mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Mjadala ulioshika kasi nchini ni madai ya Katiba mpya, hasa kutoka vyama vya upinzani.

Naweka bandiko hili baada ya kusoma michango wa ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Dk. Benson Bagonza. Nanukuu baadhi ya michango yake:

Hoja ya Katiba mpya pamoja na sababu nyingine nyingi, inalenga kupunguza au kuondoa mgongano wa hatari kati ya ukuu wa Katiba na ukuu wa Rais. Kwa hali ilivyo, Rais na Katiba wako vitani.

Rais (taasisi) tuliye naye ni mkuu kuliko Katiba, hata kama ni Katiba hii hii inayomleta madarakani. Ukuu wa Katiba hukoma pale inapomwingiza madarakani. Kinachobakia ni ukuu wa Rais asiye mwanadamu wala Mungu. Ni hatari.

Tunaposema rais, msimwangalie Rais Samia. Itazame taasisi ya urais. Hata Rais Samia siku moja anaweza kujikuta ni mhanga wa maguvu yaliyo katika taasisi hii ya urais. Tumkumbuke Chiluba na Kaunda.
Mwisho wa kunukuu.

Je, Katiba iliyopo inampa Rais mamlaka na madaraka gani kiasi cha kuwa juu ya Katiba yenyewe, ambavyo Askofu Bagoza anahoji? Hivyo hoja zangu zitajikita kwenye Ibara husika za Katiba ya JMT (1977).

Ibara ya 33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano. (2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.
Ibara hii haina ubishi kwa kuwa ndio msingi mkuu na utamaduni wa uongozi wa aina yoyote duniani, ambapo anakuwepo kiongozi mkuu. Hata wanyama porini wana kiongozi wao, itakuwa binadamu!!

Ibara 34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara. (3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Katiba imemtumbua Rais kama Kiongozi Mkuu wa Serikali ya JMT na hiyo Serikali ikapewa mamlaka juu ya mambo yote yahusuyo Tanzania Bara. Nawaza tu nani anastahili kuyasimamia badala ya Rais!!!

Ibara ya 34. -(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria. (4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Vifungu hivi, ambavyo kimsingi vinahusu utekelezaji wa shughuli za Serikali, japo bado vinampa madaraka Rais, wahusika wakuu ni watendaji katika Serikali. Isitoshe ni utekelezaji wa mambo ambayo Bunge lina mamlaka nayo, kama ilivyoainishwa kwenye Katiba.

Ibara ya 62.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge. Ibara ya 63.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo. (2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii. Vifungu hivyo bila shaka vinalipa Bunge madaraka ya Kikatiba (kulinda Katiba) juu ya Rais. Kwa sababu hiyo Rais hayuko juu ya Katiba.

Yawezekana haijatokea mgongano kati ya Bunge na Serikali kiasi cha Ibara ya 46 kutumika. Na ikitokea je, ni chombo kipi cha Dola chenye mamlaka ya kulinda Katiba? Ibara ya 46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai. Ibara ya 46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwamujibu wa masharti ya ibara hii. Ibara hii pia imeorodhesha masharti kadhaa ya kumshtaki Rais. Sharti moja kuu lenye kupigiwa kelele ni la Ibara ya 46A. -(2)(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja. Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Rasimu ya Jaji Warioba haikotofautiana sana na Katiba inayotumika ila ilianisha majukumu na madaraka ya Rais kama Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu (Soma Ibara ya 69). Ibara ya 83 ya hiyo Rasimu pia inampa kinga Rais aliyeko madarakani kama ilivyo Ibara ya 46 ya Katiba inayotumika kwa sasa. Ibara ya 84 ya Rasimu haitofautiani na ya 46A ya Katiba inayotumika kuhusu Bunge kumshitaki Rais

Kutokana na mrejesho huo, naamini Katiba iliyopo inajitosheleza kuhusu mamlaka na madaraka ya Rais ila udhaifu uko kwa waliopewa mamlaka na madaraka ya kusimamia Katiba, ambao hula kiapo kuilinda. Hata kama kutakuwa na Katiba mpya pasipo uadilifu na uwajibikaji wa wenye mamlaka na madaraka, tatizo litabaki lile lile.
 
Ardhi yote imekabidhiwa kwa Rais, ni mali ya Rais. Wewe ukipewa hati miliki ya kiwanja ama shamba unakuwa umekodishwa kwa miaka itakayo andikwa kwenye hati.

Kuna siku nchi itampata Rais mlafi atakuja kuamua kuiuza Kigamboni au Mafia ama kisiwa cha Saa 8 kwa wawekezaji. Na fedha akazitafuna yeye na jamaa zake.

Lakini pia anaweza akatoa kama zawadi kwa nchi jirani wilaya/mkoa mmojawapo wa mpakani. Na hamuwezi kumfanya kitu, si amewekewa kinga na ardhi yote ni mali take?!!!

Watu wa wilaya/mkoa husika wakileta za kuleta anaweza kuwapiga wao mpaka mashangazi zao hadi wachakae. Ikibdi hata kuwavua uraia kabisa. Mm naiona hii katiba ni janga kubwa.

Tuirekebishe hii katiba kwa faida yetu sote na vizazi vijavyo.
 
Kweli mtaji wa BAVICHA na BAWACHA ni ulimbukeni na ujinga. Kwa hiyo akishagawa hiyo wilaya au mkoa kama zawadi, na watu waliokuwepo hapo anawatoa kama zawadi?

Hebu tujaribu kujenga hoja nzito ya kutaka katiba mpya na si huu ujinga. Tunaona tu mchakato wa kutoa ardhi kwa wageni ulivyo mgumu leo unazungumzia mtu kupewa ardhi kama pakiti ya chumvi?
 
Uchu wa WATANZANIA kudai KATIBA Utafikia Hapa Siku Moja.

IMG_20210707_174714.jpg
 
Mmeanza CHADEMA na ufitinishi wenu, jamani mlivyo na matusi mi sina hata hamu na nyie.

Mmeshaambiwa msubiri nyie mnaforce! Na cha ajabu katiba mnayoitaka ni Ile mnayotaka nyie tu

Mbona katiba ya chama chenu hamuitekelezi?

Watu wamekata rufaa baraza kuu hamtaki kuitisha ila mnazidi kuwacharula!!
 
Kweli mtaji wa BAVICHA na BAWACHA ni ulimbukeni na ujinga. Kwa hiyo akishagawa hiyo wilaya au mkoa kama zawadi, na watu waliokuwepo hapo anawatoa kama zawadi? Hebu tujaribu kujenga hoja nzito ya kutaka katiba mpya na si huu ujinga. Tunaona tu mchakato wa kutoa ardhi kwa wageni ulivyo mgumu leo unazungumzia mtu kupewa ardhi kama pakiti ya chumvi?
Kuna mdau ametoa comment hapo juu kwamba mzee Mwinyi aliwapa zawadi waarabu hiyo Loliondo unayoijua wewe. Kwahiyo siyo mageni haya tunayo yaandika
 
Vifungu ulivyonukuu ni viini macho ukitaka kujua ubovu wa katiba tuliyo nayo rejea yafuatayo
1)Mwendazake alikuwa anawaambia watanzania hatapeleka maendeleo kwenye majimbo yanayowakilishwa na wapinzani.

2) Aliweza kuwatishia maDED kuwa kwa vile yeye ndiye anayelipa mishahara na marupurupu yao hatawaelewa wakimtangaza mpinzani kuwa kashinda uchaguzi.

3) Wabunge wasio na sifa za kuwa wabunge wamo bungeni na hamna wa kuchukua hatua

4) Watendaji wote serikalini pamoja na majaji ni wateule wa rais kwa hiyo hamna wa kumdhibiti

5) Kwa katiba tuliyo nayo rais kupitia waziri wa fedha ndiye anaeamua matumizi yote ya pesa za serikali na bunge ni rubber stamp. Mbunge haruhusiwi kupeleka hoja bungeni inayohusu matumizi ya pesa.

Ndiyo maana wakati ndugu zetu wa kagera walipopatwa na tetemeko la ardhi rais siyo tu hakuwasaidia bali hata msaada waliopewa na wasamalia wema alikataa kuwapa na kuishia kuwasimanga kwamba yeye hakuleta tetemeko.

Hiyo ni mifano michache na suhisho lake ni katiba mpya.
 
Ardhi yote imekabidhiws kwa rais, ni mali ya rais. Wewe ukipewa hati miliki ya kiwanja ama shamba unakuwa umekodishwa kwa miaka itakayo andikwa kwenye hati...
Umetoa hoja za msingi bila kutoa mapendezo km umiliki wa ardhi.
 
Naomba kupata ufafanuzi juu ya madaraka yaliyotopea ya nafasi ya urais wa Tanzania ni kofia ipi impayo nguvu sana Kati ya hizi tatu
1. Urais
2. Umwenyekiti
3.Uamiri mkuu wa jeshi.
 
Naomba kupata ufafanuzi juu ya madaraka yaliyotopea ya nafasi ya urais wa Tanzania ni kofia ipi impayo nguvu sana Kati ya hizi tatu
1. Urais
2. Umwenyekiti
3.Uamiri mkuu wa jeshi.
Vyote kwa pamoja kulingana na Muktadha husika.....BTW tafuta pesa haya mengine achana nayo hayana TIJA.
 
Hayo manyazfa mzee lazima uweze kuyachanga kama karata

Mtu yule yule ila anabadilika kulingana na muktadha

Ila kumbuka anabadilika nyazfa lakini dhamira ipo palepale

Ukiamua kukutumbua kokote utakapokimbilia anakugusanisha tu

Lakini hii ni nzuri sana lazima ifike mahali tuheshimiane
 
Back
Top Bottom