baada ya kufungwa na chelsea kwenye FA cup nakumbuka niliandika ndani ya thread hii ya kwamba hatuwezi kuifunga chelsea kama tunashindwa kumzuia
eden hazard namshukuru
jose huko aliko amekisikia kilio changu.
kama tutarudisha kumbukumbu kwenye mechi ya FA cup utagundua ya kwamba mourinho alimpa jukumu
phil jones kupambana na
hazard ila alishindwa kumdhibiti jambo ambalo lilipelekea madhara makubwa sana kwenye ile mechi kabla hata ya herrera kupewa kadi nyekundu, tofauti na mechi ya jana mourinho jukumu lile alilihamishia kwa midfield ambaye ni herrera (one man mark) kumdhibiti hazard na kiukweli herrera hata asingefunga goli na kutoa assist mimi ningelimchagua kuwa ni man of the match kwa jinsi alivyofanikiwa kumdhibiti eden hazard.
hazard ndie mchezaji ambaye amehusika katika utengenezaji wa mabao mengi na ndie kiungo aliyefunga mabao mengi. popote aliposimama hazard jana mita chache nyuma alisimama herrera jambo ambalo liliua counter attack style ya chelsea, style hii niliwahi kuishuhudia miaka kama 10 iliyopita wakati gattuso (jesus) anamdhibiti cristiano ronaldo ndani ya san siro.
pia jambo jengine alilofanikiwa jose ni kuwatumia lingard na rashford kama ni striker force na kukosekana kwa alonso ilikuwa ni tatizo kubwa sana halafu cha kusikitisha zaidi nimegundua central defence ya chelsea ni wazito sana.
pia jose alicheza karata yake vizuri sana baada ya kumuingiza carrick kwa sababu uwepo wa fabregas kulisababisha chelsea kubadili style na kucheza 4+2+3+1 na ukiangalia baada ya carrick kuingia timu ilibadili style na kucheza 5+1+2+1 ambapo kama kawaida herrera aliendelea na kujukumu lake la kumzuia hazard.
hazard kipindi cha mwanzo hakuweza kutengeneza nafasi hata moja, hakupiga shoot hata moja wala hakuweza ku dribble hata mara moja lakini ukimuangalia herrera 100% alifanikiwa kwenye tackle.
kiukweli kwa mambo aliyoyafanya jana jose mourinho ametukata mdomo sisi sote mashabiki maandazi na nimejigundua mimi binafsi sijui chochote kuhusiana na mpira na sistahili kuwa mshabiki wa mpira naamini hata humu wamo mashabiki kama mimi ambao hata tiketi original ya kuangalia mpira old trafford hawajawahi kuiona na wala hawajawahi kufika hata AON Complex ila ni mabingwa wa kukejeli tactics za mourinho, nimejaribu kuzipitia comment zote kuanzia page ya 366 naamini wapo member ambao wanatamani comment zao wazifute kutokana na maneno walioaandika, ila naamini yote inatokana na khofu na moyo wa dhati wa kupenda kuona timu yetu inafanikiwa.
kuanzia leo
- sitalalamika tena eti kwa sababu gani jose anampanga lingard na hata akiamua kumpa tena mkataba wa pound 200000 kwa wiki sitalalamika kwa sababu yeye ndie anafahamu kuhusiana na ubora wa lingard.
- sitalalamika tena kwa nini jose anampenda fellaini
- sitalalamika tena kwa nini martial hapewi nafasi
tumuache jose mourinho afanye kazi yake ila heshima kwenu
RRONDO
kisu cha ngariba
Belo
naamini ndani ya thread hii nyinyi ni washabiki wakweli wa manchester united