Halafu nashangaa timu ikifungwa tu lawama zote zinatupwa kwa Pogba.
Kila mtu atanza kusema Pogba haibebi timu, kwahiyo mnataka Pogba acheze kama beki, kiungo na mshambuliaji kwa pamoja?
Kwasababu tusipofunga lawama ni zake, tukizidiwa kwenye kiungo lawama ni zake, tukifungwa lawama ni zake.
Kuna kitu kimoja tunapishana juu ya Pogba,kwanini lawama zinaelekezwa kwake mara nyingi timu inapofanya vibaya na sifa huelekezwa kwake timu inapofanya vizuri ni kwasababu Pogba ndio Star wetu wa timu kwa sasa tulifahamu hili.
Anapokuwa uwanjani Camera na macho ya Wachambuzi humuangalia yeye zaidi na hata sisi mashabiki wake hii ni sawa na Messi kwa Barca,Cr7 kwa Madrid, Sanchez kwa Asernal na mastaa wa aina yake.
Kwa Man kwa sasa hata kocha anapopanga timu huanza kumuangalia Pogba ndio chaguo la kwanza, na akianza banch kunakuwa na maelezo kwa sababu ni mchezaji mwenye gharama na Star kwa timu.
Pili ni rahisi kuonekana anapofanya vizuri na vile vile ni rahisi kuonekana anapofanya vibaya kwa sababu watu wengi kuna kitu wanategemea kutoka kwake kutokana na thamani yake ndani ya timu.
Na ndio mana umeona akina Scholes, Moyes na Gary Nevile wakisema bado Pogba amekuwa hafanyi vizuri kwenye game kubwa sio ndani ya Man U tu lawama hizi amekuwa akipewa hata timu ya taifa.
Kwanini tunamtaka Pogba kudhihirisha ubora wake timu inapofanya Vibaya ni kutokana na nafasi yake ndani ya Uwanja.
Yeye ndio injini ya timu katika kushambulia kwa sasa, ni namba 8 anapopokea mpira eneo la juu kutoka kwa viungo wa ukabaji au mabeki wetu na ni namba 10 or 11 or 7 timu inaposhambulia katika eneo la ushambuliaji.
Hivyo anakuwa na Sifa za kupandisha mashambulizi au kuanzisha mashambulizi au kushambulia na kufunga inapopatikana nafasi.
Hapa nadhani utakuwa umeona aina ya uchezaji wa Zindane kipindi akiwa mchezaji na utakumbuka aljchofanya katika timu ya Taifa miaka ya 98,2002 na 2006.
Lakini vile vile kama kiungo bado anajukumu la kwanza kabisa la kuzuia mashambulizi katika eneo lake kuzuia viungo wa ukabaji wa timu pinzani na beki wa kati kupanga mashambulizi.
Sasa game ya Juzi hakufanya kile kiichotarajiwa tulizidiwa katika eneo la kiungo hasa katika eneo lake na kuwapa kazi akina Herera na Matic na walizidiwa mana ilikuwa ni viungo 2 kwa 4 wa Madrid.
Na ukiingalia timu yetu kipindi cha kwanza tulikuwa tunakaba baada ya Madrid kuvuka nusu ya uwanja hivyo utaona kuwa namba 8,9,10 na 11 hawakufanya kazi yao vema hivyo mzigo kuhamia kwa Matic,Herera na mabaki sasa na mapungufu ya beki yetu na aina ya viungo tuliokokuwa tubakabiliana nao.
Sasa kama Star wa timu alitakiwa kutuonyesha kitu tofauti na ndio mana ukaona mabadiliko ya kuja Fellain kwa ajili ya kukaba eneo la juu na kutuliza mashabilizi na mipira ya juu.
Technjcally Pogba, Mikh na Lingard ndio waliotuangusha Katika game ile.
Martial na Matta tungewafikiria mapema nadhani wangekuwa na kitu tofauti katika nafasi za Lingard na Mikh .
Fellain na Rashford na Mikh Wangekuja kama sub.
Sent using
Jamii Forums mobile app