Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Man United ikifungwa tu lawama zote zinaenda kwa Pogba, mechi ya Madrid, Rashford alikosa goli la wazi, Lukakua alikosa goli la wazi lakini lawama anatupiwa Pogba
Kukosa goli ni jambo la kawaida, hata hao messi na cr7 wanaweza kukosa, ishu ni pogba kuwa mzito wa kufanya maamuzi, kujiamini sana, na kucheza na jukwaa
 
Kukosa goli ni jambo la kawaida, hata hao messi na cr7 wanaweza kukosa, ishu ni pogba kuwa mzito wa kufanya maamuzi, kujiamini sana, na kucheza na jukwaa

Kwahiyo kukosa goli ni jambo la kawaida? Tukimaliza nafasi ya 6 kwa kukosa magoli ya wazi mtaendelea kumshambulia Pogba.
 
Sikuangalia full mechi hata moja ya pre-season licha ya highlights baada ya game ya Real Madrid niliona yafuatayo

DEFENDERS

CB back walicheza vizuri tatizo sielewi kwa nini walikuwa wancheza offside trick (karibia mara 4) na baadhi ya mabeki Lindelof na Darmian walikuwa wanajisahau na kuvunja offside kwa wapinzani.Smalling alicheza vizuri sana i think kusajiliwa kwa Lindelof kumemfanya aamke.Bailly akicheza katikati huwa anafanya ukuta unakuwa salama kabisa

FULLBACK
Mpira wa siku hizi fullback wana impact kubwa sana kwenye kuanzisha mashambulizi na kutengeneza magoli (Carvajal,Marcelo,Alves,Sandro,Bellerin,Rose,Walker,Mendy).Valencia huwa anapanda vizuri lakini final ball zake ni mbovu na huwa anachelewa sana kufanya decision to be honest United wanahitaji new RB ambaye ni mzuri kwenye kushambulia
,Darmian sio beki wa kushambulia tusubiri Shaw akiwa fit atatusaidia.Blind ni mzuri sana kwenye kushambulia lakini sio mzuri kwenye defence akichezeshwa kushoto

MIDFIELDERS
Kwa perfomance ya ile game unaweza kusema kuwa Matic alikuwa mchezaji wa United tangu zamani while Herrera na Pogba ndio wachezaji wapya.Matic amebalance defensive na offensive msimu uliopita alitoa assist 7.Usajili wa Matic unamfanya Pogba awe free lakini anatakiwa kuwa makini kufanya final decision hasa kufunga na kutoa pass za mwisho.Huu ni msimu muhimu sana kwa Pogba anapaswa kuacha kucheza na jukwaa kusajiliwa kwa Matic ina maana anapswa kutoa assist nyingi na kufunga magoli mengi zaidi

Herrera amekuwa affected na position aliyocheza msimu uliopita DM imemfanya amekuwa anacheza sana nyuma na ufanisi wake kwenda mbele umepungua,I hope atazoea kucheza mbele zaidi kama ule msimu wake wa kwanza ambao alifunga magoli mengi zaidi.Pia I hope Mourinho atampa nafasi ya kucheza Andreas Perreira huyu sina wasiwasi nae kabisa
Fellaini ataendelea kuwa best Mourinho plan B player ndio maana Jose alisema ni rahisi yeye kuondoka kuliko Fellaini

FOWARD
Hapa ndio tuna tatizo kubwa sana msimu huu Lingard,Mata,Mkhitaryan,Rashford,Martial wanapaswa kufanya kazi kubwa tofauti na msimu uliopita kumpunguzia striker(Lukaku) mzigo wa kufunga magoli. Kama Zlatan akirejea atasaidia sana kupunguza mzigo kwenye ufungaji,Licha ya Madrid kutawala sana ile mechi kama Lukaku na Rashford wangekuwa makini kwenye umaliziaji still United angeshinda ndani ya dakika 90
Thanks for this analysis,kudoz@Belo.

Kitu kizuri kwa sasa tuna kikosi kilichosheheni na kutimia ,tunamchanganyiko wa wachezaji wenye uwezo wa wastani na worldclass players.

Nadhani tukipata na mshambukiaji mmoja na winger aliyekamikika tutatawala sana soka la Ulaya kwa msimu mitatu minne ijayo.

Tupo vizuri kwa kweli kwa sasa,kila namba ina wachezaji zaidi ya wawili na wote ni moto.

We, r On fire

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo kukosa goli ni jambo la kawaida? Tukimaliza nafasi ya 6 kwa kukosa magoli ya wazi mtaendelea kumshambulia Pogba.
Yes, kama unakosa mara chache ni jambo lakawaida sana, kama wangetengenezewa nafasi kama zile zaid ya 3 kila mmoja halafu zote wakakosa tungewalaumu, lakni unatengeneza nafasi moja akikosa tutasema ni bahati mbaya, zlatan msimu uliopita ilikua jambo la kawaida, alikua anakosa magoli ya wazi mengi kuliko aliyokua akifunga ndo maana nilikua naongoza kumtupia lawama
 
fundi kumbe upo?
 
Back
Top Bottom