Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mi nafikiri umefika wakati kwa Mourinho kuanza kufikiria upya nafasi ya Wazza ndani ya Starting XI ya Man Utd, Wazza amepoteza ubora wake maradufu.

Pia afanye uamuzi sahihi wa Kiungo wa kucheza kando ya Pogba, mengineyo bado nina imani na Kocha na muda wa kurekebisha makosa upo.

Win, Draw or Loose, We are United.
Never say never, United We stand.

GGMU.
 
Kocha tunaye kwani timu alizotoka aliwezaje kupata ubingwa.
Aliwezaje kushinda?
Mou , kocha mliyenaye alikuwa na bus(basi) lake, alikuwa anali-park hilo karibu na alipo mlinda mlango, lilikuwa linaziba ukuta wote, hapiti, mbu, nzi, mende wala mbuzi. Wajanja wamebuni mbinu, walitegesha misumari na matairi ya basi yametolewa upepo wote, yapo bapa, flat tyres, kwa hiyo nafasi imepatikana ya watford, kupitisha pembe zao ,wakikukosa wanakudunga mwiba.

Watford wakiamua kukushughulikia kwa pembe au mwiba ni laima utaanza kujiuliza maswali mengi na kuhisi maumivu makali, makali kweli.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mi nafikiri umefika wakati kwa Mourinho kuanza kufikiria upya nafasi ya Wazza ndani ya Starting XI ya Man Utd, Wazza amepoteza ubora wake maradufu.

Pia afanye uamuzi sahihi wa Kiungo wa kucheza kando ya Pogba, mengineyo bado nina imani na Kocha na muda wa kurekebisha makosa upo.

Win, Draw or Loose, We are United.
Never say never, United We stand.

GGMU.
Ukimweka Rooney benchi mzigo kwa viungo wa chini utapungua na kuwafichia madudu na timu itashambulia kupitia kati
Piga benchi Rooney
Sogeza Pogba mbele
...............
 
Jamani niliwahi kusema ukionja unazoea. Baada ya liverpool kuondoa bikra man united sasa mmezoea huu mchezo. Game ya tatu sasa. Namwonea huruma sana Mourinho.
Next week mnapiga na Leicester city kwa huu mwenendo, sioni matumaini mbele.
Pole sana dadngu everlenk na shosti'ako cute b.
Bado tunachochea kifuu. Usiombe kikawaka.
 
Nnafahamu hilo ila Fellaini ana tatizo ka nidhamu.

Baada ya Juan Zuniga kufunga goli la pili akaenda kumkwatua.

Baadae amesababisha penalty.

Nimekuwa nikimwangalia Fellaini tangu akiwa Everton na hata timu ya nchi yake ya Belgium.

Mwaka 2014 Fellaini alitajwa kuwa ni mmoja wa worst signings of the season in England.

Fuatilia idadi ya kadi alizo nazo na namba ya suspensions ndiyo utaelewa.

Msimu wake wa kwanza England akichezea Everton Fellaini alipewa kadi mara 10 katika mechi 17 na ikabidi akutane na meneja wa waamuzi kuzungumzia hali hiyo na akaapa kujirekebisha ingawa baada ya mkutano huo alipewa kadi zingine 3 katika mechi 16 alizocheza hivyo kuonyesha improvement.
Nafikiri hujaangalia mpira zama za akina Lee Bowyer, Kevin Davies, Robbie Savage.

Hao walikuwa ni zaidi ya wakorofi na kadi ilikuwa jambo la kawaida.
 
14354947_10208846460732251_3227133627932809728_n.jpg
 
Hizi picha zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii naomba msiziamini ni za kutengenezwa(Photo Shop) na ukiziona toa taarifa TCRA maana ni za kichochezi.
1a160658bfb29fcbcff9749af14d8ba8.jpg

a6852fff97dc68d5fdd7b296e53f7374.jpg

NB:Mzee Arsene Masawe Wenger anaongeza sababu za kugoma kwenda sokoni,huwezi kua na £89+M uwanjani inakimbia kama headless chicken.
 
team itaka tu poa ,:hamna haja ya kulaumu . kwa ligi hii ilivyo kila timu itafungwa hakuna timu ambayo itamaliza ligi bila kufungwa.
 
BREAKING NEWS. Juventus to appear in court soon for selling a chinese product to Man United -Zhongba
Hapana mkuu.
Juve waliuza Pogba bora,Man utd wakanunua Pogba ghali,Mourinho ameamua kumtumia Pogba mbovu.
 
Nionavyo mimi,timu ni nzuri,ila sina uhakika kama Mourinho anaweza kuujua na kuutumia uzuri wa kikosi chake.
 
Dah next PL mnacheza na Leicester City timu ambayo ni nzuri kuliko Watford. If Mourinho doesn't get his act right mnaweza kupoteza points tena.
 
Back
Top Bottom