Mambo ya kuzingatia unapokula Pweza na Ngisi njiani

Genius jack

New Member
Aug 28, 2021
4
42
Leo muda wa jioni nilikuwa maeneo ya Mbezi ya Kimara nilikuwa nimesimama namsubiri rafiki yangu pembeni kwa mbele kulikuwa na mtu anauza supu ya pweza na vipande vyake na ngisi na kachori.Nikiwa pale walikuja watu kadhaa kununua nilichokiona.

Mteja alikuwa anachukua kijiti cha kuchomea anatoboa mmoja anachovya kwenye pilipili kisha anaweka mdomoni hii ilikuwa ni inajirudia mwingine akawa akishaweka mdomoni anatoboa na kijiti chake kile kile kipande cha pweza anaona sio kikubwa anavyotaka anakisogeza anatafuta kitakachomvutia, kwa kijiti kile kile ambacho tayari alikuwa anakitoa mdomoni, Ilibidi kuongezea umakini wangu eneo lile nikiwaza mimi pia nakulaga vitu hivi akaja mtu akawekewa supu akamaliza akarejesha kibakuli muuzaji akakirusha kwenye ndoo ndogo pembeni uliyokuwa na maji nusu, wakaja watu kadhaa inaonekana tayari alikuwa ni mtu mwenye wateja wake vizuri, baada ya vibakuli kadhaa kujumuika kwenye ndoo akavichovya chovya kwa kuzungusha kwenye ndoo akavikumuta akaweka mezani, walikuja watu wa rika zote pale na jinsia tofauti, niliumia moyoni maana niliwaza afya zao nilisubiri watu wapungue kisha nikamfwata akiwa mwenyewe Muuzaji anangoja wateja nikamweleza Kuna mapungufu nayaona mkuu alipoona nazungumza naye kirafiki alinisikiliza.

Mwishowe nikampa mambo ya kuzingatia

1.Vyombo unavyotumia vioshe na sabuni kisha visuuze vyema na uweke maji ya moto ukiweza nilimwonyesha vyombo alivyoviweka mezani kutumika vikiwa na mafuta mafuta.

2. Nikamweleza unapoweka mtu kuchoma waambie ukitoboa ukaweka mdomoni kitupe hicho uchukue kijiti kingine.

3. Kuepuka suala la mtu kuchovya kwenye pilipili kuweka mdomoni kisha kutumia kijiti hicho anachovya tena kwenye pilipili wawekee visahani mtu ajichukulie pweza wake na kachori au ngisi wake kisha mimina pilipili yake atumie kuepuka mwingiliano sana na contamination.

Alinishukuru maana sikuonesha kumkaripia wala kuonyesha hisia zangu nilivyoumizwa na jamaa akaniambia ww umenishauri vyema.

Wito wangu kwa ndugu tunaokula vitu barabarani wapo wengine wanaenda kununua mahindi ya kuchoma analishika hili analiacha analishika tena lingine wewe ukija unaweka mdomoni tu bila kuzingatia afya yako na lingine linakuwa pembeni lishapoa muuzaji analipasha kishkaji anakupa, yakupasa kuwa makini usijekupata minyoo Njiani, au kuhara au kuumwa tumbo au Hata uviko-19 kirahisi kupitia kula sehemu ambazo hawazingatii usafi na afya pia wauzaji wa vitu hivi nawasihi kuongeza usafi na ustarabu.

Niishie hapo natumaini wengi watabadilika kama brother niliyemshauri leo, Mbezi ya kimara.
Nawatakia biashara njema katika kujitafutia kipato.
 
Hilo Jiji lenu la Dar uchafu ni kama kaka na dada. Sijui mnakwama wapi !

Kuna siku nimekaa kwenye baa nakunywa maji ,ikabaki chupa kavu mara akatokea mama mmoja akaniomba hiyo chupa ,nikawa namwangalia kwa mbali anakoelekea,akakaa kwenye ndo yake ya juice akaanza kumimina kwenye chupa bila kuosha hiyo chupa ya maji .

Hizi juice za mtaani hazifai watu hawaoshi chupa wanazookota
 
Unapata huduma kwa kadri unacholipia, ukitaka usafi inabidi uende huko kwenye migahawa na hoteli kubwa nunua sea food platter...hizi za mtaani huwezi kukwepa mapungufu madogo madogo kama hayo
Mkuu mbali na mapungufu ukizoea hizi misosi ya mtaani ina utamu wake
 
Ni kweli kabisa mkuu sio salama, lakini kukwepa hiyo ishu ni ngumu sana.

Kwanza muda, hapo unaposema jamaa azioshe kwa uzuri hizo bakuli na wateja wanamsubiri ni ishu sana mzee, kuna wateja watachoka kusubiri atawapoteza.

Pili mkuu ni hasara kutumia izo stick hovyo hovyo namna hiyo na kwa njia hiyo atachafua vyombo vingi na muda wa kuosha hana achilia mbali kununua hizo stick mara kwa mara.
Jamaa yako huyo atajirekebisha kwa mambo machache tu mengi utakuta kama yalivyo.
 
mnafanya maisha kuwa magumu sana jamani.

kwani ukila mate yangu kitu ambacho ni ~0.0000001 unaugua ugonjwa gani??au ni kinyaa tu??
 
Nimeshuhudia Mimi mwenyewe jamaa anavyo toa vipande vya pweza ndani ya mfuko na kuviweka kwenye meza, nilishtuka Sana maana hakunawa na alipo maliza kutoa mzigo akajifuta kwenye suruari alio vaa yani ni uchafu kwenda mbele (manzese).
 
Kuna siku nimekaa kwenye baa nakunywa maji ,ikabaki chupa kavu mara akatokea mama mmoja akaniomba hiyo chupa ,nikawa namwangalia kwa mbali anakoelekea,akakaa kwenye ndo yake ya juice akaanza kumimina kwenye chupa bila kuosha hiyo chupa ya maji .

Hizi juice za mtaani hazifai watu hawaoshi chupa wanazookota
Nyingine wanaokota zimekojolewa.
 
Nimeshuhudia Mimi mwenyewe jamaa anavyo toa vipande vya pweza ndani ya mfuko na kuviweka kwenye meza, nilishtuka Sana maana hakunawa na alipo maliza kutoa mzigo akajifuta kwenye suruari alio vaa yani ni uchafu kwenda mbele (manzese).
Ila ni afazali hao ambao unaona huko ndan yanafanyika mengi san.yote kwa yote mishikaki ya nongo inanoga kuliko hiyo ya umaridadi.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Kwa theory kuna ma bwana afya na ma bibi afya wanapaswa kuangalia hali ya usalama ki afya katika uuzaji wa vyakula. Ki uhalisia huwa wanahongwa hela kidogo na wanajifanya hawajaona chochote.

Nilipoona nguvu ya hawa watu wa afya ni nje ya Tanzania. Wanapita kila sehemu inayo andaa chakula na wakikuta mazingira hayaridhishi biashara inafungwa.
 
Back
Top Bottom