikataa timu. Tunaona Fabinho aliikataa waziwazi Arsenal dhidi ya Liveroool. Kaamua kwenda liver sasa shabiki maandazi atakuja kusema arsenal haiwezi kusajili. Mwisho wa siku mchezaji ni binadamu ana maamuzi yake.
Tukubali tukatae ni wachezaji wachache wangependa kucheza chini ya Mbinu za Mourinho. Leo hii Mchezaji akigombaniwa na Gurdiola na Mou bila shaka karata inaweza kuangukia kwa Guardiola kumnasa mchezaji.
Chini ya Mourinho team inaenda kupitia kipindi cha kukataliwa na Wachezaji kama ilivyokuwa kwa Arsenal na Liverpool Kabla ya ujio wa Klop na kabla ya kuondoka kwa Asrene Wenger.
Ninapomsikia mtu anasema united haisajili namuangalia naishia kusema, huyu mtu hajui asemalo.