Tukubaliane, kutokubaliana. Spurs msimu huu ulioisha ndio timu iliyokuwa na viungo bora kabisa. Musa Dembele, kwangu huyu ndio kiungo bora kwa sasa pale epl. Jamaa anapiga soka la nguvu,(physics) la akili. Anajua. Huyu kwa wale mliowahi kumwona Patrick Viera hawa jamaa wanafanana sana kwa kila kitu.
Victor wanyama. Huyu ni zaidi ya aliyekuwa kiungo shoka Claudio Makelele. Pumzi, nguvu, stamina, anafunga. Wanyama huyu ni wa kumlinganisha na Kante. Ila kwangu Wanyama yupo juu ingawa kule primeir league wamempa Kante tuzo.
Ericksen. Kiungo mwingine mchezeshaji. Anapambana mwanzo mwisho. Ndio injini ya spurs kwa sasa.
Kiungo yeyote anapolinganishwa na Pogba ni kwa sababu ya thamani ya pogba kwa pesa mlizotumia kumpata. Na si kwa uchezaji wa uwanjani. Dembele, Hererra, Wanyama, na hata kina Toure wa city ni wszuri kuliko huyo Pogba.