Mkuu sio kwamba tunasema walichokifanya Madrid ni sahihi ila angalia tofauti kati ya hizi club, benitez hakuwa na matokeo mabaya kiivo Madrid ila staili ya uchezaji wa Madrid ulibadilika, walikua wanaangalia zaidi matokeo kuliko entertainment.
Ukiangalia Madrid ndio iliyofunga magoli mengi kwa msimu huu (47), ipo point nne nyuma ya anaeongoza ligi, na point mbili nyuma ya mahasimu wao Barca, still wapo UCL sio matokeo mabayaa kiivo,
Msimu uliopita tunaweza kusema labda kweli van gaal alikua anaijenga timu, msimu huu tulianza vizuri tukaongoza hadi ligi na kuwa point nne juu ya anaeongoza sasa, tukaanza kutolewa C1C, tukaja uefa, tukaondolewa juu ya msimamo, tukaondolewa top four, mwezi mzima wa 12 hatujaonja ushindi, tumepata ushindi baada ya kuenda mechi nane bila ushindi, ( D4 L4) tupo nyuma kwa point Tisa kwa yule anaeongoza ligi, na point tatu kwa yule aliye top four na GD zaidi ya kumi, so kwa lolote lile hata tukishinda mechi ijayo na spurs akafungwa hatuwezi kuenda top four unless tumfunge Newcastle goli zaidi ya kumi,
Licha ya kwamba watu tunawacheka Madrid kwa maamuzi yao ya kukurupuka itabidi tukubali ukweli kwamba hata sisi pia tunachekwa kwa kutumia pesa nyiiingi lakin tuna compete na timu kama west ham, spurs na CPFC, badala ya kusonga mbele tunarudi nyuma,sidhani kama mafanikio aliyoyapata Carlo Madrid angekua utd kuna mtu angekua ana lalamika.
Ukweli mchungu we are now a laughing stoke, every body is laughing at us
hii issue ya man u kutumia hela hebu tuaiangalie kwa jicho la pili.
hela tumetumia kuziba mapengo na sio kuimprove timu, kwanini nasema hivi? hebu angalia hii list
beki yote ya man u hatunayo tena
-namba mbili rafaeli
-namba tatu evra
-beki kati fedinand
-beki kati vidic
pia kuna sub kama alexander butner pia kasepa.
waliosajiliwa ni kuziba mapengo tu na top target za kuimprove tumezikosa kama vile ramos.
midfield kabaki carrick
fletcher, cleverly, anderson, giggs, nani, scholes na niliowasahau hawapo tena na sisi
striker rooney
welbeck, rvp na chicha hawapo.
hivyo ukiangalia wachezaji kama 15 hawapo unafikiri tutazibaje mapengo? usajili wetu ni wa wachezaji wa kawaida tu morgan, blind, rojo, herrera, shaw, darmian etc wote hawa si wachezaji decisive wa kubadili matokeo. na kwa idadi tuliyotumia kusajili wachezaji 10 na zaidi ni ndogo top player siku hizi ni 50+
transfer target za lvg
lvg alitupromise striker ila hakuja na target zake zote hazikuja hivyo huwezi kumpa lawama yeye 100% inabidi nusu ya lawama woodward nayeye apate hawa ni baadhi
-strootman (lvg alimtaka sana)
-muller (japo mgumu kumpata hatujajaribu)
-robben (hana namba bayern sasa hivi)
-ramos (uwezekano wa kuja ulikuwepo)
-bale (kila siku rumors haziishi)
-etc
ukiangalia hao hapo juu wote ni watu wabadilisha matokeo ya mechi. lakini hatuna hata mmoja tumebaki kuwa na team players tu. ukimtoa martial waliobakiwa wote wanategemea perfomance ya timu kubadili matokeo.